Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

MWANAMKE JEURI SEHEMU YA 04

3rd Aug, 2025 Views



Baada ya majirani kuondoka; Anshera alichukua mizigo yake kisha aliingia ndani, alizungusha macho huku na huko, alitafuta sehemu ya kukaa. Hakujua akae wapi kwa sababu makochi yalikuwa machafu, viti vibovu, kwa hasira aliamua kukaa sakafuni kisha aliwaita wazazi wake akitaka kuwauliza maswali magumu.

"Mama na baba, sasa haya ndo maisha gani? hivi nyie katika ujana wenu mlikuwa mnafanya nini?"
"We Anshera wewe!! Ndo maswali gani hayo unatuuliza sisi wazazi wako?.. Unaamua kutukosea adabu si ndiyo?"
"Hii ndio shida ya wazazi wa kibongo, ukiwahoji kuhusu mafanikio wanakuambia unawakosea adabu.... Wazazi wenzenu wana majumba mazuri, magari na biashara lakini nyinyi mpo mpo tu. Hivi mama ilikuwaje ukaolewa na baba maskini? kwani wanaume wenye pesa hukuwaona?. Na kama ulimpenda baba, kwanini hukumlazimisha atafute kwanza pesa?"
"Kwahiyo unamkataa baba yako si ndio?"
"Sio kwamba namkataa, ila hii hali ni mbaya!! Tatizo lenu nyinyi watanzania mnapenda kuridhika na maisha yenu. Mnadhani kwamba umaskini ni majaaliwa!! Mnadhani kwamba umaskini ni maisha. Wengi wenu hamjui kutafuta lakini mnataka kupata. Wengi wenu mnapenda kupanga mipango ya kuzaa kuliko kupanga mipango ya kutafuta mafanikio. Wengi wenu mnapenda kuanza kuzaa kabla ya kutafuta maisha. Hivi kwanini mlinizaa kabla hamjatafuta pesa? mliharakishia nini?.. Kwanini hamkutafuta kwanza pesa kisha mnizae mimi?"
"Mmmh" Mtu na mkewe waliguna, walikosa majibu.
"Baba na mama ebu jitazameni. Mna umri wa miaka zaidi ya 50, ina maana katika miaka yote mliyoishi mlishindwa hata kununua Tv, meza ya vioo, kabati zuri na mengineyo?"
"Mama Anshe ebu tuondoke, hii nyumba ishakuwa ndimu"
"Hii ndo shida ya kusomesha watoto nje ya nchi"
"Mna uhakika mlinisomesha nyinyi au serikali?"
"Basi mama yameisha, ngoja tukuache upumzike kwanza"

Mtu na mkewe waliamua kuondoka. Walimkimbia binti yao waliyemzaa wao wenyewe. Walimuogopa kutokana na maswali yake magumu ambayo aliuliza. Hawakujua wamjibu nini. Pia walishindwa kumfokea kwa sababu binti aliuliza maswali muhimu katika maisha.
Baada ya wazazi kuondoka; Anshera bado alikaa chini sakafuni akiwa amekasirika. Alichukia kila kitu ndani ya nyumba yao. Moyoni alipanga kubadilisha kila kitu ili waishi maisha ya kizungu. Alitaka wazazi wake wawe wanapendeza muda wote, kila siku wale nyama na wali kuku, walalie magodoro mapya, nyumba mpya na wasitegemee kilimo.

*****
Siku iliyofuata Anshera aliripoti katika ofisi za halmashauri. Alipokelewa na mkurugenzi wa halmashauri kisha alitambulishwa kwa wafanyakazi wengine. Ujio wake ulidatisha wanaume wengi ndani ya manispaa, alishobokewa na kila mtu kutokana na uzuri wake. Hata mkurugenzi wa manispaa muda wote alitabasam kwa furaha, alifurahi akiamini amepata mboga mpya kutoka marekani.
Licha ya kupokelewa vizuri lakini Anshera hakuwa na raha, alikasirika ghafla. Alichukia kutokana na uchakavu wa majengo ya halmashauri. Majengo hayakumvutia hata kidogo. Pia wafanyakazi wengi wa halmashauri walionekana kuwa choka mbaya, wengi wao hawakuvaa mavazi mazuri, walivaavaa ilimradi tu.
Hali hiyo ilimchukiza sana Anshera, yeye alitegemea ameajiriwa kwenye ofisi za ghorofa, alitegemea kuona majengo mazuri kama marekani. Pia alidhani angekutana na wafanyakazi smart; wanaovaa suti na mavazi bomba kama wamarekani. Lakini kwa bahati mbaya alikuta mambo tofauti.

Baada ya mapokezi na utambulisho huo, Mkurugenzi alimchukua Anshera alimpeleka katika ofisi yake. Macho ya Anshera yalitua kwenye kompyuta mbovu, kiti cha mbao, hakuona feni wala hakukuwa na AC, chumba cha ofisi kilikuwa kibayaaa!!
"Karibu sana binti yetu mzuri, mkuu wetu wa idara ya sheria, hii ndiyo ofisi yako" Mkurugenzi alizungumza kwa sauti ya uchangamfu akiwa anachekacheka bila sababu ya msingi.
"Kwahiyo mimi Anshera nimetolewa marekani kuja kufanya kazi kwenye ofisi hii yenye harufu mbaya?. Yaani mimi nikae kwenye kiti cha mbao? kiti hata kuzunguka hakizunguki, chumba kimejaa joto kali; mimi nishazoea baridi la USA.... Ebu tazama hii kompyuta hata kuwaka haiwaki, mafaili yamechakaa, mkurugenzi utanisamehe; mimi siwezi kufanya kazi kwenye ofisi hii" Anshera alianza balaa lake.
"Lakini binti husifananishe mambo ya marekani na Tanzania, kumbuka kwamba nchi yako bado ni maskini"
"Umaskini wenu unanihusu nini mimi? kama mlijua nyie ni maskini, kwanini mlinileta huku? mnapenda wasomi wa gharama wakati hamna uwezo wa kuwamiliki... Kwaheri mkurugenzi" Anshera aligeuka akitaka kuondoka
"Sasa unaenda wapi?"
"Nishasema siwezi kufanya kazi kwenye ofisi hii, nawapa wiki moja; irekebisheni kwanza kisha nitakuja jumatatu ijayo, nikikuta bado hamjafanya maboresho nitaondoka tena kisha sitokuja tena" Anshera alizungumza kauli ya mwisho kisha aliondoka pasipo kutazama nyuma.
Mkurugenzi alivuta pumzi ndefu kisha aliziachia. Alijua kazi ipo. Tangu awe mkurugenzi hakuwahi kukutana na mfanyakazi mwenye jeuri namna hiyo. Alikuwa na uwezo wa kumzuia au kumpa adhabu yoyote ila aliogopa kugombana na binti mrembo, pia alihofia kumpoteza katika halmashauri hiyo. Alitaka binti aendelee kuwapo mahali hapo ili apate nafasi ya kumtumia kiutu uzima.

Baada ya Anshera kuondoka, Mkurugenzi alitii maagizo ya Anshera. Siku hiyo hiyo aliita mafundi kisha aliwapa kazi ya kuboresha ofisi ya Anshera. Alinunua komputa mpya, kiti cha kuzunguka, mafaili mapya, kila kitu alibadilisha ili tu kumridhisha Anshera.

*****
Wiki iliyofuata Anshera alirudi tena ofisini, alikuta kila kitu kimewekwa sawa, hapo sasa alikubali kukaa ofisini.
Licha ya kukubali lakini hakufanya kazi yoyote. Muda mwingi alikuwa akichati kwenye simu yake, mara alitoka nje alianza kupiga picha mbele ya wafanyakazi wenzie, alijibinua mara huku, mara kule, hakuogopa mtu.
Matendo yake yalipelekea awe kivutio mbele ya wafanyakazi wenzie. Watu waliacha kufanya kazi kisha walichungulia madirishani wakimtazama Anshera.
"Wakuu ofisi imeingiliwa, tazama mtoto yule, kama kashushwa vilee!! cheki miguu ilivyo mitamu, miguu imejaa ujazo kama wotee!! Cheki mtoto alivyobinuka, shepu kama kachongwa vilee!! kifua kama under 14... Jamani nyie mwaka huu tutauwana!! Yule ni wangu!" Muhasibu wa halmashauri aliwahi nafasi.
"Yule hata mimi simuachi. Tena ngoja nimfuate mapema kabla mkurugenzi wetu hajaanza mambo yake" Afsa Ugavi nae alikuwa hoi.
""Hivi yule ni Mtanzania kweli? mbona kama toto la kizungu au kiarabu au kihindi au kikorea au kifilipino au kichotara?" Muhasibu aliuliza
"Ni muhiraki wa hapa hapa Babati Tanzania. Kwao kazaliwa yeye pekeyake, na ni msomi wa Havard" Mgavi alijibu
"Duh kumbe kasoma Harvard, aisee Halmashauri yetu imebarikiwa kuliko halmashauri zote Tanzania" Muhasibu alizungumza akiwa anatabasam, moyoni alipanga siku hiyo hiyo ni lazima amtokee Anshera.

Sio wanamume wa halmashauri tu, hata wadada na wamama wa halmashauri walipagawishwa na ujio wa Anshera. Walishangazwa na uzuri wa binti huyo. Wanawake waliunda vikundi vya umbea kisha walimjadili Anshera. Walimjadili kwa kumsengenya. Walimuonea wivu kutokana na uzuri wake.
"Mwache aje kichwakichwa, hawajui wanaume wa halmashauri hii; hawaachagi kitu." Sekretari alizungumza
"Na kwa shepu ile, kwa maringo yale, kwa kujitingisha kule, kwa kujishauwa kule, nakwambia hamalizi mwezi atajazwa mimba" Mdada wa masjala nae alitoa ya moyoni
"Halafu ile rangi yake mbona kama imezidi weupe? hajikoboi kweli yule? hata kama ni uzuri ule wake umezidi kaah!! kama malaika mxiew" Sekretari aliendelea kutoa makasiriko yaliyojaa wivu.
Mijadala ilikuwa mingi, hasa hasa kutoka kwa wanaume. Wengi wao walionyesha nia ya kutaka kumtongoza Anshera.

****
Mtu wa kwanza kufungua dimba alikuwa ni Afsa Ugavi. Alisubiri muda ambao Anshera alielekea ofisini kisha alimfuata. Kwakuwa yeye ni mfanyakazi wa ofisi hakutaka kubisha hodi, alisukuma mlango alizama ndani; Alimkuta Anshera akichati kwenye simu yake, akiwa anajizungusha kwenye kiti chake.
"Mwanasheria wetu mpya, habari yako binti mrembo" Mgavi alizungumza kwa uchangamfu akiwa anakaa kwenye kiti.
"Umeingiaje ofisini kwangu bila kuruhusiwa? na nani kakuambia ukae kwenye kiti changu? Anshera aliuliza swali akiwa bado anajizungusha kwenye kiti chake.

BALAA LIMEANZA....

USIKOSE NEXT EP....
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MWANAMKE JEURI SEHEMU YA 04  >>> https://gonga94.com/semajambo/mwanamke-jeuri-sehemu-ya-04
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest