Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Siri Ya Mvuvi Na Bahari Salha alitoka na kwenda kuwaita wazazi wake, wazazi wake wakaja kwenye kile chumba na kukuta ile pete bado ipo chini... Inaendelea... Sehemu Ya 07+8

3rd Aug, 2025 Views



... wazazi wa Salha waliniangalia lakini hawakusema chochote, wakaichukuwa ile pete na kuondoka nayo, Salha aliwafuata wazazi wake, mimi nikabaki peke yangu kwenye kile chumba lakini sielewi maana naona wananifanyia mambo ya ajabu, baada ya muda kidogo Salha alikuja na mtu mwingine ambaye alikuwa ni kama mwalimu katika ule mji wao, yule mwalimu wa kijini akamwambia Salha atoke kwenye kile chumba, kisha tukabaki wawili mimi na yule mwalimu wa kijini, yule mwalimu akaniambia nikae chini na nifumbe macho yangu, nikakaa chini na kufumba macho yangu, nilipofumba macho nilianza kuhisi mwanga mkali katika paji langu la uso, ule mwanga ulianza kuvuta nyama na misuli yangu katika mwili, nilianza kuhisi kuna vitu vinatembea ndani ya mwili wangu, huku mwili unauma kama vile nimewekewa shoti ya umeme, lakini baada ya muda mfupi maumivu yakaisha, kisha nikaanza kuhisi ubaridi unapenya ndani ya misuli yangu, badae ile hali ikapotea nikaanza kujihisi kawaida, yule mwalimu wa kijini nikaanza kuhisi kama vile ananizunguka, alizunguka hatimaye akazidi kunizunguka kwa kasi, kisha akaniambia fumbua macho yako, nilipofumbua macho niliona kile chumba chote kinazunguka kwa mwendo wa kasi na yule mwalimu na yeye anazunguka kwa mwendo wa ajabu,lakini amefumba macho,

Badae akaniambia tumia hisia zako kusimama hewani, nikamwambia siwezi akasema vuta hisia (meditation) ukiwa hewani harafu fanya kama unapaa, ikabidi nitulize mawazo yangu na kuanza (meditation) kuvuta hisia kama vile nipo hewani, kweli nilianza kujihisi nipo hewani, yule mwalimu wa kijini akaniambia nenda juu zaidi, nikavuta hisia kama napaa juu,na kweli nikajiona nipo juu zaidi, tulikuwa kwenye chumba lakini kile chumba nilikiona kama hakina mwisho, baada ya kuwa nipo juu zaidi, yule mwalimu wa kijini akaniambia hakikisha hiki chumba kinaacha kuzunguka, nikafanya ku (meditation) ili kile chumba kiache kuzunguka, na kweli baada ya muda mfupi kile chumba kikaacha kuzunguka,pamoja na yeye, nikawa nipo hewani nimeelea, yule mwalimu wa kijini akaniambia hivi ndivyo unatakiwa uwe unayatuliza mawimbi ya bahari pale inapobidi,na unapotaka kuingia ndani ya maji au chini ya bahari,

Kisha akaniambia telemka na ushuke chini kwa kasi na haraka, kweli nikashuka chini haraka, niliposhuka chini akaniambia haya potea usionekane mbele ya macho yangu, (lakini yeye bado amefumba macho) nikamuuliza napotea vipi, akaniambia potea kwa kuvuta hisia (meditation) sababu unaweza ukawa kitu chochote kwa kutumia hisia zako.kweli nikavuta hisia (meditation) nikawa kama vile sionekani, kisha kikakaa kimya, alipoona nimekaa kimya akaanza kunitafuta ndani ya kile chumba, lakini kila ninapojificha ananifuata, ila wakati huo mambo yote yanaendelea yeye anayafanya akiwa amefumba macho, nilipoona anazidi kunifuata nikazidi kujificha zaidi mpaka nikajibadirisha na kuwa kitambaa chepesi, lakini bado akawa ananifuata, yaani akawa kama vile bado ananiona, nikahisi labda ananifuata sababu bado napumua ikabidi nibane pumzi ili nisiheme, lakini bado akawa ananifuata,

Nikaona hili zoezi la kupoea mbona kama linataka kunishinda, ikabidi niende juu kabisa kwa kasi ya ajabu, baada ya kuwa nipo juu hewani viungo vyangu vilianza kupotea mikono yangu na miguu vikawa havionekani mwisho na mimi mwenyewe nikawa sijioni,yaani nikapotea mwili wangu wote, nikawa sionekani hata kwa macho yangu mwenyewe, baada ya kuwa nimepotea nilishuka polepole hadi kwenye mguu wa yule mwalimu wa kijini, wakati huo yeye bado ananitafuta,lakini hanioni nilikaa kwenye mguu wake badae nikaona anatikisa mguu ikabidi niingie ndani ya kidole chake,kisha nikatulia, alinitafuta bila kuniona mwisho akafumbua macho yake na kuanza kuangalia ni wapi nilipo, alipoona kimya wala sionekani akaanza kuniita lakini sikuitika,

Baada ya kuona ukimya umezidi,nilimuona ameanza kuwa na wasiwasi, alikata unywele wake kisha akaupuliza ule unywele ukaanza kupepeluka ndani ya kile chumba badae nikaona ule unywele ilawezekana ni mbinu ya kunitafuta, nikakifanya kile chumba kiwe na upepo ili ule unywele wake uwe unazunguka tu,mule ndani,

Badae akaona bado haisaidii aliamua kusema mwenyewe kwamba jitokeze, ilibidi nijitokeze kisha akaniambia hongera kwa kuwa na uwezo mkubwa kupita kiasi sababu ni wachache sana ambao huwa wanaweza kujificha kwa haraka, yule mwalimu wa kijini alinyoosha mkono wake na ikaja karatasi nyeupe,kisha akanikwaruza mkononi mwangu na nikatoka damu, aliniambia niipanguse ile damu kwenye kidole changu harafu niandike jina langu na la baba yangu kwenye ile karatasi, nikawa nimeandika Saad Samweli; lakini kwa kutumia damu, baada ya hapo yule mwalimu wa kijini alitoka na ile karatasi, badae Salha alikuja na kuniambia naona umefaulu vizuri" nikamuuliza ile karatasi niliyoandika kwa damu yangu inakazi gani? Salha akaniambia hiyo ni posa, sababu ulisema utanioa, Dah! nilianza kuwaza,sababu hata kumwambia kwamba nitamuoa, mimi nilimwambia ilimladi akubali nilale nae sasa haya mambo ya kujikuta nimetoa posa bila hata kutegemea. Dah!!! Lakini sikuwa na namna,

Nikamwambia Salha uliniahidi utanisaidia kuwatafuta wenzangu haya twende ukanioneshe walipo, lakini wakati huo nilikuwa sielewi chochote kinachoendelea kule nyumbani kwetu, Salha akaniambia kuna vitu inatakiwa ujifunze kabla ya kuondoka, Salha na yeye akaanza kunifundisha namna ya kutumia nguvu nilizonazo, kama vile kupambana na wachawi au kuwaona, hata pale ninapokutana na adui kwa ghafla,

Salha akaniambia kwamba yule kiongozi mkubwa ni baba yake na ndio mfalme wa eneo lote lile, kwahiyo Salha ni mtoto wa mfalme, Salha akanifundisha mambo mengi, baada ya hapo tukatoka kwenye kile chumba, na kuelekea sehemu ambayo wapo wazazi wa Salha, Baba yake na Salha akaniambia inaonekana upo vizuri kijana,lakini tutaona kwenye mtihani unaofuata...

Inaendelea... Sehemu Ya 8

~Daudi~

Tukaondoka na Salha hadi nje ya lile jumba, lakini cha ajabu jua lilikuwa lipo palepale inamaana kule jua huwa halizami, Salha akaniambia twende nikupeleke kule ambapo walipo marafiki zako, tukapanda ule mtumbwi wetu ambao umebadirika na kuwa wa kifahari, kisha tukaelekea kule walipo Riziki na Goma, wakati tupo ndani ya ule mtumbwi nikamuuliza Salha kwani huu mtumbwi huwa unaendeshwa vipi, Salha akaniambia unapotaka kuuendesha huu mtumbwi inabidi hisia zako na mtumbwi ziwe kitu kimoja,hapo ndipo utaweza kuuongoza huu mtumbwi,

Nikawa nimepata elimu kidogo namna ya kuuendesha ule mtumbwi, ilikuwa ni mbali sana kutoka eneo lile hadi kule walipo, lakini tulitumia muda mchache tukawa tumefika. lile eneo lilikuwa katikati ya bahari huko chini ya bahari, tulitelemka kutoka kwenye mtumbwi na kuanza kutembea kwa miguu, lakini ilikuwa ni sehemu ya kutisha viumbe wa ajabu na sauti zenye kutisha zilikuwa zikisikika, lakini pia yale maeneo yalikuwa ni machafu sana, ilikuwa kama sehemu ya magereza, yalikuwepo majengo marefu harafu yana vyumba vingi, tulianza kuingia jengo moja baada ya jingine nikamuuliza Salha kwani huku huwa kuna nini akaniambia huku ni magereza sehemu ambayo huwa wanafungwa wale ambao wanaingia kimakosa katika mji wetu,

Ghafla tukaanza kufuatwa na wale wanyama wa ajabu na wasioeleweka mimi niliogopa sababu walikuwa ni wengi na wanatisha, Salha akaniambia usiogope wala usiwapige na usiwasemeshe, tukaendelea kwenda tukaingia jengo moja tukawakuta Riziki na Goma wamefungiwa kwenye chumba, Salha akaniuliza ndio hawa unaowatafuta? nikamwambia ndio, Riziki na Goma walikuwa wamefungiwa mule lakini wao hawakutuona, nilitaka kuwasemesha Salha akaniambia waache kwanza twende tukaongee na msimamizi wa hili eneo, tukaelekea sehemu ambayo alipo huyo msimamizi, tulipofika tulimkuta myama wa ajabu harafu ni mkubwa na anamiguu mingi pamoja na mikono mingi, yule mnyama akasema karibu mwana wa mfalme naona umeniletea chakula kingine, (lakini kwa sauti kubwa kweli) Salha akasema hapana lakini kuna wafungwa nimekuja kuwachukua, yule mnyama akasema kuna ma,elfu ya wafungwa katika hili eneo je ni wafungwa wapi ambao unawataka, Salha akasema nadhani umeshawatambua, yule mnyama akasema kama umekuja kuwachukua wale wafungwa inabidi niwafunge mdogo na masikio pamoja na kuwatoa macho, Salha akasema niachie mwenyewe yote hayo nitayafanya mimi,

Yule mnyama alitoa inshala baada ya muda Salha akaniambia marafiki zako tayari wapo kwenye mtumbwi lakini utawachukua kwa masharti sababu inaonekana mmoja wenu huwa anajaribu kuja huku mara kwa mara na haijulikani huwa anakuja kufuata nini,lakini yeyote kati yao endapo atataka kutoa ushahidi kwa mdomo hakikisha unamfanya anakuwa bubu,na akitaka kutoa ushahidi kwa macho hakikisha unamfanya anakuwa kipofu, na akitaka kutoa ushahidi kwa masikio hakikisha unamfanya anakuwa kiziwi, lakini pia akitaka kutoa ushahidi kwa inshala hakikisha anakuwa kilema. baada ya hapo tukaondoka na Salha hadi karibu na mtumbwi Salha alinikumbatia na kuniambia mtihani unaofuata usije ukaniangusha nakupenda sana,kisha akapotea,

Ikabidi nielekee pale ulipo mtumbwi wetu lakini nikawakuta Riziki na Goma wamekuwa kama vile wameganda hawasemi chochote wapo kimya ndani ya ule mtumbwi, na mimi nilipokaa ndani ya ule mtumbwi nikaganda, hivyo wote watatu tukawa kama mazuzu,tumeganda na hatujielewi, tukawa kama tumezimia,

Baada ya muda tulikuja kuzinduka tukiwa juu ya bahari na mtumbwi wetu, kila mmoja anauliza tupo wapi, baada ya muda mfupi tukawaona wavuvi wenzetu wakiwa wanakuja na mitumbwi yao, walifika wakatuchua pamoja na mtumbwi wetu wakatupeleka hadi ng'ambo ya bahari wakaangalia usafiri wakatupeleka hospitali sababu wenzangu wao walionekana kudhoofika miilia yao, hivyo ikabidi wote tupelekwe hospitali kwanza. lakini huko hospitali mama yake na Riziki pia amelazwa, tulifikishwa hospitali na kuanza kupewa matibabu lakini watu walikuwa wanashangaa sababu ndio mara ya kwanza wavuvi kupotea siku kadhaa na kurudi wakiwa hai, kwahiyo kila mtu alikuwa na hamu ya kusikia tulichokutana nacho wakati tumepotea,

Wakati tupo hospitali mimi nikawa naona watu wa ajabu ndani ya hospitali,sababu mimi hata kiafya nilikuwa nipo vizuri sio kama wenzangu, nilianza kuona watu wanakuja na kuanza kula na wagonjwa pale hospitali, nilikuwa nashangaa mbona wanakuja watu wachafu na wana nywele ndefu harafu wanafika na kuanza kula bila kunawa, niliona watu wa ajabu ambao sikuwahi kuwaona, baada ya kupatiwa matibabu Riziki na Goma wakawa na uafadhali.

Mama alikuja pale hospitali akiwa na hofu kubwa lakini alinikuta ni mzima pamoja na wenzangu, ikabidi wote tuletewe chakula lakini wakati tumenawa tunataka kuanza kula wale watu wa ajabu walikuja na kusimama karibu yetu, mimi kwakuwa ninawaona nikawa nimetulia lakini Riziki na Goma wakaanza kula,lakini ile wanaanza tu,kula wale watu wa ajabu na wao wakaanza kula tena bila hata kunawa, mimi nilishidwa kula nikawa nawaangalia na kujiuliza inamaana Riziki na Goma hawaoni, Mh! mimi kwakweli sikula kile chakula, wauguzi wakaniuliza mbona hauli nikawaambia sipo sawa nitakula hata badae, mmoja wa wale watu wa ajabu alisogea karibu yangu na kutaka kunichoma na kidole chake katika jicho langu, nilikwepesha jicho na kuusukuma mkono wake, wale wenzie wote waliacha kula na kuanza kuniangalia, waliniangalia wakagundua kumbe ninaowaona, walitoka wote na kukimbia nje, wakati huo hakuna aliyekuwa anaona kinachoendelea,

Baada ya Riziki na Goma kumaliza kula watu walitaka angalau wasikie machache kuhusu kile kilichotukuta baharini, kwakuwa Goma ndio kiongozi wetu yeye alisema kwamba mtumbwi ulipigwa na mawimbi na kupoteza mwelekeo,ndio tukajikuta tumepotea, lakini Riziki alipoulizwa yeye alianza kusimulia A/z, kama ilivyokuwa, nikaona Riziki anataka kusema kila kitu, nilipoona Riziki anataka kutoa siri niliung'ata ulimi wangu kwa meno, Riziki alijikuta anaanza kuwa na kigugumizi na kushindwa kuongea, madaktar walijaribu kumpatia huduma labda atakuwa sawa lakini hakuna, badae alifika ndugu yake na Riziki na kumkuta Riziki hawezi hata kuongea kwakuwa na mama yake na Riziki alikuwa katika ile hospitali, ilibidi twende wote tukamuangalie, lakini Riziki alienda kumuona mama yake akiwa tayari ni bubu yaani Riziki wakati huo hawezi hata kuongea, mama yake na Riziki hali yake ilikuwa ni mbaya sana lakini nilipomuangalia vizuri mama yake na Riziki niligundua kwamba mama yake na Riziki kuna vitu vinatembea mwilini mwake,

Nikaona ngoja nijaribu kumsaidia lakini wakati nataka kumsaidia kupitia nguvu nilizonazo, wale watu wa ajabu wakawa wamekuja na kiongozi wao, yule kiongozi wao alifika na kunipulizia dawa, kisha nikakosa nguvu na kuanguka chini, nilipoanguka walinibeba lakini mmoja wao alibaki pale hospitali, kisha wakanibeba na kunipeleka katika mti mkubwa ambao upo karibu na maeneo ya pale hospitali...

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Siri Ya Mvuvi Na Bahari Salha alitoka na kwenda kuwaita wazazi wake, wazazi wake wakaja kwenye kile chumba na kukuta ile pete bado ipo chini... Inaendelea... Sehemu Ya 07+8  >>> https://gonga94.com/semajambo/siri-ya-mvuvi-na-bahari-salha-alitoka-na-kwenda-kuwaita-wazazi-wake-wazazi-wake-wakaja-kwenye-kile-c
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest