Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

MY LUNA SEHEMU YA : 10

3rd Aug, 2025 Views 19



Siku ya pili palipo kucha, Leila aliamka mapema sana akiwa ana smile vibaya mno. Hela aliyokuwa ameipata usiku ule mmoja kwa kudansi hakutegemea kama angeipata kiulaini tena kwa dakika 10 za kutingisha nyama nyama zake😋.

Kwa haraka akavaa nguo zake, akaziweka pesa vizuri kwenye pochi kisha akaondoka kuelekea hospitali.

Alipofika wodini, aliwakuta wauguzi wakiandaa kifaa cha dialysis. Daktari alipomuona Leila alimwita pembeni na kusema,

“Kama mmeshapata kiasi cha awali, tunaweza kuanza matibabu sasa hivi”

Leila alifungua pochi yake akatoa kiasi chote cha pesa na kumpa
“Hii hapa, daktari. Tafadhali mfanyie lolote linalohitajika. Sitaki kumwona Lulu akiteseka tena”

“Asante umeleta hela kwa wakati maana alikua anateseka sana! Niachie mimi iyo kazi, Lulu atakua sawa kabisa”

“Asante Dokta”

Basi Lulu alisafishiwa figo, na hali yake ilianza kuimarika. Leila alilia kimoyomoyo akimwangalia mdogo wake huku akijipiga kifua kua kweli alipambana.

Baada ya kuhakikisha Lulu yuko salama, Leila alimuacha na mama, akawapa kiasi cha hela ya ziada kwa matumizi ya siku chache, kisha akaondoka kuelekea Club ONE kwa mazoezi.

Club ilikuwa kimya mchana huo. Muziki ulikuwa wa chini, taa hazikuwa zimewashwa sana. Ndani chumba cha kubadilisha nguo alimkuta Sinyati akifanya mazoezi mbele ya kioo kikubwa, akijifunza mitindo mipya ya kuzungusha kiuno.

“Shoga na mimi nifundishe iyo staili, nimeipenda” alisema Leila huku Sinyati akimgeukia

“Wacha wee! Umekuja wa moto, usijali hapa ndo mahala pake! Staili zote nitakufundisha”

“Ayo ndo mambo nayotaka kuyasikia shoga angu”

“By the way, vipi kuhusu Lulu? Kila kitu kimeenda sawa?? Mama hajashtuka kuhusu hela??”

“Kila kitu kimekwenda sawa, nimemuacha anaendelea vizuri na hela ya ziada nimewapa! Na mama hajajua kama hela nimeitoa huku! Kwa akili zake anadhani niza Zayn”

“Ila sio mbaya kikubwa Lulu kapata matibabu. So, tuanze mazoezi?”

“Okay”

Siku hiyo ikawa mwanzo wa mafunzo rasmi. Sinyati alimfundisha Leila kila kitu alichojua kuanzia jinsi ya kutumia jicho lake kuwasoma wanaume, jinsi ya kunengua bila kuonekana mvivu, jinsi ya kujiamini bila kuonekana mrahisi.

“Usimruhusu mwanaume yeyote akuguse. Pesa zao ndio unataka, si miili yao” alisema kwa msisitizo.

“Sawa Madam”😊

Leila alipambana maana Mwili wake ulizoea kuchanja madafu🤣, sasa ukawa unajifunza namna ya kuvutia macho ya wanaume na kuwatamanisha.

Ilikuwa ngumu mwanzoni, lakini kila siku alizidi kuwa bora. Na kila usiku baada ya mazoezi, alikaa pembeni akiwasikiliza madansa wazoefu, akijifunza mbinu zao na kupokea ushauri.

Wiki nzima akawa anajifua, na biashara ya kuuza madafu aliifunga kabisa na mkokoteni wake aliuuza.

Weekend ilipowadia, Club ONE ikafurika kuliko kawaida na yote kwasababu ya Leila ama niseme LUNA. Ilikuwa Jumamosi yenye vibe, na wateja walikuwa tayari kujirusha.

Ndani ya chumba cha kubadilishia nguo, Sinyati alimsaidia Leila kuvaa vazi lake la kuvutia, siku hiyo alivaa kagauni cheupe tena chepesi. Na kama kawaida kiuno kilikua wazi, upaja nje nje! Alafu akamalizia kuvaa mask yake nyeusi! Aisee Dansa tunae hatuna???🔥Yani mambo yalikua bam bam.

Muziki ulipopamba moto, DJ akatangaza sasa:

“Macho kwenye stage kumpokea mlimbwende wetu. Tamu yetu, sukari yetu! Huyu si mwingine bali ni LUNAAAAAAAAA” 🗣️🗣️🥳🥳🥳🥳

Watu wakapiga makofi, wengine wakapiga mluzi. Leila akapanda stejini huku moyo wake ukidunda kwa kasi. Alipoanza kucheza, Club nzima ikazizima.

Kiuno chake, macho yake pamoja na staili mpya ya kutumia paja aliyofundishwa na Sinyati vilifanya wanaume waanze kumwaga pesa💵💶.

Vitita, dola, na noti za elfu kumi kumi zikatanda stejini. Wengine walinunua vinywaji kwa ajili yake. Madorime na vibango venye jina la LUNA vilikua vya kutoshaa! Inshort walimpenda sana❤️❤️

“Huyu Luna ni wa wapi huyu jamani?” mwanaume mmoja alimuuliza mwenzake

“Sijawahi kuona dansa wa aina hii hapa Club One! Natamani nimuoe kabisa kama itawezekana”mwingine aliongeza.

“Na vipi kuhusu mkeo?” Mwezake akamkumbusha

“Unadhani kwa moto anao utoa Luna unafanya nikumbuke kuhusu mke?? Alaaaa! Waiter shusha dorime ingine kwaajili ya Luna” wote walicheka huku wakirudisha macho yao kwa Luna aliekua anaendelea kuwakonga mioyo.

Alipomaliza, steji ilikuwa imetapakaa pesa. Aliteremka akiwa na tabasamu akiona jinsi gani watu walivyo kua wanampenda bila kujua hata sura yake😩.

Kama kawaida hela zake zilipo kusanywa Wakazihesabu na kugundua alikuwa katunzwa zaidi ya milioni mbili taslimu. Leila alishindwa kusema neno. Alimkumbatia Sinyati,

“Hii sio ndoto, si ndio? Embu nifinye nione kama naota ama sioti”

“Ni kweli kabisa hata hauoti shoga angu”
Sinyati akamjibu.

“Hali ikiendelea kua nzuri namna hii, nitapangisha chumba changu! Nitaanza maisha upyaa”

“Vipi kuhusu Zayn!!”

“Nitahangaika na mtu ambae hanipendi?? Mkewe nimekua dansa (striper) na hana hata habari! Hajui kwanza kama nipo hai au laa. Mwezi wa nne huu hajarudi hata nyumbani embu imagine”😔

“Na kweli hana maana! Omba zako talaka ili uendelee na maisha yako”

“Lakini namhofia Mr Ghali! Sijui atakua na hali gani iwapo akisikia ninataka kuachana na mwanae”

“Leila acha kuishi kwaajili ya kuwaridhisha watu wengine. Uliolewa na Zayn sababu mojawapo ni kumridhisha baba yake. Tulitegemea ndoa ingeenda sawa ila ndo ivyo haikwenda kama ilivyo tarajiwa sasa anataka nini? Ujiue?? Aaah jamani jipende kwanza bibie”

“Nimeelewa shosti heee ndo unataka unisodoe” Leila alicheka😃

“Ndio, maana naona huelewi somo”

“Nimeelewa sasa tuliza munkari mtoto wa kike” walicheka kwa pamoja🤣☺️

Maisha yake yakaanza kubadilika. Leila Alimpa Lulu kila alichohitaji, Akampa mama yake hela ya matumizi na Leo akawa anasoma kwa raha. Urembo wake ukang’aa, mavazi yake yakabadilika, akawa na uhuru wa kifedha. Mtoto akajua skin care na kuvaa mawigi! Ama kweli hela ni sabuni ya roho🧼🫧

Najua mnataka kujua Zayn alikua wapi mda wote huo?? Basi ni hivii.. Zayn, Alizama kwenye penzi la Tatiana yuleee secretary wake. Alihamishia baadhi ya nguo zake nyumbani kwa Tatiana na hakuwahi hata kuulizia kuhusu mkewe. Ndipo huko alipokua siku zote izo. Wanaume bwana😩😩.

Ila Leila alipokua anaongea na Mr. Ghali, baba mkwe wake, alimjibu kwa furaha na jinsi Leila alivyokua amependeza basi Mr Ghali akajua ni juhudi za kijana wake kumbe hata sio🤦‍♀️.

Nae Bi Salma hakuwahi kuwa na wasiwasi. Alidhani pesa zote alizokuwa akipewa na Leila zilikuwa zinatoka kwa mumewe. Hakuwahi kujua kuwa binti yake sasa ni dansa wa club. Ila yote haya yanabadilika bila kutegemewa.

Unajua mambo yanakwenda kuwaje baina ya Leila na Zayn??
Nakuja……...
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MY LUNA SEHEMU YA : 10  >>> https://gonga94.com/semajambo/my-luna-sehemu-ya-10
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 10

majario rewards 100 Comments 0
 

BLOOD MOON EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 03

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 02

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CHANZO NI BOSS 01

majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest