Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHH🥵💘10

7th Aug, 2025 Views 33


Baada ya dakika ishirini kupita Bryan alifika akiwa kavalia tishet nyeupe na suruali ya jeans nyeusi na kichwani alivalia kofia akaenda kukaa sehemu ya Kona ya ule mgahawa . Muhudumu alifika kwenyemeza aliyokuwa kakaa.
" Habar
" Salama
" Karibu.
" Asante naomba unipatie maji chupa kubwa.
" Sawa . Muhudumu aliondoka Bryan alitoa simu yake akawa anabonyeza huku akiangalia walipokaa wakina Maria. Alikuwa anamuangalia Sana Maria anavyoongea Tena akiwa na furaha . Muhudumu alimpelekea maji akamimina kwenye grass akaendelea kunywa huku macho yakiwa kwa Maria. Kila wakati zakia alikuwa anaangalia sehemu ya kuingilia Kama atamuona Bryan.

Bryan aliwaangalia mpaka alipotosheka akaamua kuondoka akiwa kwenye gari alimtumia ujumbe zakia.
" Sitaweza kufika mkimaliza Mambo yenu mnaweza kuondoka. Zakia alisoma alafu akasema
" Aaah Sasa ndio Nini kutuweka muda wote huo.
" Kwani ulikuwa unamiadi na mtu? Maria aliuliza.
" Aaah hebu tuachane na huyu . Vipi biashara yako inaendaje?
" Kwa Sasa unaenda vizuri na tangia umeniletea Yule mteja nimekuwa nikimaliza mzigo wote kila siku.
"Nilikwambia nitakutafuta mteja mzuri.
" Alafu Sasa huwa anabiachia chenchi.
" Umeona Sasa Yule mzungubwa roho hana shida ndogondogo. Mpango wa huyo mtu kwenda kununua samaki Ni mpango wa Bryan. Kila siku hiyo mtu alienda ananunua samaki wote alipokuwa nao. Wakiwa wanaendelea kuongea ukiingia ujumbe kwenye simu ya zakia . Ujumbu huo ilitoka kwa Bryan ulikuwa unasema
" Mpige picha Maria alafu unitumie. Zakia alisoma alafu akamuangalia Maria .
" Maria hebu kaa vizuri nikupige picha. Maria hakuwa na hiyana alikubali kupigwa picha tena zenye pozi mbalimbali.
Bryan alitumiwa picha za Maria akawa anaziangalia huku anatabasamu.
Bryan alitokea kumpenda Sana Maria Ila hakuwa na ujasiri wa kumueleza hisia yake.

Siku ya jumamosi walikuwa wanacheza basketball na wenzake ulipofika muda wa mapumziko alichukua simu take na kumpigia zakia.
" Vipi Leo umeonsna nae?
" Hapana boss.
" Naomba uonane nae na umuulize anatamani kufanya biashara gani akikupa jibu unijulishe haraka.
Sawa boss. Derick waliangaliana na Jordan alafu wakacheka
" Ni Nani unataka kumfungulia biashara? Derick aliuliza
" Mbona wewe Ni wakiume alafu unaniletea habari za kimbea .
" Kweli tunahitaji kujua maana siku hizi nakuona upo tofauti sana tupe Siri ya mafanikio.
" Hamna mbona kawaida tu. Derick alipita simu ya Bryan na kukimbia nayo Bryan alinyanyuka na kuanza kumkimbiza
" Derick acha utoto nipe simu yangu.
" Nakupa simu yako Ila tulia kwanza . Walizungushana pale uwanjani Bryan akaamua kuachana nae hata hivyo simu ilikuwa na password lakini ukiiwasha unakutana na picha ya Maria akiwa kwenye tabasamu mwanana.
" Waooo kumbe Mambo yamekuwa hivi . Sasa mbona hutu shirikishi wenzio? Jordan njoo uone Romeo kampata Juliet wake. Derick alipayuka Jordan aliamka haraka akawafuata .
" Sitaki kuamini nilichokisikia, Bryan Ni kweli nilichokisikia? Bryan alitabasamu alafu akamfuata Derick akachukua simu yake. Akaenda kukaa nawenzake wakamfuata na kuanza kumuangalia usoni.
"Ni kweli nahisi nimempenda mtu lakini inakuwa ngumu kumtamkia, nahisi nikimuekeza anaweza kunikataa nikazidisha maumivu moyoni kwangu.
" Huwezi kujikatia tamaa kabla haujajaribu unatakiwa kumuweka wazi na kumuonyesha Ni jinsi gani unampenda. Kwani Ni Nani huyo Juliet wako?
" Maria ndio mwanamke ambae ninahisia nae.
" Kwahiyo umefikiria kufanya Nini?
" Nimefikiria kubadilisha kwanza maisha yake nimpatie kila atakachotaka kupitia zakia.
" Siafikiani na wewe , hili swala tuachie sisi tutamaliza kila kitu wewe tusikilizie sisi.

Itaendeleaaaaaa
KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHH🥵💘10  >>> https://gonga94.com/semajambo/bamtu-mr-sasampa-utam-wangu-mwenyeweeee-aaaasssshh-10
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest