Max alimuangalia Dala usoni kisha akatingisha kichwa na kuelekea chumbani kwake.
" Yani huyu anataka kuujaribu uvumilivu wangu na mimi nitashinda kabisa kuvumilia.
Max alienda kumtembelea dada yake Irene wakiwa wamekaa sebleni wakipata vinywaji Irene akauliza.
" Vipi shalon anaendelea je?
" Anaendelea vizuri, anafuraha, amezoea na anaamini ni mama yake.
" Hilo ni jambo zuri , Dala anaweza majukumu yake?
Anaendelea vizuri lakini siliziki na mambo yake.
" Kivipi?
" Naona ana mambo ya Uswahili sana naogopa shalon anaweza kuiga tabia za ajabu.
" Lakini kuhusu malezi ya mtoto?
" Naona anamlea vizuri na shalon anampenda mno .
" Basi hizo tabia zake wala zisikuumize kichwa unatakiwa kumuelekeza taratibu atakuelewa tu.
" Sawa lakini zinaniumiza sana kichwa kuna wakati najiuliza nashikwa na hasira natamani hata muonane na Hilda niongee nae ana kwa ana.
" Hivi bado unamfikiria huyo mwanamke mwenye roho ya kishetani?
" Sifikirii kwaajili yangu ni kwaajili ya Shalon.
" Sahau kabisa kuhusu yeye maana sidhani kama huko aliko anawakumbuka.
Kaa na Dala akupeleke binti yako na kama itakupendeza unaweza kujiongeza. Alisema Irene huku akitoa tabasamu.
" Utani nani huo dada yani mimi niwe na Dala?
" Kwani kuna ubaya?
" Ni kitu ambacho haliwezekani kabisa na wala sifikirii kuwa na mahusiano imetokea kuchukua wanawake.
" Una kichaa wewe ukosewe na Hilda ujumuishe wanawake wote.
"Tuachane na hayo. Nilipita kukuona sasa acha nirudi nyumbani nikamuone binti yangu.
" Wasalimie.
Max alirudi nyumbani kwake akamkuta dala anakunja nguo na shalon alikuwa Kalala kwenye kochi.
" Habari
" Salama.
" Mbona mtoto Kalala hapo?
"Amepigiwa na usingizi muda huu nitampeleka chumbani kwake.
" Na kwanini nguo zinakunjiwa sebleni?
" Kwani kuna tatizo nikikunjia nguo hapa?
" Huoni tatizo ? Hii ni sehemu ya kukaa na kupumzika pia wageni wanaweza kufika muda wowote.
" Jamani max mbona unagubu wewe kwanza tangia nimefika kwenye hii nyumba sijawahi kuona mgeni akija hapa.
" Hata kama hii ni seble sio chumba leo hii iwe mwanzo na mwisho kukunja nguo hapa.
" Sawa baba shalon nimekuelewa.
Dala alichukua nguo akawa anaelekea chumbani pia Max alimbeba Shalon akampeleka chumbani kwake na kumlaza kitandani.
Kesho yake maxt alikuwa ndani na mtoto wake , dala alikuwa nje anaongea na simu.
" Yani kazi nimepata shoga yangu lakini yule kaka usinione vile ni kichefuchefu hatari yani Sikai kwa amani kila unachofanya anatoa kasoro anaona kama vile sina ninalojua, yani kama mshamba flani hivi.
Kutokana na hizi tabia zake nahisi ndio maana hawezi kukaa na mwanamke hata hivyo nina wasiwasi mke wake atakuwa kamkimbia kwa sababu ya mambo yake.
Wakati dala anaongea na simu kumbe Max alikuwa amesimama kibarazani akawa amesikia kila kilichoongelewa.
Max alishindwa kuvumilia akiongelea vile akajikohoza na kumfanya Dala ageuke nyumaa. Alikata simu na kumfuata Max pale aliposimama.
" Ulikuwa unaniongelea mimi si ndio?
" Hapana.
Max alimuangalia kisha akasema.
" Kajiandae tutoke.
Dala alipita pembeni akaingia ndani kwaajili ya kujiandaa.
Akiwa anamalizia mlango uligongwa.
" Yani huyu nimeingia sasa hivi na sasa ananigingea mlango.
Dala alimaliza kujiandaa akachukua simu yake akaenda kufungua mlango akiwa anajua anaenda kukutana na Max baba kisirani lakini haikuwa hivyo alikutana na sura ya binti mrembo shalon akiwa anatabasamu.
" Jamani kumbe ni wewe kipenzi.
"Ndio , umependeza.
"Asante kipenzi.
" Niamini nataka unioake mdomo wangu uwe mzuri.
Shalon alitaka apakwe lipstik
" Sawa njooo.
Waliingia chumbani Dala akaanza kumpaka wanja na rangi ya mdomo.
" Tayari.
" Nataka kujiangalia.
Shalon alijiangalia kwenye kioo.
" Waoooo nimekuwa mzuri.
" Wewe ni mzuri siku zote.
Shalon alifurahi kuambiwa hivyo.
" Sasa tutoke kabla baba yako hajatufuata.
Dala alimbeba Shalon wakatoka nje .
" Dady niangalie nilivyokuwa mrembo. Alisema shalon , max aligeuka kumuangalia alipoona kapodolewa alikunja sura na kumuangalia Dala .
" Dala......
" Max tulia, shalon yupo hapa.
Kweli max alitulia hakutaka kumfokea mbele ya mtoto.
Dala na shalon walienda kupanda kwenye gari tena walikaa siti ya nyuma.
Max alipanda mbele na kuanza kuendesha gari.
Walielekea kwenye duka moja la nguo.
" Dala ninekuleta hapa uchague nguo nataka uchague nguo za maana ambazo ukivaa hata mtu akimuona anakuona mwanamke wa heshima, mke wa mtu na mama wa familia.
" Mmmh .... Kwahiyo unataka nivae vitenge, magauni marefu ya marinda....
" Sijamaanisha hivyo unatakiwa kuvaa nguo nzuri za kisasa na sio zilizopitwa na wakati kama huwezi kuchagua ni bora uombe msaada pia nitatoa kuzikagua.
Dala alianza kuchagua nguo huku akiwa kashika mkono Shalon watu walimsifia na kumpongeza dala kuwa ana mtoto mzuri tena yupo smart.
Kitendo cha watu kumsifia Shalon kilianza kumpa matumaini Max .
Dala alichagua nguo na Max akizikagua aliangalia zinazofaa wakalipiwa na nyingine ambazo hazikumvutia walirudisha.
Full 1000
Whatsp 0784468229.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.