Qassano akamuuliza Vicky ama mumeo ni mkorofi??
Vicky akasema hapana sijaolewa kaka yangu nipo tu nyumbani kwetu.,,,
Qassano akasema basi itakuwa busara kama nikikupeleka kwenu!!"
Vicky alikataa akasema ataenda mwenyewe tu, Qassano nae akakataa kumuacha aende mwenyewe mwisho aliona ngoja akubali tu kuepusha mazozano
Qassano akampigia simu Rahul akamwambia wataonana baadae kuna sehemu anaenda "
"Vipi kwa masha hauta enda mana ananipigia sana simu"
""Nitakwenda baada ya kutoka huku"
"Kuwa makini Kiongozi wanawake wa huku wamejawa tama sana "
Rahul akampa onyo boss wake, Qassano hakujibu alicheka kidogo tu ,
Akakusanya mizigo ya Vicky akatoa mizigo nje akaiweka ndani ya gari
Kisha akamrudia Vicky taratibu akamchukua Vicky kwa kumshika mkono taratibu mpaka ndani ya Gari
Vicky alimwambia anapo ishi, kwakuwa Qassano alikuwa ni mgeni akaamua kuweka Raman itakayo mfikisha hiyo mitaa ambayo Vicky anaishi
Kwenye gari palikuwa kimyaa kila mtu alikuwa akiwaza lake kichwani ..
Qassano aliona sehemu kuna duka la simu akakumbuka Vicky hakuwa na simu akasimamisha gari pembeni
"Unaweza kushuka kidogo "
"Kuna Usalama"
"Yeah tupate chai kidogo "
"Ah usijali kaka yangu usijali niko sawa twende tu"
"Kama wewe upo sawa mimi na mtoto hatupo sawa, inabidi ule kwa sababu yake tu"
Vicky alicheka baada ya kudadavua akilini maneno ya utani ya Qassano ikabidi tu aache ubishi wake ashuke
Kabla ya kuelekea mgahawani ,akashangaa wanaingia ndani ya Duka la simu lipo pembeni ya Mgahawa , hakutaka hata kubishana na Qassano akafata tu nyuma
" simu yako imepotea Angalia simu hapa tuchukue"
Vicky hata hakuongea neno alitembeza macho yake simu itakayo mvutia ,macho yake yakatua kwenye kisimu kidogo Juu ya batani zake kilikuwa kimeandikwa SUNELAN bila shaka hiyo ndio ilikuwa kampuni ya simu
"Aah Vicky angalia ingine hayo makampuni hayajulikani yanashida"
'Lakini kazurii"
Angalia ingine "
Vicky akatembeza jichoo akalidhishwa na simu ingine Imeandika Tecno ,T230 ,Qassano akajikuta anachekea tumboni
Mana alikua Vicky atachagua simu zile kubwaa lakini mambo ya Vicky yanamchekesha tuu
Qassano hakumsemesha tena Vicky aliichukua ile batani alioichagua akailipia Kisha akachukua simu ingine Kampuni kubwa smart phone , ilikuwa ya bei kubwa kweli kweli akailipia zote akazifunga pamoja yaan ile ndogo na kubwa zote akampatia Vicky
"Moja yako moja ya mtoto Never Say No!!"
Vicky akajikuta anacheka sana maneno ya Qassano kwa mbalii Qassano akajikuta anapenda kicheko cha Vicky yaan Vicky akicheka yeye anasikia raha
"Haya twende tukapashe tumbo then nyumbani, lakini kwenu hakuna mbwa wakali eeh mie mgeni hivyoo!!"
"Hahah ndo mana nikamwambia niache niende mwenyewe "
"Wee kwahiyo kuna mbwa wakalii??"
"Wengii"
"Serious????"
"Nakutania hahah"
"Thanks God" Qassano akaweka ishara ya msaraba huku anacheka
Qassano hakumpa nafasi ya kuagiza chai Vicky alijua akimpa nafasi hakawii kuagiza vitu vya ajabu kuogopa bajeti
*******
Recho alishangaa kuona kuna gari ya pesa nyingi inakuja Nyumbani kwao,, akazidi kushangaa ilipo ingia kabisa uwanjani kwao
Akasimama akashika kiuno kuishangaa, mama yake nae alikua jikoni akavutiwa na muungurumo wa gari unaingia kwenye uwanja wao,,, yeye hajui gari ya kitajiri wala masikini kwake yeye gari ni gari
"We gari ya nani hiyoo?" Mama Recho alimuuliza Recho huku macho yake yote yanatazama gari kwa makini
"Sa nitajuaje mimi mama"
"We ndo huishi kuleta vitu vya ajabu ajabu huku ndani"
"Mama Ume........eeeh we Mtoto Mungu wangu wewee "
Recho alikatisha kauli ya kumjibu mama yake baada ya kuona alieshuka kwenye gari
Alikimbia haraka kumuwahi Vicky , na muda huo huo akashuka ,Mr Qassano
"Ulikuwa wapi hupatikani hata kwenye simu??"
Resho akamuuliza huku anamsogelea zaidi ,Mkononi Vicky alikuwa na Ile sindano ya kuwekea Dripu.
Ilimshtua kila mtu kuwa huenda Vicky alikuwa anaumwa
Itaendelea ......
KWETU morogoro.