"Sitaondoka nitakuwa na nyinyi siku zote na wapenda sana.
Shalon akimkumbatia Dala kwa furaha kubwa na siku hiyo alikuwa ni mtu mwenye furaha sana baba yake na Irene walikuwa watazamaji na kutabasamu .
Max alisogea karibu yao na kusema .
" Haya shalon muda wa kurudi nyumbani umefika mambo mengine utaenda kuongea na mama ukiwa nyumbani.
" Sawa baba.
Max alibeba vifaa vyao, shalon hakutaka kukaaa mbali na Dala alimshika mkono wakaongozana pamoja mpaka kwenye gari.
" Max, Dala mimi sitaongozana na nyie acha niwahi nyumbani kwangu. Irene aliwaaga
" Sawa kwakuwa Dala yupo kila kitu kitakuwa sawa.
" Dala tunakutegemea kwenye hili mpaka mambo yatakapokuwa sawa.
" Usijali dada Irene nipo pamoja na nyie kwenye hili.
Iren aliondoka na Max, Dala na Shalon wakipanda kwenye gari huku Dala akiwa kampakata shalon na kumuonyesha tabasamu pia shalon alikuwa akitabasamu huku akishika uso wa Dala.
" Masikini mtoto mdogo anaonekana alikuwa anapitia magumu kaone kalivyofurahi kanafikiri mimi ndio mama yake .
Alijisemea Dala huku akimuonea huruma akajikuta akimbusu na kumfanya shalon zaidi kufurahi na furaha ya sharon ilimpa faraja flani Max, na kuhusi alifanya chaguo sahihi .
Walifika nyumbani na kwenda moja kwa moja chumbani kwa Shalon kwaajili ya kumpumzisha.
Max alitoka chumbani kwa shalon akawaacha wanapiga story na Dala huku shalon akicheka kwa furaha.
Kwakuwa pale ndani hakukuwa na mtu wa kusaidia kazi ilibidi max aingie jikoni na kuanza kupika alipomaliza alipeleka chakula chumbani kwa Shalon.
" Shalon ni muda wa kula sasa.
Shalon alimuangalia dala alafu akamwambia
" Mama naomba unilishe.
" Shalon wewe ni mkubwa sasa kwanini ulishwe? Usimsumbie mama bwana.
" Hapana kama mtoto wangu anataka kulishwa nitafanya hivyo. Songea hapa binti yangu mzuri.
Shalon alinyanyuka na kukaa mapajani kwa Dala kisha wakaanza kulishana.
Walimaliza kulishana Dala akamuweka shalon kitandani na kumtaja alale. Alimbembeleza mpaka alipopitiwa na usingizi alitoka sebleni lakini hakuona mtu lakini alihisi kuna mtu jikoni ikabidi aende akamkuta Max anasafisha viombo.
Max alipomuona alimkaribisha.
" Dala karibu ukae.
" Shalon amelala nadhani naweza kwenda nyumbani.
" Kwanza nashukuru sana Dala sikutegemea kama ungemuonyesha mapenzi binti yangu mpaka hajashituka kuwa wewe sio mama yake mzazi. Pia nilikuwa
Naomba jambo moja kama litawezekana.
" Jambo gani?
" Naomba uhamie hapa.
" Hiyo itakuwa ngumu sana kumbuka naishi na mdogo wangu anahitaji uwepo wangu.
" Sawa tutafanya kitu kwaajili ya mdogo wako .
" Umefikiria kufanya nini? Usiniambie kuwa unataka nae aje huishi hapa.
" Lakini nilifikiria hivyo.
" Hapana sipendi mdogo wangu ashuhudie maisha inayoishi.
" Basi sawa ataenda boding alafu likizo tutajua.
Dala akafikiria akaona mbona kama hela yake itaishia kulipia ada .
" Sina uwezo wa kumlipia shule ya bweni.
" Gharama zipo juu yangu na pesa niliyokuahidi ipo palepale.
" Basi sawa acha leo niende .
"Sawa.
" Naomba kesho usichelewe kuja maana Shalon huwa anaamka Mida ya saa nne ningependa muda huo uwepo hapa.
" Nitajitahidi kufika mapema kabla ya huo muda.
Max aliingiza mkono kwenye mfuko wake wa suruali akatoa Wallet na kutoa kiasi cha pesa.
" Shika hii.
" Ya kazi gani?
" Utafanya nauli muda umeenda sana.
" Ninayo.
" Naomba upokee hii tafadhali.
Dala alipokea ile pesa alafu akaondoka.
Max alienda chumbani kwa Shalon akaenda kusimama pembeni yake , alimuangalia aliona jinsi shalon alivyokuwa Kalala usingizi mzuri wa amani na sura yake ilikuwa na tabasamu ilionekana alifurahishwa na kitendo cha kukutana na Dala akijua ndio mama yake .
Max alimfungulia vizuri kisha akatoka chumbani na kwenda sebleni kuangalia mpira.
Kwa upande wa Dala alifika nyumbani kwake alikaa na mdogo wake na kumueleza kuwa amepata kazi mpya.
" Shakira mdogo wangu nimepata kazi mpya .....
Kabla hajamaliza kuongea Shakira alidakia.
"Subiri kwanza, kazi iliyopata niya usiku?
" Hapana....
" Afadhali sikuwa napenda kazi zako za kutoka usiku unarudi asubuhi watu walikuwa wanakusema vibaya kuhusu wewe.
" Achana na mambo ya watu . Ila kazi niliyopata sitakaa hapa na wewe unatakiwa kuhama shule unaenda kusoma shule ya bweni.
" Dada unapesa ya kunipeleka huko?
" Usijali kuhusu hilo kila kitu kitaenda sawa.
Shakira alimuangalia dada yake huku akiwa na mashaka .
" Mbona unaniangalia hivyo?
" Hapana .
" Basi nenda Kalale kesho tuamke mapema nikupeleke sehemu ninayoenda kufanya kazi na ikiwezekana swala la kwenda shule lianze mara moja .
" Sawa.
Shakira alinyanyuka na kwenda kuandaa kwaajili ya kulala.
Usiku max akiwa alikuwa amepigiwa na usingizi sebleni mara alihisi kama anatingishwa. Alifumbua macho kuangalia alimuona Shalon kasimama huku akifikicha macho.
" Binti yangu kipenzi mbona upo hapa?
" Mama yuko wapi? Max alinyanyuka kwenye kochi akakaa.
" Mama.... Yupo.....
Hayupo chumbani nimeenda kuangalia hakuna mtu , dad niambie mama yangu ameondoka ameniacha tena , mama yangu hanipendi?
Aliongea shalon kwa sauti ya kutaka kulia.
Max akimvuta binti yake akamkumbatia .
" Hapana mwanangu mama yupo.
" Lakini hayupo ndani.
" Nisikilize nikwambie mama yako kaenda kuchukua vitu vyake vyote kesho mapema sana atakuwa hapa.
" Kama asipo kuja.
" Ni lazima aje sababu anakupenda sana.
Shalon aliachia tabasamu .
" Sasa twende ukalale.
" Nitaenda kama utalala na mimi.
" Sawa mrembo wangu.
Max alizima taa wakaelekea chumbani kwa Shalon, shalon alipanda kitandani max akamfunika vizuri na kuanza kumsomea kitabu cha hadithi mpaka usingizi ulipompitia.
Na alikosa usingizi alikaa huku akiwa anamfikiria mke wake jinsi alivyomua cha na kuonekana hana shida kabisa kuhusu wao na wala hajali pia alijiuliza itakuwaje kama Dalah hataweza kukaa muda mrefu na shalon.
" Sijui nimwambie nini shalon ili anielewe maana sina imani sana na Dalah mwanamke muuza bar hivi anaweza kumpa maisha gani binti yangu? Hapa natakiwa kuwa imara na ikiwezekana baada ya muda flani nimwambie shalon ukweli kuwa Dala sio mama yake na asahau kuhusu mama mimi ndio kila kitu kwake.
*SEHEMU YA TANO*
MAX aliwaza sana mpaka akapitiwa na usingizi.
Kulipokucha aliamka mapema akachukua simu yake akasngalia saa .
" Saa mbili acha nimpigie simu Dala awahi kuja kabla shalon hajaanza kusumbua.
Alipiga simu ya Dalah ikaanza kuita. Baada ya sekunde kadhaa simu ulipokelewa.
Wakati huo ndio kwanza Dalah alikuwa anatoka usingizini.
" Hallow boss.
" Mbona kama bado upo usingizini.
" Hapana nimeamka muda kidogo.
" Naomba baada ya dakika kumi uwe umefika Shalon akiamka akuone ukiwa hapa.
" Dakika kumi?
" Ndio , jana usiku kanisumbua sana kuhusu wewe.
" Dakika kumi labda kwa ndege ila kwa usafiri wa huku kwetu wala nisikudanganye .
" Usipende daladala chukua taxi.
" Sawa lakini....
" Ni nauli au? Kama tatizo nauli nitakuja kulipa.
" Sawa boss, lakini vipi kuhusu mpango wa mdogo wangu?
" Kila kitu tuliongeza jana kwani umesahau?
" Nakumbuka kila kitu.
" Basi wahikuja na nimeshafanya mipango leo hii hii anaenda shule kuendelea na masomo.
" We Max unanitania au?
" Usipite muda njooni haraka.
Max alimaliza kuongea akakata simu. Dala kuanza kuhimiza Shakira afanye haraka wawahi kuondoka.
" Shakira fanya haraka tunatakiwa kuwahi kwa Max
" sawa dada lakini kama itakuwa salama kwako na kama sio salama naomba tuacha sitamani upate shida kwaajili yangu dada.
" Shakira niamini mimi kila kitu kipo sawa huko naenda kufanya kazi ya kulea mtoto tu na kuhusu shule tayari umeshatafutiwa
" Kwahiyo mshahara wako ndio unanilipia ada?
" Ndio.
" Kwani unapokea mshahara shilingi ngapi?
" Ohoooo naona sasa maswali yanazidi wewe jua swala moja la kusoma mambo mengine hayakuhusu.
Dalah alijibu kwa ukali baada ya shakira kuwa na maswali mengi.
Shakira alikuwa mpole alichukua kila kilichokuwa cha muhimu wakafungasha kisha wakatoka na mabegi yao.
" Nisubiri hapo napeleka funguo kwa mama happy.
" Sawa.
Dalah alipeleka funguo kwa jirani yao kisha akarudi kumchukua Shakira na safari ya kwenda kwa max ikaanza.
Walifika nyumbani kwa max wakamkuta Shalon na baba yake wamesimama nje wakiwa wanawasubiri.
Shalon alipomuona Dalah akimkimbilia na kumkumbatia.
" Mama ulienda wapi?
" Nilienda kumchukua Shakira.
" Kwani yeye ni nani?
" Mmmh ni mdogo wangu.
" Umemleta nije kucheza nae?
" Ndio leo utacheza nae .
Shalon alimuangalia ahakila huku akitabasamu ,
Shakira alikuwa anamshangaa dada yake kuitwa mama.
" Mama , dady kapika chai twende tukanywe .
Shalon alimshika mkono Dalah wakawa wanaingia ndani na kwenda kukaa kwenye meza ya dinning wakaanza kunywa chai.
Max alimaliza kunywa chai akanyanyuka na kusema.
" Dala nipo nje ukimaliza nakuhitaji kwaajili ya maongezi.
" Sawa nakuja sasa hivi.
Max alitangulia nje baada ya muda Dala alinyanyuka.
Shalon bali na Shakira nakuja sasa hivi.
" Haya mama.
Shalon alimuangalia Shakira huku akiwa anatabasamu alionekana kuwa na upendo na kuvutiwa kuwaona nyumbani kwao.
Dala alitoka nje akaangaza macho akamuona Max amekaa kwenye benchi bustanini. Alipiga hatua kumfuata.
" Niambie max.
" Ni kuhusu Shakira anatakiwa kuanza shule leo kwasababu yupo darasa la mtihani haitakuwa vizuri kumchelewesha.
" Asante sana max kwa kujali.
" Dala mahali mdogo wako na kumpatia kila anachotakiwa kupata na mimi ninatumai hivyo kwa Shalon.
" Usiwe na wasiwasi max nitamlea Shalon kama mtoto wangu wa kumzaa yani mwenyewe utafurahi mbona.
Max alimuangalia kuanzia juu mpaka chini kisha akasema.
" Nina mengi sana ya kuongea na wewe ila kwa sasa acha tumpeleke Shakira shule. Nenda kajiandaeni tuondoke.
" Sawa. Alijibu Dala kisha akawa anaondoka
Kabla hajafika mbali max alimuita.
Dala alisimama na kugeuka kumuangalia.
" Tunakwenda ni sehemu ya heshima naomba ubadili hiyo suruali yako uliyokubana ingependeza kama ungevaa gauni ya kukustiri maungo yako.
" Sawa.
Dala aliondoka lakin bado max akimsindikiza kwa macho . Dala alikuwa kabarikiwa umbo zuri sana hakika mwanaume Rijali hawezi kujizuia kumuangalia mara mbili mbili au kutokumtamani. Huenda Max nae alikuwa kwenye wakati mgumu.
Dala alienda chumbani akibadilisha nguo kisha wakachukua begi la Shakira kisha Shakira alimshika mkono Shalon wakaenda kupanda kwenye gari na safari ya kuelekea shule ilianza .
Walifika kwenye shule moja iliyokuwa nje ya mji lakini ilionekana ni shule nzuri sana na yenye mazingira ya kuvutia Shakira alivutiwa na muonekano wa ile shule.
" Shakira umeionaje hii shule? Max aliuliza.
" Inamuonekano mzuri nimepanda.
" Ok nimeshafanya malipo ya ada na kila kitu. Utapatuwa sare za shule na kila kitu kinachohitajika.
" Asante sana.
" Ukiwa na shida utanitafuta na hii ni namba yangu ya simu. Alisema max huku alimkabidhi kadi yenye namba zake.
" Asante sana .
Alishukuru Shakira huku machozi yakitaka kutoka.
" Jamani mdogo wangu umeona hii bahati iliyokushukia?
" Ndio dada .
" Unatakiwa kuwa makini pia soma kwa bidii.
" Sitakuangusha kwa hilo dada.
Baada ya kuongea waliagana na Shakira alafu waliondoka wakarudi nyumbani.
Usiku Dala na Shalon walikuwa wamekaa sebleni wakicheza na Max alikuwa akiwaangalia. Max alionekana kuwa na mengi ya kuongea na Dala lakini alishindwa sababu shalon hakumpa nafasi Dala alimganda na kumfuata kila anapoenda.
" Dala muda umeenda sana naomba ukambembeleze shalon alale.
" Sawa baba shalon. Shalon mama ni muda wa kulala twende zetu.
Shalon hakubisha aliongozana na dala huku wakiwa wameshikana mkono.
Alipanda kitandani ,dala alimbembeleza mpaka alipopitiwa na usingizi. Alipokuwa anataka kuondoka mara Max alifika.
" Shhhhhhi usije ukapiga kelele amelala.
" Ok njoo. Aliongea Max kwa sauti ndogo kisha dala alinyanyuka taratibu na kumfuata Max sebleni.
Dala alikaa kwenye kiti na kumsikiliza Max anachotaka kuongea.
JE NINI KITAENDELEAAA!! "
OFAAAA KUPATA YOTE NI 1000 TU
NJO....
WHATSAP 0755090082.