Bryan alifikiria Sana jinsi ya kumuingia Maria lakini alikosa jibu Kuna wakati alitamani kupotezea na kuendelea na maisha yake lakini moyo wake uliendelea kumsaliti. Ilifika wakati alikuwa akimuota mpaka kwenye njozi zake.
Siku moja Bryan alikuwa ametua ofisini kwake huku akiwa anaangalia picha ya Maria iliyokuwa kwenye loptop Mara zakia aliingia alipofika alishangaa kuona picha ya Maria kwenye loptop ya boss. Bryan alifunika loptop Yake.
" Samahani boss nimekuja kukumwambi ratiba ya leo, baada ya lunch unatakiwa kwenda kwenye kikao cha wafanyakazi wa B.L Transport. ( Hii Ni kampuni ya usafirishaji anayomiliki Bryan)
" Sawa. Zakia alitaka kutoka Bryan akamrudisha.
" Zakia kunakazi nataka kukupa Niya nje ya ofisi Ila nitakulipa day zuri endapo utanifanikishia . Zakia aliposikia kulipwa dau zuri alitabasamu.
" Sawa boss Ni kazi gani hiyo?
" Nataka uwe karibu na Maria , Yani niamaanisha uwe rafiki Yake. Zakia alinyamaza kimnya kwa muda.
" Sawa lakini sijui alipo.
" Nitakufahamisha alipo Ila ukifanya hii kazi unatakiwa kunipa mrejesho alafu Maria hatakiwi kujua chochote kuhusu mpango wetu.
" Sawa boss.
" Unaweza ukaenda .
Siku moja Maria akiwa Katikati ya soko la samaki akiparua samaki za mteja. Zakia alisimama mbele ya meza yake Maria bila kuangalia Ni Nani alimkaribisha
" Karibu .
" Maria kumbe unafanya biashara huku? Maria alinyanyua macho akamuangalia
" Khaaa zakia .
" Ndio Ni Mimi unajua sikutegemea kujikuta sehemu hii.
" Ndio hivyo nipo huku siku hizi . Karibu nikuhudumie.
" Asante malizia kumuhudumia mteja alafu utanihudumia.
Maria alimaliza kumuhudumia mteja wake na mteja alipoondika walimsikiliza zakia.
" Karibu unataka samaki wa aina gani? Zakia hakujibu aliendelea kumkagua.
" Vipi mbona unamuangalia hivyo ?
" Maria unawezaje kufanya kazi kwenye mazingira Kama haya ona nzi hapo ulipo unanuka shombo. Maria alitabasamu kidogo alafu akaguna
" mmmh zakia naona umeambukizwa dharau na boss wako hii kazi Mimi naithamini mno ndio kila kitu kwangu ....
" Jamani Mimi sijadharau Ila nakuhurumia naona Ni kazi ngumu Sana kwako.
" Ndio Ni ngumu Ila nitafanyaje kila ninapoenda kuomba kazi hakuna nimeona Bora nijichanganye huku ili maisha yaende.
" Daaa upo mwaya. Hivi namba yako ya simu ni Ile Ile?
" Ndio
" Sawa Basi nitakutafuta. Zakia alifungua pochi yake akatoa shilling elfu tano akampa.
" Shika hii utanunulia vocha shoga yangu.
" Hii hela unayonipa unataka samaki au umenipa ya vocha?
" Hiyo ya vocha kipenzi naomba upokee.
Maria aliipokea Ile hela na kuhifadhi .
" Asante.
" Usijali Sasa Leo sitachukua samaki Ila siku nyingine nitakuja kukuungisha na nitakuwa mteja wako mzuri. Zakia aliondoka lakini alimuacha Maria na maswali mengi kichwani kwake
Mmh huyu mtu mbona kabadilika hivi kweli amenipa hela au natia huruma Sana kutokana na hii kazi ninayofanya? Lakini mbona watu wengi ne wanafanya. Maria aliwaza Sana mpaka alipokuwa kushituliwa na mteja akiyetaka kununua samaki.
Siku zilivyozidi kusogea ndivyo ushoga Kati ya Maria na zakia ulikuwa. Zakia alimtembelea Maria nyumbani kwake pia Maria alienda nyumbani kwa zakia. Siku moja Bryan alimwambia zakia.
" Naomba kesho umshawishi Maria muende sehemu mkapate chakula alafu mkiwa huko utanijulisha.
" Sawa. Bryan alivuta droo akatoa pesa akampatia .
" Hizi zitawasaidia kwenye Mambo yenu.
" Sawa boss. Zakia alichukua zile hela akatoka alifika ofisini kwake akawa anajiuliza
" Nini kinaendelea Kati ya boss na Maria? Hivi ninachokifikiria kitakuwa sawa? Hivi boss anaweza akawa anamtaja Maria? Mmmh hapana sio rahisi Sasa boss anataka Nini kwa Maria? Zakia alimpa Maria taarifa za wao kutoka kesho . Maria akamwambia wafanye muda wa jioni ndio atakuwa na muda mzuri. Zakia alikubali na kumfikishia taarifa Bryan kuwa watatoka jioni .
Hatimae kesho ilifika majira ya saa kumi Maria alikuwa nyumbani kwake akijiandaa baada ya kumaliza alimpigia simu zakia akamuuliza sehemu watakayokutana. Zakia alimwambia wakutane village palm. Maria alichukua usafiri mpaka village Palm akamkuta zakia kashafika .
" Umefika saa nyingi?
" Hapana Ni kana dakika tano tu. Maria alikaa akaagiza kinywaji huku wakiwa wanasubilia chakula walichoagiza. Waliendelea kunywa vinywaji huku wakiendelea kupiga story. Zakia alimtumia ujumbe Bryan akamwambia sehemu walipo. Bryan akamjibu atakuwa hapo muda sio mrefu. Zakia alitulia huku akiwa na shauku ya kutaka kujua kinachoendelea Kati ya boss wake
KWETU morogoro.