Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

Nipe yote Dady 52~53

5th Aug, 2025 Views 51



Selim nilipokea na kuongea "hello babe "
hakujibu akauliza "uko wapi ?'" Nilikaa kimya kwa sekunde maana nilihofia kwann asijibu salamu yangu ila kauliza niko wapi.

Sasa nilivyo mjinga nikamdanganya kuwa niko kazin,akajibu poa na kukata sm nikampigia tena hakupokea nikamtumia meseji na kumuuliza "babe ni shida mbona kama hauko sawa" ujumbe ilifika ila hakujibu mh nikaona hapa kuna kitu .

Sasa nika mpigia sim Nasra na kumuuliza kama walishatoka kazin akasema bado kwann nikajibu hapana napiga sm yake hapokei ,akawa amesema huenda akawa bz basi alivyonijibu vile nikatulia mda huo huo akingia Jacob .

Tulisalimia na kukaa akaagiza kinywaji na kuanza kupiga story za enzi hizo ikawa full kicheko , tulipiga sana story mpaka mda ulipoenda nikaaganae na kuondoka nyumbani.

Sasa nafika nyumbani Selim hakuwepo ila Nasra alikuwa ameshafika nikaona kumuuliza itakuwa kama naonesha hatuko sawa basi nikamtafuta Selim hakupokea sm nikatuma na text hakujibu , wasi wasi uliniingia nikajiuliza huyu mtu vp mbona amekuwa tofauti.

Niliwaza nikahisi huenda nitakuwa nimekosa ila mbona sioni kosa langu lilipo basi nikaona ngoja nipike chakula kile anachopenda ili kama anamood mbaya nimsaidie kuwa sawa.

Nikaingia jikoni na kuandaa chakula ila tayar Nasra alishapika sasa kwakuwa nilikuwa nimetaka kumpikia kile anapenda nikapika , Nasra akaja kunipa kampani huku tukipiga story jamani kipindi hiki Nasra alikuwa tofauti sio kama kipindi kile alichokuwa anajifanya mpole na kujifunika funika sasaiv alikuwa mtu wa tofauti kwanzia ongea baadhi ya tabia hata kuvaa hakuwa akijufunika kama zamani zaidi akawa anavaa kawaida tu.

basi nilipika na kusubiri arudi nakumbuka mda huo ilikuwa saa moja na mda ambao huwa anarudi ni saa kumi na moja , baada ya kuweka kila kitu vizuri nikakaa seblen huku tukicheza game na Salum (mtoto wa Nasra ).
Mda ulienda mpaka ikafika saa mbili uvumilivu ukanishinda nikaingia chumbani na kumtafuta Jabir maana nae alikuwa hajarudi, alipopokea nikamuuliza akasema hajui wala hajaongea nae toka asubuhi.

Mh nikaona sasa hapa usikute kukawa na shida na sijui nikamwambia mama mkwe kwamba mwanao hapokei sm zangu sijui yuko kazin au kwenye folen , mama mkwe akaniambia huenda atakuwa bize kazin akamuuliza Nasra akamjibu kuwa walitoka wote ila akasema ana apointmet na mtu .

Kusikia hivyo nikatulia japo kichwani nikawa nawaza hiyo appointment ni yanani mpaka ashindwe kupokea sm zangu, basi bwana saa tatu na robo ndio akafika mtoto wakike nikatoka na kwenda kumpokea hata kabla hajashuka kwenye gari.

Alifungua mlango nikamsalimia akajibu kama vile anahasira na mimi ila nikaona subiri apumzike kwanza ndio nijue shida nini , tukaingia ndani moja kwa moja hadi chumbani nikataka kumsaidia kuvua akakataa na kusema yuko sawa kuvua mwenyewe.

Sikutaka ugomvi nikakaa pembeni na kumuangalia akaenda kuoga ,nikamuuliza kama anataka kulia chakula chumbani au mezani akataka mezani .

Basi tukaongozana mpaka mezani na wengine wakakaa maana wote walisema hawawezi kula mpaka baba mwenye nyumba afike , baada ya kukaa mezani kama kawaida nikataka kumpakulia akakataa na kutaka kupakua mwenyewe mimi haya .

Akachukua sahani na paya ya kupakulia akamuuliza Nasra " huu wali umepika wewe ee?" Nasra alijibu ndio nikawahi na kusema .

"Chakula chako hiki hapa" niliongea na kumsogezea hotpot cha ajabu aliisogeza pembeni bila kuongea chochote na kuchukua kile alichopika Nasra akapakua na kula huku akimuongelesha mambo ya kazin.

Nisiwe muongo nilijisikia vibaya ila nikajikaza na kuchukua kile chakul nilichokuwa nimemuandalia nikapakua na kula , story zao zikabadilika mpaka kwenye kuhadithiana movies sijui hata lini nimewahi kumuona Selim akiangalia Movies kwanza hua hapendi ila nashangaa wanaanza kuhadithiana .

Nilikaa kimya huku nikiendelea kula alipomaliza akainuka na kumshukuru Nasra kwa kuchakula na akasifia kuwa anajua kupika sana .

Nasra alijibu asante na kusema "ila chakula changu hakijawahi kuwa kitamu kama cha Norah kwa hiyo usinijaze"

Selim akamjibu " Nikitamu kwa macho ila mdomoni hakina radha " nyie nilivyokuwa najisikia najua mwenyewe nilikula chakula ila nikawa nahisi hakishiki .

Basi bwana nilivyomaliza kula nikaamka na kutoa vyombo alivyotumia Selim na vyangu nikaaga na kwenda chumbani,nikamkuta Selim yuko bz na pc yake ,nilikaa pembeni yake na kujilaza begani akanitoa haraka na kusema " niko bz alafu nimechoka ".

Nilimuangalia na kusema "Mume wangu nimekosa nini mbona unahasira na mimi?" alinigeukia na kuniambia "kwann niwe na hasira na wewe ?'"

'"Sijui ila naona wazi una hasira na mimi na sijui shida nini"

"Sina mda wa kupoteza kwa vitu vyakijinga namna hii "

"Okay je kuna mtu amekukwaza huko kazin au kuna mambo hayaendi sawa ?'"

"Norah mbona unakuwa na akili nzito nimekwambia hamna kitu unakazana kuongea shida yako nini haswa"

"Selim we ni mume wangu nimeishi na wewe mwaka wa sita sasa nakujua vizuri hivyo tafadhali kama kuna kitu nimekosea nisamehe mume wangu na kama kuna kingine huko ofisin niambie "

"Nikwambie ili iweje ?"

"Ili tuweze kuongea na kuona namna ya kuweka sawa "

"Unafikili nimambo ya kijinga kama unayoshinda unafanya siku nzima au kazi yangu inaonekana inaweza kufanyika hata namtu asie na akili"

"Selim "

"Naomba mda wa peke yangu " nilitaka kuongea akainuka na kuondoka ,nilibaki nimekaa namuangalia majibu yake yaliniumiza niwazi anahasira na mimi lakini nimefanya ninu mimi mpaka kufikia hatua ya kunifanyia hivi.

Nilikaa dakika kadhaa nikatoka na kwenda kumuangalia alikoenda nikakuta seblen hayupo chumba cha kazi hayupo nikazunguka kwengine nikakuta hayupo .

Nilipomkosa nikapanda juu nako hayupo eeh nikaona bwanae atakuja kulala mwenyewe nikapanda kichumbani na kusogea dirishani nikitaka kufunga dirisha

sinikaona Selim amekaa na Nasra nyie moyo ulifanya paa nikataka kushuka ila nikasita na kuvuta kiti pembeni na kukaa nikawaangalia kibaya nikawa sioni nyoso zao maana walinipa mgongo .
Basi nilikaa kwa mda mrefu wakiwa pale walipochoka kuongea wakainuka na kuondoka na mimi nikarudisha kiti sehemu yake na kupanda kitandani kimyaa

Alikuja na kupanda kitandani akanipa mgongo na kulala , kesho yake asubuhi nikaamka na kuandaa chai nikarudi chumbani na kumuamsha ili ajiandae akaamka bila hata kuitikia salamu hakuitika akainuka na kuingia bafuni.

Mimi tena nikachukua nguo zake na kupasi kisha nikashuka chini kumuwekea maji kwenye chupa yake ,akaja Nasra na kusema "hee unamtengenezea maji mengine tena maana nilikuwa tayar nimeshatengeneza "

Nilimuangalia kwa tabasamu kisha nikamshukuru na kuweka yale maji kwenye friji akasema "haina shida mpe tu hayo haya nitakunywa mimi "

"Sawa kama utabeba poa ila usijilazimishe anaweza kunywa akirudi hayana shida" nilimjibu na kuondoka nafika chumbani nakuta amevaa nguo zingine tofauti na zile nilizomuwekea

Nikamuuliza kwann akajibu hajazipenda basi nikakaa kimya akavaa na kuondoka bila kunywa chai ,nilibaki najiuliza maswali mengi nisipate jibu sahihi .

Siku iliisha akiwa hivyo hivyo kesho yake tena ikapita mambo ni vile vile aisee nilihisi kuvurugwa maana nibora mtu akununie kwa kosa unalolijua au ujue hayuko sawa kuliko vituko alivyokuwa ananifanyia Selim.

Nilijitahidi kushuka nakuuliza nini shida ila hakuongea la maana zaidi ya kunitolea kauli za kashfa , nikavumilia bado nikapika vyakula anavyopenda hata chumba nikatandika na kuweka zile rangi anazopenda ila wapi nikasema labda hataki hivi ninavyovaa nikaanza kuvaa kistara ila wapi mwisho nikachoka na kuwa mkali ili kama anakitu aseme na kama hanitaki tena pia aseme

Weee nilivyoongea hivyo aliwaka akafoka sasa namimi ninatabia nikishapanick huwa siwezi kuongea kwa sauti ya chini na sio sauti tu hata neno likija ziwezi kulichuja sasa sinikaanza na mimi kufoka yani foka nifoke ukawa ugomvi haswa

Mara nyingi mtu mwenye hasira huwa hawezi kuongea uongo ataongea lile liloujaza moyo wake ,kwa sauti na uhakika Selim alinitamkia kuwa anajuta kunioa kwani wakati ananipenda aliniona mwanamke ninaejiheshimu na kujithamini ila amegundua mimi ni malaya na ninatabia chafu nikheri Nasra .

Hiyo kauli ilikuwa zaidi ya kofi au ngumu yani nibora angenipiga kuliko kukiambia vile mimi malaya nina tabia chafu kheri Nasra kwamba anajutia kuwa na mimi ? kwa lipi ina maana sasahivi anatamani angemuoa Nasra sio mimi .

Nilikaa kimya machozi yakanitoka taratibu nikaa chini ,hakuongeza neno akafungua mlango na kuondoka wala hakurudi tena usiku huo
KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Nipe yote Dady 52~53  >>> https://gonga94.com/semajambo/nipe-yote-dady-52-53
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Ratiba ya Simulizi

  • USINITANGAZE 02 ❤❤ 05-08-2025 19:00

Ratiba ya Simulizi

  • USINITANGAZE 03 ❤❤ 06-08-2025 04:00

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest