Zayn alianza kuhisi harufu ya usaliti kutoka kwa Tatiana lakini kwakua alikua anajiamini kwa uhandsome wake na utajiri, hakudhani kama anaweza kusalitiwa. Embu kwanza ncheke🤣🤣.
Ila ukweli ni kwamba, Tatiana alikua kweli anamsaliti kisiri siri. Tena na mwanaume ambae alishawai kusoma nae, mbaya zaidi alikuaga first Love wake. Najua mnajua jinsi gani first Love walivyo na nguvu🤣.
Anyways Siku hiyo, Zayn alimfuatilia nyuma Tatiana alipomuaga kuwa anaenda kumsalimia mama yake. Alimuona akisimama kwenye kituo cha daladala ambapo dakika tano zilipita ndipo likaja gari aina ya ICT na kusimama mbele yake.
Dereva alishuka, akazunguka upande wa pili aliposimama Tatiana, akamkumbatia na kumbusu mbele za watu kisha wakapakia kwenye gari na kuondoka pamoja💔.
Zayn alizubaa kama sanamu la makumbusho, macho yalijaa mshangao na hasira juu. Hapo hapo, bila kusema neno, akageuza na kurudi nyumbani kwake alikokua hajaingia miezi minne toka ahamie kwa Tatiana.
Huko Nyumbani, mlango hakuwa umefungwa kwa ndani, akasukuma na kuingia kwa nguvu kama jambazi aliyekosea mlango.
Nyumba ilikua vile vile jinsi alivyokua ameiacha ila pia ilikua safi mno na ilinukia vizuri. Alipokwenda jikoni na kufunguaFriji alikuta limeshona vibaya mno kuanzia maziwa, juice za boksi sita, mpaka nyama ya kuku, ya ng’ombe, samaki, soseji hadi matunda ya kila aina yalikuwepo.
Akashangaa maana Benki zote alikua kazifunga. Leila alipata wapi hela? Kwa akili ya mwanaume mwenye wivu na chuki, jibu likawa ni moja tu, kuwa Leila anadanga💔.
Aliamua kumsubiri arudi ili ajieleze. Lakini kilichomshangaza zaidi ni kuwa Leila hakurudi mapema kama zamani. Saa nne hadi saa tano, hakua amerudi🤔.
Ilipofika saa tisa usiku, Leila aliingia bila kujua kama mumewe amerudi. Alikua amechoka, macho yakiwa yamejaa usiingizi na kichwa kilimuuma maana kelele za club sio poa.
Zayn alimuangalia Leila kwa macho ya mtu aliyepoteza bahasha yenye hela zaidi ya milioni. Alishindwa kuamini kuwa huyu ndie yule Leila mkewe, mchanja madafu kule coco beach.
“Unatoka wapi?” Aliuliza kwa kejeli
“Haikuhusu” Leila alimjibu pasipo kumuangalia usoni
“Unadhani sijui ulikuwa kwa wanaume? Hata harufu yako inaashiria umetoka huko”
“Basi kama unajua, haina haja ya kuuliza”
“Kumbe! Kama umeamua kujiuza, niambie nikupe talaka yako fasta ili uondoke nyumbani kwangu upate uhuru wa kujiuza vizuri” 😏
“Mambo yangu hayajakaa sawa ila tutapanga kuhusu talaka” Leila hakusubiri ajibiwe, alifungua mlango wa chumba chake na kuingia taratibu ili akapumzike.
Zayn alibaki sebuleni, ameduwaa. Kwa mara ya kwanza, alimuona Leila akimjibu vibaya tena kwa dharau! Hakuwai kufanya ivyo kabla!
Hakutaka kumfikiria sana maana mawazo aliyokua nayo juu ya Tatiana yalimtosha ivyo alielekea chumbani kwake na kujitupa kitandani.
Asubuhi yake siku iliyofuata, saa moja kamili, Zayn aliamka kama kawaida. Alijua Leila angemuandalia chai kama zamani, lakini alipofika mezani hakukua hata na kikombe cha maji ya moto.
Alicheka kwa dharau, akavaa viatu vyake na kutoka kuelekea kazini. Alipofika alipaki gari lake parking, ile anashuka tu akakutana na Tatiana aliekua akimngoja toka saa kumi na mbili asubui.
“Please Zayn, nisamehe. Najuta! Ile haikuwa serious…” Tatiana alimkamata mkono😭
“Unajua kama tupo kazini na mimi Boss wako? Have some respect Usinifanye nikupe barua ya kuachishwa kazi” Zayn alichukia😡
“Toka lini ukajali kuhusu eneo la kazi? Tumekua tukionyesha mapenzi yetu hata mbele ya wafanyakazi wengine Zayn please usinifanyie ivo” 😭
“Well mambo yamebadilika! Kama unataka kuendelea kufanya kazi hapa kua na adabu mbele ya Boss wako”
“Zayn… tafadhali”
“Tatiana we’re done. Also siitwi Zayn, naitwa Boss! Nahisi tumeelewana”
Tatiana alibaki amesimama pale parking, machozi yakimtiririka kama tapu iliyochomoka kwenye bomba🤣🤣. Zayn alimpotezea, akaingia ofisini bila hata kumgeukia.
Je huu ndo mwanzo wa kuzaliwa kwa penzi baina ya Zayn na Leila?? Embu ngoja tuone.
Nakuja………..