Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

MWANAMKE JEURI Sehemu ya 02

3rd Aug, 2025 Views



"Ndiyo. Tulikusomesha marekani ili upate ujuzi mkubwa wa kuja kuisaidia nchi yako. Tunataka Tanzania iwe kama marekani. Tunataka ukienda Babati ukatumie elimu yako ya Harvard katika kukuza maendeleo ya halmashauri yako. Hivyo basi kesho utasafiri kuja Tanzania, ukifika riport katika ofisi za utumishi ili uchukue barua yako, hii ni amri! nikutakie safari njema" Baada ya maelezo hayo afsa utumishi alikata simu.
"Hallo... hallo... hallo... aaah ndo mambo gani hayaaaa!! Nishasema siitaki nchi yenu ya hovyo, sasa mbona mnanilazimisha? kwani ni lazima nije niishi na nyinyi? yaani kwakuwa mlinisomesha ndo mnataka kunilazimisha nifanye kazi kwenye kanchi kenu?.. Mambo ya kifala hayo!!" Anshera alifoka kwa nguvu. Alinuna na kuvimba uso, alimaindi kweli kweli.

Licha ya hasira zake lakini hakuwa na jinsi, hakuwa na nguvu za kubishana na serikali yake ya Tanzania. Kwa masikitiko makubwa Anshera aliahirisha mpango wake wa kubadili uraia. Aligeuka nyuma kisha alirudi hosteli; alikusanya vitu vyake alipanga kwenye begi, alikabidhi chumba chake kwenye uongozi wa chuo kisha aliaga rasmi.

****
Siku iliyofuata Anshera alianza safari yake ya kurudi Tanzania. Ni safari ambayo hakuipenda hata kidogo, akiwa ndani ya ndege muda wote alikuwa analia tu, alijuta kwanini alizaliwa Babati Tanzania, alikasirika kiasi kwamba alitamani ndege idondoke ili afe kuliko kwenda kuishi na wabongo.
"Siamini kama narudi kwa waswahili. Yaani chuo nimesoma Harvard University halafu naenda kuajiriwa bongo? Ina maana hata kuolewa nitaolewa na wanaume wa kibongo? Aaah mi staki bwana!!" Anshera aliendelea kulaani safari hiyo, aliendelea kuwachukia wabongo. Moyoni alipanga akifika Babati hatoongea na mtu yeyote zaidi ya wazazi wake tu. Aliwaza kwamba hatokuwa na rafiki yeyote, na wala hatopenda mazoea na mtu yeyote wa Babati.
Baada ya safari ndefu hatimaye walifika Dar katika uwanja wa ndege wa Mwalimu nyerere, alikodi Taxi ambayo ilimpeleka katika ofisi za utumishi, alichukua barua ya ajira kisha alielekea hotelini. Alilala hotel kwa siku moja, siku iliyofuata alielekea nyumbani kwake Babati mjini.

****
Ni miaka mitano ilipita tangu Anshera aondoke Babati. Wakati anaondoka aliacha mji ukiwa mdogo sana. Nyumba zilikuwa mbalimbali, biashara zilikuwa chache, hata watu walikuwa ni wachache.
Lakini baada ya kurudi alikuta mazingira yamebadilika sana. Nyumba zilikuwa nyingi, biashara nyingi ziliongezeka, watu wengi waliongezeka, vichochoro vilikuwa vingi kiasi kwamba Anshera alisahau njia ya kwenda nyumbani kwake.
Alishika simu yake alijaribu kumpigia mama na baba yake lakini simu zao hazikupatikana. Hakujali sana, aliendelea na safari. Kutokana na kiburi hakutaka kuuliza mtu, hakusalimia watu, hakujibu salamu za watu hata wale waliomfahamu.
"Ooh jamanii Anshera karudiiii... Anshee karibu nyumbani jamanii umependeza, umekuwa kama mzungu, nipe begi nikusaidie kupeleka nyumbani kwenu" Alizungumza mdada mmoja aitwaye Sindi. Licha ya kelele nyingi za Sindi lakini Anshera hakujibu wala hakutoa begi, aliendelea na safari zake.
"We Anshera wewe mbona huongei, husimami wala hunitazami? Kwani hunijui Mimi Sindi? Tulisoma wote shule ya msingi" Sindi alijitambulisha
"Hey keep quit, I don't know you. Pia huwa siongei na watu waliofeli darasa la saba, siongei na wanawake waliopata mimba shuleni, na pia siongei na wanawake waliojaa mateso. Mind your busines!! Stupid!!" Anshera alijibu kwa jeuri na dharau. Alimuacha mdada wa watu akiwa ameganda kama roboti.
Aliendelea na safari. Pia aliamua kujitanda mtandio kichwani ili hasifahamike mbele za watu wa mtaani kwake. Alitembea akiwa anavuta kumbukumbu ya njia iendayo nyumbani kwake. Alitembea kwa kubahatisha tu. Mara aliingia hapa, alitokea kule, nyumba yao hakuiona.
Alitamani kuuliza watu lakini alipotezea, hakutaka kuonekana mshamba. Sasa akiwa anahangaika huku na kule kwa bahati mbaya alitokea katika uchochoro wa mateja, wavuta bangi, wakwapuaji na wahuni wa mtaa.
"We! we! we! we dada husipite huko, husipite kwenye hiyo njia, wewe ni mgeni mtaa huu?" ilikuwa ni sauti ya jamaa mmoja aitwaye Antura. Licha ya kuzuiliwa lakini Anshera aliendelea na safari.
"Hivi we dada hunisikii au? husipite njia hiyo imekatazwa"
"Heeey!! we bogaz husinipigie kelele. Unanijua mimi? Umepata wapi nguvu, uwezo na kibali cha kuongea na mimi?... Mtu umefubaa hivyo, mweusi kama lami, manguo mabaya, unanuka ubabati, sura mbaya, maskini wa kutupwa halafu unapata wapi pumzi ya kuniongelesha? Who are you by the way?" Anshera alijibu kwa sauti yenye hasira kali akiwa anamtazama Antura usoni.
"Sio lazima unifahamu, ila mimi ni mkazi wa maeneo haya"
"Ooh! hutaki kunitajia jina lako si ndio? hutaki kunipa CV zako au sio?... Sasa kwa taarifa yako mimi huwa nazungumza na watu waliofika chuo kikuu tu. Je wewe una elimu gani?"
"Chuo kikuu"
"Umesoma hapa Tanzania au nje ya nchi? Chuo gani? kozi gani? umeajiriwa?"
"Nimesoma hapa hapa Tanzania, kozi ya uhasibu katika chuo cha IAA, sijaajiriwa"
"Pumbavu we!! Mimi nilidhani umesoma nje ya nchi, nilidhani nawe umesoma ulaya kama mimi. Halafu hiyo IAA ni chuo kikuu au Taasisi? hivi wewe una akili kweli? yaani umesoma kwenye taasisi ya hapa hapa Babati halafu unataka kuongea na mimi? kwa vigezo gani?... Ni heri hata ungesoma Mzumbe, Udsm, Sua au Udom angalau ningekusikiliza kidogo!! kwanza uhasibu ndo kozi gani? Hapa duniani kuna mtu hajui kufanya mahesabu? Yaani umesomea uhasibu halafu unataka kuongea na mimi? hivi unajua mimi ni nani? "
"Wewe ni nani?"
"Mimi ni Amicus Curiae, ukiniletea ujinga nitakufunga"
"Utanifunga kivipi sasa? kwani Amicus Curiae ndio nini?"
"Ona sasa hujui hata maana yake halafu unataka kuniongelesha. Nasikitika umenipotezea muda mwingi sana!. Kweli mimi Anshera ni wa kusimama njiani kuongea na Jobless?... Nilidhani una ajira kubwa serikalini kumbe mtu mwenyewe ni mlala hoi!!... Kilaza mkubwa wewe!! Wewe ni wa kunizuia mimi nisipite kwenye njia hii? unanichukuliaje kwa mfano? unadhani mimi siijui mitaa hii? naijua sana. Sasa naondoka, ole wako unisemeshe tena!!" Kwa kiburi na dharau Anshera aligeuka nyuma kisha aliendelea na safari, alipita kwenye njia ile ile ambayo alikatazwa.
Licha ya kwamba ilikuwa ni mchana lakini uchochoro ulitisha, hazikusikika kelele wala sauti za mtu yeyote, uchochoro ulikuwa kimyaa. Pia hakukuwa na mtu yeyote aliyepita maeneo hayo zaidi ya Anshera ambaye alitembea kwa kujiamini, bila hofu wala woga. Mkono mmoja alibeba begi kubwa, mkono mwingine alishika simu yake ya Iphone macho matatu na begani aliweka mkoba wake uliojaa Dollar.
Sasa akiwa anaendelea na safari mara ghafla njiani alikutana na wahuni wawili wakiwa wanavuta bangi, mkononi walishika bisibisi. Anshera alishtuka, mapigo ya moyo wake yalianza kwenda kasi. Fasta aligeuka nyuma akitaka kurudi alikotoka lakini kwa bahati mbaya alikutana na wahuni wengine wawili wakiwa wamebeba visu mkononi. Anshera alitaka kupiga kelele lakini alitulizwa kwa kuwekewa kisu shingoni.

MMH JAMANI NINI KITAMKUTA ANSHERA?

FOLLOW PAGE.....
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MWANAMKE JEURI Sehemu ya 02  >>> https://gonga94.com/semajambo/mwanamke-jeuri-sehemu-ya-02
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest