Yaan nilishangaaa kumbe alilipwa laki moja tu huyu babu mbona anadhambi hivyo kumbe mimi nateseka nashindwa kufurahi na watoto wangu na mwanaume wangu , kwa sababu ya laki moja tu eeeh mungu weee huyu mzee ni njaa au ndo laana za mizimu yakee
Juddy alimwambia fanya unavyoona sawa nachojua mie hatukurusha jini kwa huyo maraya zaidi ya kuufungia mwili kwenye chupa basi !! "
Alianza tena kuondoka yule.mzee akacheka akamwambia
"We bint wewe kumbe huna akili kiasi hicho kwahiyo ulitaka nikuambie kila kitu kazi inavyofanya??"
"Nilikupa pesa zangu ,nimekupa pesa na tulielewana imekuwaje unanigeuka??"
"Nimekundua huyu mtoto hakuwa na kosa lolote wewe na uhuni wako ndio ulisababisha ukamkosa mwanaume wako"
Juddy alikuwa mbishi na alisema wafanye Vyovyote wanavyotaka wao
Inno alimuita akamwambia utarudishiwa pesa zako zote juddy, embu tulifanye hili lisiwe gumu we bint!!"
Alivyoona inno anamuomba ndo akazidi kiburi ,alimsonya na kuondoka zake tena huku anarusha maneno ya kashfa kwetu wote
Juddy alikuwa na hasira mnoo hata sijui hasira zake zilitoka wapi wapi aiseee
Huwezi amini Juddy aliondoka akamuacha hata na huyo zakia mwenyewe , hakutaka hata kugeuka nyumaa , tulibaki tunatazamana tu bile neno lolote
Hayaa nawasikiliza nyie!!!" Yule mzee alituuliza huku anatutupia macho kwa zamu,
Inno alichukua simu yake akapiga nyumbani, aliwaelezea kila kitu hata wao waliona ugumu kweli kweli
Mama mkwe aliomba kuongea na huyo mzee akamuuliza hakuna njia nyingine baba
Aliambiwa njia ni mbili tu kutoa yeye akawa salama au mimi nae akadhulika , mama akasema embu nipeni siku ya leo na kesho nitatoa majibu lazima nizame kwenye maombi..
Alex alikasirika akamwambia mama mbona tumepoteza sana muda tunazidi kupoteza mudaa salma anaumia ujue mama alijibu ni leo tu alex naomba unisamehe
Nilimuomba alex akubali kwa kushika mkono wake huku natikisa kichwa alikubali lakini kishingo upande sana
Kesho yake mama alipiga simu akasema amekwenda kuongea na juddy kule kazini kwake lakini amesema huo muda hana yaan yeye mawazo yake huyo mganga hawezi kufanya kitu mpaka yeye mwenyewe akubali kutegua basi mama akasema kiukweli mungu ndio anajua yote tumemkabidhi yeye
Naomba mje na salma wangu akiwa mzima kabisa yaan najuta ile siku ya kwanza kumkaribisha juddy kwenye nyumba yangu najuta sanaaa !!"
Mama alitoa baraka zake , yule mzee akasema tunaanza kazi usiku wa leo kuna baadhi ya vifaa vinatakiwa vinunuliwe , akawa amemuelekeza inno sehemu ya kununua kuna duka la asili lipo kibaha kule
Inno alienda akaja na Nguo kama shuka shuka hivi nyekundu na nyeupe
Pembe la ng'ombe ,mafuta ya kondoo aliambiwa
Na mbuzi mweupe akaja navyo vyotee
Baada ya kufika yule babu akasema kuna vifaa vingine vipo hapa hapa mtavilipia ,yaan huyu mzee pesa zote zile alipewa bado alisema tumpe za vifaa khaa anatamaa huyu mzeee duuh
Alisema sijui kucha za simba ,sijui yeye hizo kucha za simba alizitoa wapi??
Yaan alitaja ma vitu mengi ya ajabu ajabu sanaaa
Lakini tulifata tu unafikiri tutafanya nini sasaaa ??
ITAENDELEA....
KWETU morogoro.