Max alichukua bahasha ya kaki na kumpatia Dala.
" Ni nini hii?
" Pokea kwanza.
Dala alipokea huku akiwa anamuangalia Max usoni.
" Dala hapo kuna sheria muhimu za hii nyumba n maelezo ya jinsi ya kumlea binti yangu, soma kwa makini.
Dala alifungua ile bahasha na kutoa karatasi na kuanza kusoma mstari hadi mstari , alipomaliza alishusha pumzi na kusema .
" Haya kweli ni maisha mapya.
" Umesoma vizuri na umeelewa?
Dala alirudisha macho yake kwenye karatasi na kuendelea kusoma.
Alitumia dakika kadhaa kusoma zile karatasi kisha akasema
" Kifupi baba shalon unataka kunibana sana yani sitakiwi kutoka hapa ndani , hutaki niwe na mazoea na watu wa nje wala kuongea nao kumbuka mimi ni binadamu kuna kupata matatizo hao watu ndio watakuwa msaada kwangu na kwa mwanao.
" Sasa hapo unataka kukaribisha umbea ndani kwangu pia unataka shalon ajue mapema kuwa wewe sio mama yake mzazi.
Dala kumbuka sitaki binti yangu apate malezi ya hovyo nataka alelewe kwenye maadili mema , nidhamu na elimu bora na wewe ndio utakuwa msaada mkubwa. Pia usinisahau kuwa upo hapa kama mama wa mwanangu na sio mtumishi.
" Sawa nimekuelewa lakini kuna mengine unatakiwa kubadilisha.
" Sina cha kuongea zaidi nenda kapumzike. Uwe na usiku mwema.
Max alinyanyuka akaenda chumbani kwake na kumuacha dala akiwa amekaa.
" Mbona kama anataka kunibana sana na kuninyima uhuru wangu nilijua itakuwa kazi rahisi yani kama maigizo flani lakini masharti mengine yatanibana . Lakini inabidi nifanye kwasababu ya Sharifa. Dala alijiibgwlea mwenyewe badae akaamua kwenda kulala.
Kesho yake asubuhi na mapema Dala aliamka na kwenda chumbani kwa Shalon kumuangalia , alimkuta shalon bado Kalala ikambidi atoke na kwenda jikoni kuandaa kifungua kinywa . Wakati huo alikuwa kavaa night dress fupi iliyokuwa juu ya mapaja alichukua epron akavaa na kuanza kupika.
Max alikurupuka kutoka usingizini akajinyoosha baada ya hapo alielekea chumbani kwa Shalon alipofungua mlango alimkuta shalon anashuka kitandani.
" Habari kipenzi changu. Alisema Max huku akiwa anaenda kumkumbatia na kumbusu shavuni.
" Baba ,mama yuko wapi?
" Mmmm hebu twende tu kamuangalie. Alijibu Max sababu akuwa anajua kama bado yupo chumbani kwake au la.
Shalon alishuka kitandani wakashikana mikono na baba yake na kutoka nje ya chumba chake wakiwa kwenye korido walisikia harufu nzuri ya chakula
" Dady , mama anapika?
" Bila shaka atakuwa jikoni.
" Twende tumfuate
Walielekea jikoni na kumkuta akiwa kainama sehemu ya mwili na nguo yake ya ndani ilionekana Max alimzibaa Shalon usoni kisha akasema.
" Dala unafanya nini?
Dala alinyanyuka haraka.
" Kwani vipi si nipo hapa napima au sitakiwi kuingia jikoni na kupika?
Max hakujibu alitoa mkono wake usoni kwa Shalon kisha akaenda kuchukua kitambaa kilichokuwa kimetandikwa meza ya jikoni na kumfunga kiunoni.
" Unafanya nini?
" Hivi ni akili yako kutembea uchi ndani ya nyumba ambayo kuna mtoto ?
" Lakini alikuwa amelala...
Kabla dala hajamaliza kuongea shalon alimfuata na kumkumbatia.
" Mamaaa....
" Mwanangu mzuri umeamkaje?
" Salama.
" Haukuja kuniangalia .
" Nilikuja mama lakini bado ulikuwa umelala .
" Shalon nenda chumbani kwako kapige mswaki nakuja sasa hivi.
" Sawa lakini nataka mama aje.
" Sawa mwanangu nakuja sasa hivi acha niongee na baba.
Shalon aliondoka na kuwaacha wawili. Max alimuangalia dala usoni huku akiwa kakunja uso.
" Mbona unaniangalia vibaya?
" Sheria nyingine ya hapa ndani ni mwiko kuvaa nguo fupi , zinazobana yani ambazo hazina maadili hii ni nyumba ya familia sio bar wala danguro.
Aliongea max kwa ukali na kumfanya Dala amuangalie usoni kwa mshangao .
" Nadhani badala ya kuniiangalia ungeenda chumbani kwako kubadili huyo nguo.
Dala hakuongea kitu alivua eplon alafu akaelekea chumbani kwake huku akilalamika.
'' hii ipo nje ya makubaliano yetu kabisa yani nimekuja kulea mtoto lakini napangiwa kila kitu cha kufanya hata kuvaa nguo pia napangiwa nini nivae na nini nisivae.
Aliingia chumbani akafungua begi lake na kuanza kuchagua nguo ya kubadili
Alitoa dela refu na kuvaa kisha akarudi jikoni kuendelea na kazi huku malalamiko yakiendelea.
" Ona sasa hii nguo ndefu inavyonitega itasababisha nianguke.
Alikunja na kuibana kwapani.
Baada ya kuandaa kifungua kinywa aliwaita shalon na baba yake waje kula.
Max na shalon walikaa kwenye viti lakini shalon alikuwa bado kasimama.
" Vipi mbona umesimama? Max aliuliza
" Nasubiri ruhusa kutoka kwako boss , maana hukawii kuleta sher....... Kabla hajamaliza kusema alichotaka kusema max alimuita jina lake kwa ukali.
" Dala....
Shalon alitulia akiwa anawaangalia , max alipungua hasira na kusema
" Hebu kaa hapo tunywe chai kuna mambo mengi ya kufanya.
" Mama njoo ukae hapa , nipoozee chai yangu ya moto.
" Sawa binti yangu mrembo. Alisema dala huku akikaa kwenye kiti kilichokuwa karibu na shalon.
Maisha yaliendelea lakini max alikuwa ni mtu wa kumkosoa na kumpangia Dala jinsi ya kuishi pale ndani , alihisi Dala hawezi kumpa malezi mazuri binti yake kutokana na mazingira aliyotoka.
Siku moja majira ya saa kumi jioni baada ya shalon kuamka Dala alimuandalia juice wakakaa jikoni huku Shalon akimsimulia habari za shuleni kwao.
" Mama nataka kesho unipeleke shule wewe na baba .
" Sawa tutaongea na baba yako akikubali nitaenda.
" Kwani hataki uende?
" Hapana hawezi kukataa , tutaenda pamoja.
" Sawa. Alafu nataka kuangalia katuni.
" Sawa kunywa kwanza juice.
" Nitakunywa nikiwa naangalia katuni pia nilikuwa nataka na popcone.
" Mmmh mtoto unapenda uzungu wewe, sawa ni wakati wako baba yako ana pesa.
" Kwani wewe huna pesa?
" Mmm ninazo. Haya shuka kwenye kiti twende sebleni.
Walielekea sebleni Dala akawasha katuni wakawa wanaangalia katuni na michezo ya watoto. Dala nae alijisahau akawa amezubaa anaangalia katuni . Ghafla alishituka baada ya kuona kabondwa na kitu alipoangalia aliona popcone, alimuangalia shalon, Shalon alikuwa anacheka huku akiendelea kumtupia .
" Shalon acha kuchezea chakula.
" Ni mchezo nataka tucheze rafiki zangu huwa wanacheza na mama zao na mimi nataka tucheze, unikimbize.
Walianza kukimbizana huku wakirushiana mito ya makocha waliruka ruka kwenye makochi na kufanya kila kitu kukaa vibaya pale ndani.
Wakiwa wanaendelea kucheza mara Max alifika bila wao kujua. Alipoingia ndani alikuta kila kitu kipo hivyo.
" Dala unafanya nini?
Sauti ya Max uliwashitua wakaacha fujo zao, shalon alimkimbilia baba yake na kumkumbatia , walisalimiana . Huku Dala alianza kuokota mito na kuweka kila kitu sehemu yake.
Max alipiga hatua kumfuata.
" Ni nini hiki kinaendelea? Hii ni nyumba au soko?
" Dady usimuite Dala Muite mama Shalon kama baba Alice anavyomuita mama Alice.
" Nimekuelewa nenda chumbani nataka kuongea na mama yako.
Shalon alienda chumbani kwake akawa acha wao wawili.
" Dala haya ni malezi gani unayomlea huyu mtoto?
" Max unajua sikuelewi unataka binti yako aishi maisha gani hautaki kumpatia hata muda wa kucheza na kufanya akili yake ichangamke , yani akitoka shule anaoga kisha analala akiamka anakunywa juice anashika madaftari anafanya homework. Kuruka, na kuzunguka huko nje hutaki yani unataka akili yake ipoe na igande kama uji mzito uliopoa.
" Unanifundisha jinsi ya kulea mtoto wangu?
" Hapana , lakini kama umetaka niwe kama mama wa huyu mtoto nipe nafasi ya kumuonyesha malezi yangu.
" Haujawahi kuwa na mtoto .....
" Usiniambie kumalizia kuongea . Ni kweli sijazaa lakini nimemlea Shakira tangia akiwa mdogo na sasa yuko pale na akili yake inafanya kazi barabara. Licha ya kuwa dada yake nilikuwa nafanya kazi za ajabu lakini sikuwahi kukubali kuona anaharibikiwa.
" Kwahiyo ushauri wako ni upi?
" Nipe nafasi ya kuishi na huyu mtoto ndani ya mwezi mmoja utaona mabadiliko.
" Sawa basi usisahau kumfundisha hesabu na masomo mengine ya shule.
Dala alimuangalia kisha akasema.
" Sijawahi kuwa mwalimu wa hesabu ni mwalimu wa malezi. Na kuhusu elimu nisikudanganye nimeishia darasa la nne c kingereza nilikuwa najua egg, ball , apple na dog basi na masomo ya shalon ni kingereza tena sijui kiingereza cha wapi mimi nitaweza wapi kumfundisha ?
JE NINI KITAENDELEAAA!! "
OFAAAA KUPATA YOTE NI 1000 TU
NJO....
WHATSAP 0755090082.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.