Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

I LOV U DADY๐Ÿ’˜โค๏ธ๐Ÿ’˜ 01

9th Aug, 2025 Views 73



Njooni niwasimulie hadithi yangu leo๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚wangapi humu mliolewa na wachumba msiowafahamu?

Yani mi my wenu ndoa yangu ilikuja kama kimbunga ghafla tu shwaaa jiandae unaolewa kibaya zaidi mtu anaenioa wala sikuwa namfahamu๐Ÿ˜‚

Yani maisha ya kijijini jamani๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚unalala singo kesho unaamka unaambiwa jiandae unaolewa๐Ÿ˜ด

That time nimehitimu form four wakati nasubilia matokeo nilikuwa tu home kwa wazazi wangu sina jipya nipo nipo tu..

Siku moja nimetoka zangu mizungukoni nikakuta gari kali pale nje kwetu mmhhh sisi mbona hatuna ndugu tajiri mwenye gari hili gari ni lanani๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

nikakimbilia ndani kuchungulia kunani๐Ÿ˜ฉ๐Ÿ˜ฉnimefika ndani nikakutana na ugeni mzito๐Ÿ˜ณnikashangaaa hawa kina nani?? Kucheki vizuri nikamuona mama mchungaji wa kanisani kwetu na mama mwingine mzuri kweli..

Niliwasalimia kwa heshima na adabu kisha nikaingia chumbani ili nisikilize wanaongea nini๐Ÿ˜‚mi nae kambea๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œsitaki kupitwa

kwa bahati mbaya wakati nimefika ndo wageni walikuwa wanataka kuondoka nahisi walikuwa wanasubilia tu mimi nifike wanione..

Nimefika chumbani natega sikio nisikilize maongezi mara nikasikia mama ananiita Maya njoo mara moja mamangu..

Nikarudi tena sebleni walipo wageni๐Ÿ˜ฉ๐Ÿ˜ฉ nikashangaa wazazi wangu wanasema binti yetu sisi ndo huyu hapa jina lake ndo hilo Maya...

Mmhhh nikajiuliza mbona utambulisho kulikoni au nauzwaaa๐Ÿฅบ๐Ÿฅบ...mama kwani nimefanyaje๐Ÿ˜ฐnilihoji kwa kutia huruma mpaka watu wote pale wakacheka๐Ÿ˜‚

Mama akaniambia usijali binti yangu tutaongeaa kwa sasa tuwatoe kwanza wageni then tutarudi kuongeaa..

Basi bwana tuliwatoa wageni mpaka nje lilipo gari lao yule mama mwingine rafiki wa mama mchungaji akawa ananiangalia kweli..

Tulipofika lilipo gari tukawaaga yule mama akamwambia baba nitasubiria majibu yenu jamani msiniangushe...

Basi wageni waliondoka mimi hapo sielewi chochote natoa macho tu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚...

Baada ya wageni kusepa wazazi wakaniweka kitak wakaniambia oh binti yetu kwa sasa umeshakua unajua binti kama wewe kabla hujaanza kuharibika ni vyema uolewe ili ukayaanze maisha yako mapya kwa mumeo na wakwe zako..

Kama unavyojua kuolewa hilo ni jambo la kheri na baraka na pia ni furaha sana kwetu wazazi kuona binti yetu umekua na unaenda kuyaanza maisha yako mapya..

Mmhhh niliposikia zile kauli mbona kama za kuagwa kuagwa jamani๐Ÿ˜ฐ๐Ÿ˜ฐ๐Ÿ˜ฐsikutia neno nikaendelea kusikiliza..

Baba na mama waliendelea kuongea mara ooh binti anapokua atapata mwenzi wake wataoana waende kuanzisha familia yao...

Khaaaa๐Ÿฅบ๐Ÿฅบ๐Ÿฅบmbona siwaelewi mnaongea nini mbona siwaelewi๐Ÿฅน๐Ÿฅน..

Ikabidi wafunguke ooh huyo mama alokuja hapa alikuwa anatafuta binti kwa ajili ya kijana wake na amekupenda wewe hivo jiandae kwa ajili ya ndoa..

I was like what๐Ÿ˜ง๐Ÿ˜งmama mbona mnafanya vitu kwa urahisi hivyo๐Ÿฅน๐Ÿฅนkwani mmesahau natakiwa kuendelea na masomo??

Akadakia baba hata usome mpaka wapi binti yetu ni lazima tu utaihitaji ndoa..

Mama naye akasema ndoa haimzuii mtu kusoma binti yangu unaweza ukaolewa na bado ukaenda shule...

Lakini mama mshika mbili moja humponyoka๐Ÿฅน๐Ÿฅนalafu mama mimi bado ni mdogo kuingia kwenye ndoa kwanini mnarahisisha vitu?๐Ÿฅน๐Ÿฅน

Hebu kaa kimya maya๐Ÿฅบ๐Ÿฅบkwa udogo gani ulionao??...baba yako kanioa nikiwa mdogo kuliko wewe na bado niko nae na tuna furaha haya wewe ndoa inakushindaje kwani unaibeba kichwani??.

Wewe kaa ukijua mchumba ameshapatikana na ujiandae kwa ajili ya ndoa full stop...

Weee nililiaaaa๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™ˆ nilihisi kama wazee wanataka kuniuza fulani hivi... nilikimbilia chumbani huku michozi inanitoka ndi..

Nimefika chumbani ile nataka kubana mlango mara maza huyu hapa....

Akanitupia picha hapo kitandani akaniambia liaaa weeee ukitosheka ujiandae kwa ajili ya mwenzio picha yake hiyo hapoโ˜น๏ธโ˜น๏ธ..

Weeee๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆhebu nimuone kwanza huyo mwenzangu anafananaje isijekuwa kinyago cha mpapule๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ nilichungulia ile picha huku nikijipangusa machozi nyieeee kuna watu wanazaa bwana๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ

Likijana la watu kama limechorwa vile uuuwwwww hayo macho yake sasa kama ananiita vile๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ

Wakati nalia na picha chumbani mara kwa mbali nikasikia mama anaongea na simu..

"Helloo eeh tayari binti yetu tumeshamwelezea kila kitu ye hana kipingamizi anataka tu kijana aje waonane...

Khaaaaaa๐Ÿ˜ณ๐Ÿ˜ณ๐Ÿ˜ณ

itaendeleaaaaaa..

KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

I LOV U DADY๐Ÿ’˜โค๏ธ๐Ÿ’˜ 01  >>> https://gonga94.com/semajambo/i-lov-u-dady-01
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest