Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

MWANAMKE JEURI SEHEMU YA 7

3rd Aug, 2025 Views 2



MTUNZI: FRANK TIRUS KAPINGA

SEHEMU YA 7

"Sio hivyo tu bali binti huyu ni mchelewaji na mtoro, anafika kazini akijisikia. Ukimfuata ofisini kwake muda wote anachati tu, hasikilizi shida ya mtu hadi aamue yeye. Kwakuwa yeye ni mkuu wa idara anadharau wafanyakazi wa ngazi ya chini. Umri wake ni miaka 24 tu, lakini wafanyakazi wote aliowazidi mshahara anawaita wadogo zake" Mratibu wa halmashauri nae alimwaga malalamiko yake, ilibidi madiwani wacheke na kusikitika kwanza kisha walimtazama Anshera ambaye muda wote alikuwa anachati kwenye simu yake.
"We binti... Wewe... We binti wee" Mwenyekiti wa baraza la madiwani alimuita Anshera ambaye alikuwa akiperuzi mitandaoni.
"A-bee" Anshera alishtuka, aliwatazama madiwani.
"Hivi wewe upo na sisi kweli?"
"Kwani hapa nipo na nani? Hamnioni au?" Anshera alianza balaa lake. Madiwani walikosa pozi! Walibaki wanashangaa tu.

"Hivi wewe binti unajua sisi ni kina nani?"
"Nyie si ni madiwani wa kata au?... Kwani kuna tatizo?"
"Tatizo ni kwamba wafanyakazi wenzio wanalalamika kuwa wewe ni mvivu, mtoro, jeuri, una dharau, unairudisha nyuma halmashauri kimapato. Tulidhani wanakusingizia kumbe ni kweli. Kwa tabia uliyotuonyesha muda huu inathibitisha kwamba haufai kabisa"
"Ama kweli Africa is poor because is poor. Yaani badala ya kuandaa kikao cha kujadili maendeleo ya halmashauri yetu, eti mnakaa hapa kujadili tabia zangu. Mmeandaa vinywaji, vyakula na posho za kunijadili mimi. Hivi nyie wabongo mlirogwa na nani?. Halafu kabla hamjaanza kujadili ukamilifu wangu, ngoja kwanza niwaulize; je mna uhakiki nyinyi wenyewe mmekamilika katika kutekeleza majukumu yenu?.... Je mna uhakika wananchi wenu wana amani, maji, barabara, afya na maendeleo ya kutosha?"
"Wewe unatuhoji kama nani?" Madiwani walimuuliza Anshera
"Na nyinyi mnanihoji kama nani? kwani nyie ndio mlinileta hapa kutoka marekani?"
""Kwahiyo unatuvimbia kisa uliletwa hapa na Rais si ndio?"
"Ndiyo. Rais alinileta kwa makusudi yake. Je nyinyi mnataka kupingana na teuzi za Raisi wa nchi yenu?"

Hapo ndo patamu sasa!! Madiwani walibaki wanatazamana tu!! Walikosa swaga, walikosa maswali, walikosa maneno. Licha ya kwamba walikasirika sana lakini hawakujua wamfanye nini Anshera ambaye aliletwa kwenye halmashauri na muheshimiwa Rais. Madiwani baada ya kuona Anshera anaongea sana, waliamua kuwa wapole;

"Binti tunaomba turudi kwenye mada yetu. Jibu mashtaka yanayokukabili, je maneno yanayosemwa kuhusu wewe yana ukweli?"
"Inawezekana ni kweli nina jeuri, lakini jeuri zangu ni kwa wale wanaotaka kunijaribu tu. Ebu tazama, walalamikaji wote ni wanaume, mnajua ni kwanini wanaume hawa wananichukia?"
"Ni kwanini?"
"Kwa sababu ukimuondoa mkurugenzi wetu, wanaume wengine wote waliobaki walinitongoza lakini niliwakatalia. Hasira zao ndizo zimepelekea wanichukie na watake niachishwe kazi"
"Aaah kumbeeee" Madiwani walishangaa
"Habari ndio hiyo. Wananisingizia mambo mabaya lakini ukweli ni kwamba mimi ndiye mfanyakazi bora katika halmashauri hii, mimi ndiye mtu pekee ambaye kila siku nawahi kazini, nashirikiana na kila mtu hapa ofisini lakini wafanyakazi wenzangu hawanipi ushirikiano wa kutosha; Wanaume wameninunia kisa siwataki. Wanawake wananionea wivu kisa mimi ni mzuri kuliko wao. Mimi ndiye mfanyakazi pekee ambaye nina malengo makubwa ya kukuza mapato ya hii, lakini wafanyakazi wenzangu wananiangusha" Anshera aliwageuka wenzie, maneno yake yalisababisha miguno na mishangao mingi kutoka kwa wafanyakazi wengine.
"Mkurugenzi ebu tuambie ukweli. Wewe ndiye msimamizi mkuu wa halmashauri hii, bila shaka unatambua mienendo ya wafanyakazi wako. Tunaomba utuambie ukweli kuhusu mgogoro huu. Je ni nani yuko sahihi kati ya binti na walalamikaji?" Mwenyekiti wa baraza la madiwani alimuuliza mkurugenzi.

Mkurugenzi alitulia akitafakari. Ukweli aliujua. Alitambua kwamba ni kweli Anshera ana tabia mbaya ila hakutaka kumpoteza. Aliogopa kumkosa binti huyo. Aliona ni vema amtetee ili siku akimuhitaji ampate kirahisi.
"Mkurugenzi mbona upo kimya?... Tuambie ni nani yupo sahihi?"
"Binti ndiye yupo sahihi sana. Msomi huyu wa Harvard ni hazina kwetu, ni lazima tumlinde kwa gharama yoyote ile. Kuhusu suala la mapato kupungua hili ni jukumu letu sote, hatuwezi kushusha lawama kwa mtu mmoja. Ebu fikiria binti huyu ana miezi mitano tu ndani ya halmashauri hii, lakini leo hii lawama zote anapewa yeye, hamuoni kama kuna kitu hapo?... Hamuoni kama binti huyu anafanyiwa fitina zisizo na sababu?"
"ila ni kweli kabisa" Madiwani walianza kukubali.
"Na ndio maana nilikataa kumfuta kazi binti huyu, ni msomi mwenye madini mengi kichwani. Mabinti wengi warembo huwa hawana akili, lakini huyu Anshera ana akili nyingi mno"
"Basi tumekuelewa!! na kuanzia sasa mgogoro huu umekwisha, binti ataendelea kuwapo hapa, muacheni afanye kazi yake kwa amani. Kikao hichi kimefungwa, tuwatakie majukumu mema"
Hatimaye Anshera alishinda. Kesi kubwa iliisha kirahisi kweli kweli. Madiwani waliondoka, walalamikaji nao waliondoka kishingo upande, waliondoka wakiwa hawajaridhishwa na maamuzi yaliyotolewa, hata hivyo walishindwa kubisha. Anshera alielekea ofisini kwake akiwa anatabasamu kwa furaha ya ushindi alioupata.
Mkurugenzi nae alielekea ofisini kwake, lakini baada ya kufika ofisini alikumbuka kitu, alikumbuka kuwa huo ndio muda sahihi wa kumtongoza Anshera. Aliamini atampata kirahisi kwakuwa alimtetea kwenye kesi. Bila kupoteza muda mkurugenzi aligeuka nyuma kisha alielekea ofisini kwa Anshera, alimkuta akicheza game kwenye kompyuta ya ofisi.
"Ooh binti mzuri naona unaburudika hapo, kwa raha zako" Mkurugenzi alimtania Anshera, alivuta kiti alikaa.
"Yeah, nafurahia ushindi wa kesi yangu" Anshera alijibu
"Ah ah ah! Lakini unatakiwa unishukuru sana mimi"
"Nikushukuru wewe kwa sababu gani?"
"Mmh! ina maana hukuona namna ambavyo nilikutetea?"
"Kwani nawe ulitaka kunikandamiza kama wenzio?"
"Bila shaka unaelewa kila kitu. Ukweli ni kwamba yale yaliyosemwa ni ya kweli kabisa. Mienendo yako ni mibaya sana, wewe ni mvivu, una dharau na jeuri nyingi sana"
"Kwahiyo?"
"Nilishawishiwa kukuondoa hapa ofisini, pia nina mamlaka ya kukufuta kazi lakini nimeamua kukaa upande wako. Nimeamua kukutetea tu, unajua ni kwanini?"
"Sasa si useme"
"Anshera wewe ni binti mzuri sana, una kila kitu katika mwili wako, unafaa kwa matumizi ya kiutu uzima. Naomba uwe nami, nitahakikisha kila siku unalipwa posho mbalimbali, hutofanya kazi zozote, nitakuwa nakupa likizo za mara kwa mara ili upumzike."

JE ANSHERA ATAKUBALI?

HUSIKOSE KUFUATILIA EPISODE IJAYO

NICHEKI WASAP 0743857349.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MWANAMKE JEURI SEHEMU YA 7  >>> https://gonga94.com/semajambo/mwanamke-jeuri-sehemu-ya-7
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest