Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

NILIZANI MWIZI KUMBE MMMM💘💐💘 SEHEMU YA (56)

5th Aug, 2025 Views 133



Nilijirushaa mbelee, khaa sikuamini hakiamungu yaan miguu yangu ilikuwa inanguvu kata nilipo taka kuanguka niliweza kujizuia et mungu wangu hii ninii

Nilibaki nashangaaa hichi kitu gani mungu wangu mi naweza kutembea nilisimama wima kwa miguu yangu nikiwa uchi kabisaaa hata sikujali

"Alex naweza kutembeaaaa!!!" Nilipiga kelele huku namwambia alex wangu
Nilipo mwangalia alikuwa amesimama kimyaa ananitazamaa tu mie yaan ni yule mtu aliepigwa na butwaa kabaki amezubaaa tu

"Alex!!!" Nilimuita tena yaani nina furaha walai nina furahaaaaaa

Yaan nilikiwa natakani nitoke mbio hapo muda huo huo mpaka nyumbani kwa miguu yangu

Jamani mie nina nguvu kabisa sio kwamba et ni dhaifu hakuna sema tu nimekonda mnooo yaan nimekondaaa vibaya sanaa

Alex alikuja haraka akanikumbatia jamani alini buss karibu mwili wote hakujali hata yale ma damu nilikuwanayo tena yananuka sanaaa

"Salma upo sawa" aliniuliza huku ananishika shika mwili wotee anatetemeka nikamwambia Alex mi nipo sawa alex
Yule babu ndo akatushtua akasema bado kazi haijaisha mama toka kwenye huo uduala hapo
Alikuwa anaongea huku anatazama juu ilibidi nasie wote tutazame juu

Ndo naona ule moshi mkubwa kweli unarudi chini kwa kasi kweli , tulitoka haraka na Alex wangu tukakimbia pembeni yaan hapo sina nguo na nilivyokondeana kama stick za meno ,

Alex alitoa shati lake kanambia vaa hii nilivaa haraka atleast lilikuwa lefu kidogo akavua na suruali yake akabaki na pensi ya ndani akanambia nivae
Nilivaa basi nilikuwa kama zile midoli za kufukuzia kunguru mashambani
Wanachomeka miti afu wanaivisha nguo mmh ndo nilikuwa mie yaan ni kituko aisee kituko

Ule moshi ulifika ukaingia ndani kwenye mbuzi kupitia lile Tundu alilochomwa na mkuki ,
Baada ya muda ulitoka tena ukapaa angani, yule babu akatuambia mi kazi yangu imeisha imebaki kwenu kukamilisha mlicho niahidi yaan anataka pesa ,mzee mshenzi huyu mfyuuuu

Alex alinikumbatiaaaa , yule babu akasema nyoosheni hii njia mbele kuna Bwana nenda kaonge hapo sasa hivi

Tulienda na Alex wangu akaniogesha yaan hakuna aliekuwa anaamini walai tena
Mimi.mwenyewe siamini aisee siamini , nilivaa tena zile zile nguo za alex japo zilikuwa chafuu tayari..

Alex akanambia nataka nikubebe mke wangu nikamwmbia jamani vile nin hamu ya kutembea alex weee embu niache mie nitembee yaan hapa nina hamuuu nikimbie hata hapa na dar ujuee ,,
Alex alicheka akasema sawa kwahiyo wiki ijayo tufunge zetu.ndoa et

"Haa we alex mi hivii nilivyo mifupa.Gauni halinitoshi bwanaaa"

"Unataka tena tusubiri aaah mi sitaki hivyo Salma"

." Hahaha Ngoja basi tufike hata nyumbani bwanaaa".

Yaan tulikuwa na furaha sana ,tunatokeza tu
Pale kwenye mtu , inno alikuja mbio akanibeba Juu juu jamani ni alinibusu alinibusu mpaka mdomoni afu mbele ya Alex na Subira wake

"Jamani dadaaaaa!!!" Subira nae alikuja mbio huku analia ,zakia nae alikuwa analia

Alex akawaambia nyie mnalilia nini wakati leo tunatakiwa kufurahiii , yaan anaongea huku na yeye analiaaa
Inno akamcheka kweli et we jamaa huachagi mambo yako wewe , embu twendeni huku kwanza

Inno alichukua simu akaanza kupigia watu wote nyumbani yaan hakuna aliekuwa anaamini mama anasema embu njooni sasa haraka bado mnafanya nini hukooo
Alex alimuahidi yule babu kuwa kesho atazileta pesa zote alizomuahidi
Kiukweli nilikuwa namchukia sana huyu babu japo alinisaidia kwanza nilikuwa nawaza ina maana tusingekuwa na pesa mi nilikuwa nakufa hivi??

Yaan haya ndo yangekuwa maisha yangu mpaka nakufaa??

Nilimchukia hata sikumwambia asante wala shukrani wala sikumchekea yaan hata kumtazama kabisa sikutaka
Kwanza alex alikuwa anamchekea chekea anamwambia babu tunashukuru sana mi nawaza huyu nae sijui analishukuru la nini hilii

Nahamu kwanza ya kwenda kutazama watoto wangu mie , yaan nina hamu ya kuwapakata watoto wangu hata kwa hii ya mwisho wasikie joto la mama yao japo kunyonyesha ndio siwezi tenaaa ..

Yule babu alinipa dawa za kuoga na kupaka kwenye kidonda hata hivyo.kilikuwa kimekauka tayari
Alituaga ananiongelesha mie anajichekesha mi nimekaza kweli kweliii
Nilimuuliza hivii , ile muda ndio tunatoka nikamgeukia nikamuuliza

"Kwahiyo, Juddy akija kukupandia dau ugonjwa utarudi kwanguuu???" Nilimuuliza tena sauti niliikaza kwa hasira nilishindwa kabisa kujizuiaaa

"Aah kwanini bint mi sitibu mtu kwa sababu ya pesa bint yangu " alinijibu huku anajichekesha

"Mmmh vizuri , jitahidi sana kufata utu ja si kudhuru kila mtu"
Alex alinishika mkono akaniminya , nikageuka kuondoka zangu

Nilitembea huku kila hatua yangu ninamshukuru mungu wangu yaan huu ni uponyaji wa hali ya juu amenifanyia nilimshukuru sana et.leo naweza kuongea naweza kutembea tena gafla hiivii asante mungu wangu

Tuliingia kwenye gari na safari ya kurudi Dar ilianza zakia alikuwa ananiomba msamaha humo kila sec jamani namwambia zakia mdogo wangu mi sina tena kinyogo na wewe lakini sihitaji kukaa Karibu nawewe nashkuru kwa kunisaidia huwenda yale maombi yetu naamini ndio yamekuleta kwetu mungu akubariki kwa hiloo

Tulifika nyumbani hapo kulikuwa na ndugu kibao yaan , mama yangu alilia sanaaa alipo niona akasema mungu mungu mkubwa jamani ana njia nyingi za kuponya,

mama mkwe akaniletea watoto wangu sijawahi maskini kuwakumbatia mpaka sasa wanatambaa yaan niliwabeba huku nalia jamani watoto wangu wamefanana na mimi mtupuuu yaan hakuna hata mmoja aliefanana na alex

Nikamwambia alex mbona hawa watoto wamekutaaa hivyo akasema sio kweli we ndio wamekukataa
Nikasema mmh sio.kweli akasema we huoni Wamechukua kikojoleo changuu

Yaan niliona aibuuu mana alinambia mbele ya kina mama hahaha nilicheka tu kujibalaguza ila nikapitisha mkono wa chini nilimsinaaaa

ITAENDELEA.....
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NILIZANI MWIZI KUMBE MMMM💘💐💘 SEHEMU YA (56)  >>> https://gonga94.com/semajambo/nilizani-mwizi-kumbe-mmmm-sehemu-ya-56
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Ratiba ya Simulizi

  • USINITANGAZE 02 ❤❤ 05-08-2025 19:00

Ratiba ya Simulizi

  • USINITANGAZE 03 ❤❤ 06-08-2025 04:00

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest