Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

Chozi la mdogo wangu SURA YA SITA

7th Aug, 2025 Views 13



Sikku zilikatika hatimaye mwezi ukayoyoma, muda wote huo Dorini na Frank waliishi kwa kuteseka sana, kula yao tabu lala yao ndiyo utawahurumia kabisa. Muda wote makazi yao yalikuwa ni yaleyale kwenye dampo, sehemu ambayo karibu takataka za mji mzima zilitupwa hapo na kama ujuavyo harufu inayo patikana kwenye dampo ilivyo mbaya, hapo ndipo watoto hawa walijikuta wakipageuza kuwa maskani yao. Si Dorini wala Frank wote wamekonda wamebaki mifupa tuu, yaani aliyewahi kuwaona mwezi mmoja nyuma na angewaona leo hangeweza kuamini kama watoto wale ndiyo hawa, yaani wamechakaa hawatamaniki, weusi tii waliojaa masizi ya uchafu mwili mzima. Chawa, kunguni, viroboto na hata utitiri waligeuza miili ya watoto hawa wadogo kuwa makazi yao huku damu zao ndiyo zikiwa chakula na kinywaji kwa wadudu hao wasumbufu na wenye kukera sana.
Ama kwa hakika pale wanapolala watoto hawa wewe ungeambiwa lala hata usiku mmoja ungelijutia asubuhi yake maana ungeishi kwa kujikuna mwili mzima kwa muwasho wa vipele vitokanavyo na wadudu wanao patikana eneo lile.
Katika mwezi huo hali ya afya ya Frank ilikuwa mbaya na pesa za matibabu Dorini hana, akawa wa kulia na kuomba msaada akipata angalau kiasi kidogo alimnunulia mdogo wake panado japo tu atulize maumivu ya kichwa. Basi kwenye pitapita yake Dorini aliweza kupewa elfu mbili akawa amemnunulia dozi moja ya kwinini na kumpatia mdogo wake, akanunua pia chakula na kumpatia. Baada ya kula tu Frank alitapika palepale matapishi yaliyo changanyikana na damu na akaishiwa nguvu kabisa akabaki kumuangalia dada yake aliye kuwa akilia sana. Ghafla Frank alionekana kukaa kimya, mwili wake ukawa wa baridi, umboni mweusi wa jicho ukaanza kupanda na kupotea, Dorini aliposikiliza kama anapumua akatambua kuwa hapumui. “Maskini, nini kimempata mdogo wangu!” alilalama Dorini kwa huzuni huku kwa haraka akimnyanyua na kumuwahisha kwenye hospitali ya wilaya ambayo haikuwa mbali sana kutokea pale dampo. Alipokelewa kwa kasi kubwa sana na wauguzi waliokuwa zamu siku ile ambapo Frank akaanza kuhudumiwa na muda mfupi baadaye alipata ahueni baada ya madaktari kupambana kuinusuru roho yake iliyokuwa ikipotea gizani, yaani kifo kilikuwa tayari mlangoni, kilichokuwa kimebaki ni yeye kufa. Basi daktari alimuita Dorini ndani na kupewa karatasi iliyoonyesha orodha ya dawa zaidi zilizopaswa kununuliwa ili Frank apate kupona kabisa na pia iliyoonyesha mpaka muda huo alikuwa akidaiwa shilingi ngapi.
Unajua msomaji maamuzi mabovu ya wazazi, yanaweza kuwaweka watoto kwenye wakati mgumu sana, na ndiyo sababu kubwa inayofanya kuwepo kwa wimbi kubwa la watoto wa mtaani. Ni baada ya kila mmoja kujiona kuwa mwenye haki kuliko mwenzake na maamuzi anayo yaamua anaona kuwa yapo sawa kabisa, anashindwa kukumbuka kuwa hayo maamuzi anayo yaamua yanaweza kumfanya mtoto awe kwenye wakati mgumu sana. Dorini anajikuta anaingia kwenye majukumu mazito sana yote kwasababu ya ugomvi wa wazazi wake, pia maamuzi mabaya ya wazazi ilhali kila mmoja kujiona kuwa yupo sawa.
Kunasiri ambayo wanaume wengi hawaijui, hivi unajua kuwa yule mwanamke aliyekuzalia mtoto wa kwanza ndio amekamata mafanikio yako ya kimaisha na hata ya kimaendeleo? Vijana wengi hupenda sana kuchezea mabinti na kwa bahati ikitokea binti akapata mimba basi kijana huyo humtelekeza akiwa na mtoto au mimba kama siyo kuikataa mimba hiyo. Leo kuna kitu nataka nikukumbushe kuwa huyo mwanamke aliye kuzalia mtoto wa kwanza hata kama siyo wa ndoa kikubwa mtoto huyo ni wako basi huyo ndiye mke wako wa halali, kama ulikuwa na mpango wa kumuacha badili maamuzi maana pigo utakalo lipata baada ya yeye kudondosha chozi, laana na ile laumu hata kidogo siyo la kitoto, litakuwa pigo la kihistoria kwenye maisha yako.
Je ni njia gani ufanye kama ikitokea wewe umempatia msichana mimba na ukamtelekeza na kuoa binti mwingine na kumuacha yule wa kwanza?, je umuache huyu wa pili umrudie yeye au uwaoe wote?.
Sipo kutoa majibu moja kwa moja, hiyo imepita tu, bali tupo hapa na mfululizo wa simulizi yetu tunayo endelea nayo iitwacho “Chozi la Mdogo Wangu”. Ukijiunga kwenye group letu la simulizi tunagusia pia habari za elimu juu ya mahusiano, uchumi na mengineyo na wote tuna shauriana na kuchangia bila kujali hoja ya mtu. Namna ya kujiunga ni kutuma neno Niunge kwenda kwa Istagram message nasi tutakutumia kiunganishi (link) ya kujiunga kwenye group letu la WhatSapp.
(Tafadhali tambuwa sio kila Layman Donsue utakaye mkuta huko Instagram ni mimi angalia kwanza post zake hapo ndipo utaweza kutambua Layman Donsue wa kweli, maana siku hizi kuna matapeli lukuki wanatumia majina ya watu kujinufaisha wenyewe)
Dorini baada ya kusomewa bili hiyo aliyopewa na daktari mwili ulimsisimka laiti angekuwa na presha angesha kufa ila yeye alilia ukizingatia alikuwa mdogo. Daktari aliona kila kitu alichokuwa akifanya maana alikuwa akishika kichwa na kunyanyuka kwenye kiti na kuzunguka zunguka huku mdomo wake ukitamka neno “no” akimaanisha hapana, neno hili alilirudia mara nyingi sana, huku daktari huyo kichwani akijiuliza wazazi wa watoto hao wapo wapi ila majibu hakuyapata akawa amemsihi aketi chini kwenye kiti waongee kidogo na aache kujichanganya kichwa kwenye umri mdogo.
Baada ya Dorini kukaa daktari akaanzisha mazungumuzo.
“Mama yako yupo wapi?”
Dorini alimuangalia yule daktari hapohapo akaanza kulia tena huku akisema kwa sauti iliyo jaa kwikwi
“Mama alifukuzwa na baba zamani kidogo”
Kwa mshituko kidogo daktari aliuliza
“Alifukuzwa na baba yako?..na huyo baba yako yupo wapi kwani?”
Dorini alifuta machozi yake na kusema
“Alitutelekeza baada ya yeye kukosana na mamdogo”
Daktari alimuonea huruma sana binti huyu mdogo kisha akamuuliza tena
“Kwa hiyo nyumbani mnaishi peke yenu”
Dorini alitabasamu kidogo kisha akaendelea kusema
“Ukweli dokta huu mwezi wa tatu sasa, hatuishi ndani ya nyumba navyokwambia hivi tumekuwa tukilala dampo baada ya kodi ya nyumba baba aliyo kuwa amelipa kuisha”
Palepale daktari alidondosha machozi baada ya kuliona tabasamu la Dorini kwenye wakati mgumu hivyo, akaendelea kumuuliza
“Una umri gani binti”
“Nina umri wa miaka saba”
“Mdogo wako jee?”
“Ana miaka mitatu sasa”
“Mlikuwa mkila nini kwa muda wote huo binti?”
“Vyakula vichafu vinavyotupwa kutoka mahotelini japo kuna wakati nilikuwa nafanya kazi nikipata fedha tunakula chakula cha hotelini”
“Pole sana binti, ngoja nitamshughulikia mdogo wako mpaka apone na kwa sababu wazazi wenu wamewaacha mimi nitawachukua ili muendelee na masomo”
“Ooh, nitashukuru sana dokta”, aliitikia Dorini.
Daktari yule alibakia kumlinganisha huyo Dorini na maelezo yake na jinsi alivyo akaona kabisa hao wazazi wake walikiacha chombo kizuri yaani mtoto mdogo kiasi kile ila anajieleza kwa umakini vile zaidi ya mtu mzima, alibakia kushangaa sana

Follow page yangu Story za Riwaya Tanzania.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Chozi la mdogo wangu SURA YA SITA  >>> https://gonga94.com/semajambo/chozi-la-mdogo-wangu-sura-ya-sita
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest