Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

MWANAMKE JEURI SEHEMU YA 06

3rd Aug, 2025 Views 27



MTUNZI: FRANK TITUS KAPINGA

SEHEMU YA 06

Baada ya kufika benki Antura alitoa fedha million 5 kisha alimkabidhi Anshera. Na baada ya kukabidhi pesa hizo, jamaa aliondoka pasipo kuzungumza neno lolote, aliwaacha Anshera na Afande wakiwa wameganda kama midori vile!!
"Hivi huyu mtu ni kapuku kweli au anatuigizia?. Amepata wapi pesa zote hizi? kwanza anafanya kazi gani? mbona ananichanganya!!" Anshera alivurugwa na Antura.

"Hata mimi sielewi, sijui amezipata wapi zote hizi; Vipi unataka nimfuatilie ili nijue anafanya biashara gani?"
"Achana nae, mimi sina ujinga wa kumfuatilia mswahili. Muhimu ni kwamba tumepata pesa zetu za buree. Shika hizi ni zako, na hizi ni zangu. Kesi ifutwe" Waligawana pasu kwa pasu.
"Sawa mwanasheria"
Kesi ya mchongo iliishia hapo, afande alirudi kituoni kwaajili ya kufuta kesi. Anshera alielekea nyumbani kwake akiwa amejaa pesa za rushwa na uonevu. Alitembea kwa furaha na kujiamini sana, alijisikia fahari kutokana na uwezo wake wa kuwaendesha watu kwa jinsi atakayo.

******
Antura Mitkas Manyota, ni mfanyabiashara wa madini, pia ni mmiliki wa kampuni ya uuzaji na ununuzi wa madini iliyopo Geita na Daressalaam. Ana mgodi ambao kila mwaka humuingizia pesa za kutosha. Katika mgodi wake ameajiri vijana wengi ambao wanafanya kazi usiku na mchana. Yeye mwenyewe kazi yake kubwa ni kusimamia uchimbaji na uuzaji wa madini hayo.
Licha ya kumiliki kampuni na nyumba zilizopo katika mikoa ya Dar na Geita lakini Antura alipenda kuishi Babati. Aliishi Babati ili apate muda mwingi wa kufurahia maisha pamoja na wazazi wake. Pia alimiliki mashamba mengi ndani ya wilaya ya Babati, muda mwingi alitembelea mashambani kusimamia mashamba yake.
Antura licha ya kwamba hakuwa maarufu lakini alipendwa na watu wengi sana. Alipendwa kwa sababu alitoa misaada mbalimbli kwa watu mbalimbali katika sekta mbalimbali. Licha ya kupendwa huko lakini jamaa hakutaka kujikweza wala kujigamba, alikuwa mpole sana. Hata mavazi yake yalikuwa ni ya kawaida tu. Hakutaka kujiweka mbali na watu wa mtaani kwake.

Umri wake ni miaka 31 tu. Licha ya pesa zake lakini hakubahatika kuoa, hakuwa na mpenzi wala hakuwa na mtoto. Na hicho ndicho kilimuumiza sana kichwa. Jamaa alitamani kupata mke, alitamani kupata mtoto, alitamani kuishi katika maisha ya ndoa takatifu, lakini utata ni kwamba hakubahatika kupata mwanamke sahihi. Wanawake wengi hawakuwa na mapenzi ya kweli, walimpendea pesa, aliwapiga chini kwa sababu hawakumfaa na wala hakuwapenda. Yeye alihitaji mwanamke atakayempenda kwa moyo wake.

*****
Sasa baada ya kutolewa mahabusu Antura alirudi nyumbani akiwa anatabasamu sana. Muda mwingi alichekacheka na kumshukuru Mungu. Hata mara baada ya kufika nyumbani alishindwa kabisa kukaa chini!! muda wote alijizungusha mara hapa, mara pale, alitabasamu kwa raha!!

"Asante Mungu wangu!!! Asante kwa hichi nilichokiona. Ni muda mrefu nimekuwa nikitafuta mwanamke sahihi wa maisha yangu, mwanamke atakayependwa na moyo wangu, hatimaye nimemuona kwa macho yangu. Nimemuona na nimempenda sana. ila anaonekana ni mtata kweli kweli!! Sidhani kama atanifaa, na sidhani kama atanipenda kwa mapenzi ya kweli, naogopa hasije akanipendea pesa kama wenzie. ili nijue kama anafaa au hafai inabidi nikamtongoze kwa makubaliano ya kumpatia pesa. Kama atakubali kupokea pesa zangu nitagundua kuwa hanifai. Lakini kama atakataa kuchukua pesa zangu nitagundua kuwa ananipenda" Antura aliwaza akiwa ameganda sebuleni, usoni alitoa tabasamu lililojaa hofu na shauku ya kutaka kujua kama anapendwa au hapendwi.

******
Ni mwezi mmoja ulipita tangu Anshera aingie kazini. Ndani ya mwezi huo mmoja tayari aligombana na asilimia 80% ya wafanyakazi wote. Katika asilimia 80%; Asilimia 75% walikuwa ni wanaume; aligombana nao mara baada ya kutongozwa kisha aliwakatalia kwa dharau. Asilimia 5% walikuwa ni wanawake, aligombana nao kwa sababu alikataa kuwa rafiki yao.
Wafanyakazi walipata hasira juu ya Anshera, waliona haiwezekani wasumbuliwe na mtu mmoja. Kwa hasira waliamua kumtenga. Hawakumpa ushirikiano wowote katika kazi. Lakini pia walikubaliana kumuondoa ndani ya halmashauri.
Walimfuata mkurugenzi wa halmashauri kisha walimueleza kila kitu kuhusu Anshera. Walimueleza kwamba binti huyo licha ya kusoma Harvard lakini hakuwa na maajabu yoyote katika kufanya kazi. Alikuwa ni mvivu, hana ubunifu, ana dharau, hana akili, hajui kubuni au kushauri sheria zozote. Pia ujio wake haukuongeza kitu chochote katika halmashauri yao. Walimtaka mkurugenzi amuachishe kazi Anshera au amuhamishe wilaya.
Mkurugenzi alipokea malalamiko hayo lakini hakuwa tayari kumuondoa binti huyo. Aliona ni hasara kubwa kumpoteza binti mzuri kama huyo. Kwa hasira mkurugenzi aliwafukuza wafanyakazi wake pia aliwapa onyo waachane na suala hilo la kutaka kumfukuza Anshera.

****
Licha ya kufukuzwa na kupigwa marufuku lakini wafanyakazi hawakukoma. Walifikisha malalamiko yao katika baraza la madiwani ambao ndio viongozi wa ngazi ya juu katika halmashauri hiyo. Madiwani waliitisha kikao cha dharula kwaajili ya kumjadili Anshera. Kikao hicho kilihudhuriwa na madiwani kutoka kata mbalimbali, mkurugenzi wa halmashauri, viongozi wa idara mbalimbali katika halmashauri pamoja na Anshera mwenyewe. Katika kikao hicho walalamikaji waliendelea kumponda Anshera kama ifuatavyo;
"Huyu binti hafai... Aondoke tu" Wakuu wa idara walipayuka maneno.
"Kwanza sio muwajibikaji kazini, hapendi kushauri wala kushauriwa; hana ushirikiano na wafanyakazi wenzie. Binti huyu aliletwa hapa ili alete maendeleo, lakini hana lolote. Idara yake ya sheria imeshindwa kusimamia mali na kutetea haki za halmashauri. Tangu ateuliwe kuwa mkuu wa idara ya sheria halmashauri yetu imeshindwa kesi zote zilizopo mahakamani, tumepoteza mamillion mengi katika kuendesha kesi hizo, hali hiyo imepelekea mapato yetu kupungua kwa kiasi kikubwa. Huyu binti hajui kutetea maslahi ya halmashauri, tumeingia mikataba hewa mingi sana. Hajui kushauri sheria ndogo ndogo ambazo zitasaidia katika kusuluhisha migogoro mbalimbali." Mweka hazina alilalamika mbele ya baraza la madiwani.
"Sio hivyo tu bali binti huyu ni mchelewaji na mtoro, anafika kazini akijisikia. Ukimfuata ofisini kwake muda wote anachati tu, hasikilizi shida ya mtu hadi aamue yeye. Kwakuwa yeye ni mkuu wa idara anadharau wafanyakazi wa ngazi ya chini. Umri wake ni miaka 24 tu, lakini wafanyakazi wote aliowazidi mshahara anawaita wadogo zake" Mratibu wa halmashauri nae alimwaga malalamiko yake, ilibidi madiwani wacheke na kusikitika kwanza kisha walimtazama Anshera ambaye muda wote alikuwa anachati kwenye simu yake.
"We binti... Wewe... We binti wee" Mwenyekiti wa baraza la madiwani alimuita Anshera ambaye alikuwa akiperuzi mitandaoni.
"A-bee" Anshera alishtuka, aliwatazama madiwani.
"Hivi wewe upo na sisi kweli?"
"Kwani hapa nipo na nani? Hamnioni au?" Anshera alianza balaa lake. Madiwani walikosa pozi! Walibaki wanashangaa tu

PATAMU HAPOOO, USIKOSE NEXT EP

WASAP 0743857349

FRANK KAPINGA.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MWANAMKE JEURI SEHEMU YA 06  >>> https://gonga94.com/semajambo/mwanamke-jeuri-sehemu-ya-06
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest