Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Siri Ya Mvuvi Na Bahari kisha wakanibeba na kunipeleka katika mti mkubwa ambao upo karibu na maeneo ya pale hospitali... Inaendelea... Sehemu Ya 09

3rd Aug, 2025 Views 25



Waliponifikisha kwenye ule mti, ule mti uligawanyika katikati ikawa kama mlango wakaniingiza umo, tulipoingia ndani ya ule mti kumbe alikuwemo mkubwa wao, walionikamata wakasema huyu alikuwa anatuangalia, yule mkubwa wao akaniambia samahani kwa kukusumbua, aliniangalia,kisha akawaambia wale wilionikamata, muachieni na mumrudishe mlipomtoa, sikuelewa kinachoendelea, walinichukua na kunirudia waliponitoa, kule hospitali, lakini hakuna mtu ambaye alielewa kama mimi niliondoka, niliporudishwa hospitali, kutokana na wale watu wa ajabu nikajikuta sina tena nguvu za kumsaidia mama yake na Riziki. tulikaa pale hospitali lakini hali ya Riziki kutokuongea ikawa ni jumla, nikajaribu ninavyoweza lakini nikashindwa kumrudisha katika hali yake ya kawaida,

Baada ya muda Latifa alikuja na yeye pale hospitali kuja kuniona, kwakuwa sisi tunaendelea vizuri kiafya tukaruhusiwa kwenda nyumbani, lakini Riziki tukamuacha pale hospitali akipatiwa matibabu pamoja na mama yake. badae tulikaa na Goma tukapanga namna ya kumsaidia Riziki, hata hivyo Goma alikuwa hajui kama mimi ndiye niliyemfanya Riziki kuwa bubu. ilibidi nifanye mpango wa kuonana na Salha, nilipoonana na Salha nikamwambia kuhusu Riziki na mama yake, Salha akaniambia mama yake na Riziki atapona muda ukifika,wala usiwe na wasiwasi, nikamwambia Salha lakini Riziki na yeye nimeshindwa kumrudisha katika hali yake tunamsaidia vipi, Salha akasema kuhusu Riziki muache kwanza tutajua namna ya kumsaidia, zilipita siku chache mama yake na Riziki akawa amepona kazi ikabaki kwa Riziki,

Mama baada ya tukio la mimi kupotea akaniambia niachane na kazi ya uvuvi, lakini swala la kuachana na uvuvi nikaona ni gumu lakini nikamkubalia ili yaishe, lakini mama alikuwa hafahamu kama mimi natembea na jini ambaye anaitwa Salha. Badae nikakutana na Goma kwa ajili ya kuongea,nae sababu nilihisi huwenda anajuwa mengi kuhusu matukio yanayoendelea baharini, nilikutana na Goma, Goma akaniambia ule mtumbwi umewazamisha watu wengi akiwemo kaka yangu pamoja na baba yako, mimi baada ya kuona kaka yangu amepotelea baharini nilifanya uchunguzi nikagundua ule mtumbwi ndio unahusika kwa watu kupotea, ikabidi nianze kuwa nafuatilia kuhusu ule mtumbwi,

Nimefuatilia hadi nikajuwa namna ya kuuendesha, lakini nilipoenda kwa waganga wa kienyeji wakaniambia inabidi nitafute mtu wa kushika ile kamba ili hata kama nikizama ndani ya bahari kutoka iwe ni rahisi, kwahiyo wewe uliposhindwa kuishikilia ile kamba ndio maana mimi nikashindwa kurudi nikawa nimebaki kule chini,na Riziki kosa lake ni kujitupa ndani ya maji ndio maana tukaenda wote,hata wakati ule nilikuwa nakuja kuchukuwa mtumbwi wakati nyie ni walinzi, nilikuwa natafuta mtu mwenye ujasiri, na katika watu wote ambao nilibahatika kwenda nao baharini wewe ndio mtu wa kwanza kuishika ile kamba mpaka nikaingia, kwahiyo baba yako na kaka yangu wote wapo kule chini ya bahari...

(nilianza kuwaza inawezekana vipi miaka yote ile baba yangu awe mzima nikaona Goma sio mtu wa kumuamini)

...kwahiyo kama unataka kumuokoa baba yako inabidi tukatafute njia ya kutupeleka hadi kwenye sehemu husika, sababu kukamatwa kwangu nilikamatwa sababu nilipita njia isiyokuwa sahihi. Nikamuuliza sasa kama ulikamatwa ni nani aliyekuja kukutoa huko ulipokuwa, Goma akasema sifahamu ni nani aliyekuja kutuokoa. ikabidi tupange mpango wa kumsaidia kwanza Riziki harafu sisi tutaona ni siku gani tutaenda kutafuta mlango wa kuingilia kwenye ule mji wa chini ya bahari. badae mimi nikaenda kumsalimia Riziki sababu wakati huo alikuwa tayari amesharudishwa nyumbani, lakini nilikuwa namhurumia sana kutokana na hali yake ya kuwa bubu, maisha yakaendelea wakati huo tunasubiri siku ya kwenda tutafuta njia ya kwenda kwenye mji wa chini ya bahari,

Lakini mimi nilianza kuwa na kiherehere cha kuwaonesha watu kwamba nina uwezo, watu walikuwa wanaona kama ni ujanja ujanja tu, lakini kweli nilikiwa na nguvu za kijini, wakati mwingine nilikuwa namuonesha miujiza Latifa nilikuwa nachukuwa shilingi na kuiweka katika kiganja changu na kuipoteza huku Latifa anaangalia, Latifa alikuwa anachukulia ni utani tu, Latifa akawa ameniambia inabidi tufanye mpango wa kuoana mapema,sababu muda unazidi kwenda,

Nikaongea na mama kwakuwa kuna pesa yangu alikuwa akiihifadhi,tukafanya mpango wa kupeleka mahari nyumbani kwao na Latifa, tukawa tumepeleka mahari na kupanga siku ya harusi, lakini wakati huo nilikuwa nimeshaanza kusahau kabisa kuhusu Salha, nikaona kama vile mimi na Salha tumeshaachana,mawazo yangu yote yakarudi kwa Latifa, lakini pia ndugu zake na Riziki walikuwa bado wanahangaika kutafuta dawa ya kumtibia Riziki, zikawa zimepita siku nyingi hatujaonana na Goma,wala kwenda kuvua samaki, lakini pia Salha nikawa namaliza siku kadhaa bila kuonana nae,

Nakumbuka siku moja nikiwa namuonesha mazingaombwe Latifa, ghafla alitokea Salha na kuniambia hukupewa nguvu kwa ajili ya kizichezea hivyo acha mara moja, Salha akaniambia kuna kazi hukuimaliza nyumbani kwetu kwahiyo inabidi ufanye maandalizi na mazoezi ya kuzitumia nguvu zako,sababu hivi karibuni kutakuwa na mashindano na hutakiwi kukosekana. Latifa hakuona chochote, lakini wakati huo mimi nilikuwa natamani kuachana na Salha ili nibaki na Latifa, sababu nyumbani kwao na Latifa nimeshatoa hadi mahari na siku ya harusi tayari imepangwa,

Siku ya kwenda kutafuta mlango wa kuingia kwenye mji wa chini ya bahari ikawa umefika, tukakutana na Goma tayari kwa ajili ya kuingia baharini kwenda kuutafuta ule mji, lakini kabla hatujapanda kwenye mtumbwi, nilimuona Salha kwa pembeni amesimama anatuangalia na nyakati zilikuwa ni za,usiku Salha akaniambia kama unataka rafiki yako apone basi acha kwenda huko unapotaka kwenda na uongozane na mimi kwenda kumalizia mtihani wako...

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Siri Ya Mvuvi Na Bahari kisha wakanibeba na kunipeleka katika mti mkubwa ambao upo karibu na maeneo ya pale hospitali... Inaendelea... Sehemu Ya 09  >>> https://gonga94.com/semajambo/siri-ya-mvuvi-na-bahari-kisha-wakanibeba-na-kunipeleka-katika-mti-mkubwa-ambao-upo-karibu-na-maeneo-
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest