Kesho kulipokucha mapema Sana Maria alijiandaa na kuelekea hotel alipofika alipokekewa na Freya.
" Maria siamini kana umekuja ulikuwa wapi siku zote hizo?
" Nipo ahangaika na maisha. Freya aliangaza macho kuangalia Kama Kuna mtu karibu Kisha akamvuta Maria karibu yake
" Umeona na boss?
" Hapana ndio nimekuja kuonana nae.
" Mmmh Yani Bora uondoke maana nasikia ana hasira na wewe sijui hata umemfanya Nini?
" Najua ananitafutia Sana ndio maana nipo hapa nijue hizo hasira zake ili tunapizane kwa wema nahitaji kuishi kwa amani sitaki kuwindwa Kama swala bugani.
" Mmh unajiamini Nini....
" Najiamini Sana kwanza Sina nidhamu ya uwoga .
" Sawa acha Mimi nikafanya kazi nisije nikapoteza ugali wangu si unamjua Tena boss wetu. Freya aliondoka akamuacha Maria akiwa amekaa anamsubiria Bryan .
Baada ya saa moja kupita Bryan alifika na kuelekea ofisini kwake Maria alienda mpaka ofisini kwa zakia wakasalimiana
" Kulikoni umeamua kujileta mwenyewe?
" Ndio si mlikuwa mnanitafuta wewe na boss wako Sasa nahitaji kuonana nae.
" Sawa ngoja nimpigie simu. Zakia alipiga simu Bryan akapokea
" Boss Maria yupo hapa anataka kukuona.
" Maria?
" Ndio.
" Mruhusu. Zakia alikata simu alafu akamruhusu Maria aingie ofisini kwa Bryan. Malia alienda alipofika mlangoni alisimama kwanza na kushusha pumzi ndefu Kisha akagonga mlango.
" Ingia. Bryan alimkaribisha Maria akafungua mlango na kuingia. Alifika na kusimamabeke ya meza ya Bryan
" Habari za asubuhi.
Alisalimia na Bryan aliitikia kwa sauti ya chini huku akiwa kamkazia macho usoni. Maria aliogopa lakini akajilaza na kusema
" Nasikia unanitafuta Sana nimeamua kuja ili tunapizane Mimi siwezi kuishi bila amani. Kwakuwa ulisema nimekutukana ikiwa wewe ndio ulinitukana Mimi nakubali nimekuja unilipizie ukitaka nitukane au nipige ili hasira zako ziishi na usinitafute Tena. Wakati Maria anaongea Bryan alikuwa kakaa kwenye kiti huku akiwa kaegamia na mikono aliikunja akawa anamuangalia moja kwa moja.
" Ndio hivyo nilivyokwambia tunapizane tuili tusisumbuane. Bryan alinyanyua simu akapiga kwa secretary wake
" Niletee grass ya juice ya passion. Maria alimuangalia huku akiwa anajisemea
"Haya madharau Sasa Ina maana ananiona Mimi chizi naongea hanijibu alafu anaagizia juice.
Mara mlango ulifunguliwa zakia aliingia akiwa na grass ya juice akajiweka mezani.
" Unahitaji kitu kingine boss?
" Hapana unaweza ukaenda . Zakia alitoka , Bryan akasimama na kusogea mpaka alipo Maria .
" Eheee umesema naweza kufanya Nini ili tumalizane?
" Vyovyote unavyotaka wewe Ila itakuwa unanionea tu.
" Ulisema nikupige? Bryan aliuliza , Maria akamtolea macho akijua anataka kuchapwa vibao. Bryan alinyanyua mkono Maria akafumba macho haraka akajua kibao kinamshukia kumbe Bryan alinyanyua mkono na kushika kichwa chake. Maria alipoona hapigwi alifumbua jicho moja badae akafumbua macho yote.
" Naona umeshindwa kufanya unachata kufanya Mimi naondoka na naomba usinitafute Tena. Bryan alinyanyua Grass ya juice akampatia
" Mmm unanioa ya nini?
" Umeongea Sana kunywa upooze Koo.
" Ni kweli nimeongea Sana Ila siwezi kunywa, sijui hata umeweka Nini. Bryan alinyanyua Grass akanywa kutaka kumuaminisha hakuna kitu alafu akampatia. Maria aliichukua na kunywa moja kwa moja alipomaliza akashusha grass na kuweka mezani.
" Natumai hii ndio adhabu uliyonipatia naomba usinitafute tena niacheniishi kwa amani. Alipomaliza kuongea aliondoka na Bryan yakufanya chochote zaidi ya kumuangalia
Akachukua simu yake Kisha akapiga wakati simu inaita alienda kusimama dirishani akawa anaangalia nje akamuona Maria anaondoka, simu ilipopokelewa akasema
" Mfuatilie Maria kwa Siri lakini asijue Kama anafuatiliwa. Alipomaliza kuongea alikata simu akarudi kwenye kiti chake alivuta loptop Yake na kuendelea kufanya kazi.
Maria alienda kukutana na Liya.
" Niambie kakufanya je? Liya aliuliza
" Hajanifanya chochote zaidi ya kuniangalia na kunipa juice ninywe.liya alishituka
" Eeeee kwahiyo kukutafuta note na kuchoma mafuta ameishia kukupa juice na kumuangalia Kama picha.
Hata Mimi nashangaa sikutegemea Yani.
"Mmm kwa sisi wataalamu wa Mambo ya hisia za mapenzi tumesha elewa kinachoendelea hapa.
" Wewe na hayo mapenzi yako utajua , Kati yangu na Yule kisiran Hakuna mwenye hisia na mwenzie.
" Usiusemee moyo wa mtu.
" Basi kwa Mimi binafsi ndio sifikirii kabisa. Kwanza ningejua Ni upuuzi Wala nisingepoteza muda wangu saizi ningekuwa sokoni naingiza Mia mbili mbili zangu.
Usiku Bryan alikuwa chumbani kwake sehemu ya Baraza akipunga upepo huku akinywa mvinyo akili na mawazo yake yalikuwa kwa Maria alikumbuka Mambo yote yaliyotokea asubuhi hasa pale Maria alipofumba macho ndipo alipomuangalia vizuri na kuufaidi urembo wake wa asili. Japo Maria alikuwa anajali ngumu kimaisha lakini alikuwa mrembo na mwenye ngozi nzuri nyororo . Taswira ya sura ya Maria ilikuwa unazunguka kichwani kwa Bryan. Bryan alinyanyua Grass ya mvinyo na kunywa wote Kisha akairudisha grass mezani akashika paji lake la uso na mkono wa kushoto na kusema
" Ooo Maria, sijui nitaongea rugha gani kwako ili unielewe. Tangia mwanzo nilivutiwa na kila kitu chako Ila ujeuri wangu uliharibu kuficha hisia lakini kwasasa naenda kushindwa hisia zinaenda kushinda majivuno . Oooh Maria ,
KWETU morogoro.