Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

MWANAMKE JEURI SEHEMU YA 01

3rd Aug, 2025 Views 25



Ilikuwa ni siku ya kwanza ya ndoa yao. Mke alikataa kumpikia chakula mumewe, alikataa kufanya kazi za ndani, alikataa kulala chumba kimoja na mumewe, pia alikataa katakata kufanya tendo la ndoa na mumewe. Alimnyima kwa kumpiga mateke, viwiko na vipepsi.
"Nimesema husiniguse, ukiendelea kunisumbua tutaachana leo leo"
"Mke wangu husinifanyie hivyo, nipe basi hata mara moja tu"
"Sikupi, na sitaki unisumbue. Kwanza ondoka hapa kitandani, nenda kalale kwenye chumba kingine"
"Kwanini sasa?"
"Kwa sababu mimi ni mtu mkubwa serikalini, kamwe siwezi kutolewa usichana wangu na mwanaume hasiyefanya kazi ikulu. Yaani mimi niumie sehemu zangu za siri, nitokwe damu kwaajili yako wewe ambaye hauna cheo chochote serikalini? thubutu"
"Lakini tambua kuwa wewe ni mke wangu, ulikubali nikuoe. Tena nimekuoa kwa mahari nyingi sana. Mimi sijakuoa ili uwe pambo la nyumba yangu, bali ili tujenge familia na kuishi pamoja"
"Kumbe umenioa ili unijaze mimba? yaani mimi mkuu wa mkoa; nibebe mimba yako kisha niingie leba, nijifungue kwa uchungu kwaajili ya kuzaa mtoto wako? ila wewe una wazimu kweli! Kama mambo yenyewe ndio hayo ni heri ndoa ife, ila mahari zako sirudishi."

JE WANANDOA HAWA NI AKINA NANI? WANAPENDANA KWELI? ILIKUWAJE HADI WALIONA? UNADHANI NDOA YAO ILIDUMU AU ILIKUFA?... HIVI UNAJUA NINI KILITOKEA? FUATILIA MKASA HUU KWA MAKINI KABISA!!...........

*****
Anaitwa Anshera Brogoz Matuka, Ni binti msomi wa shahada ya sheria katika chuo cha Harvard nchini marekani. Alisomeshwa na serikali ya Tanzania kupita Scholarship; Ni mara baada ya kufanya vizuri katika mitihani yake ya kidato cha sita. Umri wake ni miaka 24 tu, licha ya umri huo mdogo lakini anajiamini sana, anajikubali kupitiliza, haogopi mtu na wala hapendi kuwaamini watu wengine. Hiyo yote ni kutokana na ubora wa elimu yake aliyoipata katika chuo namba moja duniani (Chuo cha Harvard).

Anshera ni binti mwenye maringo na misimamo mikali sana. Maringo na misimamo yake ni kwa sababu ya uzuri wa umbo, shepu na sura yake ya Kihiraki.

Baada ya kuhitimu masomo yake nchini marekani Anshera hakutaka kurudi Tanzania. Hakutaka kwenda kuishi na waswahili. Hakutaka kwenda kuishi katika nchi maskini, nchi yenye umeme wa mgao, nchi ambayo raia wake hawana pesa lakini wanakesha mitandaoni, nchi ambayo waajiriwa wa serikali wanalazimisha wasio na ajira wajiajiri. Nchi ambayo wanaotenda mambo ya hovyo ndio wanapata umaarufu mkubwa kuliko wanaotenda mambo mazuri. Nchi ambayo machawa, wachekeshaji na wambea mashuhuri wanapewa kipaumbele katika fani ya uandishi wa habari na utangazaji. Nchi yenye wanaume wanaotongoza asubuhi kisha jioni wanataka penzi. Nchi yenye wanaume wanaopenda kuharibu wasichana kisha wanashindwa kuwaoa kutokana na ugumu wa maisha. Nchi yenye wasichana wengi tegemezi, wasichana wanaotongozwa saa mbili kisha saa tatu wanaomba vocha, wasichana wasiojua kujitunza wala kujiheshimu.
Anshera hakutaka kuishi kwenye nchi ya hovyo.

Alitaka abaki marekani ili aolewe na wamarekani wenye pesa na tabia njema za kutochezea wanawake. Alitaka aajiriwe marekani kisha ajenge na kuishi katika nchi hiyo ya kitajiri. Yeye aliamini kwamba elimu yake ya Harvard ina hadhi kubwa kuliko elimu za watanzania wengi waliosoma katika vyuo vya Tanzania, hivyo basi hakutaka kwenda tanzania kujichanganya na watu wenye elimu za hovyo, alitaka abaki marekani kwenye watu wenye elimu ya hadhi yake.

Ili kutimiza malengo yake Anshera alipanga kuchukua uraia wa Marekani. Alitaka kufanya maamuzi hayo kimya kimya pasipo kumshirikisha mtu yeyote, hata wazazi wake hakuwashirikisha.

Siku iliyofuata Anshera alikusanya vyeti na vitambulisho vyake kisha alielekea katika ofisi za uhamiaji kubadili uraia. Akiwa njiani kuelekea ofisini mara simu yake iliita, alitazama alikuta amepigiwa na ofisi ya utumishi kutoka Tanzania.

"Hujambo Anshera, unazungumza na afsa utumishi wa serikali ya Tanzania, habari za huko marekani"
"Sijambo, marekani hatujambo. Na vipi kuhusu nyinyi wabongo?"
"Anshera kumbuka kuwa hata wewe ni Mtanzania"
"Ilikuwa zamani, kwa sasa sina uraia wowote. Ila muda si mrefu nitakuwa raia wa marekani"
"Una mipango gani? Au unataka kubadili uraia?... Anshera kumbuka kwamba serikali ya Tanzania ndiyo ilikupeleka marekani, ilikuchagulia chuo, ilikusomesha na ilikulea kwa gharama zote. Hata muda huu bado unatumia pesa za serikali ya Tanzania, ni kosa kubwa sana kuisaliti nchi yako. Nchi ilikusomesha ili uje kuikomboa katika idara ya sheria, na ndio maana leo hii nimekupigia simu kwa sababu unahitajika katika nchi yako"
"Unasemaje? Nahitajika katika nchi gani? hapana siji, kwanza niko bize na masomo"
"Sote tunajua kuwa umehitimu masomo yako ya sheria. Hauna ubize wowote, hauna ajira yoyote na ndio maana tumekupigia. Nina barua yako ya kikazi, imetoka kwa muheshimiwa Rais, barua hii inakuhitaji hurudi Tanzania haraka. Umeajiriwa kuwa mwanasheria wa halmashauri yako ya Babati"
"Aaaaah! Yaani mimi nitoke huku kwenye ofisi kubwa kisha niende nikafanye kazi Tanzania? nyie ukorofi huoo!! Kweli mimi Anshera ni wa kufanya kazi Babati?"
"Ndiyo. Tulikusomesha marekani ili upate ujuzi mkubwa wa kuja kuisaidia nchi yako ya Tanzania. Tunataka Tanzania iwe kama marekani. Tunataka uende Babati ukatumie elimu yako ya Harvard katika kukuza maendeleo ya halmashauri ile. Hivyo basi kesho utasafiri kuja Tanzania, ukifika moja kwa moja riport katika ofisi za utumishi ili uchukue barua yako, hii ni amri! nikutakie safari njema" Afsa utumishi alikata simu.
"Hallo... hallo... hallo... aaah sasa ndo mambo gani hayaaaa!! Nishasema siitaki nchi yenu ya hovyo, kwanini mnanilazimisha? kwani ni lazima nije niishi na nyinyi? yaani kwakuwa mlinisomesha ndo mnataka kunilazimisha nifanye kazi kwenye kanchi kenu?.. Mambo ya kifala hayo!!" Anshera alifoka kwa nguvu. Alinuna na kuvimba uso, alimaindi kweli kweli.

PICHA NDIO KWANZA LIMEANZA, JE ANSHERA ATARUDI BONGO AU HATORUDI?... AKIKATAA ITAKUWAJE? NA AKIRUDI ITAKUWAJE? USIKOSE MUENDELEZO.....

STORI HII IMEKAMILIKA, NA ITAPATIKANA KATIKA KITABU. KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NAMI KWA NJIA YA WHATSAPP TU (0743857349)

SHARE KWA WINGI, PIA UNAWEZA KUREPOST KWENYE ACCOUNT YAKO ILI IWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

STORI NI NYINGI ILA TUNAHITAJI WATU ZAIDI ILI TUZISOME KWA PAMOJA, NA NDIO MAANA NAWASISITIZA KUALIKA WATU KATIKA PAGE HII MPYA . KUTAG NA KUINVITE NI RAHISI TU HASA KWA WALE WANAOTUMIA SMARTPHONE.

NAWAKUBALI WATU WANGU WA NGUVU..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MWANAMKE JEURI SEHEMU YA 01  >>> https://gonga94.com/semajambo/mwanamke-jeuri-sehemu-ya-01
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest