Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

MWANAUME WA AJABU SEHEMU YA 24

3rd Aug, 2025 Views 2





SEHEMU YA 24

"Bwana we si unijibu... Unafanya au hufanyi?... Tena naomba uniambie ukweli ili nijue, husinifiche kitu hata kimoja. Najua wewe ni mcha Mungu, ukinidanganya shauri yako, utapata laana kwa Mungu!!... Wewe niambie ukweli, je huwa unafanya au hufanyi?... Umewai kufanya au hujawai?"
Nilimuuliza maswali ya kipuuzi lakini niliona fresh tu, nilitaka nipate ukweli ili nijue kama anapatikana au hapatikani. ili kama kuumia niumie, kama kuteseka niteseke, kama kufa kwa presha nife, au kama kufurahi na nifurahi. Kwakuwa kaka ni mtu wa dini niliamini ataniambia ukweli kuhusu maisha yake ya kimahusiano!!

Baada ya kumuuliza maswali hayo kaka alikodoa macho alinishangaa, alishindwa kunielewa. Bila shaka aliona nimemuuliza maswali ya ajabu kweli kweli. Licha ya kunitazama kwa kasi lakini sikuogopa, bado nilitaka aniambie ukweli.
"Mbona unaniangalia tu bila kuniambia chochote? Nipe jibu" Nilimwambia
"Hivi ni maswali gani hayo ambayo unaniuliza? hujui kuwa mimi ni kaka yako?.. Hiyo kufanya au kutofanya inakuhusu nini wewe?"
"Haya bwana kama hutaki kuniambia" Nilinuna
"Sikiliza nikuambie, mimi siwezi kufanya huo ujinga hadi nifunge ndoa. Kwa sasa nasaka pesa ili wewe upate elimu uitakayo, utimize ndoto zako na uishi maisha mazuri. Hayo mambo mengine nitayakuta kwenye ndoa"
"Kama kweli hufanyi naomba husifanye. Pia kama bado hauna mpenzi, nakuomba husitafute mpenzi hadi mimi nimalize shule. Hata ikitokea wanawake wanakutongoza wakatalie.. Sawa kaka?"
"Sasa kwanini nifanye hivyo?"
"Wewe kubali tu. Nikubalie maneno yangu"
"Mmh! sawa nimekuelewa"
Baada ya kaka kukubali maombi yangu, nilitabasamu kwa furaha. Kwanza nilifurahi kwa sababu hakuwa na mpenzi wala hakuwai kuzini. Lakini pia nilifurahi kwa sababu aliniahidi hatotafuta mpenzi wala hatofanya upuuzi hadi pale nitakapohitimu chuo. Tuliendelea na safari, baada ya masaa machache tulifika nyumbani Mtwara, maisha mengine yaliendelea.

*****
Mwezi huo huo wa 9, baada ya kutoka jeshini sikutaka kupoteza muda. Wakati wenzangu wakiomba vyuo vya hapa Tanzania, mimi niliomba nafasi ya kusoma urubani katika shule ya urubani iliyopo afrika kusini. Kwa mujibu wa sheria za urubani nilipaswa kuanzia katika ngazi ya chini ya PPL (RIVATE PILOT LICENCE). Hapa nilipaswa kujifunza kuongoza ndege binafsi kabla sijajifunza kuongoza ndege za abiria. Nilitakiwa kupata mafunzo hayo ya PPL kwa miezi 5 hadi 6 (inategemea na uelewa wa mtu)
Katika harakati za kuomba chuo hicho sikuwa peke yangu, nilikuwa na kaka. Tuliomba kupitia mtandao (online), tulijaza form kisha tuliituma maombi. Uzuri wa vyuo vya urubani ni kwamba wao hawahitaji vigezo vingi. Wanachotaka ni umri sahihi hasa hasa kuanzia miaka 17/18, uwe unajua kuongea kingereza vizuri, pia uwe na cheti kizuri cha afya. Na jambo jingine ni kwamba uwe una pesa za kutosha kwa sababu mafunzo hayo yana gharama sana.
Baada ya wiki moja majibu yangu yalirudi kupitia email, nilipata nafasi ya kujiunga na chuo ambacho nilituma maombi. Nilisafiri pamoja na kaka tulielekea Afrika Kusini. Yeye licha ya kwamba aliishia darasa la saba lakini ndiye aliniongoza katika kutimiza ndoto yangu ya urubani.
Tulifika South Africa kwenye shule husika, kaka alikamilisha malipo ya ada kwa ajili ya masomo ya nadharia na vitendo. Lakini pia aliniunganisha na kozi ya kujifunza kingereza cha kusoma, kuandika na kuzungumza vizuri zaidi, kozi hiyo ilifanyika katika shule ile ile ya urubani.
Baada ya kukamilisha taratibu zote kaka aliondoka. Mimi nilianza mafunzo yangu. Katika mafunzo ya urubani nilifundishwa mambo mengi kuhusu anga, jinsi ya kukabiliana na hali ya hewa na mambo mengineyo.
Katika ngazi ya PPL nilifanya mitihani 8, yote nilifaulu. Baada ya kukamilisha mitihani ya nadharia tulihamia kwenye vitendo, hapo sasa shughuli ilianza!! Nilitakiwa kupaisha ndege angani. Hapo ndipo palizua utata kati yangu mimi na mkufunzi wangu.
Mkufunzi wangu wa vitendo alikuwa ni mzungu, raia wa pale pale afrika kusini. Jina lake ni Jackson. Yeye alikuwa ni mtaalamu wa mafunzo ya ndege binafsi. Alikuwa ni mwalimu mzoefu ambaye aliaminiwa sana na chuo kile. Kupitia utaalamu na uzoefu wake alitoa marubani wengi sana wa ndege binafsi.
Mwalimu huyo sio tu alisifika kwa sababu ya utaalamu wake wa kuongoza ndege binafsi. Lakini pia alisifika kutokana na ukongwe wake wa kudumu katika chuo hicho. Alisifika kutokana na uwezo wake wa kuzungumza lugha 6 ikiwamo kiswahili. Alipendwa sana kutokana na nidhamu yake katika kazi, heshima yake kwa watu wote, upendo wa kweli kwa wanafunzi wake. Kubwa zaidi ni kwamba alikuwa na uwezo wa kumfundisha na kumuelewesha mwanafunzi kwa muda mfupi sana.
Baada ya kukabidhiwa mwalimu; Mafunzo yangu ya vitendo yalianza rasmi. Mafunzo yalifanyika kwa kutumia helcopter ndogo ambayo iliandaliwa kwaajili ya wanafunzi. Mimi na mwalimu Jackson tulivaa mavazi ya kirubani kisha tuliingia kwenye helcopter hiyo. Sote tulikaa mbele ila mwenzangu ndiye alipaswa kuendesha ndege hiyo. Mimi kazi yangu ilikuwa ni kutazama anachokifanya, kusikiliza maelekezo yake na kujifunza kwa vitendo.
Kwakuwa mambo mengi nilijifunza kupitia nadharia, matendo yalikuwa marahisi tu. Pia kutokana na utaalamu wa mwalimu Jackson; niliweza kuelewa kwa haraka sana. Mafunzo yalifanyika kwa kurudia rudia! Yalifanyika kwa masaa maalumu.
Mara ya kwanza mwalimu Jack aliendesha ndege, lakini mara ya pili nilikabidhiwa usukani. Niliendesha kwa kufuata maelekezo ya mwalimu Jack na waongozaji wengine ambao walikaa ofisini. Mwanzo ulikuwa mgumu sana!! Licha ya kupewa maelekezo mengi lakini niliendesha kwa woga, nilitetemeka kiasi kwamba helcopter ilianza kuyumbayumba!!
"Husiogope.... kuwa makini tazama mbele... Hakikisha haugongi kitu chochote hasa hasa ndege warukao.... Na ikitokea ndege imekuzidi uwezo hakikisha unaipeleka katika kina kifefu cha bahari ili kupunguza ukubwa wa ajali." Mwalimu Jackson aliniambia
"Sawa mwalimu" Nilimjibu.
Safari iliendelea. Mafunzo hayo yalifanyika katika eneo la wazi. Eneo ambalo lilijaa mchanga mwingi, pembezoni mwa bahari. Kuanzia round ya 1 hadi 10 niliendesha kwa kuweweseka na kuyumbayumba. Lakini kuanzia round ya 11 niliendesha kwa uhodari mkubwa sana. Niliweza kuwasha mitambo na kupaisha helcopter juu, pia niliweza kuisongesha mbele bila kuyumba.
Licha ya uhodari huo lakini bado kuna kitu kimoja ambacho kilinisumbua. Nilishindwa kushusha ndege ardhini na kuisimamisha kwa umakini na usalama mkubwa. Mara zote ambazo nilijaribu, nilishindwa. Mwalimu Jack ndiye alikuwa anaishusha badala yangu.
Tayari nilimaliza masaa 47 kati ya 50 ambayo nilitakiwa kufikisha ili nipewe cheti. Pia tayari nilimaliza siku 10 za mafunzo kwa vitendo. Katika siku hizo nilifunzwa kuendesha ndege mchana na usiku. Nilifunzwa kuendesha katika mazingira mbalimbali.
Nilibakiza masaa matatu tu kumaliza mafunzo hayo. Hata hivyo kulingana na riport ya mwalimu wangu ni kwamba tayari niliweza kuendesha ndege binafsi kwa asilimia 95%. Zilibakia asilimia 5 tu za kumalizia. Nilifurahi sana, pia nilifurahi kufundishwa na mwalimu huyo ambaye alionekana kuwa mtu mwema sana!!
Mara nyingi alipenda kunitazama kwa muda mrefu kisha alitabasam. Nilimuuliza kwanini anapenda kunitazama sana, alinijibu kwamba Mungu ni Fundi. Sikumuelewa alimaanisha nini. Pia sikumuhoji sana kwa sababu hicho sicho kilichonipeleka South!! Mimi nilikomaa na mafunzo yangu tu.

****
Siku ya 11 tulipumzika. Nikiwa hotelini kwangu nilitumia siku hiyo kuwasiliana na kaka Dhakir. Tuliwasiliana kupitia video call. Nilimueleza namna ambavyo niliweza kuendesha ndege, pia nilimwambia imebaki siku moja kumalizia mafunzo yangu ya PPL. Kaka alifurahi sana, aliniambia anajiandaa kuja South Africa kwaajili ya kukamilisha taratibu za mafunzo ya pili ( CPL - Ndege za abiria na biashara).
Sasa nikiwa naendelea kuongea na kaka, mara mlango wa chumba changu uligongwa. Kwakuwa ilikuwa ni asubuhi nilihisi labda ni muhudumu wa hoteli ameniletea chai. Kwa hasira sikutaka kwenda kufungua. Niliona ni heri nikose chakula kuliko kuharibu mazungumzo yangu na kaka.
Nilidhani mtu yule ataacha kugonga mlango lakini hakuacha, aliendelea kugonga tu. Nilikasirika sana!! Kwa hasira nilienda kufungua mlango nikiwa bado naendelea kuongea na kaka. Baada ya kufungua mlango nilidhani nitakutana na muhudumu, lakini hakuwa muhudumu, alikuwa ni mwalimu Jackson.
Nilishtuka sana kumuona!! ilibidi nimuage kaka Dhakir kisha nilikata video call. Baada ya kukata simu nilimtazama mwalimu Jack, nilimuona akichekacheka tu. Sijui alicheka nini!! Pia sikujua alikijuaje chumba ninachokaa. Na sikujua alifuata nini mahala hapo.
"Mwalimu.." Nilimuita mara bada ya kuona ananitazama tu bila kuongea kitu chochote.
"Naam!! Naam mwanafunzi wangu." Aliongea akiwa ananikagua kuanzia juu hadi chini. Nilishindwa kumuelewa.
"Nimeshtuka kukuona hapa. Vipi kuna mafunzo yoyote ili nijiandae tuelekee mafunzoni?"
"Hapana! hapana... Mimi sijafika hapa kwaajili ya mafunzo. Nimefika hapa kwa sababu nina mazungumzo muhimu na wewe. Kama hutojali naomba tuingie ndani ili nikuambie"
"Samahani. Sitoweza kukuruhusu uingie ndani. ila naweza kutoka nje kisha tukazungumza"
"Ni mazungumzo muhimu kwako, hatupaswi kuzungumza sehemu iliyo wazi. Ebu ngoja niingie ndani ili tuzungumze"
Aliingia bila kuruhusiwa. Alienda kukaa kwenye godoro kisha alinitazama mimi, aliniita ili tuzungumze. Kwakuwa yeye ni mwalimu wangu nilihisi labda kuna taarifa muhimu anataka kunipa kuhusu mafunzo yangu yaliyobaki. Taratibu nilimfuata ila sikukaa kitandani, nilisimama pembeni yake kisha nilimtazama na kumwambia;
"Nakusikiliza mwalimu"
"Lakini si ungekaa kwanza kitandani" Aliniambia akiwa bado anaendelea kuukagua mwili wangu.
"Husijali. Ongea nitakuelewa tu"
"Si unajua kuwa kesho tunamalizia mafunzo yako ya PPL? pia si unajua kuwa mimi ndiye nitakuandikia ripoti yako?... Pia si unajua kuwa tumebakiza kipengele kimoja cha muhimu?"
"Ndiyo najua mwalimu"
"Sasa nimekuja hapa kukueleza kwamba mimi ndiye mwalimu wa marubani wote unaowajua na kuwasikia hapa duniani. Tangu nianze kazi hii nina miaka zaidi ya 30 katika chuo hiki. Mimi ndiye mtu pekee nitakayeruhusu wewe upewe leseni yako. Kama utashindwa kuelewana na mimi, sitokamilisha mafunzo yako, pia leseni hutopata"
"Sawa nimekuelewa, lakini kwani kuna tatizo? au kuna mahala nilikukosea?"
"Hapana, hujawai kunikosea"
"Sasa nawezaje kushindwa kuelewana na wewe?"
"Wow! hapo ndipo nilipokuwa napataka. Unajua nini binti mrembo?... Hakika sikudhani kama Tanzania ina mabinti wazuri kiasi hiki. Hivi wewe ni Mtanzania, mkorea, mphilipino, mhindonesia au ni muarabu?"
"Mtanzania"
"Mmh! Zamani wakati najifunza kiswahili niliwahi kwenda Tanzania, lakini mbona sikuwahi kuona wanawake wazuri kama wewe?. Au walikuwa bado hawajazaliwa?"
"Sijui" Nilijibu kwa ufupi.
"Hivi yule jamaa aliyekuleta hapa, ambaye alikulipia ada, ni mumeo au ni nani yako?"
"Kaka yangu"
"Ooh asante Mungu!! afadhali ni kaka yako. Nilidhani ni mumeo, kumbe siye. Kwani wewe umeolewa?"
"Bado" Nilijibu nikiwa nimekasirika. Maswali yake yalinichosha.
"Ooh jamani najihisi mwenye bahati. Nilidhani umeolewa kumbe bado. Sasa binti unajua nini?... Kiukweli mimi nakupenda sana. Nataka nikuoe. Utachagua wewe tuishi hapa South Africa au tukaishi kwenu Tanzania. Gharama zako za kusomea CPL nitakulipia mimi. Na ukikubali ombi langu nitahakikisha unakuwa rubani mkubwa sana, nitakutafutia ajira katika taasisi kubwa za ndege, au ikiwezekana tutaenda kuishi ulaya!! Vipi upo tayari?"

COMMENT ZIWE NDEFU NDEFU, NAPITA KUSOMA.

BADO NAPOKEA ODA ZA VITABU VYA SIMULIZI HII, NICHEKI WASAP 0743857349.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MWANAUME WA AJABU SEHEMU YA 24  >>> https://gonga94.com/semajambo/mwanaume-wa-ajabu-sehemu-ya-24
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest