Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

MY LUNA 🎭💕 🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋 SEHEMU YA : 22

21st Aug, 2025 Views 159

OFAA 500 HAIPOSTIWI TENA

SIMULIZI :

Leila alipoingia chumbani kwake, hakuweza kuzuia machozi yaliyokuwa yakitiririka taratibu mashavuni mwake. Akiwa na maumivu mguuni na moyoni, alijilazimisha kwenda kuoga kuondoa uchafu wa jasho, uchovu wa dansi, na huzuni ya kugundulika.

Akatoka bafuni akiwa na kitenge kidogo kilichozunguka kiuno. Alikaa kitandani taratibu, akijiuliza kama kweli Zayn alimaanisha maneno aliyosema usiku ule. Je, alijua tangu lini kwamba yeye ni Luna??🤔

Kabla hajamaliza kutafakari, mlango wa chumba chake ukafunguliwa taratibu. Zayn alikua amerudi kwa maana alienda kununua boksi la huduma ya kwanza.

Bila kusema hata neno moja, aliketi pembeni mwa kitanda na kuanza kubadilisha bandeji kwenye mguu wa Leila kwa umakini mkubwa. Hakuna alie msemesha mwenzake kila mtu alikua kimya🤐.

Baada ya kumaliza, Zayn alifunga boksi lake, akainuka na kutoka chumbani bila hata kugeuka nyuma. Mlango ulipofungwa, Leila alijitupa kitandani na kujifunika uso kwa mto. Ni aibu ila pia ni raha kuona Zayn anamjali🥰.

Asubuhi ilipofika, Leila alipoamka, alikuta chai safi mezani. Mkate wa siagi, chai ya tangawizi, na mayai ya kuchemsha. Hakukuwa na mtu sebuleni. Zayn alikuwa ameondoka tayari kwenda kazini.

Eti Zayn kamuandalia breakfast?? Hakuwai kuwaza kama angemfanyia kitu kama icho. Alikaa mezani akajipongeza kwa chai aliyoandaliwa. Baada ya kifungua kinywa, Leila alichukua simu yake na kumpigia rafiki yake Sinyati.

“Hallo Sinya…”

“Heee bby, habari zako? Ulifika salama jana?”

Leila akavuta pumzi ndefu, “Sinya… Zayn anajua kila kitu.”

“Eeeh? Ana…anajua nini?” Sinyati alishtuka😳.

“Anajua kuwa Luna ni mimi. Akanipeleka mpaka nyumbani… akanisihi niache kucheza mbele ya wanaume… Sinya, alikuwa serious!”

Sinyati alikaa kimya sekunde kadhaa kisha akasema, “Na wewe je? Unahisi vipi juu yake?”

Leila alinyamaza, kisha kwa sauti ya chini alisema, “Sinya nampenda Zayn. Na kama atasema tuanze upya, niko tayari kumsamehe. Lakini kama atarudi kule kule, basi mimi nitachukua talaka yangu. Sina tena nguvu ya kuchezea moyo wangu”😔

“Daah! Ufanye maamuzi sahihi”

“Ndio ila unajua kaniandalia mpaka breakfast! Yani najihisi vizuri mno”

“Khaa! Mbona hizi habari zilitaka kunipita”

“Acha tu Sinyaa! Nahisi kama naota vile”

“Ila usisheherekee mapema ndugu yangu mpaka usikie atakuambia nini! Je atataka muendeleze ndoa ama muachane kama alivyokua amepanga”

“Sawa nimekuelewa Sinya! Subiri tuone”☺️

Upande wa pili, Zayn naye hakuwa sawa. Alimaliza kikao kazini lakini kichwa chake kilikuwa kizito. Mawazo yalizidi kumlemea. Hakutaka kurudi nyumbani mara moja. Alielekea kwa rafiki yake Kevin, mtu wake wa kumshauri.

“Bro…” Zayn alikaa kwenye sofa huku akitikisa kichwa, “Luna ni Leila.”

Kevin aliyekuwa akichezea laptop alipigwa butwaa, “Whaat? You mean your wife Leila is Luna?”😳

Zayn akainamisha kichwa, “Yes. Mke wangu ndiye Luna. Ndio maana moyo wangu ulikuwa unavurugika. Nilimchunguza wiki nzima nikapata uhakika”

Kevin alisogeza laptop pembeni, “Zayn, bro… kama unampenda Luna, then unampenda mkeo. Simple as that”

Zayn alitulia. “Yes I do. Nampenda mke wangu. Bro, nampenda kweli, kweli”

Kevin alimtazama kwa makini, “Basi, kama kweli unampenda, muambie ukweli. Mwambie kila kitu. Amini usiamini, hiyo ndiyo njia pekee ya kuanza upya”
Je nini kitaendelea Pata mwendelezo kwa bonge Moja la ofaaaa full yaani mpaka mwisho kwa 500 TU no ya malipo 0750411324 SUBIRA SEFU njoo na muamala wako uhudumiwe hatupoi hatuboi mambo ni 🔥🔥🔥
HAIPOSTIWI TENA OFA 500.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MY LUNA 🎭💕 🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋 SEHEMU YA : 22  >>> https://gonga94.com/semajambo/my-luna-sehemu-ya-22

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest