Baada ya Selim kutoka kwa hasira aliingia Nasra na mama mkwe wakawa wanauliza kimetokea nini , nilifuta machozi na kujibu hamna kitu ila ni mabishano kidogo tu .
Walitoka na kuniacha mwenyewe nikabaki nikitafakari mambo yote toka siku aliyobadilika Selim , mawazo yangu yaliniambia huenda anatoka na Nasra ila moyo ulikataa kwani namuamini sana Selim .
Nikahisi huenda ni hasira tu basi nikalala kesho yake asubuhi sikuwa na mood ya kwenda kazin ,nikaandaa chai na kumpigia Selim ila hakupokea nikachukua sm ya Nasra na kutuma meseji nikisema "hello uko salama " ilifika nikaka kusubiri kujibiwa .
Hapo Nasra alikuwa chumbani kwake , nikawa nimekaa kusubiri haikuchukua mda akajibu " Yeah niko sawa vp nyie "
Niliiangalia na kujibu "Ndio tuko sawa nilitaka kujua kama uko sawa ila Norah naona hayuko sawa "
Alijibu "achana nae atakuwa sawa kwa mda wake " nilijibu sawa kisha nikasema uwe na siku njema .
Nilimaliza kujibu nikafuta meseji zote na kurudisha sm nilipoitoa kisha nikarudi chumbani kwangu huku nikiangalia sm yangu hakuwa amejibu ujumbe niliotuma.
Siku iliisha akiwa hajarudi nyumbani wala hakujibu meseji zangu , usiku wa saa nne nikiwa kitandani akaja na kufika kulala bila hata kunisemesha na mimi sikutaka kuongea nikalala kimyaa .
Kesho yake nikaamka na kuandaa chai kisha nikawaandaa watoto na kuingia kuoga wala sikumuandalia nguo nikavaa na kuondoka.
Siku hiyo ikapita bila hata kuongea nae baadae jioni Nasra akaniambia "Norah naona hamko sawa na mumeo jitahidi muongee yaishe maana mahusiano au ndoa ikijaa ugomvi hufungua milango ya shetani kwa hiyo jitahidi kuweka kila kitu sawa "
"Usijali dear nitaweka kila kitu sawa na huyo shetani hatapata nafasi yoyote" alitabasamu na kuniambia "haya ".
Nilikaa nikawaza nakuwazua nikapima na kupima mwisho nikaona bora nikae kimya atakapo taka kuongea na mimi ataongea ndio ilikuwa inauma ila sikuwa na namna .
Basi maisha yakaendelea mambo yakiwa vile vile nikipika chakula hali akipika chakula mwingine anakula ,nikiandaa nguo havai wala hata salamu zangu haziitikii ila Nasra wanaongea na kucheka nikawa nakaa kuwangalia tu .
Ile hali iliendelea kama wiki mbili nikaona sasa hapa tunapoelekea sio kuzuri ndoa itavunjika hivi hivi kwa hiyo cha msingi nishuke , siku hiyo nikatoka kazin mapema nikaandaa chakula vizuri chumbani nikapaweka vizuri kukawa kunanukia kila kona .
Nilivyomaliza nikajiweka katika hali ya usafi kisha nikaa kusubiri , nakwambia nilikaa saa moja saa mbili saa tatu saa nne hapo nimeshapiga sim kama mara kumi hazipokelewi nikatuma text kibao hazijibu .
Nilichoka na kuamua kumpigia Nasra akapokea na kuniambia wamepata safari ya dharura hivyo hawapo nchini ,nilichoka nikajibu "haya sawa muwe na usiku mwema na kazi njema pia " nilimaliza kuongea na kukata hata kabla Nasra hajanijibu.
Kweli nilipata hasira na kuona wazi kwamba Selim ananidharau anawezaje kufanya mambo kama haya kweli anasafiri bila kuniambia chochote na sio kwamba ameenda mwenyewe kaenda na dada yangu hivi anataka nifikilie nini haswa .
Usiku ule sikulala mawazo yalikuwa mengi kila nikifikilia jinsi mambo yanavyoenda nachoka mwili na roho, mwisho niliamua kuchukua maamzi magumu ili niwe na amani maana habari za kulia na mapenzi siwezi .
Yani maisha yanivuruge mapenzi ya nivuruge wekuweza , nilisubiri asubuhi na mapema nikaamka na kujiandaa nikamwambia dada aandae watoto vizuri kisha huyoo nikaenda kazin.
Jioni nilivyotoka nikaenda kwa Amaira nakuta macho yamivimba kama ametoka kulia , alivyoniona tu akaanza kulia sasa na mimi nilivyo na machungu yangu nikakaa na kuanguwa kilio cha kutisha kwanza Amaira alinyamanza na kuanza kunibembeleza huku akiuliza shida nini .
Kwani nilikuwa hata na nguvu ya kumwambia ,nililiaa wee mpaka uchungu wangu ulipoisha nikainuka na kuingia jikon kwa watu nikachukua chakula na kukaa chini nikalaa hadi nikasaza .
Baada ya kuamaliza kula nikaanza kumueleza kila kitu, alinipa pole na kuniambia kila kitu kitakuwa sawa , basi bwana maamuzi niliyochukua ni kukaa mbali na nyumbani kwa hiyo nikalala kwa Amaira hapo najiambia kuwa nitakuta missed call kibao ila hadi naamka asubuhi hata meseji ya bahati mbaya sikuiona .
Nikasema sawa basi nikaende kazin mpaka inafika mchana sijaona sim yoyote , nikaona nimtumie ujumbe " Naona umepata wakuendana nae hongera sana " ulifika kabla hajajibu nikaufuta haraka .
Amaira akaniambia " Unajua Norah hiki ulichokifanya sio kizuri hivi ulishaona mwanaume analala nje leo alafu mwanamke nae kesho akalala nje ya nyumba yake eti kwasababu jana mwanaume hakulala nyumani ? jibu ni hapana.
kwahiyo wewe hapo unachotakiwa kufanya saivi rudi nyumbani kwako umsubiri arudi ili muongee ujue hatma ya hayo yote lakin ukisema ukae huku nakuhakikishia utakuza mambo na kuonekana huna hekima ." nilifikilia nikaona kweli anaongea point basi nikajikusanya na kurudi nyumbani .
Nilifika na kukuta mama mkwe yuko bize anaangalia tv nikijitoa ufahamu na kusalimia kama vile nimelala nyumbani na yeye hakuniuliza wala kuongea chochote.
Nilikaa siku ya kwanza kimya siku ya pili kimya nyie moyo ulikuwa unauma nakula chakula nahisi hakipandi , ndoa hizi Mungu atusaidie .
Siku ya tatu ilipita tena kimya nikasema nijitoe ufahamu nimtafute kwani alipokea , kile kitendo chakuwa napiga simu hazipokelewi kiliniumiza sana nikaamua kumtumia ujumbe wa kuhitaji talaka yangu ili nijue moja tu kwamba nimeachika maana siwezu kukaa kwenye ndoa kama hii ambayo hata sielewi inaendaje ,kwanza licha
ya mambo kuwa tofauti kitendo chakuwa karibu na Nasra mpaka kusafiri nae bila taarifa yoyote kilinipa picha mbaya na kuhisi huenda wakawa na mahusiano .
Meseji ilienda akasoma na kunibu ...............
KWETU morogoro.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.