Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

BLOOD MOON EPISODE 1

3rd Aug, 2025 Views 27


"Lucas....lucas....weee lucas...we mbwa si nakuita" mwisho mwalimu aliita kwa hasira, lakini hata hivo Lucas hakushtuka,alikuwa mbali sana katika ulimwengu ambao wengi wanaamini haukuwahi kutokea. Alishtuka baada kupigwa nakitu usoni, "we muda wote huo mie nakuita unajifanya hunisikii" madam Ester aliongea kwa hasira. "Samahani mwalimu, kwa kweli leo sijiskii vizuri" Lucas alijitetea, "sasa kama unaumwa kwanini umekuja shule" madam aihoji tena. "ah si unajua mama tena kalazimisha" Lucas alijibu huku akitabasamu.
Lucas ni mtot pekee wa familia ya kitajiri sana ndani ya mji wa Free state, anaishi na mama yake tu. Ni kijana mwenye roho ya upendo na mwenye heshima sana, yuko tofauti sana vijana wengine wanaotokea katika familia za kiyajiri ndani ya mji huo. Kwa umri ana miaka kumi na sita lakini kwa jinsi mwiliwake ulivyojengeka kimazoezi anaoanekana kama mtu mwenye miaka ishirini na kuendelea. "kama vipi we nenda zako nyumabni ukapumzike" madam Ester alimruhusu Lucas aende zake nyumbani, bila kuchelewa Lucas aliinuka na kuchukua begi lake na kuondoka.
Bado njia nzima alikuwa amepotea katika mawazo, "jamani msinipige sina nia ya kumdhuru mtu" Lucas aliisikia sauti hiyo kwa mbali sana lakini akaipotezea. "sasa mimi nimefanya nini mpaka mnataka kunipiga au kutemebea njiani ndio kosa langu, kwani mi sina haki ya kutembea kama nyinyi" bado sauti hiyo aliiskia lakini wakat huu aliiskia kwa nguvu zaidi na iliojaa hasira. Aligeuka na kuanza kumtafuta anaeongea maeno hayo lakini hakyfanikiwa kumuona bali aliona kikundi kidogo cha watoto wakiwa wamezunguka kitu. Alipojaribu kusogea aligundua kuwa sauti inatokea pale, bila kuchelewa alitembea kwa haraka kwenda kujaribu kumuombea wasimpige.
Alipigwa na butwaa baada kugundua kuwa anaetaka kupigwa alikuwa ni mbwa, alijaribu kutafuta mtu mwengine ambae alikuwa akiomba mssada lakini bado sauti ilitokea pale. "hebu muachieni huyo mnyama" aliongea kuwaambia wale vijana, "hatuwezi kumuacha huyu, amemuua sungura wangu" kijana mmoja aliongea kwa hasira huku akijaribu kumpiga fimbo yule mbwa. "sasa hata ukimuua huyo sungura wako atafufuka hebu kuwa na akili wewe" Lucas alijibu kwa hasira mpak wale vijana wakaogopa. wakati wote huo yule mbwa alikuwa katulia tuli, "sasa ole wake mtu yoyote amguse huyo mbwa" aliongea kwa hasira aliowafanya wale vijana waondoke shingo upande. alipohakikisha wameshapotea katika upeo wake wa macho nae alianza safari ya kuelekea kwao.
Lakini alipoangalia nyuma yule mbwa alikuwa akimfata na alipojaribu kumfukuza hakukubali. Alijaribu sana lakini mbwa aligoma kabisa kuondoka hivo hakuwa na jinsi zaidi kumuacha tu. Dikika kumi baadae Lucas alifika kwao na kuingia ndani lakini yule mbwa alibakia nje. "hee mboona umerudi mapema leo " mama yake aliuliza baada ya kumuona, "nilikuwa sijisikii vizuri ndio maana nimerudi" Lucas alijibu na kuelekea chumabni kwake. Dakika tano baadae alimsikia mama yake akimuita, aliitika mara moja na kushuka chini, "wewe mbona huruma hivo" mama yake aliongea, "kwanini". "yaani umekuja na uyo mnyama halafu umemuacha nje, huoni kama ananjaa na amekufata akitegemea utamapa chakula japo kidogo" mama yake aliongea kwa hasira. Lucas wala hakushangaa kwa sababu alikuwa anajua ni kwa jinsi gani mama yake alivyokuwa akiwapenda wanyama.
Baada ya maongezi machache na mama yake aliekea nje na kumfungulia geti yule mbwa kisha akaondoka. lakini alipogeuka nyuma alimuona akiwa kasimama kulekule nje, "Oya kama vipi ingia ndani basi" Lucas aliongea kama utani. Yule mbwa aliinamisha kichwa chini kama ishara ya kishukuru na kuingia. Lucas alielekea jikonkoni na kchukua sahani kubwa, alielekea kwenye hotpot na kutia chakula kingi kisha akampelekea yule mbwa kisha yeye akarudi zake ndani. Aliingia chumbani kwake na kijilaza kitandani na haukupita muda usingizi ukamchukua.
"wuuuuuuuu...ghrrrrr" milio hiyo ya mbwa iliendelea kusikika na kumzidisha wasiwasi Lucas. Lkaini kutokana na wepesi wa miguu yake kwenye kukimbia Lucas alifanikiwa kumkimbia kiumbe huyo anaeliya kama mbwa lakini anatembea kama binadamu. Mwili wake mweusi ulimfanya iwe ni vigumu kuonekana katika kiza, meno yake marefu na yaliochongeka ilitosha kuamini kuwa kiumbe huyo ni hatari sana huku akipambwa na mikono mirefu sambamba na kucha ndefu. Lucas alijuwa huo ndio mwisho wa maisha yake,wakati anakimbia alijikwaa na kuanguka chini na aliposimama alijikuta akiwa uso uso kwa na kiumbe huyo na sasa alifanikiwa kumuona vizuri kwa msaada wa mbala mwezi. Alitamani ardhi ipasuke ili aingie, mara yule kiumbe aliinua mkono wake kulia na kuushusha kwa nguvu. "mamaaaaaa" Lucas alizinduka kutoka usingizini huku kijasho kikimtoka na mapigo ya moyo yalikuwa yakienda kasi sana. "Lucas una nini mwanangu" mama yake aliingia na kukumbatia huku akimuuliza swali hilo.
Baada kuhakikisha Lucas ameshatulia, mama yake alimwambia akae chini amwambie ameota kitu gani. "unajua mama hii ndoto naiota kwa muda sasa lakini mara zote huwa naskia sauti ya mbwa mwitu na minguromo lakini simuoni ila leo ndio nimemuona kwa kweli sijawahi kuona kiumbe kinachitisha kama kile" Lucas alimweleza mama yake kila kitu alichokiona katika ndoto yake. "sasa nahisi muda umefika" aliongea mama yake na kuinuka baada kuisikia ndoto ya Lucas, "muda umefika kivipi" Lucas aliuliza kisha akaendelea "mbona sikuelewi mama". "We utaelewa tu"alijibu kisha akaendelea "panga nguo zako". "Tunaenda wapi" Lucas alihoji, "nimemekwambia panga nguo zako,tunapokwenda utapajua tukishafika" mama yake alijibu kwa hasira.
Lucas aliona hakuna haja ya kuendelea kulumbana na mama yake, alitoa begi lake ndogo na kupanga nguo kadhaa. Usiku ulipowadia walitoka, "mchukue na yule mbwa" mama yake aliongea. Lucas bila kuuliza alizunguka nyuma ya nyumba na kumkuta yule mbwa kama aliyekuwa akimsubiri. Alimbeba na kurudi nae kwenye gari na safari ikaanza. Mama yake alikanyaga nafuta kisawasawa na kumuwacha Lucas mdomo wazi kwasababu siku zote alijua mama yake hapendi gari iendeshwe mwendo kasi. Wakati safari ikiendelea Lucas alipitiwa na usingizi mzito na kutokomea katika ulimwengu wa ndoto.
Alikuja kushtuka baada kutingishwa na mama yake, "tumeshafika", Lucas alijifikicha macho lakini alipoangalia vizuri moyo ulianza kumenda mbio huku kijasho chembamba kikaanza kumtoka. "mama hii sehemu ndio ile nnayoiona kwenye ndoto", mama yake hakumjibi kitu bali alitoa mabegi na kumwambia amfuate. Lucas alishangazwa na mabadiliko ya ghafla kwa mamaake, lakini alipotezea na kumfata. Walifika mbele ya mlango mkubwa na hapo mamaake akasema maneno kwa lugha asioifahamu Lucas, mara mlango ukafunguka wenyewe. Lucas alibaki ameshangaa tu huku akimfata mamaake kwa nyuma. wakiongozwa na mwanga hafifu, walitembea kwa muda wa dakika tano mpaka walipofika kwenye mlango mwengine. Hapo tena mamaake aliongea maneno ya ajabu na mlango ukafunguka, kasoro macho yadondoke Lucas baada kwa jinsi nyumba walioingia ilivyokuwa nzuri huku ikinakshiwa na sakafu iliopambwa na marumaru za almasi na kuta zilizopambwa kwa madini tofauti tofauti.

EPISODE 2

Alikuja kushtuka baada kutingishwa na mama yake, "tumeshafika", Lucas alijifikicha macho lakini alipoangalia vizuri moyo ulianza kumenda mbio huku kijasho chembamba kikaanza kumtoka. "mama hii sehemu ndio ile nnayoiona kwenye ndoto", mama yake hakumjibi kitu bali alitoa mabegi na kumwambia amfuate. Lucas alishangazwa na mabadiliko ya ghafla kwa mamaake, lakini alipotezea na kumfata. Walifika mbele ya mlango mkubwa na hapo mamaake akasema maneno kwa lugha asioifahamu Lucas, mara mlango ukafunguka wenyewe. Lucas alibaki ameshangaa tu huku akimfata mamaake kwa nyuma. wakiongozwa na mwanga hafifu, walitembea kwa muda wa dakika tano mpaka walipofika kwenye mlango mwengine. Hapo tena mamaake aliongea maneno ya ajabu na mlango ukafunguka, kasoro macho yadondoke Lucas baada kwa jinsi nyumba walioingia ilivyokuwa nzuri huku ikinakshiwa na sakafu iliopambwa na marumaru za almasi na kuta zilizopambwa kwa madini tofauti tofauti.
wakati akiendelea kushangaa mamaake alimshika mkono na kumvuta kupandisha nae ngazi "hichi ndio kitakachokuwa chumba chako kuanzia leo" mamaake aliongea baada kufika katika chumba kimoja kikubwa sana mithili ya vile vyumba vya wafalame wa zamani sana. "una maana gani kusema hivyo" Lucas aliuliza, "namaanisha kuwa kuanzia leo tutakuwa tunaishi huku" alijibiwa kwa ufupi sana. "Lakini mama marafaiki zangu wote wapo mjini" alilalamika Lucas baada kuambiwa hivyo na mama yako. "wale wote uliokuwa nao mjini nataka uwasahau, kuanzia leo rafiki yako atakuwa yule ambae atakukubali kwa jinsi ulivyo" mama huyo aliongea tena na kumaliza mjadala huo kwa kuondoka.
Lucas hakuelewa kilichokuwa kinaendelea, lakini kilichomshangazani kwa jinsi mamaake alivyobadilika. Alikuwa tafuati na yule aliemzoea, baada mamaake kuondoka Lucas alielekea chumbani kwake nakujilaza kitandani akitafakari mambo yote yaliotokea. Akiwa dibwi zito la mawazo usngizi ulimchukua, alikuja kushtuka baada malngo wake kugongwa. Aliinuka kivivu kwenda kuufungua na kukuta aliekuwa nagonga ni mama yake. "nifwate" kisha mamaake akaondoka, Lucas bila hiyana alimfata mama yake taratibu huku bado akiwa haelewi jinsi mambo yananvyotokea. Walifika mbele ya mlango mkubwa na mamaake aliongea maneno ya ajabu na mlango ukafunguka. Lilikuwa ni holi kubwa lililojaa picha za watu wa kale na vitu vingi sana ambavyo Lucas alikuwa kaiviona kwenye TV tena katika zile filamu za kutisha kama dracula na van helsin.
"unamjua ni nani huyo kwnye hio picha kubwa ni nani?" aliuliza mamaake, Lucas aliiangalia ile pica kwa umakini kisha akajaribu kuvuta kumbumbu alimuona mtu yule kwenye picha ghafla alishutuka baada kupata jibu kichwani mwake lakini alionekana kutokubaliana na jibu hilo kwa sababu tarehe iliyondikwa kwenye picha ile ni 01/01/1190. Alianza kugeuka taratibu na kumuangalia mamaake kisha akasema "mbona kama kafanana na wewe huyu", "Huyo hajafanana na mimi bali huyo ni mimi mwenyewe" alijibu mamaake huku akitabasamu jambo ambalo lilimanya Lucas atoe macho utadhani mjusi aliebanwa na mlango. "mama acha kunitania" aliongea kiutani Lucas, "khah! sasa nikutanie kwa nini" mamaake alimjibu huku akitendelea kutabasamu.
"unajua mwanangu kuna mambo mengi unatakiwa kuyajua kuhusiana na familia yako" aliongea mamaake huku akimshika mkono Lucas na kuelekea nae mezani. "sasa leo wacha nikueleze kingaubaga kila kitu unachotakiwa kujua" aliendelea. Baada ya kukaa kwenye meza, "sasa kama wewe ni yule msichana kwenye picha, umewezaje kuishi mpaka leo" Lucas aliuliza kwa mshangao. "na ndio kitu nnachitaka kukueleza" alijibu kisha akendelea "natumai umesoma soma vitabu vingi pamoja na kuangalia filamu nyingi zinazoelezea uwepo wa viumbe vya ajabu ambavo mara nyingi vinachukua maumbile ya binaadamu", "ndio si kama dracula, underworld na abraham lincoline" . "haswaa ni kama hizo, miaka mingi sana iliopita kweli vimbe hao walikuwepo na mpaka sasa wapo na wananishi miongoni mwetu bila sisi kuwatambua" aliongea mamaake na kisha akamuangalia Lucas machoni.
"miaka takriban elfu moja na kidogo iliyopita" alianza kusimulia mama Lucas kisha akaendelea " kpindi ambacho hakukuwa na gari ,ndege,treni wala meli za vyuma kama siku hizi. Kipindi amabcho dunia ilkuwa ikitawalia na falme tofauti tofauti. Katika ufalme mmoja uliojulikana kama ufalme wa blackford (kingdom of blackford) amabao uliongozwa na mfalme Morris wa pili. Mfalme aliesifika kwa ukarimu wake na kupendwa sana na watu wake, alikuwa na mke mzuri lakini alibahatika kupata watoto wawili. Wa kike amabe aliitwa Princess Tiflla na wa mwisho wa kiume alieitwa Prince Falcone, Princess Tiflla alizaliwa mwaka 1150 na Prince Falcone alizaliwa mwaka 1155. Ndugu hawa wawili walipendana sana na kila mtu aliwapenda sana. Sasa princess Tiflla ndio mimi na ndio kwenye ile picha na prince Falcone ni mjomba wako", Lucas alitamani kucheka lakini alivumilia, aliona kamam mama yake anamtania. Lakini alijua kufanya hivyo kungemchafua mama yake ambae alionekana kuwa makini na jambo alilokuwa analisema.
"siku moja nilikuwa nikitembea tembea katika msitu uliokaribu sana na ngome ya babaangu, mara ghafla akatokea mbwa mwitu. alikuwa akija upande kwa kasi ya hali ya juu sana huku ute ukimtoka, ukweli nilikuwa sijui nifanye nini na aliponikaribia tu aliruka. Nilifunga macho lakini nilishangaa kuona hakunifikia, nlipofungua macho nilimkuta kijana mmoja mchafu sana akiwa mbele yangu na yule mbwa akiwa pembeni akijikusnya baada kupewa kikumbo kizito na kijana huyo. Aliniambia nisijali kwani yeye angenilinda kutoka kwa mbwa huyo alionekana kuwa na hasira sana. Kisha akatoa kisu chake kidogo na kujiweka vizuri kwaajili ya kupambana na mnyama huyo, ghafla mbwa yule alichomoka kama mshale kwenye upinde na kumva kijana yule, walibiringitishana mara kadhaa na baada ya mpambano wa dakika kama tano hivi wote wawili walitulia. Nilidhani wote wawili wamekufa lakini niliondoa mwazo hayo baada kumuona yule kijana akiinuka japo kwa tabu sana na alikuawa na alama za meno shingoni pamoja makucha katika baadhi sehemu nyingine za mwili.
Kisha alisogea mpaka niliposimama na kuniuliza "vipi princess uko salama, hajkuumiza pahali yule mbwa" lakini kabla sijamjibu walinzi walifika haraka na kuanza kumpiga kila nlipojitahidi kuwaambia wamuache hawakusikia, waliendelea kumpiga mpaka akapoteza fahamu na kisha wakamkokota na kumtia gerezani. Mfalme ambae ni baba yangu aliporudi kutoka katika safri zake za kukagua mipaka, mlinzi mkuu alimpa taarifa kwamba walimkuta kijana akitaka kundhuru, kwa hasira baba aliamrisha yule kijana aletwe mbele yake ajibu mashtaka na kama angekutwa na hatia basi angehukumiwa kifo. Watu wengi walikusanyika kushuhudia jambi hil, yule kijana aliletwa mbele ya mfalme na mimi nikiwepo hapo. "kijana unatuhumiwa kwa kosa la kutaka kumdhuru princess, je ni kweli?" aliuliza mfalme, "mtukufu mfalme ubarikiwe na miungu yote na wakupe maisha marefu, mimi sikuwa na nia ya kumdhuru princess bali ni kumsaidia tu kama fadhila zangu kwako kwa jinsi unavyotujali wananchi wako" aliongea kijana yule kwa kujiamini sana. "kijana hebu nieleze ulitaka kumsaidiaje na wakati alieleta habari anasema ulikuwa na nia ya kumdhuru". "hapana mtukufu mfalme, mimi nilikuwa katuka mawindo nilipomuona princess akitembea karibu na pori lakini kwa mbali niliweza kumuona mbwa mwitu akiwa anamnyatia, baada kuona hivo nilijaribu kumshtua lakini hakunisikia hivo nikaamua kumuwahi yule mbwa kabla hajamdhuru princess, nilifanikiwa kumuua na nlipokuwa nahakikisha kama princess hajapata jeraha lolote kutoka kwa mbwa ndipo walinzi wako walifika na kunikamata kwa madai eti nilikuwa nataka kumdhuru princess" alijitetea kijana huyo. "una ushahidi wowote" aliuliza Syrus ambae alikuwa ni mshauri wa mkono wa kulia wa mfalme "ndio, nimepata majeraha kadhaa kutoka kwa mnyama yule" alijibu yule kijana na kuinua shingo yake ilionekana kuwa na vitobo vinne vya meno, pia aliinua fulana yake na kuonyesha kidonda kilicotokana na kucha za mbwa huyo.

FULL 1500
0699286085.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BLOOD MOON EPISODE 1  >>> https://gonga94.com/semajambo/blood-moon-episode-1
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest