Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

*SEHEMU YA SITA* SALMA MTAA WA SABA ❣️

5th Aug, 2025 Views 24



Baada ya kupeana namba za simu waliendelea kuwasiliana mara kwa mara hata kutembeleana.
Taratibu walijikuta wanaanzisha uwiano rasmi na kuwa wapenzi .
Fariss alishikwa haswa na penzi la Salma baada ya kupandishwa asali alitamani kuchunga mzinga.
Mara kwa mara Fariss alikuwa akizunguka mitaa ya mtaa wa saba .

Kuna siku alipiga saba simu ya Salma lakini simu ilikuwa haipokelewi.
" Kwanini zapikei simu yangu, atakuwa wapi mpaka anashindwa kupokea simu yangu . Fariss alijiuliza maswali kama kwamba ana wivu.
Aliendelea kupiga tena na tena lakini haikupokelewa aliamua kufunga safari kuelekea mtaani kwa Salma alijua kivyovyote atajua alipo akifika huko.

Alipofika mtaa wa saba alimuuliza mama mmoja ambae anakasnga samaki Mida ya jioni na mara nyingi huwa wanaenda na Salma anamnunulia samaki.
" Habari mama Johari.
" Salama, karibu.
" Asante. Samahani hivi siku ya leo umemuona Salma ?
" Mmmmh leo sijamuona ila unaona mtaa ulivyopoa hivi mabinti wote wapo hapo mbele kwa mzee Tindu kuna harusi nahisi hata Salma yupo hapo maana hawakosagi kwenye sherehe za mtaani.
" Ni mbali sana ua?
" Sio mbali ni hapo mtaa wa pili tu.
" Daaa sijui nitafika je?
Mama Johari aliangaza macho jana vile anatafuta mtu, mara alimuona binti mmoja akamuita
" Hasnat hebu njoo.
Yule binti alienda alipo mama Johari.
" Moeleke huyu kaka kwa mzee Tindu, na ukifika huko mtafutie Salma na umekabidhi kwa huyu kaka.
" Sawa.

Hasnat na Fariss waliongozana mpaka mtaa wenye shuhuri huko kulikuwa na vigoma watu walicheza kufuru huku walinyanyuka vijora juu na kutingisha sehemu zao za nyuma na wanaume waliwambambia kwa nyuma na mmoja wao aliokuwa akicheza hivyo alikuwa Salma.
Farris alipofika tu akifanikiwa kumuona Salma akiwa anacheza huku kijana mmoja akiwa kumshikilia kiuno, Salma alikatika bila kujali na mwili wake ulikuwa umelowa kwa jasho.
Fariss alimuangalia huku akiwa kakunja sura.
" Kaka umemuona dada Salma?
" Ndio kamuite mwambie Fariss anakuita.
" Sawa.
Hasnat alijipenyeza kwenye kundi la watu waliokuwa wakicheza mpaka akamfikia Salma.
" Dada Salma unaitwa.
Hasmat alimwambia lakini Salma hakusikilizwa alikuwa Bize anacheza.
" Kuna kaka mmoja anakuita kule.
" Wewe acha usumbufu toka hapa.
Aliongea yule kaka anayecheza na Salma alafu akamsukuma Hasnat.
Fariss aliona lile tukio na wakati huo Hasnat alikuwa anarudi kwa Fariss kumpa jibu.
" Kaka Salma wala hanisikii pale Mzuka umepanda ni ngumu kuelewa.
Farris hakujibu kitu alijipenyeza kwa watu akamfuata Salma alipofika hakutaka kuongea alimshika mkono na kumvuta mpaka wigo la Salma likadindoka chini.
" Wewe vipi? Salma aliongea kwa jazba bila hata kuona ni nani aliemvuta. Alipomuona vizuri na kumtambua alishusha jazba lakini yule kijana aliekuwa anacheza nae alimsukuma Fariss.
" Oya vipi unakuja kuvamia watu ...
" Alafu wewe kuheshimu unamsukumia nini sasa. Salma aliingilia
" Aaaaah kwahiyo unanikana si ndio.
" Nakuja kwani nakujua?
" Poa.
Fariss hakutaka kupoteza muda akimvuta na kumtoa kwenye kundi la watu.
" Fariss niache basi niokote wigi langu.
Fariss alikuwa kama hasikii walitoka kwenye msongamano wa watu wakaenda kwenye gari. Fariss alifungua mlango na kumtaka Salma aingie.
" Ingia hapo.
" Lakini wigi langu limeanguka kule ngoja nikachukue.
" Nimesema ingia ndani ya gari, sitaki kutumia nguvu.
" Farris siingii unajua kile kiwigi nimekopa jana hata mia sijalipa alafu niache lipotee hivihivi.
" Sijali kuhusu hilo ingia ndani ya gari.
Fariss alimuingiza kwa nguvu kwenye gari na kubamiza mlango kisha bar akaenda kupanda na kuwasha gari.
" Unavyonifanyia sio kabisa, kwani hukuweza kunitoa pale taratibu mpaka iniburuze yani pale umeacha jambo kesho mtaa wa saba itakuwa gumzo ni Salma kuburuzwa kama mwizi.
Salma aliongea lakini Fariss hakuongea aliendelea kuendesha gari .
" Yani mimi naongea wewe ndio kwanza upo Bize sikujua kama wewe mwanaume ni jeuri hivi lakini hata mimi unikuta sema leo umenikuta mashetani yangu yametulia.

Walifika sehemu Fariss walisimamisha gari kisha akageuka kumuangalia Salma kwa hasira.
" Hivi unanichukuliaje wewe msichana?
" Mimi nakuchukuliaje au wewe una nichukuliwe mimi?
" Salma unajua sipendi ujinga na kila siku naongea jambo moja la wewe kuheshimu sitaki kuchangia penzi na mwanaume yoyote lakini mbona hunisikii?
" Eeeeeee.... Hayo mbona mapya kwangu kwani umenifumania na nani?
" Yule mpuuzi aliekuwa anakuambia pale ni nani?
Salma alimuangalia kisha akaanguka kicheko mpaka akapiga makofi.
" Kwahiyo unanicheka jinsi nilivyokuwa bwege nachukulia mwanamke wangu na mimi niponipo tu?
" Hayo umesema wewe na kwa taarifa tu ni kwamba tangia nilipoanza uhusiano na wewe sijawahi kuwa na mwanaume mwingine alafu ukiniangalia mimi naweza kuwa na yule kibaka?
" Sasa kama ni Kibaka hana hadhi ya kuwa na wewe kwanini uliruhusu kushikwa kiuno alafu namtuma mtu aje akuite unajifanya huna habari?
" Niliongea tu na kucheza.
" Sio kucheza ulinogewa na kuambiwa.
" Makubwa haya.
" Yani napiga simu karibua missed call mia kumbe mtu umekumbatiwa unakata viungo vya kishetani.
Fariss aliongea kwa hasira sana ikabidi Salma ajishushe.
Alinyoosha mkono wake na kushika kidevu cha Fariss kwa upole kisha akaeleza jicho lake na kusema.
Baby punguza hasira haya mbona yanazu ngumzika washa gari twende zetu.
Kwa mbinu aliyotumia Salma Fariss alijikuta hana pingamizi hasira zote ziliyeyuka akawasha gari wakaelekea hotelini.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*SEHEMU YA SITA* SALMA MTAA WA SABA ❣️  >>> https://gonga94.com/semajambo/sehemu-ya-sita-salma-mtaa-wa-saba
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Ratiba ya Simulizi

  • USINITANGAZE 02 ❤❤ 05-08-2025 19:00

Ratiba ya Simulizi

  • USINITANGAZE 03 ❤❤ 06-08-2025 04:00

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest