"kijana hebu nieleze ulitaka kumsaidiaje na wakati alieleta habari anasema ulikuwa na nia ya kumdhuru". "hapana mtukufu mfalme, mimi nilikuwa katuka mawindo nilipomuona princess akitembea karibu na pori lakini kwa mbali niliweza kumuona mbwa mwitu akiwa anamnyatia, baada kuona hivo nilijaribu kumshtua lakini hakunisikia hivo nikaamua kumuwahi yule mbwa kabla hajamdhuru princess, nilifanikiwa kumuua na nlipokuwa nahakikisha kama princess hajapata jeraha lolote kutoka kwa mbwa ndipo walinzi wako walifika na kunikamata kwa madai eti nilikuwa nataka kumdhuru princess" alijitetea kijana huyo. "una ushahidi wowote" aliuliza Syrus ambae alikuwa ni mshauri wa mkono wa kulia wa mfalme "ndio, nimepata majeraha kadhaa kutoka kwa mnyama yule" alijibu yule kijana na kuinua shingo yake ilionekana kuwa na vitobo vinne vya meno, pia aliinua fulana yake na kuonyesha kidonda kilicotokana na kucha za mbwa huyo.
"Martias chukua askari wanne, nendeni mkaulete mwili wa mbwa alietaka kumdhuru mwanangu" Mfalme alitoa amri na bila kuchelewa askari alirpewa agizo hilo alichukua vijana kadhaa na kuelekea nao msituni. Haukupita muda mrefu walirudi wakiwa na mzoga wa mbwa "kijana mbwa mwenyewe ndie huyo" aliuliza Mfalme, "ndio mtukufu mfalme" alijibu yule kijana. Baba alinigeukia na kuniuliza kama maneno na ushahidi ulioletwa ni kweli, nilimjibu ndio. "Kutokana na ushahidi, nasema huyu kijana hana kosa lolote" mfalme aliimaliza kesi hiyo na kuwaamuru watu kutawanyika lakini akamwambia yule kijana abakie.
"kijana asante kwa msaada wako" baba aliongea,"huna haja ya kunishukuru mtukufu mfalme, nimefanya wajibu wangu tu" alijibu yule kijana. "una maanisha nini kusema hivyo" Mfalme alihoji tena kisha akauliza "kwani we jina lako ni nani?". "mi naitwa Gordon James mtukufu mfalme" alijibu yule kijana, mfalme kuskia alishtuka kidogo. "unamaanisha wewe ni mtoto wa James Hunter" "ndio, mtukufu mfalme", "kijana baba yako alikuwa mtu wangu wa karibu sana, niliishi nae kama kaka yangu lakini maadui zetu wamemtanguliza kwa mungu, nina uhakika saa hiv atakua anakunywa mvinyo na miungu huko alipo". "hapana mtukufu mfalme, aliekufa vitani kwa ajili ya nchi yake ndie anaekunywa mvinyo na miungu". "we funga mdomo nilimshuhudia kwa macho yangu mawili akifa vitani" mfalme alibadilika ghafla na kuwa mkali. "nisamehe mtukufu mfalme, lakini babaangu alirudi nyumbani akiwa anataoka damu nyingi sana na alikuwa akijilaumu kwa nini aliruhusu mshale uuguse mwili wako jambo ambalo lilimuumiza sana na kunambia iwe siri kati yetu. Kabla hajaaga dunia ndio akanambia "mwanangu hakuna kitu chenye thamani kama kumtumikia mfalme na damu yake, ikitokea siku ukahitajika msaada wako kwa mfalme ama kwa nchi yetu basi fanya kitu hicho kama wajibu na usitake malipo ya aina yoyte ile, kwani malipo yake yapo kwa miungu tu. Hakuna anaeweza kukulipa hapa duniani" hayo ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho kabla kufumba macho na kwa sababu aliniambia akifanisimlete kwako bali nimzike kawaida tu na mimi kuunza ahadi nikafanya hivyo".
"baba yako alikuwa shujaa na sio kama anavyosema,mshale wala haukunigusa" aliongea mfalme "sasa nakupa amri nenda ukaufukue mwili wa baba yako na uulete tuufanyie maziko sahihi". Baada amri hiyo hakutakiwa kusema chochote zaidi ya kuinuka na kuelekea nyumbani kwao kwa kazi ya kuufukua mwili wa baba yake. Kwa mwendo wa haraka alitembea mpaka kwao na kuanza kufuku kufukkua mwili wa baba yake. Aliifanya kazi hiyo kwa muda wa nusu saa. wakati mfalme akiendelea kutafakari ushujaa generali ghafla mlamgo ukafunguliwa na kijana Gordon akaingia na jeneza kubwa, watu wote ndani ya ngome hiyo walishangaa baada kumuona kijana mdogo kama huyo akiwa amebeba jeneza kubwa kama lile. Gordona alilitua geneza lile mbele ya mfalme na kisha akasema "mtukufu mfalme nimeileta maiti ya marehemu baba yangu kama ulivyoniamrisha japo kuw ntakuwa nimevunja ahadi niliyo muahidi baba yangu" huka machozi yakimtoka.
Mfalme alilisogelea jeneza lile na kulifungua lakini alishangaa baada ya kuona bado damu mbichi ikitoka kwenye mwili wa James Hunter. "kweli huyu mtu alikuwa ni chaguo la miungu maana mpaka sasa bado mwili wake unatoka damu kama mtu aliyekufa muda mfupi tu uliopita." mfalme aliongea huku akiangalia juu. Bila kuchelewa alitoa amri kuni zikusanywe haraka sana na maandalizi ya mazishi rasmi yakaanza. Kila kitu kilikamilika na mwili ukawekwa juu ya kuni na panga lake kubwa likawekwa mikononi mwake likifuatiwa na ngao nzito ya chuma. "mtukufu mfalme baba yangu alisema nibebe panga pamoja na ngao yake katika kuimarisha amani ya nchi yetu" aliongea Gordon huku akitokwa na machozi, "kijana shujaa yoyote huzikwa na panga pamoja na ngao yake na kama kweli alitaka urithi kazi yake basi tunaamini vitu hivyo havitaungua kabisa" alijibu mfalme na kisha akatoa amri moto uwashwe, "mtukufu mfalme naomba niuwashe mimi" Gordon aliomba na kukubaliwa. Alibeba mti wenye moto juu na kwenda kuwasha, baada kuwaka moto huo mkali kila mtu alirudi nyuma lakini Gordon alisimama palepalr hatua kama tatu kutoka kwenye moto huo.
Moto uliendelea kuwaka kwa ukali zaidi ghafla Gordon alianza kutembea kuelekea ndani kabisa ya moto huo. Baadhi ya askari walitaka kwenda kumzuia lakini mfalme aliwapa ishara wamuache mwisho kabisa alitokomea ndani ya moto huo mkali. Watu wote walijua tayari ameshaungua lakini mimi nilianza kuona kivuli kwa mbali kikija kutoka kwenye moto huo. Na hapo hapo Gordon alitoka kwenye moto huo akiwa mtupu nguo zake zote zikiwa zimeungua, mkono wa kulia alikuwa na panga na mkono mkono wa kushoto alikuwa ngao ya baba yake. Watu wote walishanga kumuona hajaungua hata kidogo.
Mfalme aliamuru askari mmoja akamfunike na shuka na baada ya maziko kuisha alimwita tena ka ajili ya kumuhoji. "umewezaje kuingia kwenye moto bila kuungua" aliuliza mfalme, "mtukufu mfalme wakati nikiwa pembeni ya ule moto niliskia mtu akiinta mwanzo nilisita lakini nikamsikia akinambia nipite kwani ule moto hautaniunguza, ukweli nilijkuta tu nikianza kutembea na baada kufika sehemu alipo baba niliwakuta viumbe wengine wa ajabu wakiwa wamemzunguka baba. Niliogopa lakini mmoja alieonekana kuwa kiongozi akanambia nisiogope, kwani wao ni wema tu. Alijitambulisha kwa jina Altera akasema yeye ni mfalme wa miungu tunayoabudu na alikuja pale kutimiza ahadi yake ya mwisho kunilabidhi upanga halisi wa baba yangu pamoja na ngao yake. Baada kunipa vitu hivyo akanambia nitoke kwenye moto na niwaeleze watu kuwa Generali James Hunter ameungana na wengine katika kumbi kubwa na kunywa mvinyo na miungu" alimaliza kuogea na kumfanya mfalme na kila aliekuwa pale ashangae.
"nikuulize swali kijana" aliuliza mfalme, "kwako nikuuliza tu huna haja ya kuniomaba" alijbu kinyenyekevu kabisa. "hivi baba yako alikuwa anafanya kazi gani akiwa nyumabani", "kwa kweli muda mwingi baba alikwenda milimani kusali na hiyo ndio kazi kubwa aliokuwa akiifanya pamoja na kutoa sadaka kwa miungu kila wiki, alichinja mnyama mmoja. Na ndivyo alivyokuwa akinihusia kila siku kuwa hata kama nitakuwa na nguvu na ushujaa kuliko yoyote basi nisisache kuwashukuru miungu na kuwapa sadaka" alimaliza Gordon kuongea na kmuangalia mfalme. Baada ya kuskia hayo mfalme alisimama na kuongea "kuanzia leo kijana Gordon atakuwa mlinzi wa princess Tiffla" kisha akafunga kikao bila kuruhusu mwaswali ya aina yoyote.
Wengi walishangaa na kujiuliza ni kwanini amempa mtoto mdogo kama Gordon jukumu kubwa kama lile lakini kwa sababu ilikuwa ni amri ya mfalme kila mtu aliikunali. Maisha mapya kwa Gordon yakaanza, akiwa kama mlinzi wangu. Siku zilipita, miezi ikakata na miaka ikasogea bila upata tatizo lolote katika ufalme wetu. Siku moja baba alipokea ujumbe kutoka falme jirani uliomtaka atoe wanajeshi elfu moja ili waende wakasaidie, aliwaita mawaziri wake na kulijadili swala hilo lakini mwisho kabisa walikubaliana kuwa wasipeleke hata mtu mmoja. Barua iliandikwa na kutmwa katika falme ile na haukupita muda walijibu kwa kurejesha kichwa cha mjumbe aliepeleka barua ile. Na hapo baba akajua wazi kuwa ametangaza vita ambayo itaondoa amani kabisa falme yetu. na kweli baada ya mwaka mmoja tulivamiwa na watu wengi walipoteza maisha.
Hapo tena ikawahakuna budi kuandaa jeshi na kuelekea vitani kwa ajili ya kupigania falme yetu lakini hali ilikuwa mbaya sana kutokana na kuwa maadui zetu walikuwa wengi sana. Vita yakwanza tulipoteza wanajeshi wengi na hilo lilikuwa pigo kubwa sana kwa baba, aliumia sana na hasa ukizingatia kadri siku zilivyokwenda ndio watu wengi walipoteza maisha. Hata Gordon aliumia sana kwa sababu nara zote aliachwa ili anilinde mimi lakini siku moja alinijia huku akitoka machozi na kuniomba nimruhusu akaungane na mfalme katika uwanja vita na aliniahidi kuwa ataniletea kichwa kichwa mfalme wa upinzani kama zawadi ya kumpa ruhusa. Wakati huo alikuwa na miaka kumi na nane lakini alionekanakana kama mtu mwenye miaka thalathini.
EPISODE 4
Hapo tena ikawahakuna budi kuandaa jeshi na kuelekea vitani kwa ajili ya kupigania falme yetu lakini hali ilikuwa mbaya sana kutokana na kuwa maadui zetu walikuwa wengi sana. Vita yakwanza tulipoteza wanajeshi wengi na hilo lilikuwa pigo kubwa sana kwa baba, aliumia sana na hasa ukizingatia kadri siku zilivyokwenda ndio watu wengi walipoteza maisha. Hata Gordon aliumia sana kwa sababu nara zote aliachwa ili anilinde mimi lakini siku moja alinijia huku akitoka machozi na kuniomba nimruhusu akaungane na mfalme katika uwanja vita na aliniahidi kuwa ataniletea kichwa kichwa mfalme wa upinzani kama zawadi ya kumpa ruhusa. Wakati huo alikuwa na miaka kumi na nane lakini alionekanakana kama mtu mwenye miaka thalathini.
Nilimruhusu na mara moja aliondoka na kuelekea uwanja wa vita, mfalme alishangaa alipomuona na kumuuliza kupitia ruhusa ya nani amekwenda huko. alimueleza kila kitu ikwemo na ahadi aliyotoa, baba akamuuliza na kama angeshindwa je, akajibu akatwe mikono yote miwili na miguu yote. Baba kusikiaa hivo alitabasamu na kumruhusu aungane na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea vitani. Hadi muda huwa vita ilikuwa ishachukua mwaka mmoja. Siku ya pili mapema waliekea uwanjani lakini wanajeshi wengi walikuwa washakata tamaa. Amri ilitolewa na vita ilianza, vita hiyo ilirindima kwa muda huku tukuzidi kupoteza wanajeshi wengi na ilibidi mwisho turudi nyuma tujipange upya. Na hapo ndio Gordon aliomba ruhusa ya kuongea "mnajua kwanini tunapigwa, ni kwasababu katika akili zetu tumeshakubali kupigwa na hivyo tunapoteza muelekeo. Nadhani mnajua kuwa wakifanikiwa kuchukua ufalme wetu, watawabaka mama zetu, dada zetu, wake zetu na kutufanya watumwa wao, ivi kwanini hamuna shukurani kwa mfalme wetu, mafalme ambae anatuona wote tupo sawa tu. Japo kwa mara moja tumuonyeshe kuwa kufa kwa ajili ni kitu kidogo sana kulingana na upendo wake aliouonyesha kwetu. Nani uko tayari kuungana na mimi kuelekea uwanjani na hii ndio itakuwa vita yetu ya mwisho bora tufe wote lakini hatitarudi nyuma mpaka kieleweke" alimaliza kuongea, wote walikuwa wakimshangaa.
Aliinuka na kubeba upanga wake na kuelekea alipo mfalme na kusema "mtukufu mfalme hivi sasa natoa mguu wangu katika kambi hii naelekea uwanjani na nakuahidi sitarudi nyuma hadi nikipate kichwa cha huyo mpuuzi naomba unibariki" mfalme alitoa panga lake na kumuekea begani kisha akasema "nenda kwa amani mwanangu na usirudi mpaka utakapo kipata kichwa chake". Gordon aliinuka na kuondoka, alipofika katika uwanja wa vita alipiga magoti na kuangalia juu kisha akasema "ewe mfalme wa miungu ninaomba unipe nguvu na uwe nami katika vita yote hii" alimaliza na kuinuka na kuanza kutembea taratibu. Mmoja kati ya wanajeshi wa maadui alimfata lakini alijikuta akiishia chini na kupoteza maisha, walipoona hivyo walianza kumiminika na vita ilianza tena upya. Akiwa peke yake bila msaada wowote ule, alipigana vita hiyo na kufanikiwa kukisambaratisha kikosi cha kwanza cha maadui zetu.
Baada ya kushuhudia maajabu hayo wanajeshi wetu waliingiwa na moyo wa ujasiri na kuungana nae katika mshikemshike huo. Hadi kiza kinaingia walifanikiwa kuwapunguza wanzajeshi wengi na kuwafanya maadui zetu warudi nyuma. Wote walirudi kambini isipokuwa Gordon peke yake,wengi walidhani kashakufa hivyo walielekea uwanjani kuitafuta maiti yake bila mafanikio. Siku ya pili asubuhi wakiwa wamepumzika waliskia farasi akija upande wao na alipokaribia waligundua kuwa alikuwa ni Gordon. Walimpokea kwa shangwe na moja kwa moja alielekea kwa mfalme. "nimerudi ewe mtukufu mfalme" aliongea huku akimkabidhi mfalme box dogo la mbao, alipolifungua alikuta kichwa cha mpinzani wake. Kwa furaha mfalme aliinuka na kutangaza ushidi, walijiandaa na kuelekea katika uwanja wa vita huku akiwa na kile kichwa mkononi, maadui baada kuona vile walishusha silaha chini na kupiga magoti kwa kumpa heshima mfalme wao mpya.
Vita iliisha na watu wote walirudi nyumbani na kama alivyoahidi Gordon alinikabidhi kicwa cha mfalme wa upinzani. Mfalme aliitisha tafrija kubwa ya kuwapongeza wote waliopigan avita ile ngumu na kuwalaki wale wanafamilia waliopoteza ndugu zao katika vita ile. Wakati watu wakiendelea kusheherekea, ghafla mfalme alianguka na kuanza kutoka damu mdomoni. Amri ilitoka na mfalme akabebwa na kupelekwa chumbani kwake namadaktari esliitwa kwa ajili kumchunguza amepatwa nini. Baada muda walitoka wale madaaktari kutuambia kuwa mfalme amechomwa mwiba wenye sumu kali sana na hivyo sumu hiyo ilishasambaa mwili mzima kilichobaki ni kusubiri muda ufike akaungane na miungu yetu. Nililia sana huku nikijiuliza kwanini mambo hayo yalikuwa yanatokea kwetu tu, Gordon alinifariji na kunambia hata kama atakufa lakini daima milele atakuwa anatuangalia akiwa na miungu yetu. Tuliingia chumbani na kumkuta akiwa amelala, tukaona bora tutoke tumuache lakini kabla hatujafanya hivo tulimsikia akituita.
Tulisogea mpaka kitandani na kukaa pembeni yake, "Gordon" aliita mfalme kisha akaendelea "nikifa mwanangu Tiffla ndie atakaeshika utawala, lakini hawezi kuuobgoza ufalme huu peke yake atahitaji mtu wa kumsaidia hasa katika nyakati ngumu" aliposema hivyo mimi nilielewa amemaanisha nini. HApo akatoa agizo waitwe wazee wa dini nalo likatekelezwa haraka sana. Dakika chache baadae walifka. "wazee wangu mimi muda wangu wa kuishi umekwisha lakini kabla sijaondoka katika ulimwengu huu nataka nivunje mila na desturi za tawala hii" aliongea hivyo na kuwashangaza wazee waliokuepo pale. "kupitia Jina la Mungu Alteria,mfalme wa miungu yote ninamkabidhi princess Tiffla kwa generali Gordon awe malkia wake na mfalme wa utawala huu" baada kumaliza kuongea hayo alitoa karatasi ndogo iliandikwa na kusaini.
KItendo cha kumaliza kusaini tu, kalamu ilianguka kumaanisha kuwa tayari alishaaga dunia. Kwa mara ya kwanza niliona michirizi ya machozi katika mashavu ya Gordon kisha akasema "kupitia utukufu wako nakuahidi kuwa nitahakikisha nalinda amani ya taifa hili mpaka mwisho wa uhai wangu na kama kufa basi nitakufa nalo" alijikata kidole na kumchora baba kwa damu katika paji la uso kumaanisha ahadi hiyo itavunjika kwa kufa tu. Taarifa za kifo cha mfalme zilisambaa kila kona ya utawala wetu, na watu wengi walihuzunishwa na kifo hicho. Taratibu za mazishi zilianza na kila mtu katika utawala wetu alihudhuria mazishi yake. tulimaliza kila kitu maandalizi ya kuapishwa mtawala mpya yakaanza.
Siku ya kuapishwa ilifika huku mdogo wangu Falcone akiwa na matumaini kuwa yeye ndie atakaekuwa mtawala atakaefuata. Watu wote walikuwepo katika ukumbi mkubwa ndani ya ufalme wetu. Muda wa kutangazwa ulifika, wazee wa dini walifika kwasababu wao ndio wanaofanya kazi hiyo. Mzee mmoja alisimama mbele ya umati mzima na kusema "kupitia utukufu wa mfalme alietutoka muda mfupi tu uliopita na kwa kauli yake ya mwisho, kwa niaba ya wazee wa dini ninamtangaza princess Tiffla kuwa malkia wa taifa hili" kabla hajaendelea mdogo wangu aliingilia kati "lakini mimi ni mtoto wa kiume ndio natakiwa kuriti kiti cha ufalme". "Huna haja ya kuongea kwani kauli ya mwisho ya mfalme ni kuwa amekikabidhi kiti chake cha utawala kwa Generali Gordon awe mfalme wa tawala hii na mume wa dadaako". Watu wite walishangaa kusikia hivyo, Gordon aliitwa akavishwa taji la ufalme na hapo amri ya kumsalimu mfalme mpya ikatoka. Watu waote kwa pamoja waliinama na kusema "utukuzwe ewe mfalme wetu", baada ya kumaliza kutoa heshima yao Mfalme Gordon alisimama na kuongea "amani na upendo ni ngao ya utawala huu na ninawaahidi nitailinda mpaka mwisho wa maisha yangu".
Misha yaliendelea vizuri kama kawiada, ikiwa ni miaka mitano tokea Gordon apewe ufalme. Mdogo wangu Falcone alianza kupanga mbinu za kutondoa madarakani. Mara kadhaa alijaribu kutuma wauwaji wamuue Gordon lakini haikuwezakana kabisa. Baada kuona mbinu zote zimefeli akaamua kutafuta msaada kupitia nguvu za giza. Na kweli alifanikiwa kwa kiasi kukubwa sana lakini kama unavyojua kila kitu kina malipo, hakuna cha bure. Kwa uroho wa madaraka aliuza roho yake kwa majini na kadri muda ulivyoyoma alikuwa anabadilika na kuwa kiumbe wa ajabu sana. Ulifikia wakati alishindwa kutembea mchana na hivyo akaona bora aondoke katika tawala yetu. Siku kadhaa tokea aondoke zililetwa ripoti kuwa kuna viumbe wa ajabu wanauwa watu na kila siku idadi yao ilikuwa inaongezeka. Gordon baada kuona hali imezidi kuwa mbaya aliamua kufunga safari kuelekea milimani kwa ajili ya kutafuta msaada kutoka kwa miungu. Hata hivyo hali ilizidi kuwa mbaya, siku moja Gordon aliota kuna mlima mrefu sana na hakuna binaadamu aliyewahi kufika katika kilele cha mlima huo. Juu kabisa kwenye mlima huo ndo kuna majibu ya maswali yake yote, asubuhi mapema alinieleza na kunambia kuwa ana funga safari kwenda kuutafuta mlima huo.
FULL 1500
0699286085.