Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

NIPE YOTE DADY SEHEMU YA 50

3rd Aug, 2025 Views 90


Sherehe ilivurugika watu wakachanganyikiwa bwana harusi akanifuata na kuniambia "mke wangu yuko wapi?"

nilimuangalia kwa sekunde kadhaa na kujibu' "samahani nahisi kama sijakusikia vizuri unasema ?"

"Nakuuliza mke wangu yuko wapi maana wewe na team yako mlikuwa nae mda wote iweje apotee ghafla ?"

"We kweli chenga kwahiyo unataka kusema tumemtorosha au vp"

"ndio maana yake Naira hawezi kutoroka mwenyewe nyie nyote mnahusika sasa nikiwa kama mume wake halali nasema hivi namta mke wangu sasahivi "

Nilikucha mikono yangu na kumuangalia chini mpaka juu kisha nikamjibu" Siku zote nilikuwa nakuheshimu nikijua unaakili kumbe nilikuwa nakosea, kwahiyo umesimama hapa na mtumbo wako huo kama pakacha na kuniambia upuuzi wako unauhakika mimi ndio nimehusika?

Halafu naona umeshajipatia cheo kabla ya muda eti mume ,kaka ukijiangalia vizuri unaona kama unafaa kuwa mume wa Naira au umerogwa akili?'" nilivyoongea hivyo akapata hasira na kutaka kunipiga weee nikamwambua thubutu shika hata upinde wanguo yangu nikuoneshe kuzimu ilivyo mwana haramu wewe mfyuu.

Jamani niliongea hivyo huku nikiwa najiamini kuna ulinzi wakutosha ,kwanza Selim alikuwepo hivyo kivyovyote vile angenunua ugomvi .

Ila pamoja na Selim kuwepo eneo lile hakujua kama nimehusika kumtorosha Naira maana niliona akijua anaweza asinielewe basi bwana harusi akataka kunifanyia fujo .

Ney na Amaira wakawahi mabishano yakaanza Selim aliposikia nae akaja hakutaka kuuliza wala kuongea alinishika mkono na kunitaka tuondoke eneo lile , mara Dully akanishika mkono kuzuia nisiondoke .

Weee niliiona hasira ya Selim ndani ya sekunde chache ,alikasirika na kuongea " bro achia mkono wa mke wangu sasahivi"

"Siwezi kumuachia mpaka atakapo niambia mke wangu yuko wapi" alooh bila kuchelewa aliwekwa ngumi vurugu zikaanza uzuri watu walikuwa wengi wakawahi kuamua ugomvi na kututoa eneo lile maana tulijifanya kupanick kuliko kawaida .

Baada ya kutolewa pale na kuingia kwenye gari nikashangaa Selim ananiuliza " yuko wapi Naira mnauhakika ameenda sehemu salama maana anaweza kuonekana itakuwa shida" bila kupepesa macho nikamuuliza .

" unamaana gani kusema hivyo kwamba ninajua alipo au nahusika?"aliniangalia na kusema "Kwahiyo unadhani sijui kama mmemtorosha ?"

"Selim misijafanya"

"Acha ujinga naelewa kila kitu halafu huu mchezo mlio ufanya sio mzuri siku nyingine msije kurudia hiyo ni moja mbili unakesi ya kunificha maana ulitakiwa uniambie kila kitu vp kama leo ungepigwa unafikili ningemfanya nini huyo jamaa"

"Ungempiga kama ulivyompiga " aliniangalia bila kuongea akawasha gari na kuondoka mpaka nje ya hotel nikamuuliza .

"Vp mbona umekuja huku ?"

" Nimekuwa mbali na wewe kwa mwezi sasa hivyo ninahitaji kutumia wakati huu kuenjoy napia unapaswa kunilipa mshahara wangu kama bodyguard wako "

"Mh sawa ila hiyo yakukulipa umefeli kama ungetaka nikulipe basi ungehakikisha yule mpuuzi hajanigusa hata kinyweleo ila umekuwa mzembe mpaka akavuka mipaka yake so dear bodyguard nasikitika kukwambia kuwa umepoteza point zako .
Alicheka kisha tukashuka na kuingia ndani akalipia haoo tukaenda kujuvinjali, niliwatumia ujumbe Naira Ney na Amaira kisha nikazima simu .

siku mbili zilipita tukiwa hoteln huku nyumbani mama mkwe hakuambiwa wala hakujua niko wapi basi akawa akimtumia ujumbe mwanae anasema eti ninawiki nzima sipo nyumbani na mara ya mwiso niliondoka na mwanaume tena nikiwa nimevaa hivyo.

Selim akawa amemjibu kuwa muache afanye kile anachoona nisawa siku akichoka atatulia 😂angejua kama tuko wote wala asingejisumbua kutuma hizo jumbe zake .

Basi wiki iliisha tukiwa wenyewe na tulikaa kwa amani kwasababu tulijua Jabir yupo pia kulikuwa na camera ambazo zilisetiwa mpaka kwenye pc ya Selim hivyo kila kilichokuwa kinaendelea nyumbani tulikiona .

Upande wa Naira baada ya kutoroka alienda nje ya mji na kukaa hoteln tukawa tukiwasiliana kama kawaida.

Kwa Amaira yeye alikuwa anateseka na mapezi huku ex anamsumbua kule mr kachumbari nae anamsumbua na huku anajisumbua kumuwaza asie muwaza yaani vurugu mechi.

Tulikaa hoteln mpaka pale tulipoona sasa tunatakiwa kurudi nyumbani, kwakua mara ya mwisho niliondoka na gari langu na Selim hakuwa nyumbani tukawa tumerudi na gari yangu kufika mama mkwe si akajua ni mimi maana mda wote alikuwa hajui kama kijana wake amesharudi na niko nae .

Basi hata kabla sijashuka akaanza kufoka malaya wewe sijui unadanga nakwambia nitakutoa kwenye maisha ya mwanangu mara anashangaa tunashuka wawili, akaaa kimya kwanza huku akimeza fundo la mate 😂.

Nilitembea kwa madaha na kumsalimia hakujibu akauliza "Selim umemtoa wapi huyu mchafu wa tabia "

Selim alishusha pumzi na kuniangalia kisha akajibu "Nimemtoa kwa mwanaume wake ambae ni mimi,mh mmeshindaje zasiku "

"Subiri mnataka kuingia wapi ? huwezi kuingia ndani kama hujaniambia huyu mwanamke alikuwa wapi maana mara ya mwisho katoka hapa anasema ameenda kwente harusi sasaivi unasema kwamba umemtoa kwa mwanaume wake ambae ni wewe hii yote ni kwasababu unamfichia makosa sasa nikiwa kama mama yako humu ndani haingii mpe talaka yake aondoke"

"Mama nimekwambia nilikuwa kuwa nae hivyo ondoa shaka na tuingie ndani"

"Selim nimesema hivi nikiwa kama mama yako na kwa mamlaka aliyoniachia baba yako marehemu nikichanganya na yakwangu na sema hivi muache huyu mwanamke hakufai wala hatufai"

"Mama umri wako uneshasogea ukiongea utapata kizungu zungu kwahiyo ingekuwa kama ungeingia ndani ukapumzika ,na kuhusu huyu asiefaa achana nae napenda visivyofaa ndio maana hadi leo niko nae"

Alimaliza kuongea akanishika mkono na kuingia ndani mama mkwe nae akaingia huku akifoka tulifika seblen tukakutana na Nasra akainuka na kutusalimia tukaitikia kwa furaha pale akatusifia kuwa tumependeza sana nikajibu asante na kuongea na dada wa kazi kidogo kisha nikaingia Chumbani.

Siku hiyo ilipita kesho yake Nasra akaomba kuongea na mimi sikuwa na shida nikaenda kwake na kumsikiliza, " Norah samahani kwakuchukua mda ako ila nimekuita hapa ili kuongea na wewe mambo kadhaa napia ninahitaji msaada wako kama ndugu yangu."

nilitabasamu na kujibu"ondoa shaka na kuwa na amani kusema chochote" alikaa kimya kwa mda nikaona machozi yanamtoka nilishtuka na kumuuliza shida nn mbona analia ? alinishika mikono na kusema

Itaendeleaaaaaa
KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NIPE YOTE DADY SEHEMU YA 50  >>> https://gonga94.com/semajambo/nipe-yote-dady-sehemu-ya-50
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest