Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

SIMULIZI : NYOTA YANGU SEHEMU 13

3rd Aug, 2025 Views 28



ENDELEA......
Baada ya kuudaka mkono wa Samir wote walinishangaa. Taratibu nilishusha mkono wa Samir, Samir alikuwa ananiangalia kwa hamaki na Samira alikuwa ametulia nyuma ya mgongo wangu.

"I'm sorry". Nilimuomba Samir msamaha.

"Tangu lini mwanamke akawa juu ya mwanaume, hii ni ndoa au ndoano". Wifi Najma aliongea hayo.

"Kelele na wewe, unaongea Nini?". Mama alimfokea Wifi.

"Si unaona lakini anamzuia mumewe kufanya anachotaka. Kuna ndoa hapo mama kama ameanza kudaka mkono wa mumewe".

"Baba Samir nisamehe". Nilimuomba Tena msamaha Samir. Samir hakunijibu. Aliondoka kuelekea juu chumbani.

"Nisamehe mama". Nilimuomba mama mkwe wangu msamaha, mama alinisogelea na kunishika shavuni kwangu huku anatabasamu alimaanisha amenisamehe.

"Nilimshika Samira vizuri na kumkokota pandanisha nae juu chumbani kwake. Nilimfikisha chumbani kwake. Nilimlaza kitandani nikamfunika vizuri shuka. Nilipotaka kuondoka Samira alinishika mkono na kuzungumza.

"Tafadhali usiniache, usiniache". Aliongea kama vile anaweweseka. Nilikaa kitandani pembeni yake. Nilianza kumbembeleza. Alipitiwa na usingizi ndipo nilitoka chumbani kwake.

Nilienda chumbani kwangu nilimkuta Samir amekaa kitandani amechukia balaa. Nilikaa pembeni yake na kuegemea bega lake. Niliushika mkono wake Kwa utaratibu na kuanza kuupapasa mkono wake.

" Mume wangu". Kwa mala ya kwanza Nilimuita Samir mume wangu na yeye bila hiana aliitikia Kwa sauti nzito ya dume la mbegu.

"Nisamehe kwa kukuzuia kumuadhibu mtoto".

"Ni sawa".

"Ila itoshe Sasa. Naomba usitumie hasira pale anapokosea, huenda Samir ameshakuwa sugu na ndo maana hata hakuogopi kabisa. Tunatakiwa kumfundisha Kwa upendo huenda atabadilika na sio kutumia nguvu".

"Nimekuelewa na ni kweli upo sahihi". Baada ya kuyamaliza Mimi na Samir niliingia zangu bafuni kuoga na baada ya hapo nilipanda zangu kitandani.

Samir aliniambia nisogee karibu yake. Bila hiana nilimsogelea, alinilaza kifuani kwake. Nyie nilijihisi nipo paradise. Samir anakifua kizuri acheni kabisa. Basi nilikuwa nayasikilizia mapigo ya moyo wake yanavyodunda. Niligundua ameanza kunipenda maana yalikuwa yanadunda Kwa Kasi sana kama yangu tu 😜.

Tulilala wenyewe mie na mume wangu. Usiku wetu ulikuwa mzuri ni usiku wa wapendanao.

Palikucha asubuhi kama kawaida nilimuandaa mume wangu kwaajili ya kwenda kazini na baada ya hapo nilienda kusaidiana na dada wa kazi kuandaa chai. Baada ya Kila kitu kuwa sawa nilienda chumbani kwa Samira pia. Nilimkuta ameamka anajinyoosha. Alivyoniona alikunja uso.

"Umeamkaje mwanangu?". Nilimuuliza Samira huku usoni mwangu nikiwa nimepambwa na tabasamu Bomba.

"Nilishakwambia achana na maisha yangu, mbona una shobo wewe?". Samira aliongea Kwa paniki ila hata sikumjali.

Aliinuka pale kitandani alienda chooni. Nilianza kuandika kitanda chake. Samira alitoka chooni na kunikuta naandika kitanda alipotaka kunizuia nilimstopisha Kwa mkono wangu Tena nilikuwa serious kabisa sicheki.

"Kwaiyo unataka uendelee kulala sehemu kama panya?". Ona chumba kilivyo. Samira ujue wewe ni mtoto wa kike, Leo kesho una kwako hii aibu utaiweka wapi. Jifunze kuwa msafi, sio usafi wa nje tu kuvaa, kusuka ili uonekana umependeza, hata ndani kwako jitahidi usafi. Ona chumba kilivyo kama wanaishi panya. Ona mpaka vichupi vilivyozagaa chini, ona hayo makaratasi". Ni kweli chumba Cha Samira kilikuwa kichafu balaa. Ni kawaida mpaka asafishe dada wa kazi.

"Bhana wewe achana na maisha yangu".

"Nishazoea hiyo kauli Yako. Huna jipya". Niliyasema hayo na kuendelea kutandika kitanda. Samira alitoka chumbani Kwa hasira. Na Mimi baada ya kumaliza kutandika nilielekea chumbani kwangu. Huko nilimkuta Samir ameshaamka anajiandaa. Nilimsaidia kumuandaa yaani mahaba yalikuwa ndindindi. Samir alikuwa ananiangalia tu usoni mwangu na mie nilikuwa busy kumfunga vishikizo vya shati na baada ya hapo nilimtengeneza kola la shati ndipo nilimshtukia kuwa ananiangalia. Tulitazamana usoni Kwa muda kidogo.

Samir alianza kunisogeza kichwa chake usoni mwangu aliponifikia Kwa ukaribu sana nilufumba macho. Samir alinibusu kwenye paji la uso. Msisimko nilioupata jamani 😜. Hakuna busu tamu kama la kwenye paji la uso Huwa Lina ka filling flani hivi yaani unajikuta wewe ndo alfa na omega Kwa Mr wako. Busu la kwenye paji la uso limebeba upendo wa dhati na hisia za kweli kabisa. Ukiona mwenzi wako anapenda kukubusu hapo nakuhakikishia ujue unapendwa kinoma Yani.

Basi filling niliyoipata ni Ile ya alfa na omega. Nilihisi Raha ya ajabu. Baada ya Samir kunibusu alinikumbatia na mimi nilipokea kumbato lake.

Siku zilikatika. Huku Jafari nae akiendelea kunisumbua. Sikuwa na namna zaidi ya kuendelea kumtuliza Kwa pesa. Jioni Moja nilikuwa na shamla shamla za kuandaa chakula jikoni na mdada wa kazi japo Mimi sikuwa mpishi ila nilikuwa namsaidia vitu vidogo vidogo.

Mama mkwe nae alikuwa na heka heka zake mwenyewe. Siku hiyo tulipika chakula kile anachokipenda mume wangu. Baada ya Kila kitu kuwa tayari niliingia chumbani kwangu. Nilihakikisha ninavaa vizuri Kwa kupendeza. Tangu nimeolewa nilikuwa navaa nguo za kunistili vizuri maana ndiyo nguo milizokutana nazo kabatini. Sio kwamba familia ya Samir ilikuwa imekolea dini sana ila nilifundwa mke wa mtu lazima ajistili. Mwili wake anafaa kuuona mume wake tu.

Basi nilivalia gauni langu refu la pink na mtandio wangu mweupe. Nilijipodoa vizuri usoni maana kwenye maswala ya kupodoka kwangu sio haba kabisa. Nilipendeza kweli kweli. Nilivalia Vito vyangu vya thamani na kupulizia marashi yangu. Baada ya hapo nilitandika vizuri chumbani na kumwagia mauwa mekundu huku mengine niliyachora Kwa maandishi yasemayo(I LOVE MY HUSBAND SAMIR).

Nilipohakikisha kumenoga nilitoka chumbani nilitoka. Mama mkwe alivyoniona nimependeza hakuacha kunisifia. Wifi Najma alibaki kunishangaa tu naona alikuwa anasema tu moyoni kumbe wifi yangu ni chombo ya kwendraaaa 😅😅😅.

Muda mchache tulisikia honi ya gari. Tulijua Moja Kwa moja ni baba mjengo. Haraka nilimpandisha chumbani kwangu na kujibanza nyuma ya mlango. Dadika chache mlango ulifunguliwa aliingia Samir kabda hajakitalii chumba nilimuwai na kumfumba macho Kwa mikono yangu.

"Forever your mine. Surprise my husband". Niliyasema hayo na kuitoa mikono yangu machoni kwa Samir ...............PENZI PENZINI SASA YAANI NI FULL MAHABATI🥰💃.....BADO NDEFU SANA WADAU WANGU.KWA BEI YA 1000 UTAISOMA KWA RAHA ZAKO.

NAMBA YA MALIPO 0743770612 JINA JOFREY.

UKISHALIPIA NICHEKI WHATSAPP KWQ NAMBA 0683009150..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SIMULIZI : NYOTA YANGU SEHEMU 13  >>> https://gonga94.com/semajambo/simulizi-nyota-yangu-sehemu-13
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest