"Huwezi kuondoka namna hiyo ,nakukumbusha unatakiwa kutimiza ahadi yako "
alisema Winnie
" Ahadi ipi tena na tumeshacheza game pamoja hii inamaanisha hakuna ahadi nyingine yoyote "
aliongea Elian huku amekunja sura
" Oh kweli wewe na u CEO wako wote huo kumbe kichwa Nazi " aliongea Winnie huku anacheka
" Winnie tuheshimiane unaweza kuniita mimi majina ya ajabu "
alifoka Elian
" Ndiyo wewe kichwa Nazi ulikubali wewe mwenyewe ukiwa na akili zako timamu na bila kulazimishwa Sasa iweje saizi unikane bila hata aibu "
aliongea Winnie bila uoga hata kidogo Elian alimuangalia Winnie kwa hasira .
" Wewe ...."
Elian alishindwa kuendelea
" Nini ?"
Winnie aliongea huku ameshika kiuno
" Mmmh kama nilikuahidi basi nitatimiza ahadi yangu lakini kwa muda wangu sitaki kukumbushia kila wakati "
Elian alimpita Winnie akaingia ndani
" Mambo si ndo hayo Sasa "
Siku ya weekend Winnie na Elian walienda mgahawani
" Sehemu gani hii unaniletea ?"
Elian aliuliza kwa hasira
" Mmmh hii ndo sehemu ninayopendelea na nilipenda siku moja nije na mpenzi wangu "
" Kumbuka sisi sio wapenzi wa kweli na hii sehemu sio hadhi yangu hata kidogo "
" Usihukumu kitu ukiwa hujui chochote subiri uonje chakula Chao harafu utaniambie chakula cha hapa na hizo hoteli zenu za nyota Tano kipi kipo Bomba "
" Mama tatu kama kawaida Leo Fanya sahani mbili "
Winnie alitoa oda
" Leo naona umekuja na kidume sio mashoga zako waongeaji kama chiriku "
alisema mama tatu kwa utani
" Hahaha kwani unamuonaje mama tatu anafaa kuwa mume eti ?"
Winnie alikuwa busy kupiga story na mama tatu , Elian alikuwa kimya alimkata Winnie jicho la chini chini
" Anafaa kabisa huyo lakini naona kutabasamu sio mambo yake muda wote amenuna tangia afike mgahawani kama tunaugomvi nae " alisema mama tatu
" Ndo alivyo huyu mama tatu hata tusimlaumu sana kwani hukuwahi kusikia Kuna watu wanazaliwa bila bandama Yani Hawa huwa hawacheki kabisaaa"
" Hahahah basi kazi unayo binti "
mama tatu alitenga chakula alichoagizwa
" Nani anafaa kuwa mume ?"
Aliuliza Elian
" Si wewe au kuna mwingine hapa "
" Labda kwenye ndoto zako "
Elian alisogeza sahani alianza kuchezea kile chakula alikiangalia kwa kinyaa
Winnie muda huo alikuwa anakata matonge
" Acha kuchezea chakula ndo tabia gani hiyo kama hutaki kula si uache "
Winnie alitaka kuchukua sahani ya Elian , Elian alimzuia alichota kijiko kimoja akala.alijikuta anasikilizia utamu wa chakula
" Enhee niambie umekionaje chakula ?" Aliuliza Winnie
" Ni kitamu lakini ...." Elian alitaka kuweka kasoro ya uongo hakutaka kushindwa
" Lakini nini sema tu umeshindwa migahawa ya nyota Tano haina vyakula vitamu kama hivi vya uswahilini "
" Sawa nimekubali nimeshindwa ,umefurahi sasa?"
" Sanaaaa Yani hujui tu " Winnie aliongea huku anatabasamu
Baada ya kutoka mgahawani walienda beach lakini haikuwa beach ya kulipia Elian alizidi kujionea maajabu
" Kwanini tupo hapa tena ?"
Elian alimuuliza Winnie huku anakagua mazingira
" Kwani huoni watu wanafanya nini hapa maswali gani hayo tena Elian jamani ,twende tukakae pale chini"
Winnie alimvuta mkono Elian walienda kukaa chini
" Kwenye maisha yangu nilitamani siku moja kuangalia jua linavyozama upande wa baharini nikiwa na mpenzi wangu "
Winnie aliendelea kuushika mkono wa Elian
Elian alitabasamu ni kweli jua lilionekana vizuri sana likiwa linazama sio kama hakuwahi kuona jua likizama upande wa baharini maishani mwake bali alihisi vizuri kwasababu pembeni yake alikuwepo Winnie
Baada ya kuangalia jua likizama walirudi nyumbani
" Twende tukaangalie movie chumbani kwangu "
alisema Winnie
" Hapana nimechoka sana na wewe ndo sababu niache nipumzike maybe weekend nyingine "
Elian alielekea chumbani kwake
" Ameshaanza kukera Sasa "
Winnie aliingia chumbani kwake simu yake ilianza kuita mpigaji alikuwa ni Sonia
" Mambo shostiiiii " aliongea Winnie huku anajilaza kitandani
" Koma mtoto wa kike tangia lini mimi na wewe tukawa mashosti "
Sonia aliongea kwa kufoka
" Ndo yamekuwa hayo "
" Ndiyo wewe inakuwaje unahia kwa mwanaume hata humjui vizuri na hata kunishirikisha nikupe ushauri hukutaka "
" Nisamehe shoo sikutaka kukuongezea mzigo na ulikuwa na matatizo "
" Asante kwa kujali lakini sijapenda "
" Nisamehe shoga angu unajua ukininunia nitakosa amani " alisema Winnie
" Hata sijakununia shoga angu naanzaje kwanza kukununia nilikuwa tu na wasiwasi juu yako eenh niambie imekuwaje mpaka unamuamini huyo kaka namna hiyo ?" Sonia alimuuliza Winnie
" Basi tu najikuta namuamini afu sio mzinguajo kabisa si unajua wale watu wanaishi kizungu "
" Weee usiniambie kwahiyo shoga angu umejiopolea bonge la bwana "
alisema Sonia
" Mmmh usilolijua huyu kaka ni anaenda kwa muda na rtiba zake hataki kabisa kuharibiwa ratiba zake anajali lakini hayuko romantic kivule ila ngoja ni mnyooshe kidogo "
" Hehehe aiii ngoja nikaandae chakula kabla bi maza hajanijia juu"
" Sawa shoo basi tutaonana juma 3 kazini "
Winnie aliagana na Sonia
Jumatatu wakiwa kazini Sonia na Tracy walimuuliza Winnie mambo mengi kumuhusu Elian
" Unasema ana mtoto wa miaka 17 ?"
Sonia aliuliza kwa kupayuka walimu wote ofisini waliwageukia
" Samahanini "
Sonia aliomba samahani huku anacheka Cheka
" Ndiyo na ni handsome kama baba yake na ametokea kunipenda sana ila kwa Sasa ameenda kusoma marekani "
" Ila kuwa makini " alisema Tracy
" Hata msijali vipenzi "
Siku hazikawii weekend nyingine ilifika tena
" Leo tunaenda kuangalia sinema kwenye jumba la sinema sio nyumbani na baada ya hapo tutaenda kuendesha baiskeli " Winnie alimwambia Elian
" Kata kuendesha baiskeli kwenye plan zako "
aliongea Elian kwa amri
" Kwanini basi nikate na ratiba yangu ipo hivyo "
" Kwasababu siwezi kufnya mambo ya kitoto "
Elian aliendelea kusoma kitabu chake
" Sawa basi hatutaenda popote si ndo unachokitaka "
Winnie aliondoka kwa hasira
" Utakuwa umenisaudia sana "
Elian aliongea kwa dharau muda ilizidi kwenda lisaa limoja mpaka kufika jioni hakuwa amemuona tena Winnie
" Mr Charles miss Pinky Yuko wapi ? Au ametoka ?"
Aliuliza Elian
" Yupo chumbani kwake na tangia asubuhi baada ya kifungua kinywa hakutaka kula kitu chochote na anaonekana amekasirika sana "
Elian alienda chumbani kwa Winnie alimkuta anaangalia movie
" Kwanini umejifungia tu chumbani na hutaki kula ?"
Aliuliza Elian lakini Winnie alikuwa kama ameziba masikio hakumjibu chochote
" Kama umekasirika kwa kile nilichokisema asubuhi nisamehe nitatimiza unachokitaka "
Winnie alitabasamu
" Panda kitandani nataka tungalie movie pamoja "
Elian alitabasamu akapanda kitandani Winnie aliweka movie aliyotumiwa na Sonia akiamini ni ya action kama movie anazozipenda lakini haikuwa hivyo ilikuwa ni movie inayohusu mahusiano zaidi Elian na Winnie walijikuta wameangakua Elian hakutaka kuvumilia alimsogelea Winnie na kuanza kumkiss
" Sorry sikupanga hili ni kama akili yangu ilikuwa haifanyi kazi "
alisema Elian huku anasogea nyuma Winnie alimzuia Elian kwa kuvuta kola ya shit lake
" Endelea usiache " alisema Winnie , Elian hakutaka kufikilia sana alimshika Winnie kiunoni akamsogeza karibu yake na kuanza kumkiss hawakuishi hapo walijikuta wakilala pamoja Elian alikuwa wa kwanza kuamka alimuangalia Winnie usoni akatabasamu ,mlango wa chumba Cha Winnie uligongwa Elian alienda kufungua
" Nini shida Mr Charles?" Aliuliza Elian ,Mr Charles alimuangalia Elian akatabasamu Elian alikuwa amefunga taulo tu na yupo chumbani kwa Winnie
" Aaah Mr Elian nimepata simu kutoka kwa secr8 wako anasema unahitajika haraka sana ofisini kunaabo ya kuyaweka sawa "
." Okay asante kwa kufikisha ujumbe mpigie simu mwambie ndani ya nusu saa nitakuwa huko "
Elian aliingia chumbani kwa Winnie alichukua nguo zake akaenda chumbani kwake alivalia suti yake nzuri ya kijivu na kuondoka Winnie aliamka kutoka usingizi lakini hakumkuta Elian
." Mmmmh sijui nitamuangaliaje huyu kaka ni wazi ataniona mimi ni mwanamke rahisi sana "
Winnie alianza kujilaumu alichukua simu yake akamtumia Elian message : kilichotokea kati yetu ni makosa tufanye kama hakuwahi kutokea kitu chochote naamini na wewe pia ungetaka iwe hivyo
Full 1000
Whatsp 0784468229.