Msiba ulifanyika tukamuhifadhi mpendwa wetu kisha tukakaa siku mbili na kutandua msiba , mama mkwe alikuwa mtu wa kulia kila siku nilijitahidi kukaa nae karibu maana alihitaji kuangaliwa kwa ukaribu.
Kwakuwa Selim alikuwa ndio mtoto mkubwa wa kiume alihitajika kuendesha miladi yote ya kifamilia hata hivyo ndio lilikuwa agizo la baba yake ,basi maisha yalibadilika kwa kipindi kichacheSelim akawa bize kuliko kawaida sikuona shida nikawa nampa moyo,na mama mkwe akawa mwenye mawazo sana ikabidi nikae nae hivyo vituko vyake sasa,nakwambia ilikuwa naamka asubuhi
Namuandalia chai nikiweka mezani na kwenda kumkaribisha anaitikia tu ila kuja kula haji, mtakunywa mpaka manamaliza yuko kimya kama msipomshtua anajifanya kusahau.
Ilienda hivyo hivyo mpaka ikafikia mda akawa anasema nimpelekee chumbani tena anasema baada ya kuweka mezani ukamuita kama mara tano ndio anajibu niletee chumbani.
Bila shida mtoto wawatu nachukua na kumpelekea ,hakuishia hapo akaanza kusema hawezi kula usiku nikasema sawa mfiwa bado anamajonzi .
Nikawa naingia jikoni saa kumi napika mpaka kufika saa kumi na mbili chakula naweka mezani,akawa anakula ikifika usiku unasikia " Mh kwahiyo kama nilikula jioni usiku ndio sili tena maana naona hamna share yangu" , mwali mie kuona hivyo tena nikamuhesabia mara mbili yani jioni na usiku .
Sasa baada ya kuanza kumuhesabia na usiku akawa anasema hali maana tumbo limezoea, sasa nikawa namuuliza "Mama kama tumbo limezoea mbona tukianza kula unaanza kulalalmika ?"
Wee kumuuliza hivyo nikosa la jinahi anaanza kwahiyo nikiwa na njaa nisiseme ? Unataka nilale nanjaa wakati mwanangu anatafuta?"
"Sawa mama samahani nimekosa " basi akisikia neno samahani anafurahi na kutulia ,hali iliiendelea ikafika mda akawa anasema hawezi kufua wala kufanya chochote maana bado mwili wake haijawa sawa .
Weee nikaona huu sasa ushenzi nikampigia Selim na kumwambia "Selim mama yako anakoelekea nikunitafutia shida tena sio shida ni kesi"
"Amefanya nini?"
"Nampikia chakula anakula kwakujivuta bado kufua nguo zake anasema hawezi kufua nikiweka kwenye machine anasema hataki maana nguo zinachoka haraka "
"Hahahaha "
"Unacheka kwamba ninachekesha si ndio?"
"Hapana sikucheki ila nacheka maana naona umemlea sana mpaka anakuzoea,kwani sinishalikwambia akizingia zichapeni ila msiuane ila naona umeamua kumtumikia na anafanya makusudi sasa endelea kumfanyia kazi sawa mkwe bora"
"Kwahiyo badala unishauri au uongee nae unaniambia nidunde ili akifa uoe mwanamke mwingine?"
Bwanae kufa afe yule kwanza ukimuangalia unamuona dhaifu kiasi hicho,we sikia huyo anachokifanya ni nikutumua kufiwa kama mgongo wakukupeleksha .
Eti mwili hauna nguvu anauzee gani wakushi shindwa kufanya kazi mbona alikuwa anafua nguo za mumewe hadi anaondoka si juzi tu hapo hata miezi miwili bado au unataka kuniambia marehemu kaondoka na nguvu za mkewe "
"Bwanaee nimeshatoa taarifa mapema kama vipi mtafutie mfanyakazi maana hivi vituko nimeshindwa kufanya shughuli zangu"
"Umetumwa uache kufanya hizo shughuli zako we uko kwako simama na sheria zako ,alafu siku nyingine usiniletee kesi zakijinga namna hii malizana nae huko huko ,kwanza nimekumiss njoo hata siku mbili basi"
"Nije alafu hii familia yako nimuachie nani "
"Umuachie nani kwani umekuja nao duniani au we ndo pumzi yao, Jabir yupo muache na watoto njoo nikupe raha mtoto wakike"
"Ushaanza kuongea utumbo " niliongea na kukata sim kisha nikatoka chumbani na kwenda kwa Jabir .
Nilifika nikakaa na kuongea nae kumwambia inshu ya mama mkwe akajibu" sikia hamna haja ya kuleta wasicha wawili wawili ngoja nimuite mama " kusikia aunt Suna nikakataa maana humu ndani kutakuwa na drama zakutosha .
Mwisho nikaona bora nilete wasichana wawili mmoja awe wakunisaidia kazi zangu mwingine awe maalumu kwaajili ya mama mkwe .
Baada ya kuchukua maamzi hayo niliendelea na mambo yangu huku nikisubiri wapatikane , haikupita wiki nikawapata kazi ikaanza akawa anasema ooh nimekuwa mzigo kwako mpaka umeamua kuniletea msichana wa kazi .
Sikutaka kubishana nae akabaki akifanya visa vyake nakaa kimya na akitaka kitu chochote nje na chakula namwambia msichana wake , huyo msichana sasa akitumwa akachelewa atamtukana na akikaa vibaya na makofi juu.
Hali hiyo sikuweza kuikalia kimya maana sio sawa mtu anyanyaswe ndani ya nyumba yangu ,kwahiyo nikawa nakuwa mkali haswa .
Visa viliendelea mpaka ikabidi nimuachishe kazi yule binti niliemtafutia na kuchukuliwa na Ney, baada ya hapo niliweka sheria mpya kama hataki kufuata anaruhusiwa kwenda kwake.
Alielewa na kutulia kama mtu kweli,basi maisha yaliendelea huku Selim akiwa anakuja nyumbani wiki wiki anaondoka ,kwa uwezo wa Mungu nikawa nimemaliza chuo tukabaki na swala la Naira na ndoa yake ya mchongo.
Sasa wakati nikiwa bize na biashara zangu Mama mkwe akaanza vitabia vyake akawa anaamka asubuhi anaenda kwa Nasra anakaa huko mpaka mchana ndio anarudi nyumbani ,akifika akikalibishwa chakula anasema kashiba ,siku nyingine akianapigiwa simu kuulizwa anasema anakula akirudi anasema hali kwahiyo vyakula vikawa vinajaa kwenye friji.
Siku hiyo asubuhi nikaamka mapema nikaandaa chai huku nikiwa na haraka ya kwenda nyumbani kwa Naira maana siku hiyo ilikuwa ni siku yake ya ndoa na kama mnavyojua alipanga kuwakomesha wazazi pamoja na huyo bwana.
Basi nilikunywa Chai kisha nikataka kutoka nikasikia mama mkwe anasema
"Norah niletee chai Chumbani kwangu alafu kuna nguo nilimwambia msichana wako apasi ila hadi saizi hajapasi" nilimuangalia na kumjibu
"Mama miguu unayo chai hii hapa chukua nenda chumbani kwako kaa kunywa na hizo nguo msichana saizi anakazi nyingi kama una haraka sana pasi mwenyewe "
"Norah wewe ni wakuniambia mimi nipasi mwenyewe wakati mfanyakazi yupo? Kwa hiyo mnaninyanyasa kwasababu nimefiwa na mume wangu"
"Mama kufiwa na chai havihusiani ,kama bado unauchungu sana kaa ulie ukichoka kalale"
Alianza kufoka sikumjali nikachukua chai na kupelekea jikoni kisha nikamwambia msichaa kama ikifika saa nne hajanywa basi ale vitafunwa vyote, baa da ya akuongea nilitoka na kwenda kwenye harusi.
Nilifika na kuuliza nini natakiwa kufanya Naira akasema mama tulia hapo hata usijichoshe ,basi bwana nilikaa na wenzangu chumbani mpaka mda wa kwenda salon ulipofika .
Tukajiandaa vizuri na kumpeleka bibi harusi wetu , tulifika nikampamba mwenyewe nilivyomaliza nikapamba na wengine kisha tukasubiri mda kidogo huku tukiwa tunaendelea na story.
Basi mda ulipofika tukaingia kwenye gari na kurudi nyumbani, watu shangwe la ukweli .
Tulimuingiza bibi harusi ndani na kusubiri ujio wa bwana harusi ambapo haikuchukua mda akafika ,hapo ndio mpango wa kuondoka ukaanza .
Kwakuwa tulishapanga mda mrefu haikutupa shida kwahiyo tukajifanya kuwa bize nje huku ndani Naira kashabadili nguo akavaa nikabu tukamwambia asitoke mpaka tutakapo mtumia meseji.
Niliset mazingira vizuri kisha nikatuma meseji ilipomfikia akachomoka kupitia mlango wa nyuma na kuingia kwenye gari ambalo tulikuwa tumeliandaa kisha akasepa.
Baada ya kuondoka mama mtu akaja na kuniambia mda tayari ndoa inatakiwa ifungwe nikasema haya tukaongozana mpaka chumbani hapo wengine wanajifanya wako bz hakuna mfano .
Tulifika bibi harusi hayupo acha mama wawatu aanze kuhaha tafuta uliza kimya akahisi huenda kaenda msalani ila huko nako hayupo,taarifa za bibi harusi kutokuonekana zikaenea watu wakaingiwa na taharuki sisi tukaungana na familia kujifanya tunahuzuni na kuvurugwa wangejua
KWETU morogoro.