Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

MWANAMKE JEURI SEHEMU YA 05

3rd Aug, 2025 Views 2



MTUNZI: FRANK TITUS KAPINGA

SEHEMU YA 05

Mtu wa kwanza kufungua dimba alikuwa ni Afsa Ugavi. Alisubiri muda ambao Anshera alielekea ofisini kisha alimfuata. Kwakuwa yeye ni mfanyakazi wa ofisi hakutaka kubisha hodi, alisukuma mlango alizama ndani; Alimkuta Anshera akichati kwenye simu yake, akiwa anajizungusha kwenye kiti chake.
"Mwanasheria wetu mpya, habari yako binti mrembo" Mgavi alizungumza kwa uchangamfu akiwa anakaa kwenye kiti.
"Umeingiaje ofisini kwangu bila ruhusa? halafu nani amekuambia ukae kwenye kiti changu? Anshera aliuliza swali akiwa bado anajizungusha kwenye kiti chake.

"Duh! Kwani hujui kwamba mimi ni mfanyakazi mwenzio?... Mimi ni mkuu wa idara ya manunuzi. Ulitaka niruhusiwe na nani wakati hii ni ofisi yetu? na hiki ni kiti cha halmashauri yetu" Mgavi alizungumza akiwa anamshangaa Anshera.
"Soma pale juu, pameandikwaje?"
"OFISI YA MWANASHERIA MKUU" Mgavi alisoma
"Je wewe ni mwanasheria?"
"Hapana."
"Sasa hizo shobo zako unatoa wapi?..... Kwanini nyie wabongo mnashindwa kuheshimu ofisi za watu?. Ni sheria ipi inayoruhusu mfanyakazi aingie kwenye ofisi ya mfanyakazi mwenzie bila ruhusa?.... Je ikitokea kitu kimeibiwa humu ndani; nitalaumiwa mimi au wewe?"
"Nisamehe mwanasheria, tusifike huko. Mimi sijafika hapa kulumbana, nimekuja nina jambo langu"
"Jambo gani?"
"Hapo ndo penyewe sasa!! naomba unisikilize kwa makini"
"Sihitaji maneno mengi, go straight to the point"
"Am going jaman kah!! Nisimeze mate. Mwenzio nimekupenda. Natamani niwe rafiki yako wa kwanza hapa ofisini, lakini pia natamani uwe mwanamke wangu kimahusiano"
"Bro hawatongozagi hivyo, umekurupuka. Kwanza ebu nitazame vizuri.. Nikague kuanzia juu hadi chini"
"Tayari nimekucheck"
"Je una uhakika unaweza kupata mwanamke mzuri kama mimi?"
"Uhakika sina, ila si unaweza tu kunitunuku"
"Matokeo yako ya form 6 ulipata division ngapi?"
"Mimi sikusoma form five na six, nilipitia diploma"
"Haya toka toka toka ofisini kwangu! pumbavu wee!!.. Yaani mtu umepata division four halafu unataka kunipata mimi?. Mtu umepitia diploma, maana yake hujawai kwenda jeshini. Mwanaume umelegea legelege, hivi unapata wapi ujasiri wa kunitongoza mimi niliyepitia MAKOTOPOLA?... huniogopi? nyau wewe! ebu kwenda nje"
Mgavi alijisikia vibaya!! aliona mambo yashakuwa makubwa, haraka haraka alisimama kisha alitoka nje. Kimya kimya alirudi ofisini kwake pasipo kuongea na mtu. Licha ya kuaibishwa lakini hakumuambia mtu yeyote, aliuchuna kimya.
Mtu wa pili kumfuata Anshera alikuwa ni Muhasibu. Yeye baada ya kuingia ofisini kwa Anshera, hakuruhusiwa kukaa kwenye kiti, aliambiwa aeleze shida yake akiwa amesimama. Muhasibu alishangaa, hakutegemea mapokezi ya namna hiyo.
"Dada mgeni ndo mapokezi gani haya unanifanyia?" Muhasibu alilalamika
"Kama huna shida basi ondoka" Anshera alijibu
"Shida ninayo. Unajua nini mrembo?... Nitafurahi sana endapo kama leo hii usiku tutatoka out, tunywe, tule na tulale, nataka ujisikie furaha kufanya kazi kwenye halmashauri yetu. Kwa upande wangu mimi sioni hasara kupoteza pesa nyingi kwaajili yako. Vipi upo tayari?" Muhasibu alizungumza akiwa anatabasam.
"Unapokea mshahara kiasi gani?"
"Million 1"
"Hizo million moja wewe mwenyewe zinakutosha kweli?... umejenga? una gari? tayari umetimiza malengo ya maisha yako?... Hivi nyie wanaume mbona mna akili ndogo sana? Mtu una kipato cha million moja halafu unataka kutoka na mimi mwenye matumizi ya million 100, utaniweza kweli?... Sikiliza we jamaa, hako kahela kako nenda katafute mwanamke mwenye thamani ya elfu 20 kisha umtoe out, ikiwezekana umtongoze awe mkeo ili mtengeneze maisha. Ukijichanganya kwangu nitakula pesa zako halafu hutoambulia chochote, umenielewa?... Haya ondoka, nenda kacheze unakochezaga"
Muhasibu aliondoka mara baada ya kufukuzwa. Wafanyakazi wengi walijaribu bahati zao lakini waliambulia matusi na dharau kutoka kwa Anshera. Hakuna ambaye alikubaliwa, hata namba ya simu walinyimwa. Anshera hakuhitaji rafiki, mpenzi wala mtu wa karibu. Hakuhitaji kuzoeana na mswahili yeyote. Na kuhusu mapenzi, sio kwamba hakutaka mapenzi, ila hakutaka kupata mwanaume wa kibongo. Aliwadharau wanaume wote wa Tanzania, aliwaona hawana vigezo.
"Walidhani mimi ni jamvi la wenyeji na wageni au sio? ah ah ah kumbe hawanijui. Kwanza katika ofisi hii sioni mwanaume anayenifaa. Hakuna mwanaume atakayenipata ndani ya Babati hii, Manyara hii, mkoa wowote na nchi kwa ujumla. Nikitaka kuolewa nitaenda Marekani au ulaya kutafuta wanaume wa hadhi yangu." Anshera aliwaza akiwa amekasirika, alichoshwa na usumbufu wa wanaume wa kibongo. Licha ya kwamba siku hiyo aligombana na wafanyakazi wengi lakini hakuogopa wala nini.

*****
Ni mwezi mzima ulipita tangu Antura ashikiliwe na kituo cha polisi kwa kosa la kutaka kumbaka Anshera. ilikuwa ni kesi ambayo iliendeshwa kwa njia za hovyo hovyo tu. Kesi ilifika mahakamani lakini iliahirishwa kutokana na mlalamikaji (Anshera) kukosa ushahidi. Ilibidi hakimu apange siku nyingine kwaajili ya kusikiliza kesi hiyo, lakini kabla tarehe nyingine haijafika Anshera aliwahi kituo cha polisi kwaajili ya kuvunja kesi hiyo.
"Ndugu afande habari yako" Anshera alimsalimia afsa polisi aliyeshikilia jalada la kesi hiyo.
"Salama tu mwanasheria, vipi tayari umepata ushahidi?"
"Hapana. Na wala isikupe shida kwa sababu mimi ndiye mwenye kesi. Mimi ndiye nina uwezo wa kumfunga au kutomfunga mtuhumiwa"
"Una maana gani?"
"Waliotaka kunifanyia kile kitendo ni watu wengine, huyu mkaka aliyewekwa sero hausiki hata kidogo."
"Eeh! kumbe hahusiki? sasa kama unalijua hilo kwanini unamtesa namna hii?"
"Nimeamua kumkomesha tu ili ashike adabu yake. Unajua ni kwanini?... Ni kwa sababu wale jamaa waliotaka kunibaka walinichania nguo zangu lakini hawakubahatika kuona mwili wangu wa ndani, lakini yule mkaka wakati anakuja kunisaidia alinikuta nikijiweka sawa, kwa bahati mbaya alibahatika kuona kifua changu chote na kiuno changu! Nilikasirika sana, licha ya kwamba aliniokoa lakini sikutaka aone maungo yangu! Na ndio maana nimeamua kumuweka sero"
"Pole sana muheshimiwa, kwahiyo tunafanyaje sasa?... Tumuachie huru au inakuwaje?"
"Siwezi kumuacha bure bure!! Ni lazima alipe faini ya kuuona mwili wangu wa ndani. Nenda kamuambie hivi; Kama anataka nimuachie huru, inabidi anilipe faini million 5. Akilipa fedha hiyo tutagawana mimi na wewe kisha tutafuta kesi. Akishindwa kulipa ataendelea kusota mahabusu. Nafanya hivyo ili kumkomoa tu. Najua hana uwezo wa kunilipa, hana pesa zozote, ila ngoja nimkomeshe tu!! Ni heri ashindwe kunilipa ili aendelee kusota mahabusu" Anshera aliongea kwa kujiamini akiwa anatabasam, licha ya kwamba yeye ni mwanasheria lakini aliongoza kwa kuvunja sheria. Alijiamini kutokana na uzuri wa umbo na sura yake, ubora wa elimu yake ya Harvard, pamoja na ukubwa wa cheo chake serikalini.

Afande alitii maagizo ya mwanasheria wa halmashauri. Alielekea sero alikutana na Antura, Alimueleza kwamba ili aachiwe huru anapaswa atoe million 5. Antura alicheka sana kwa sababu alielewa nini kinaendelea. Alifahamu kwamba kesi hiyo ni ya uongo ila hakutaka kubisha sana, alikubali kulipa faini hiyo.
"Sawa nipo tayari kulipa"
"Eeh! we kijana umekubali kutoa million 5?" Polisi alishangaa
"Ndiyo, nyie si mnataka pesa? nyie si ndo wenye sheria na mamlaka? mnataka kutukandamiza sisi tusio na makosa, niko tayari kuwapa pesa zenu"
"Aisee! kwahiyo tukupe muda gani ili ututafutie pesa hiyo?"
"Muda wa nini? Kwanza mmenipotezea muda mwingi sana, nina mambo mengi ya kufanya. Nilidhani mtanitendea haki lakini kumbe hata nyinyi polisi hamna maana!! Nimegundua kwamba vyombo vingi vya haki ndivyo vinaongoza kwa kuharibu haki. Naomba tuelekee benki nikawape pesa zenu" Antura alijibu kwa kujiamini.

Ama kweli umdhaniaye siye kumbe ndiye. Afande alikosa pozi, alishindwa kuamini hata kidogo. Alimtoa Antura nje kisha waliungana na Anshera walielekea benki. Baada ya kufika benki Antura alitoa fedha million 5 kisha alimkabidhi Anshera. Na baada ya kukabidhi pesa hizo, jamaa aliondoka pasipo kuzungumza neno lolote, aliwaacha Anshera na Afande wakiwa wameganda kama midori vile!!
"Hivi huyu mtu ni kapuku kweli au anatuigizia?. Amepata wapi pesa zote hizi? kwanza anafanya kazi gani? mbona ananichanganya!!" Anshera alivurugwa na Antura.

USIKOSE NEXT EP....

Stori za wanaojitambua.
by Manshyne.

Whatsapp 0743857349.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MWANAMKE JEURI SEHEMU YA 05  >>> https://gonga94.com/semajambo/mwanamke-jeuri-sehemu-ya-05
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest