Nikamwambia we acha wehu muonee, akasema et mama kwahiyo ndoa yangu lini
Baba akasema yaan baba mkwe akasema ndo kwanza mmefika jamani hata tule tu
Mama akasema afya ya salma bado ni dhaifu sana mi nafikiri tungemwangalia akarudi kwenye uimara wake kabisaa ndio ndoa ifungwe
Mi nikasema jamaniiii mbona mi nipo vizuri tuu , hapo mwenyewe nina hamu na ndoa sanaaaa
Inno akasema , bora ungerudisha kwanzaa mwili wako ukapata ule Urembo wako asilia ,subira asije kukuzidi bureee ukumbini
Mmmh nikasema wee msinambie , Inno akasema harusi itakuwa siku mojaaa
Jamani mbona siwezi kusubiri zaidi
Subira akanambia yaan sitaki uje Useme mi nilipendeza kukuzidi kwasababu et mi sijakondaaa ohooo..
Kwakweli sikuwa na mood ya kuwa na
Zakia karibu sikumtaka kabisa hata kwa bahati mbaya , alikuwa nyumbani tangu tumefika na ilikuwa siku ya pili hivi
Nilimwambia alex simpendi zakia nikimuona nahisi hasira sana
Alex akasema sawa ,ataondoka , muda huo huo alimwita zakia akampatia pesa akamwambia tunashukuru kwa msaada wako zakia naomba uondooke hapa na tusije kuonana tena hata kwa bahati mbaya mke wangu hajisikii vizuri akikuona
Zakia alinitazama akasema naelewa Salma lakini nashkuru sana kwa kunisamehe hiyo tu kwangu inatosha
Lakini nina ombi la mwisho naomba kwenye harusi yenu nije walau kuwaona tu
Nilikataa kabisaaa sitaki mwenzangu yaan simtaki zakia aende huko akasema sawa haina shida
Aliondoka bwana Hata sijui alienda wapi atajua mwenyewe mie hayanihusu kabisaa
Mi niliendelea na maisha, Alex alikuwa anahakikisha nafanya mazoezi kila siku asubuhi na Jioni, mpangilio wa chakula kizuri kile cha lishe
Yaan nilikuwa nampangilio wa kila kitu kuanzia kula kunywa mazoezi muda wa kulala na vingine
Watoto wangu walikuwa hata hawanishaukii sanaaa wao ni bibi yao tu yaan ni bibi tuu muda wotee..
Siku zilienda afya yangu ikawa inaenda inaimarika Nilianza kupata ki mwili changu kwa mbali nilianza kung'aa na kupendeza
Alex alikuwa yupo hapaa yaani benet na mimi , Kazi alishaacha kitamboo anasema ye vyeti vyae vizuri sana muda wowote akihitaji kazi anapata
Alichokuwa anatambia ni Biashara zake Alex alikuwa na Biashara nyingi zilikuwa zinaingiza sana pesa
Ile Restaurant yangu subira alikuwa anaiongoza vizuri sana ilikuwa kubwa na tayari ilikuwa imezaa matawi mengine makubwa tu yalikuwa mawili ...
Bwana baada ya miezi kadhaa nilirudi kuwa vizuri sana yaan nilikuwa salma yule nikazidi hadi mwanzo nilinenepa nikapendeza sanaaa
Hapo mipango ya ndoa ikaanza kuwekwa sawa, niliomba alex atoe posa kidogo tu mana Garama alitumia nyingi lakini yeye alikataa akasema atatoa pesa zitakazo takiwa alitoa sababu kibao nikasema sawa mi sina neno ..
Huku inno na subira hapa mie na alex mambo yalikuwa yametaradadi , mama yangu maskini alikuwa na raha sanaaa yaan alitangaza kila kona kuwa anaoza ma bint zake siku moja ,
Kila kitu kilikamilika ilikuwa bado kama wiki moja hivi ya harusi
Siku hiyo tulienda kariakoo kwenye maduka ya magauni ,tulikuwa wote wanne mie na subira , Inno na Alex.
Tulienda kutafuta gauni dada za kutambia, sijamkuta muuzaji wa hizo nguo ni juddy afu ni duka ambalo Tuliona online lina nguo nzuri sana
Sio sie sie tu hata yeye alishtuka mnoo baada ya kutuona alishtuka sana yaan mpaka ile kujiamini ilimtoka
Alex alitaka kuondoka lakini inno akamshika akamwambia kuwa hapa sio kwake ye ni mfanyakazi tu, tulishaongea na mwenye duka
Basi tuliingia lakini juddy alikuwa amepauka sanaaa afya yake ni kama ilikuwa na shida hivi japo alikuwa amevaa vizuri amepaka mafuta lakini wala hakuwa amependeza ngozi yake ilikuwa imesinyaa sanaa kama mtu mwenye maradhi furani
Sie tulichukua nguo zetu ,tukaondoka zetu bila hata kumsemesha Wala yeye hakutufatilia yaan alikua kama yupo bize sana kumbe hakuna hata
Tulipo kuwa kwenye gari, Inno akasema mi nilijua hata alishaga kufa huyu mwanamke kumbe yupo , tukacheka wote subiraa akasema ila amekuwa dhaifu sana sana au nyie mmemuoa yupo sawa
Basi mada alikuwa ni yeye njia nzimaaa mpaka tunafika home
Mwisho tuliachana nae tu
Mambo bwana yakaenda enda mwisho , hatimane siku iliyokuwa inasubiriwa kwa miaka mingi ilifika
Mimi na alex tulikuwa mke na mume Rasm Huku rasmi kabisa Subira na inno pia wakiwa mke wa mume , niliiona furaha ya mama yangu sana nilifurahi pia
Tulienda zetu honeymoon nje kabisa ya nchi, huko tuka enjoy mnooo yaan mnooo na hiviii Watoto mama alibaki nao yaan bibi yao hata kunipa watoto mie hataki na vile wanampenda bibi yao basi bwana ..
. Inno na subira wao walienda Arusha
Tulikaa huko mwezi mzima , Alex akanambia tukienda tuanze maisha mapya mke wangu ,
Niliapa sitaki kuweka rafiki karibu sitaki shoga sitaki jirani yaan ni mimi na familia yangu nimekoma koma koma kabisaaaa..
Tulirudi nyumbani , nikiwa nimezidi kupendeza sanaaa,
Mama akanambia salma una mimba wewe nikasema mamaaa mimba watoto ndio kwanza wana miezi 6 Jamanii
Hata mwili wangu haujapumzika nimetoka kwenye maradhi makubwa
Hata tulipo kuwa kule Alex akanambia tukirudi nitumie kwanza uzazi wa mpango mana mwili wangu bado haujakaa sawa ndiyo tulikubaliana , sa mama ananambia et nina mimba mmh
Tulikuwa tumerudi kama wiki hiivi imepita zakia alipiga simu ya inno akamwambia kuwa Juddy amepata strock leo siku ya tatu yupo hospital, inno akasema nataka nije kumuona aiseee
. Kweli alienda inno na alex huko hospital wakaja kusema hali ya Juddy kweli ni mbaya yaan amepooza anaangalia tu ndio kitu anaweza basii
KWETU morogoro.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.