Rahul akatoka haraka kuelekea alipo Mr Alberto ,
Masaa matatu masha ndio alikuwa anaachiwa kwenye mikono ya Boazi anahema kama ametoka kwenye mashindano ya mbio miguu inamtetemeka
Mbio alizokimbizwa hazikuwa zile alozoea
Akasimama kwenda ndani miguu ikakataa akajikuta anarudi tena kwenye kochi
Boazi akamtuliza avute pumzi , hapo ilikuwa ni kimya kimyaa...
Rahul akafika hospital ,Mr Alberto alikuwa akimsubiri nje
"Daah utanifanya nichanganyikiwe ujuee!!" Rahul akalalamika kiutani
"Bora wewe aisee mie ndo nilikuwa na data "
"Ilikuwaje??"
Mr Alberto akamsimulia jinsi alivyokutana na hiyo ajali
"Twende basi nikamuone"
"Amelala kesho utamuona "
Rahul alikuwa anafahamika hapa kwamba boss wao hakuna aliekuwa anamjua mr Alberto, kwahiyo alivyofika Rahul alimtambulisha Mr Alberto kama V.V.I.P Customer
Kwasababu mwenyewe hakuwa tayari kujulikana kama ndie mmiliki wa hapo
Walipiga story sanaa na Rahul wakapeana habari nyingii, lakini Mr Alberto alipo omba simu ya Rahul ampigie simu masha , Rahul akamwambia kesho utazungumza nae itakuwa ameshalala usimsumbue
Hakuwa tu anataka aongee na masha , Sio mashaa tu hata Rahul hakuwa anampenda wala kumkubali kabisa masha siku zote alikuwa anasema Masha ni Gold Digger yaan msichana mwenye Tamaa nyingiii sanaa
Mr Alberto alimuomba Rahul akapumzike wataonana kesho , Rahul akamshauri waondoke wote yeye atatafuta Muuguzi mmoja watamlipa ziada ili akae kumuuguza Vicky mpaka atakapo pona
Lakini Mr Alberto alikataa akamwambia yule dada ni mjamzito mimi ndio nimesababisha awe vile kwahiyo nitawabika hata usijali
Rahul hakubishana nae sana mana anamjua boss wake huwa anajali sana watu kuliko hata yeye anavyo jali mambo yake binafs
Rahul akaondoka zake kwakua Rahul alishamtambulisha kuwa ni Mtu maalumu walimuongezea kitanda kingine ndani wodi ya Vicky ikampa urahisi yeye kupumzika ukizingatia tangu afike Nchini hajatulia kabisa
Asubuhi panakucha ndio Masha anashtuliwa na kengele ya Geti kwamba kuna mtu nje anaomba kufunguliwa getii
Alikuwa amelala juu ya kifua cha Boaz pale pale juu ya kochi tena akiwa mtupu Boazi alikuwa na boxa yake hafifuu iliyokuwa imejichokea na joto la mwili ..
"Mungu wangu,,,weweee ,,,weee boazi!!!! Khaaa ,,weweee!!"
Alimpiga kibao baada ya kuona anamuita muda mrefu haitiki
"Eeh madam"
"Embu vaa haraka!"
Boazi alivaa haraka haraka ,Masha yeye alikuwa ameshajifunga taulo lake
"Sikia wewe tulicho fanyaa huu ni ujingaa ,na Ujinga huu usije tena kujirudia abadani unanielewa??? Fanya kama hujawahi kuuona mwili wangu kabisaaa "
"Nimekuelewa naomba unisamehe madam"
"Toka nenda huko kuna mtu ana bisha hodi"
Boazi alitoka kwa mapana 60 (mie sichezagi mechi za kitoto madam hahah utakuja tu kwa lile boli la jana aah utaniita tu tena hahaha)
Boazi akatoka anajipiga kifua kwa raha zake alikuwa na uhakika na shuguli yake kwa madam wake huyo Masha
Akafungua Geti kama sio yule alimgalagaza Boss usiku wa jana ,
"Boazi mbona unachukua mda mrefu kufungua jamaniii aah " mmoja wa wafanyakazi wa ndani akalalamika baada ya kuwa wamegonga muda mrefu bila kufunguliwa
"Vipii Boss mkubwa alikuja ndani jana "
"Mana sio kwa kufukuzwa kule hahaha"
Wakapokezana kuongea huku wanacheka Boazi alicheka akawaambia Hakuna aliekuja
"Kwahiyo we ulibaki na Gomaa na hujafanya kitu hahaha"
Acheni utani bwanaa" Boazi akapotezea baada ya kuona Masha kwa mbalii kama anawatazama Dirishan juu ya chumba chake
Wakaingia ndani kuanza majukumu yao,
********
Vicky ndio alikuwa mtu wa kwanza kuamka , hali yake alioona nzuri Qassano alikuwa bado amelala na hakuonesha hata dalili za kuamka kwa wakati huo ...
Alioga akavaa nguo ingine kati ya zile nguo alizokuwa ameletewa na Qassano, kafanya mambo yake yote ndio Qassano akaamka
'"Ooh ungeacha ningefanya tu bibie embu" Qassano alimpokonya Vicky nguo alikuwa anakinja anaziweka kwenye mfuko
"Aah naweza hata usijali "
"Hapana Embu achaa hutakiwi kufanya" Qassano akazipanga zile nguo vizuri kwenye mfuko
Akamwambia anatoka mara moja atarudi mchana ,Vicky akamwambia mi nipo Vizuri nataka kwenda nyumbani pia niko sawa ...
"Unaenda nyumbani??? Hapana unatakiwa kubaki chini ya uangalizi at least two days "
"Niko sawa kaka yangu ,hata usiwe na shaka As log as Doctor amesema sina shinda naamini nitakuwa sawa, Natakiwa kwenda nyumbani mana hawana taarifa zozote na simu yangu haipatikani watakuwa na wasi wasi sanaa, Asante kwa ulivyonisaidia mpaka hapa mungu atakubariki kaka yangu"
Maneno ya Vicky yakamkata mdomo Qassano akabaki kimya hakuwa nala kuongezea
"Chukua hii itakusaidia siku mbili tatu ,kukiwa na shida yeyote nijulishe"
"Ooh asante asante kaka anguu, wala usiwe na shakaa mie nipo sawa na nitakuwa sawa kunitibia inatosha hakuna haja ya hela "
Qassano alitoa pesa kumpa Vicky akazikataa huku anatabasam ,Qassano alishangaaa
Akasema "lakini nimekuharibia biashara yako ,nimekuharibia mipango kwa ajili yangu umelala hapa ukaacha kufanya shuguli zako"
"Acha bwana ,Hata usijali" Vicky akainua mfuko wake anataka kuondoka ,Qassano akamshika mkono bado alikuwa anamtafakari huyu bint vipii sio rahisi mtu kukataa pesa ujue?? Tena Tanzania??
Muda ambao Mr Alberto au Qassano anataka kuenda kwa Mashaa ndio Vicky anaamsha mambo mengineee ...
Mr atafanya niniii ?? Kwenda kwa Masha au kubaki kumbembeleza Vicky???
ITAENDELEA.....
KWETU morogoro.