@Kila Mtu
🥥🥥🥥🥥🥥🥥🥥🥥🥥🥥🥥🥥🥥🥥🥥🥥
Fariss alishusha pumzi huku mikono yake ikiwa kichwani .
" Meyael yule msichana amechukua simu yangu.
" Hahahaha....
" Unacheka?
" Sicheki kwa mazuri ila Salma wa mtaa wa saba kakuweza kakugeuza mtaji.
" Hivi huyu ni mwanamke gani ? Kila tabia za ajabu anazo yeye . Sijawahi kukutana na mtu mwenye ulimi mkali kama yule, nadhani hata Kibaka wa Tandale hawezi kunizidi ujanja kiasi hiki.
" Lakini bro ukweli ni kwamba yule dada ni kichwa ana conference ya hali ya juu. Hata mimi nimemuogopa aisee.
Fariss alitulia huku akiwa anatafakari jambo Meyael akauliza.
" Sasa tunafanya je kuhusu simu yako?
"Hapa hakuna kingine cha kufanya nageuza gari naenda kumtafuta .
" Utampatia wapi kaka hiyo andika umeshalizwa .
" Hapana siwezi kukubali simu yangu ipoteze kirahisi hivyo lazima nitampata , nitatumia gharama zozote kuipata simu yangu.
Kuna vitu vingi vya muhimu kwenye ile simu.
Fariss aligeuza gari na kuanza kurudi mtaa wa saba. Alipofika karibu na walipotaka kumgonga Salma alisimamisha gari pembeni na kushuka haraka akaelekea sehemu akawakuta wanawake wamekaa wanasukana nywele.
" Habari za sauti wakina dada.
" Salama.
" Samahani naomba kuuliza kitu.
" Uliza tu kaka.
"kuna dada mmoja Mjanja Mjanja hivi , muda mfupi alikuwa maeneo haya amevalia dela la rangi ya blue ina mpasuko mrefu na masikioni alikuwa kavalia hereni kubwa za duara.
Wale wakina dada waliangaliana kisha wakamuangalia Fariss. Mmoja wao akauliza
" Unamuongezea Salma?
" Ewaaaaa huyo huyo .
" Sawa , sasa nyoosha na hii barabara ukifika nyumba ya nne ingia na kichochoro ile nyumba ya nne nyuma kuna nyumba nyingine ina rangi ya bluu basi gonga hapohapo ndio kwa kina salama.
" Bingo. Fariss alishangilia kimnyakimnya kisha akasema.
" Asanteni sana dada zangu.
Bila kuchelewa alienda alikosimamisha gari akapanda na kuanza kuendesha.
" Vipi umefanikiwa?
" Ndio sasa subiri timbwili linaloenda kutokea huko yani yule msichana simuachi salama kumuonyesha mimi ni nani namchukua naenda kumlaza ndani hata siku mbili ili ajue kuwa kuna watu wa kuchezewa na sisi wengine hatupotezi muda kwenye mambo ya kijinga.
Meyael alitulia kimnya ndio kwanza alichukua chupa yake ya maji baridi akawa anakunywa maana alimuelewa Fariss akiamua kufanya jambo huwa hacheki kwahiyo kilichokuwa kinaenda kutokea ni kisasi cha simu na yote yaliyotokea kwa siku hiyo.
Waliofika sehemu waliyokuwa wameelekezwa Fariss alisimamisha gari.
" Unaenda au vipi?
" Mimi sitaki kusikia kelele wewe nenda kamalizane nae.
Fariss alishuka kwenye gari akafunga mlango kisha akaingia kichochoro na kuiona nyumba aliyoelekezwa.
Alifuata ile nyumba akasimama kwenye mlango mkuu wa kuingilia ndani na kuanza kugonga kwa fujo.
Wakati huo Salma alikuwa akipepea jiko lake la mkaa kwaajili ya kubandika mboga.
" Ohoooo kumekucha watu wa kudai wameshafika, na wakimuona huyu kuku maneno yatawatoka ngoja kwanza nimfuche huku.
Alichukua ile sufuria iliyokuwa na kuku akiweka chini ya meza na kuifunika vizuri kisha akawa anaelekea mlangoni huku akisema
" Jamani basi tumesikia mtavunja huo mlango.
Baada ya sekunde chache Salma alifika mlangoni huku akiwa kavalia kanga yake moja akafungua mlango na kukutana na sura ya Fariss . Wakati huo fariss alikuwa kakunja uso lakini baada ya kuona muonekano wa Salma matuta ya usoni kwa fariss yalifutika.
" Una matatizo gani? Mbona unagonga mlango kwa fujo hivyo?
"Kilichinileta hapa ni kitu kimoja tu Nataka simu yangu.
Salma alimuangalia Fariss huku akionyesha tabasamu hafifu usoni kwake . Kisha akasema
" Nilijua tu utafuata simu yako. Simu yako ipo salama , sikuwa na shida nayo ila nilichukua makusudi ili ulipe kwa dharau zako na maneno yako ya kejeri kusema kuwa mboga zangu hata mbwa wako hawezi kula.
Nimeamua kukuonyesha sio kila mtu niwakubeza.
" Hivi unajua ni kiasi gani umenipotezea muda wangu?
" Wewe ni mbinafsi sana kwani hukuona jinsi ulivyoupoteza muda wangu?
" Hebu acha kunipotezea muda nipe simu yangu.
" Nitakupa lakini unatakiwa kujua kila mtu anahitaji heshima,ukiheshimu wengine na wewe utaheshimiwa.
Alisema Salma kisha akageuka kuingia ndani. Fariss macho yalimtoka kwa jinsi alivyokuwa akimuangalia Salma anavyotembea na huko nyuma kutetemeka mithili ya jenereta lililowashwa.
" Mmmmh..... Hii balaa Fariss nimekuwa mdogo kama piliton. Amejua kuituliza moyo wangu.
Baada ya muda Salma alirudi akiwa kashika simu ya Fariss mkononi. Kwa madoido Salma alimkabidhi Fariss simu yake
" Shika simu yake.
Farris alichukua simu akaiangalia mara ghafla akashitukia kakumbatia.
Fariss aliduwaza na kuganda.
Salma alivunja kumbatio na kuweka mikono yake nyuma.
" Karibu tena mtaa wa saba sisi ni wakarimu sana.
Fariss alimuangalia sana usoni kisha akageuka kuondoka bila kusema chochote.
Fariss alipiga hatua chache kutembea mara akasikia anaitwa.
" Hey.
Fariss aligeuka kumuangalia.
" Ninatumaini siku sio nyingi utakuja tena hapa.
Farris alimuangalia Salma bila kuelewa , lakini macho ya Salma yalikuwa na jambo, yalikuwa na mvuto wa kike pia sauti yake ilienda kutuliza ghadhabu za Farris.
" Usichelewe kuja tafadhali maana sitaweza kusubiri kwa muda mrefu.
Taratibu Salma alifunga mlango . Farris alirudi kwenye gari akiwa kapoa.
Meyael alipomuona alishangaa kumuona jamaa kapoa ni tofauti alivyokuwa kaenda wa moto.
" Vipi bro mbona kama umevunjika moyo ? Umepata simu yako kweli?
" Farris alivuta pumzi ndefu alafu akashusha na kusema.
"Meyael yule mtoto ni noma , ana roho ya simba, nilichokikuta huko siwezi kuhadithia ila tambua akili yangu haipo sawa na hapa nilipo kajikuta natamani kumuona tena......🤔🤔 Nyieeeee....Mambo ni ya motooo.😂 Kwani wewe auogopi Usipite bila kulike na kukomeniti fanya ku share kabisa ili sehemu inayofuata isikukose maana ndiyo sehemu balaaa🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥.
Jamani comment zenu zikiwa nyingi naleta mwendelezo fasta.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.