Maria aliondoka na kwenda kuanza maisha mapya baada ya wiki moja kupita alirudi nyumbani kwakina Liya akachukuu vitu vyake . Liya alikuwa na wasiwasi juu ya urafiki wao alimuuliza
" Maria umenikasirikia? Maria alitabasamu Kisha akasema
" mjinga wewe kwanini nikukasirikie, wewe Ni zaidi ya rafiki imekuwa ndugu kwangu.
" Lakini baba ....
" Shiiii sitaki uongelee yaliyopita huenda baba yako alikuwa na maana alipotaka niondoke. Umeona Sasa hivi nimeanza kujitegemea pia akili ya kutafuta kazi ilikuja haraka hivyo baba alinitakia mema. Liya alimsogelea akamkumbatia
" Daima nipo pamoja na wewe ukiwa na tatizo niambie alafu nahitaji kupafahamu unapoishi.
" Hilo lazima kesho mapema nitakuja kukuchukua.
" Kwanini usiwe leo?
" Leo haitawezekana kipenzi nimepata kazi ya kuhudumia kwenye sherehe moja hivi.
" Ooh sawa.
Waliagana Maria akaondoka . Majira ya saa kumi na mbili jioni Maria alienda sehemu aliyopata kazi kwa siku hiyo
Aliungana na wenzie wakaenda kuvalia sare ya kuhudumia ilikuwa Ni sketi fupi nyeusi na shati jeupe la mikono mirefu . wakaanza kufanya kazi ya kupanga vinywaji pamoja na kupika vyakula.
Majira ya saa mbili usiku part ilianza vijana wakitajiri walifika na magari Yao ya kifahari na walikuwa wamevalia mavazi yenye thamani Bryan nae alikuwa miongoni wa wageni waalikwa.walipofika mlangoni walichukua mask wakavaa ndipo wakaingia ndani . Huko ndani kulikuwa na sauti kubwa ya muziki Jordan aliingia huku akiwa anacheza . Rafiki yao Derick muhusika wa hiyo sherehe aliwafuata na kuwakaribisha.
" Daa unajua siaminikana Bryan anakuja maana huyu jamaa ana masharti Sana.
" Unatakiwa kunishukuru nimefanya kazi kubwa kumshawishi. Jordan alisema
" Hapo siwezi kubisha nakupa pongezi njooni huku tuendelee kufurahia. Walienda kuungana na wenzao huku wakina Maria wakiendelea kusambaza vinywaji. Sehemu walivyokuwa wamekaa wakina Bryan kulikuwa na wasichana waliokuwa wakijipitisha kile kitendo kilimketra Sana Bryan maana huwa hapendi shobo pia hataki kuwa na ukaribu na watoto wa kike. Kwa upande wa wenzake ilikuwa kawaida wasichana waliwashika shika na wengine walinyanyuka na kwenda kucheza nao muziki. Kwenye meza yao watu wote walinyanyuka na kumuacha Bryan akiwa anakunywa kinywaji . Mara alitokea Dada mmoja na kwenda kukaa jirani yake.
" Mambo. Yule Dada alimsalimia huku akibadilisha mikao ya kumtega Bryan alimuangalia alafu akaendelea kunywa kinywaji chake. Yule Dada alisogea karibu na kumshika begani Bryan aliutoa mkono wa Yule Dada alafu akavua mask yake akamkazia macho.
" Wewe hebu niangalie vizuri hivi unahadhi ya kushika hii nguo, unajua thamani yake?
" Samahani lakini nilikuwa nahitaji kampani yako, tunaweza kwenda kucheza pamoja? Bryan alinyanyuka bila kujibu alafu akaondoka na kwenda kusimama pembeni. Derick alimfuata
" Vipi mbona umekuja kusimama huku alafu umekaa kichovu twende tukacheze mziki.
" Hapana sitaki kuungana na hivyo viumbe mnavyovifurahia. Derick aliangua kicheko alafu akamwambia.
" Hivi bado haujapona ule ugonjwa wako? Sasa unatakiwa kwenda kuonana na doctor ili upate Tiba . Wanawake Ni upande wetu wa Pili hutakiwi kuwachukua kiasi hicho, unatakiwa kusahau yaliyopita.
" Siwezi Derick kila siku huwabnakumbuka kile alichonitenda Miriam kamwe siwezi kupona vidonda alivyo nisababishia na sidhani Kama ipo siku nitasahau na kuamua kumtafuta kiumbe abaeitwa mwanamke na kukaa nae pamoja.
" Hahahaha acha kunifurahisha najua unajikaza tu Ila ipo siku utapatikana na wewe mwenyewe utakiri kuwa umependa. Bryan alitoa tabasamu lenye dharau Kisha akamuona muhudumu anapita na vinywaji akamuita. Yule muhudumu alienda na kuwahudumia . Wakati anawahidumia Bryan alinyanyua uso wake na kumuangalia muhudumu aliye wahudumia ndipo akamuona Maria. Alimuangalia kwa makini Kisha akaita
Maria. Maria alimuangalia alipoona kuwa Ni Bryan alitamani kuondoka lakini alishindwa kwakuwa alikuwa kazini.
" Boss....
" Ulifikiri hatutaweza kuonana?
" Sijawahi kukukimbia alafu naomba uniache nimalize kazi yangu nikimaliza tutaonana.
" Hapana. Derick alimuangalia Maria Kisha Bryan alafu akauliza
" Mnafahamiana? Hakuna aliemjibu. Bryan alikuwa kamkazia macho Maria na Maria alikuwa anatetemeka kwa uwoga alikumbuka kauli ya Bryan aliyo mwambia ameianzisha Vita nae. Bryan alimshika mkono na kumvuta Maria akiwa kashika trei yake ya vinywaji, Derick alikuwa amesimama akiwaangalia kwanza hakuamini alichokiona maana Byran na wanawake Ni vitu viwili tofauti. Akiwa anashangaa Jordan alifika na kumuuliza
" Bryan kaenda wapi?
" Katoka na binti mmoja ...
" Acha utani Bryan kapata mwanamke?
" Nahisi hivyo kajiopolea muhudumu mmoja. Jordan aliangua kicheko mpaka akainama
" Acha utani bwana
" Sikutanii hata Mimi sikuamini nilichokiona lakini ndio hivyo kampata Maria wake wamevutana huko nje.
" Umesema nani?
" Maria. Jordan. Alishituka
" Yako wapi?
" Wamevutana huko nje wameona hapa hawataelewana na hizi kelele za muziki. Jordan alitoka nje haraka na kuanza kuangaza macho ndipo alipowaona wakiwa wamesimama huku Maria akiwa kashikilia trei.
Kabla Bryan hajaanza kuongea Maria alianza kujitetea.
" Lakini ulinielewa vibaya Mimi sikuwa na maana uliyofikiria...... Jordan valifika walipokuwa wamesimama
" Bryan Kuna Nini?
" Hakuna kitu unaweza ukaenda.
" Huyu dada anahitajika ndani kwenda kuhudumia watu.
" Na Mimi Nina maongezi nae.
" Kumbuka hapa ameajiriwa usimuharibie kibarua chake
KWETU morogoro.