"Siwezi kufungua simu yangu na kwanini nifanye vile mnavyotaka nyie ?acheni kupoteza muda kwangu hamtopata chochote "
Winnie aligoma kufungua simu yake
" Kweli wewe ni mrembo na jasiri sana ndomana Mr Elian alikupenda kirahisi ,tunaweza kukuumiza wewe pamoja na mtoto wako kama hautatoa ushirikiano "
alisema zero Winnie alianza kuogopa alishika tumbo lake
" Tafadhali nawaomba msije mkajaribu kumuumiza mtoto wangu "
Winnie aliongea huku analia
" Kama hutaki iwe hivyo basi Fanya kila kitu tunachokwambia ,fungua simu yako na umpigie mr Elian "
alisema zero Winnie alifanya kama alivyoelekezwa
" Lete hiyo simu " vuvuzela alimnyanganya Winnie simu baada ya kusikia inaita haikupita hata sekunde tano Elian alipokea simu
" Hello ,unataka nini Winnie ?"
Elian aliuliza baada tu ya kupokea simu
" Mr Elian tumemshikilia mwanamke wako Winnie kama mateka unatakiwa kutoa milioni 5 ilikumkomboa la sivyo utamkosa "
aliongea vuvuzela kwa sauti ya amri
" Mmmh Sina uhusiano wowote na huyo mwanamke mnaweza kufanya mnavyotaka " Elian alitaka kukata simu
" Vipi kuhusu mtoto wako aliyeko tumboni kwake unataka kumpoteza pia ?" Aliuliza zero baada ya kumnyanyua simu vuvuzela
" Unasema mtoto ?siwezi kuwa na mtoto na huyo mwanamke kwanini msimwambie awatajie baba wa mtoto yeye mwenyewe "
" Lakini ni mwanamke wako "
aliongea zero kwa kupaniki kwani aliona wazi wazi wanaenda kufeli kwenye mchongo wao
" Sio mwanamke wangu ,mke wangu mtarajiwa yupo pembeni yangu akiwa amembeba mtoto wangu tumboni kwake sitaki usumbufu " Elian alikata simu ,machozi yalitiahia kutoka kwenye macho ya Winnie lakini alijizuia
" Wewe kahaba tuambie baba wa mtoto ni nani ?" Aliuliza zero kwa hasira Vuvuzela aliona namba ya riffat kwenye simu ya Winnie
" Ona bila shaka huyu ndo baba wa mtoto " vuvuzela alimpigia riffat
" Niambie Winnie wangu " aliongea riffat baada ya kupokea simu
" Tumekamata Winnie kama unataka kumpata mwanamke wake pamoja na mtoto basi inabidi ulete milioni Tano "
" What ? Kwanini mmemteka Winnie ?" Riffat alihisi kuchanganyikiwa alitamani kumwambia Tracy mana riffat alikuwa sitting room na Tracy alikuwa jikoni
" Hauna haja ya kujua yote hayo ila kama unamtaka akiwa hai Lete hizo pesa nitakutumia location unatakiwa kufika hapa kwa wakati nakupa nusu saa tu na bila polisi laa sivyo utampoteza mke wako na mtoto wako"
" Nawaomba msimfanye chochote nitafika hapo Sasa hivi na pesa mnazozitaka "
" Vizuri nakutumia location "
vuvuzela alikata simu
" Oh mungu wangu kwanini yanatokea haya yote na vipi kuhusu Elian sitakiwi kumwambia pia ? Nahisi sitakiwi kumwambia lakini yeye ndo baba wa mtoto" riffat alijikuta anajiuliza maswali na kujijibu mwenyewe ni wazi alichanganyikiwa na hakujua afanye nini
" Babe kwani una nini mbona sikuelewi?"
Tracy alimuuliza riffat
" Niko sawa tu babe ila Kuna dharula imejitokeza ofisini so nitakuacha mara moja sitochukua muda mrefu nakuahidi"
" Sawa babe wewe nenda tu ukirudi chakula kitakuwa tayari "
Riffat alitoka haraka hakubadirisha hata nguo alichukua funguo ya gari na kuondoka safari yake iliishia benki kwanza alienda kutoa milioni 5 kama alivyoambiwa alifuata maelekezo kuelekea eneo walilokubaliana kukutana na watekaji
" Amesema Yuko wapi ?" Aliuliza zero
" Anakuja Sasa ivi kuwa na subira kaka " vuvuzela na zero walienda kukaa mbali kidogo na walipomfunga kamba Winnie
" Sitakiwi kumuingiza mtu yoyote kwenye matatizo yangu nitayamaliza mwenyewe usijali mtoto mama atakulinda kwa namna yoyote"
Winnie alijiongelea mwenyewe alianza kujaribu kufungua kamba bila kuchoka mpaka alifanikiwa alinyata na kufanikiwa kufikia mlango lakini kwa bahati mbaya mlango ulitoa sauti iliyowashtua vuvuzela na zero
" Unaenda wapi ? Rudi haraka "
vuvuzela na zero walianza kumkimbiza lakini Winnie hakutaka kukubali
" Unaenda wapi na hapo mbele Kuna korongo simama haraka "
" Kuliko kukamatwa na nyie Bora nivunje hata hii miguu "
alisema Winnie Na kweli haukuwa utani mbele kidogo tu kulikuwa Kuna korongo kubwa linaloishia barabarani Winnie alishika tumbo lake kwa mikono miwili akajitupa kwa bahati nzuri hakuumia sana sehemu ya tumbo na muda huo riffat alikuwa amefika eneo Hilo na wapita njia wengine walikuwepo zero na vuvuzela walishindwa kumfuata
" Shit dili letu limepotea hivi hivi "
alikasirika vuvuzela
" Tuondoke hapa haraka sana kabla hawajaita polisi "
zero na vuvuzela waliamua kukimbia
" Winnie .. Winnie "
riffat alimshika mikononi mwake Winnie aliyekuwa amezimia
" Iteni gari ya wagonjwa "
alisema mpita njia mmoja Gari ya wagonjwa ilifika muda si mrefu Winnie alipakiwa kwenye gari na kuanza kupewa huduma ndogo ndogo wakiwa njiani kuelekea hospital
Kwa upande wa Elian alikuwa amekaa na loveness sitting room
" Elian kwanini uliwaambia wale watu kuwa humjui Winnie vipi kama ni kweli ametekwa ?"
Loveness alimuuliza Elian
" Winnie ana mimba loveness na Nina uhakika sio mtoto wangu naumia lakini acha baba wa mtoto aende akamuokoe " Elian aliendelea kumkatia loveness matunda ghafra loveness alianza kujisikia vibaya na kuzimia
" Loveness umepatwa na nini ? "
" Mr Elian kwanini tusimpeleke hospital " alisema Mr Charles
" Sawa nitampeleka " Elian alimbeba loveness mpaka kwenye gari na kumpeleka hospital Loveness alifika hospital na kupewa huduma
" Unataka kula nini ?" Elian alimuuliza loveness baada ya kuamka
" Nataka juisi ya apple na keki yangu pendwa sanaa "
alijibu loveness huku anatabasamu
" Basi nitaenda kukuletea "
Elian alienda kununua juice ya apple na keki aliyopendelea kula loveness akiwa anarudi hospital alikutana na gari ya wagonjwa Kuna nafsi ilimwambia angalia mgonjwa ni nani Alisogea na kuchungulia alimuona Winnie akiwa hajitambue amelazwa kwenye kitanda na huku mwili wake ukiwa unavuja damu kila sehemu kwasababu ya kuchomwa na miba na visiki
" Amepatwa na nini ?" Aliuliza Elian
" Amepata ajari "
alijibu dactari mmoja
" Amepata ajari gani mbona yupo hivi ?" Aliuliza Elian huku ameshika mkono wa Winnie
" Unaundugu na mgonjwa mbona unauliza maswali mengi tunaomba utupishe tumpeleke ndani akafanyiwe huduma laa sivyo atapoteza mtoto wake "
madactari walimuingiza Winnie ndani na muda huo riffat alifika na gari lake
" Riffat .."
aliita Elian lakini riffat hakumsikiliza aliingia ndani ya hospital kujaza taarifa za mgonjwa Elian alimfuata nyuma
" Unajua ana mimba ya miezi mingapi ?"
Dactari mmoja alimuuliza riffat
" Ndiyo ni miezi mitatu Sasa kama na week mbili , tafadhali dactari naomba umuokoe Winnie na mtoto wake" riffat alimuomba sana dactari, Elian yeye hakuwa akiamini alichokisikiaA
Offer offer offer
soma yote kwa sh 600
Whatsp 0784468229.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments