Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

NDOA YA MIE .9.

5th Aug, 2025 Views 2


MTNZ: ZAMRATA MBWANA (ZM)
NO: 0698095257

Tulipo 🌷 Ishia Ni Pale Imeletwa Barua ya Uchumba kwa Kina Zenafa ...

Songa Nayo...

Basi Ilipangwa Siku kwaajili ya Kuisoma Barua ya Posa au Uchumba . Kwa Kina Zenafa na Aliitwa Shekhe Pia Baba yake Zenafa Alikuwepo na Alikuwa Anatembelea Magonga Kuendelea Kuuguza Mguu wake hadi utakapo pona Kabisa

Wote Walikusanyika ikiwemo Zenafa na Dada zake na Mama yake wa kambo . Dada Zake Walikuwa Wameoga na Kujiremba Vizuri huku Wakiwa Wamejitanda Ushungi Vizuri . Tofauti na Zenafa Yeye Alikuwa Yupo yupo tu hana Habari . Basi Shekhe Alianza Kufungua Kitambaa Kilicho fungwa na pini katika Barua na Alichukua Bahasha na Kuifungua na Kuanza Kuisoma kwa Kutafsiri Maneno ya Kiarabu

Shekhe: "Asalam_Alehkum"

Mama Amina na Wanawe "Waleikum _ Msalamu Shekhe "

Shekhe Alianza Kuisoma na Kumalizia "Barua hii ya Kuomba Ulafiki kati ya Mwanangu Mahili Kazumari na Binti yako Zenafa "

"Eti nini " ?!!!!!
Wote Waliitikia kwa Mshangao
Hawa: "Eti umepigaje hapo Shekhe "

Shekhe: "Nazani Mzee Rajabu Mimi nimeishia hapo Kusoma ndo Wamemaliza ivyo na Wameweka Kiasi cha Shilingi Laki moja kama Kiomba Ulafiki Au Barua ya Uchumba "

Shekhe Alimaliza Kusoma na Kuinuka Mzee Rajabu Ambae ndo Baba yake na Zenafa Aliichukua elfu 5 Kwenye Zile hela na kumpa Shekhe kama Asante ya Kumsomea ile Barua

"Shukrani Shekhe "

"Asante Bwana Rajabu "

Shekhe Alianza Safari ya Kuondoka Zake huku Amina na Hawa Wakiwa Awaamini Macho yao kwa Kilichotokea huku Wakiwa Wanahisi Joto la Ajabu Walivua Mashungi yao na Kuanza Kujipepea .

Amina " Haiwezekani Aitwe tena yule Aje Aludie Kusoma tena Hii Barua Mimi na Wasi wasi Amekosea Kuisoma tu , Hapo Ajatajwa Zenafa "

Baba "Kwani Msichokiamini hapo ni kitu gani ? Ndo hivyo Mwenzenu ndo Ashapata Bahati Na Barua haijakosewa chochote kilicho andikwa umo ndo kilichosomwa Na haiwezekani Kuwa Amina au Hawa na Wakati Linasoma Zenafa "

Hawa" Aisee Kweli Uchawi hupo yaani Mwaka huu ndo nimeamini kama uchawi kweli upo Siku zote Nilikuwa Nasikia tu "

Zenafa Mda wote Hakuongea Neno Alibaki na Alama ya Mshangao Alivulugwa kwani Hakujua hizi Habari Zimeanzaje na Zimekuaje kuaje hadi Kufikia huku

Baba "Enhe Zenafa Nazani hizi taarifa za Posa unazitambua Sindio "

Zenafa: "Baba . Yaani Sijui ata nianzie wapi yaani Sijui kitu Chochote kuhusu Iyo Posa "

Baba "Khe! Maajabu na hili Jina la Mzee Kazumari Sindo Mtu Alienisaidia Mimi Gharama ya Matibabu Hospital "

Zenafa " Ndiyo Baba hilo jina ni Lenyewe "

Baba "Anha na Mahili ata kuwa ni Kijana wake , Mahili Kazumari "

Zenafa : "Anha Naanza Kuelewa Sasa Kumbe Kunisaidia Kote kula nia yake nije niolewe na huyo Kijana Wake Mahili"

Mama na Wanae : Wote "Khe ! Makubwa "

Zenafa Alijikuta Anapandwa na Hasila na Aliinuka kwa Jazba na Kuanza Kukimbia Kuelekea kwa Juma . Alifika Mashambani Akiwa Anahema mno Na Alikutana na Samson

"Habari Mrembo "

"Juma yupo wapi ?"

"Tulia Kwanza Shida ni nini "

Zenafa Alikaa chini huku Akiwa Anahema sana. Samson Alitoa Simu na Kumpigia Juma na Baada ya Muda kidogo Alikuwa Kashafika

"Zenafa "

"Juma Wewe ni Rafiki wa Aina gani niambie Ulikuja kwenye Maisha yangu kwa Lengo gani niambie leo hii Juma ?"

Zenafa Aliongea huku Machozi yakimmwagika kwaUchungu .

"Sikia nikwambie Zenafa . MimjSijaja kwa nia Mbaya katika Maisha yako "

"Kwaiyo mlimsaidia Baba yangu ilinije niolewe na huyo Mahili wenuSindio?

"Hapana! Hapana Zenafa Haipo hivyo "

"Sasa Basi Mwambie huyo Mzee Sipo Tayari kuolewa naUyo mtu Sijui ndo Mwanae Sijui ni nani yake Simtaki na Aniache na Maisha yangu Tafazari "

Zenafa Aliongea huku Machozi yakimtoka na Kurudi Kwao Upesi

Baba : "Zenafa Binti yangu Kwaiyo umeamuaje Mpaka Dakika hii ? Kuhusu hii Barua ya Uchumba ?"

Zenafa : "Baba Mimi Simtaki huyo Mwanaume Sitaki Kuolewa nae Mimi "

Baba : "Oh! Jibu Zuri Sana , Haya Kuolewa utaki na hapa Nyumbani Unafanya nini Cha Maana ?"

Zenafa : "Baba Mimi nitaolewa na Mwanaume nitakae Mpenda na Sio uyo "

Zenafa Alijibu kwa Hasila Huku Mdomo wake Akiwa Kauvuta Mbele

Baba : "Sawa Kumbuka huyu Mtu Ndo Alienilipia Mimi Pesa Hadi Kufika hapa Sikumuona Mtu unae Mpenda Wala Unae Mtamani , Haya Yote Uwoni Barua tu Kaweka Laki 1 We Mwenyewe Shahidi Barua za Hapa Kijijini ni Elfu 5 tu imezidi Elfu 10 Mahali elfu 50 tu haya huyu Laki 1 ? Unajua Uwezo wa Mimi Baba ako laki 1 Sijaishika kwa miaka Alafu Leo Umepata Bahati unaleta Ujinga . Apa Nyumbani Unafanya Kipi Kikubwa mno niambie ? "

Zenafa : "Yaani Baba Pesa Ndo Unataka Kuniuza Mwenzio Sindio "

Baba : "We Kelele wewe . yaani Una Bahati Naumwa Mguu ningekuwa Mzima Ningekupiga. Isiwe Shida Siumesema Utaolewa Na Mtu unae Mpenda haya Sasa Nakupa Wiki tu Iletwe Barua ya uyo Mwanaume Unae Mpenda "

Amina : "Yaani Kweli Upele Unampata Asie na Kucha yani iyo Bahati Ingenikuta Mimi na hivi Nilivyochoka Kudanga Mbona Ningemwambia uyo Ba Mkwe Aje kunichukua hata Saivi. Yani Yule Mzee Alivyo na Pesa Ata uyo Mwanae Akiwa Taila Tutajuana huko huko "

Hawa: "Yaani Wote Nyinyi naona Mna Bwata tu kwani Aiwezekani tukabadilisha nikaolewa Mimi "

Amina na Mama : "Kheee! Makubwa "

Juma Alikuwa na Mawazo Juu ya Maneno Aliyo Ongea Zenafa Na Moja kwa Moja Alikutana na Mzee Kazumari Kwenye Baa Moja ya Hapo Kijijini na Waliagiza Chipsi na Juisi Nakuanza Kula

Mzee Kazumari : "Enhe Juma Mbona upo ivo Sijakuzoea hivyo Leo Umepooza sana nini tatizo Kijana Wangu ?"

Juma : "Nikuhusu Zenafa Mzee Alinifata Baada ya Kupeleka ile Barua "

Mzee Kazumari Alishtuka mno baada ya Kusikia hivyo na Aliacha Kula zile Chipsi

"Enhe! Akasemaje ?"

"Mh! Kaja Kunilaumu sana . Nakuwa Hayupo Tayari Nakasema Nikufikishie ujumbe Kumsaidia Baba yake isiwe Sababu ya kutaka Aolewe na Kijana Wako "

"Du! Ndo Alivyosema hivyo Zenafa "

"Ndiyo Mzee "

Mzee Kazumari Alijisikia Vibaya mno

"Da! Sijui ni Kipi nafanya Au laa ! Labda nikweli Nakosea lakini Namhitaji sana Zenafa Awe Mkwe Wangu Awezi Kunielewa Kwasasa ila ni Muhimu kwake pia Zaidi Kwa Kijana Wangu . Mh ! Acha tuone itakavyokuwa Mwisho wake "

Mzee Kazumari Alionyesha Kukata tamaa Kabisa Kuhusu Suala la Zenafa kuolewa na Kijana Wake Mahili

Wiki Ilipita Sasa na Hatimae Majibu ya Barua Yalitoka Sasa na Kufika kwa Mzee Kazumari

Akiwa Katika Hotel Ndogo ya Kijiji cha Hapo Alipopanga Alikuja Shekhe kwaajili ya Kumpatia Majibu Mzee Kazumari . Ambae Alikuwa na Juma kwa Wakati uwo Katika Chumba cha Mzee Kazumari

Walisalimiana na Shekhe Alianza Kutoa Majibu

"Anha. Haya ndo Majibu yetu yanayotoka kwa Mzee Rajabu Juu ya Binti yake Zenafa "

"Ndiyo Shekhe tunakusikiliza "

"Mzee Rajabu Amekubali Ulafiki Kati ya Mahili Kazumari na Zenafa "

Mzee Kazumari ; "Oh ! Asante Mungu tena Asante sana kwakujibu Ombi langu "

Mzee Kazumari Alijawa Nafuraha mno Baada ya Kupata uwo Ujumbe kutoka kwa Shekhe . Lakini Juma Hakufulai sana Alitulia Kimya kwa Muda . ShekheAlimtajia Gharama Zote Mzee Kazumari Na Mahali kila kitu Jumla milioni 1 . Na Shekhe baadae Aliondoka Juma Alimpongeza Mzee Kazumari kwa Ushindi

Juma Aliludi katika Chumba chake Kilikua ni Cha pili Kutoka Chumba cha Mzee Kazumari Alifika na Kukaa Kitandani Alitulia Kwa Muda na Machozi yalianza Kumtoka

"Umefanya nini Zenafa ? Umekubali kuolewa na Mtu Usiye Mjua unafikiri utaweza ? nilijua ungekataa Zenafa Nakupenda Nilitaka nikwambie Nakupenda tena Siku ya Kwanza ndo ivo tu Majukumu Ya kazi Siwezi kuvumilia unaolewa na Mahili "

Alisema Juma huku Machozi yakimwagika kwa Uchungu kumbe Alikuwa Anampenda Zenafa toka mda ....

Iyo ndo Yes Boss huku Moyoni unaumia ...

ITAENDELEA 10.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NDOA YA MIE .9.  >>> https://gonga94.com/semajambo/ndoa-ya-mie-9
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

RATIBA YA SIMULI ZETU

Ratiba ya Simulizi

  • USINITANGAZE 02 ❤❤ 05-08-2025 19:00

Ratiba ya Simulizi

  • USINITANGAZE 03 ❤❤ 06-08-2025 04:00

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest