Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

NIPE YOTE DADY* *51~60* _______ SEHEMU YA 51

5th Aug, 2025 Views 143


Norah naumia sana,nimeharibu maisha yangu kwa ujinga wangu mwenyewe , nimeharibu mahusiano yangu na familia yote.

Baba hataki hata kuongea na mimi hadi ameamua kuniondoa kwenye kampuni , kinachoniumiza zaidi mpaka mama nae hataki kuniangalia mwanaume nilie zaa nae yeye pia hataki hata kutoa huduma za mtoto.

Yani kila kitu kimekuwa kibaya kwangu hapa nilipo sina hela kodi imeisha ,mtoto nae natakiwa kulipiwa ada shuleni . " aliongea kwa uchungu sana nikiwa kama ndugu yake nilijisikia vibaya na kumkumbatia huku nikimpa moyo.

Tuliongea kwa mda mrefu kisha nikarudi nyumbani na kukaa kuongea na Selim ili tuone ni namna gani tunaweza kumsaidia .

Baada ya maongezi machache tukaelewana kuwa tumpatie nafasi kwenye kampuni ya familia kuhusu kodi nikaona sawa tu nitamsaidia kulipa hata kwa miezi sita .

Baada ya hapo nikaenda nyumbani kuongea na baba ili ikiwezekana wamsamehe tu kila kitu kirudi kama kawaida maana toka alipofumaniwa na yule rafiki yake na baba mahusiano na baba yalikata kabisa hata akawa akimsalimia haitiki mama nae hivyo hivyo.

Basi nilifika baba akawa anacheza na wajukuu zake kwanza mimi nikaongea kwanza na mama " Mama samahani nimekuja leo kwa lengo la kuongea kuhusu Nasra "
"Amekutuma nini tena maana siku hizi mnaelewana wenyewe"

"Hapana sijatumwa na mtu ila najisikia vibaya kuona ule upendo wenu kwake umeisha hii sio sawa najua ndio alikosea ila hakuna mwanadamu mkamilifu kila mtu hukosea"

"Norah hayo mambo ukaongee na baba yako ndio mwenye hasira nae ila mimi nimeshaachilia "

"Hapana mama nakufahamu vizuri najua wazi bado mnakinyongo nae hivyo naomba kama mwanao msamehe tafadhali "

"We Norah nimekwambia sina kinyongo nae maana alifanya kwa mapenzi yake sasa nikaweke kinyongo ili iweje wakati ni mtu mzima aliejiamlia kujivua nguo"

"Haya sina mengi ya kuongea ila naomba ukaongee na baba muweze kumsamehe mtoto wenu yaishe maana mtamchukia hata lini au kosa lile linaondoa nafasi ya utoto moyoni."

Niliongea na kuinuka nikaingia jikon na kukaa chaumbea mwenzangu tukapiga story pale mpaka nilipoona baba ametulia ndipo nikaenda kuongea nae.

Nashukuru Mungu baba hakuleta mambo mengi zaidi akaniambia nisijali kila kitu kitakuwa sawa, basi nilipoona nimeongea nao wote nikarudi kwangu nakuendelea na ratiba zingine .

Juma tatu ilifika nikaandaa watoto vizuri wakaenda shule Selim akampitia Nasra wakaenda kazin, sikuwa na kinyongo au kutokumuamini tena maana niliona tayari amejifunza na anajutia alichofanya kwa hiyo kivyo vyote vile hawezi kufanya ujinga tena .

Kitendo cha kuelewana na Nasra ilikuwa furaha kwa mama mkwe maana mda mwingi Nasra alikuwa nyumbani kwangu ,vile visa vikapungua maisha yakawa vizuri mpaka tukaamua kumwambia ahamie nyumbani maana mtoto alikuwa anataka kukaa nyumbani kwangu mda wote nikaona kama mtoto atakaa nyumbani kwangu alafu mama yake akakaa mwenyewe niwazi atakuwa mpweke .

Familia ilikuwa kubwa yenye kujaa upendo na amani Nasra alionesha kunijali na kunipenda kuliko siku za nyuma basi bwana siku moja tulikuwa sherehe ya kutimiza miaka sita ya ndoa .

Hivyo tukaalika marafiki na ndugu kadhaa katika sherehe hiyo Ney akajitolea kupika yeye maana mwenzangu huyu alikuwa mpishi ,basi wakapika na kuweka mambo yote ya vyakula sawa .

Sasa katika zile heka heka za kupika na kuandaa vitu vya kusevia ,rafiki yake na Selim akawa anamuangalia sana mwisho akaja kuniuliza shem yule unamfahamu au mnaurafiki ?

Nikasema ndio nibest wangu kijana kasema sawa chakula chake kitamu sana , nikacheka na kumuuliza kitamu u umependa maana chakula anachosema kitamu hata hakijalika sasa anavyosema kitamu wakati bado hajala ni uongo huo .

Alicheka na kuondoka nikabaki najisema mwenyewe kijana kaingia kwenye dimbwi la mapenzi, sherehe ilifanyika pale watu wakala chakula mziki ukachezwa wakupiga story wakapiga ila Bwana Deo akawa bado bize kumuangalia Ney mimi na umbea wangu nikawa nahakikisha naangalia jamaa amependa au nini maana hakuwa hata akiongea na wenzake zaidi ya kumtolea macho mtoto wawatu.
Basi baada ya sherehe watu akaondoka Ney akawa anakusanya na kusimamia vyombo kuhakikisha vinawekwa katika hali ya usafi na salama .

Mara Deo akanifuata na kuniomba namba ya Ney nikacheka na kumzingua kidogo kisha nikampa ila huku nasubiri kichambo maana najua Ney akijua nimetoa namba yake atanichamba mpaka basi.

Basi bwana nilivyomaliza kumpa namba nikaingia ndani,ghafla Jabir akanivuta na kunisogeza pembeni ,nilishtuka na kuuliza" vp mbona tunavutana "

"Kwann umempa Deo namba ya Ney ?'"

"aaaa nimempa kwasababu ameniomba basi "

"Bina sijapenda huwezi kumpa namba yake bila kumuuliza mwenyewe " nilitaka kujibu akaondoka nikabaki nashangaa sasa kanuna nini au kutoa namba nako ni kosa ?

Nilijiuliza na kutembea kuelekea chumbani nikashangaa kuona Nasra na mama mkwe wamesimama wakiongea kama wanateta jambo la muhimu sana ,waliponiona wakashtuka na kujichekesha .

Sikutaka kuongea nikasalimia na kuingia chumbani kwangu ambapo nilibadilisha viatu na kutoka .

Nilirudi sebleni na kukaa na baadhi ya watu waliokuwa hawajaondoka , Ney alipomaliza kuweka vitu vyake sawa tukaungana nae nakuanza kupiga story za hapa na pale mpaka mda wa kuondoka ulipofika wakaondoka.

Kesho yake asubuhi niliamka na kufanya majukumu ya asubuhi kama kawaida Selim na Nasra nao wakaenda kazini, na mimi nilipomaliza kuweka vitu sawa nikaondoka .

Mchana nikiwa kazin simu yangu ikaita kuangalia namba ni ngeni nikapokea na kuuliza nani akajitambulisha kuwa ni rafiki yangu Jacob , niliposikia hivyo nikafurahi na kuongea na utani kidogo .

Jamani huyu Jacob ni rafiki yangu toka shule enzi hizo za A level na nimtu ambae tulikuwa tunaelewana sana ila tukaja kupotezana sasa kitendo cha kumpata kilinifurahisha sana .

Basi tuliongea na kupanga kuonana tukipata nafasi kisha tukaagana , siku zikapita sasa hiyo siku ya kuonana ilipofika nikatoka kazin na kwenda moja kwa moja tulikopanga kukutana .

Nilifika kwa bahati mbaya akawa amechelewa kufika ikabidi nimsubiri, nilikaa mda mfupi sm ikaita nikatoa nikijua huenda ni yeye amefika labda anataka kuniuliza nimekaa upande gani ila hikuwa yeye bali alikuwa ni............
KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NIPE YOTE DADY* *51~60* _______ SEHEMU YA 51  >>> https://gonga94.com/semajambo/nipe-yote-dady-51-60-_______-sehemu-ya-51
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

RATIBA YA SIMULI ZETU

Ratiba ya Simulizi

  • USINITANGAZE 02 ❤❤ 05-08-2025 19:00

Ratiba ya Simulizi

  • USINITANGAZE 03 ❤❤ 06-08-2025 04:00

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest