ENDELEA......
Samir alifumbua macho na kuanza kutalii humo chumbani. Alishangaa baada ya kuona mapambo kitandani yaliyoambatana na neno tamu kuhusu yeye. Alinigeukia na kunikumbatia Kwa hisia.
Kwa mala ya kwanza akili Kwa kinywa chake kuwa ananipenda.
"Nakupenda sana mke wangu Nadra". Aliyasema hayo Kwa hisia Kali huku akiwa amenikumbatia.
"Nakupenda pia mume wangu. Usije ukaniacha kwaajili ya walimwengu wenye Hila na penzi letu".
"Amini wewe ni wangu milele. Siwezi kukuacha mama. Kwa muda mchache tu umenibadilisha wallah najiona mpya kabisa". Samir aliongea hayo na pasipo kutarajia machozi yalianza kumtililika mashavuni. Kwakweli tulilia wote. Mapenzi ni hisia na hisia zenyewe ndo kama hizo Sasa.
Tuliachiana kwenye kumbato. Samir alinibusu kwenye paji la uso kama kawaida na baada ya hapo alinibusu mdomoni yaani romance ya kibabe. Nilimponyoka kwenye lile romance maana tulipokuwa tunaendea ni kule kwenye mchezo wa kibaba na kimama alafu mie nilikuwa na jambo langu.
Samir aliniangalia Kwa hisia Kali sana ni dhahiri alikuwa amezidiwa.
"Umependeza sana Leo". Alinimwagia sifa humu akiendelea kuniangalia kwa jicho la huba.
"Asante". Niliitikia kwa viaibu vya kizushi tu. Nilimwambia Samir akaoge, alienda kuoga na mimi nilimuandalia nguo za kuvaa. Baada ya kumaliza kuoga alikuta nimeandaa nguo nzuri za kuvaa alibaki kunishangaa.
"Tafadhali mume wangu usiniulize chochote. Naomba uvae". Samir alifanya nilichomwambia, tulikuwa tumevaa rangi sale. Shati alilovaa samiri ni la Pink na suruali nyeupe, mimi gauni la pink na mtandio mweupe. Tulinoga balaa.
Nilimuomba nimfunge kitambaa usoni alikubali, nilifunga kitambaa usoni na kuanza kumuongoza Kwa kumshika mkono. Tayari ilikuwa ni majira ya saa Moja usiku. Tulifika chini Sebleni nilifungua kitambaa usoni hatukuona chochote zaidi ya giza.
"Nadra!". Samir aliniita.
"Abeee!. Niliitikia kwa sauti nyororo😁.
"Kuna nini kwani mbona tupo hapa. Alafu ni giza?". Kabda sijamjibu taa ziliwashwa na mauwa yalitokuwa yanatokea juu kutuangukia. Sauti za watu mbali mbali ziliimba nyimbo ya happy birthday.
Siku hiyo ilikuwa ni kumvukizi ya siku ya kuzaliwa Kwa mume wangu kipenzi Samir.
"Happy birthday my love husband Samir". Nilimwambia hayo Kwa sauti nyororo. Samir aliniangalia Kwa furaha na bila aibu alinibusu mdomoni pasipo mimi kutarajia. Watu walianza kupiga makofi huku waliendelea kumuambia.
"Tuliachiana kwenye busu na baada ya hapo Samir alishangaa umati wa watu uliokuja kufarahi pamoja nae kwenye siku yake muhimu.
"Happy birthday my son". Mama mkwe wangu alimsogelea mwanae na kumtakia heri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake.
Samir Alimkumbatia mama yake kwa furaha
"Asantee sana mama yangu". Aliyasema hayo na tayari machozi yalimtililika mashavuni. Mama yake alimfuta machozi Kwa mikono yake.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki walioudhuria nao walimtakia heri na kumpa na zawadi. Upande wa familia yangu alikuja mama, hilliam na Husna dada wa kazi.
Samir alikata keki na kuanza kumlisha mama yake na baada ya hapo alifuata Mimi na mama yangu. Baada ya Mimi alimlisha dada yake Najma na kufuatiwa wengine. Samira hakuwepo mpaka muda huo. Baada ya tulio la keki kuisha. Tuliendelea kupiga story mbili tatu na ndugu jamaa na marafiki huku mziki laini ukilia kwenye sabufa.
Kila mtu alikuwa busy na story. Mama yangu alikuwa na mama mkwe wangu wanaongea, Mimi nilikuwa na mdogo wangu pamoja na Husna tunaongea. Samir alikuwa na marafiki zake. Na ndugu wengine walikaa kimakundi wanaongea huku msosi ukiandaliwa.
Baada ya chakula kuandaliwa. Tulikusanyika wote kwenye zurio kubwa na kula Kwa mtindo wa mduara. Tulipokuwa tunaendelea kula kwa furaha.
Samira na kundi la marafiki zake wa kike na wakiume walikuja. Walipoingia tu Samira alichomeka flash kwenye sabufa na kuweka sauti ya mwisho kabisa.
Walianza kucheza Sasa. Wewe sio Kwa mauno Yale basi na wale wanaume walikuwa wanawabaishia nyie aibu yake hiyo jamani sio ya nchi hii. Samir wangu alisimama Kwa ghadhabu alipotaka kumsogelea mwanae mama yake mdogo alimzuia.
Tulibaki wote kuwatazama tu huku ndugu wakinong'onezana chini chini. Nilimpandisha juu gorofani muda mchache nililudi sebleni nikiwa nimebadili mavazi. Namna nilivyovaa watu wote walinishangaa. Nilivaa kigauni kiufupi tena kilikucha Cha Samira mwenyewe.
Samir alibaki kuniangalia kwa hamaki, sio yeye tu watu wote. Nilisogeza mbele walipo wakina Samira nilizima mziki na kuwasukumba Samira na marafiki zake wakike. Nikawa nimesimama katikati ya marafiki wa Samira wa kiume. Nilimwambia mmoja wapo awashe sabufa. Mmoja kati ya rafiki wa Samira aliwasha sabufa.
MTUNZI NA MUANDISHI WA SIMULIZI HII NI MIMI NURU HALISI. WHATSAPP NAMBA 0683009150.
"Nataka kucheza na nyie na ule wenu msicheze". Niliwaambia wale wavulana. Tulianza kucheza Sasa. Wewe niliachia mauno hayo watu wote walibaki midomo wazi. Huku wale wavulana nao walichachuka kunibaishia japo kwauoga uoga tu maana hawakunigusa walikuwa wanasimama hatua Moja nyuma. Samir alikuwa amekasirika balaa. Alikuwa ananiangalia jicho la chuki ila mie Wala sikujali niliendelea kuachia mauno ya uzazi sikujali kama Kuna wakubwa na wadogo wananitazama...............Huyu Nadra huyu kiboko 🙌🤣🤣🤣......Muendelezo mpaka mwisho 1000 tu alafu hii story bado ndefu sana, ina vipande zaidi ya 30.
.