" Asante kwa kuniambia nitaenda kuongea nae " Winnie alienda ofisini kwa Elian
" Hi honey "
Winnie alitaka kumkiss Elian shavuni Elain akamzuia
" Ulikuwa wapi unanijia nyumbani saizi ukiwa unanukia perfume ya kiume ?"
Elian aliuliza Kwa kufoka
" Nilisahau kukwambia honey nilikuwa nyumbani kwa rafiki yang..."
Kabla Winnie hajamaliza kuongea alikatishwa na kibao Cha shavu
" Huyu ndo rafiki yako ? Yani unanifanya mimi mjinga na unanilazimisha nikupigie ikiwa Sina tabia hiyo ya kupiga mwanamke "
" Honey huyu ni rafiki yangu nakuapia "
Winnie alijaribu kumuelezea Elian lakini hakumsikiliza alimsukuma nje ya ofisi yake akafunga mlango
ilipita week nzima Elian na Winnie wakiwa hawana maelewano
Siku ya jumamosi Elian alipata mgeni nyumbani kwake
" Loveness nilisikia bado upo London ?"
Elian alimuuliza loveness
" Nimerudi kwa sasa nataka kupumzika hapa nyumbani kwako siku chake si utaniruhusu? " aliuliza loveness
" Yeah kwanini nisikupokee "
Elian alichukulia ile kama fursa ya kumuumiza Winnie wakati wa kula alimlisha loveness na kuongea nae vizuri lakini kwa upande wa Winnie hakutaka hata kuongea nae
" Kwanini upo hivi siku hizi Elian Kuna kitu nimekukosea, kwanini unanifanyia hivi jamani ?"
Winnie aliongea mwenyewe huku analia
Kwa upande wa Elian alikuwa chumbani kwa loveness
" Unaweza kuniambia Sasa kipi kinakusumbua ?"
Elian alimuuliza loveness
" Elian nakuomba hiki nitakachokwambia usimwambie mtu mwingine yoyote " loveness aliongea huku ameshika mikono ya Elian
" Kwanini umeamua kuja kuniambia mimi kama ni kitu Cha Siri ?" Elian alimuuliza loveness
" Kwasababu nakuamini sana Elian kuliko hata ninavyojiamini mimi mwenyewe , nanimekuja kwako kwasababu wewe ndo msaada wangu wa pekee uliobaki " loveness alianza kulia
" Basi usilie niambie kila kitu kinachokusumbua nakuhakikishia sitomwambia mtu yoyote na nitafanya kila ninachoweza kukusaidia kumbuka wewe ni kama mdogo wangu "
alisema Elian
" Asante sana Elian , si unakumbuka nilienda London kwa shangazi yangu Agatha baada ya baba kulazimisha sana sisi kuoana "
loveness aliweka kituo
" Ndiyo nakumbuka vizuri sana "
" Huko nilikutana na kaka mmoja anaitwa Collins tulikutana kama bahati tu na kuanza urafiki ,urafiki wetu ulitupelekea kuwa wapenzi tulikuwa pamoja kwa mwaka mmoja lakini mwezi uliopita alitoweka na mpaka hii Leo sijui atakuwa wapi na kibaya zaidi nimegundua Nina mimba yake Ina miezi miwili Sasa naogopa Elian kurudi nyumbani nitamwambia nini baba na sitaki kutoa mimba " loveness alizidisha kulia
" Shhh usilie loveness nakuahidi nitakulinda kwa namna yoyote wewe pamoja na mtoto wako na kingine nitafanya juu chini nijue ni kitu gani kimemkuta Collins wako "
Elian alimbembeleza loveness kwa kumkumbatia mlango wa chumba ulikuwa wazi Winnie aliona kila kitu machozi yalimfondoka
" Nilijua tu Sina nafasi tena au ni kuwa sikuwa na nafasi kwenye moyo wake tangia hapo awali " Winnie alirudi chumbani kwake aliangalia picha alizopiga pamoja na Elian
" Huu wote ni uongo ni maigizo kwako Elian kwanini ni mimi peke yangu ninae umia " Winnie alizitupa zile picha kwenye dustbin Aliamua kufungasha nguo zake na kuondoka kwani aliamini hakuna kilichobaki kati yake na Elian
" Miss Winnie unaenda wapi"
Mr Charles alimuuliza Winnie
" Narudi ninapo hitajika hapa Sina nafasi tena Mr Charles "
Winnie aliongea huku anatabasamu lakini moyo wake ulimuuma kama amechomwa na kitu kikali
" Mr Elian anajua kama unaondoka ?"
Mr Charles alimuuliza tena Winnie
" Hapana hajui lakini mimi ni mtu mzima nina uhakika hiki ndicho anachokitaka , kwaheri Mr Charles "
Winnie aliondoka alienda moja kwa moja nyumbani kwao
" Hatimaye mwana mpotevu amerudi kwao " alisema bi Regina
" Embu muache mtoto bhana kwani ukoje Regina "
bi flora alimtetea Winnie
" Shkamoo bibi , shkamoo mama " Winnie alienda kukaa kwenye mkeka
" Marahaba mjukuu wangu za huko utokako kwa kina Tracy hawajambo wote ?" Aliuliza bi flora
" Hawajambo wote bibi vipi baba Yuko wapi ?" Winnie alimuulizia baba yake
"Kwani hujui kama baba yako yupo kwenye duka lake saizi au ndo umeshasahau maisha ya hapa?"
Aliuliza bi Regina
" Mama jamani kwanini nisahau maisha ya nyumbani aah "
Winnie alinyanyuka akaingia ndani
" Na umeshaanza visirani vyako kwani hutaki kuambiwa " alifoka bi Regina
" Regina embu muache mtoto apumzike kwanini unakuwa mkali mkali kwa mtoto "
" Mama hata sijui kwanini ila nahisi kuna kitu hakipo sawa Nina wasiwasi sana na binti yangu japo yeye mara zote anaona kama Nina muonea"
alilalamika bi Regina
" Usiwe na mawazo mabaya Winnie anajielewa hawezi kuwa rimbukeni hata kama amebadilika lakini tunatakiwa kumuamini " alisema bi flora
" Sawa mama nitajitahidi kumuamini "
Kwa upande wa nyumbani kwa Elian alimbembeleza loveness mpaka aliponyamaza alihakikisha amekula vizuri na kupumzika
" Mr Elian Kuna kitu muhimu nataka kukwambia ni kuhusu miss Winnie " alisema Mr Charles
" Sitaki kusikia chochote kumuhusu Winnie kwa Leo kichwa changu kina waka moto sitaki kuongeza stress nyingine utaniambia kesho "
Elian alielekea chumbani hakujua kama Winnie tayari ameshaondoka Usiku ulipita bila ya Elian kumtafuta Winnie
" Kweli huna akili ulihisi anaweza hata kukuuliza uko wapi acha ujinga Winnie na umsahau wewe sio chochote kwake "
Winnie aliweka simu yake pembeni aliangalia dirishani jua lilikuwa likichomoza na hakulala usiku mzima akisubiri japo message kutoka kwa Elian
Asubuhi Elian na loveness wakiwa wanapata kifungua kinywa Elian alishangaa kwanini hakumuona Winnie
" Winnie Yuko wapi ?" Elian alimuuliza Mr Charles
" Aliondoka Jana , unajua atakuwa ameenda wapi ?"
Mr Charles alimuuliza Elian
" ameenda kusalimia nyumbani kwao aende wapi kwingine "
Elian aliacha kula akamuangalia Mr Charles
" Ndiyo ameenda nyumbani kwao lakini wakati huu hatorudi tena "
alisema Mr Charles
" Alisema hatorudi tena ?"
Elian alibaki na mshangao
" Kwanini hakuniambia kitu chochote "
Elian aliacha kula
" Sasa utafanya nini Elian?"
Loveness alimuuliza Elian
" Nitajua nini Cha kufanya "
alisema Elian kisha aliondoka
Kwa upande wa Winnie alikuwa kwenye ofisi za walimu winners primary school
" Winnie mbona kama una huzuni sana !"
Sonia alimuuliza Winnie Tracy nae alisogea kusikiliza
" Ni kweli sipo sawa weekend hii si niliwaambia Dominic ameniomba tutoke wote ?"
" Ndiyo ulitwambia kwani Kuna nini ?"
" Badala ya kwenda hotelini aliniomba twende nyumbani kwake kwasababu tulikubaliana kuwa marafiki sikuweza kukataa kumbe Elian aliniona akanifuatilia wakati natoka nyumbani kwa Dominic aliniona pia hapo ndipo ugomvi ulipoanzia na asubuhi yake alikuja mwanamke pale ndani alionekana kumjali kuliko hata mimi nikaamua tu kuondoka "Winnie aliongea huku analia
" Usilie shoga angu huenda umemuhisi vibaya Elian na huyo mwanamke sio mpenzi wake "
alisema Sonia
" Ni kweli nenda mkayamalize bhana mimi Nina uhakika Elian anakupenda "
alisema Tracy
" Sawa basi nitaenda jioni baada ya kutoka kazini "
Winnie alifuta machozi
Jioni kwenye nyumba ya Elian walipata ugeni alikuwa ni Mr zamba na mke wake bi Adeline
" Karibuni "
Elian aliwakaribisha
"Loveness Yuko wapi ?" Mr zamba aliuliza kwa kufoka
" Yupo chumbani lakini hutakiwi kumfokea uncle "
" Wewe ni nani wa kutupangia yeye ni binti yetu akikosea ni lazima kuadhibiwa "
alisema bi Adeline
" Loveness...loveness " aliita Mr zamba kwa kupayuka loveness alitoka akiwa anatetemeka sana
" Uliondoka hapa Tanzania kwenda kufanya upuuzi huko ,tunataka utuambie hiyo mimba ni ya nani ?" Alifoka Mr zamba
" Daddy ,mom naombeni mnisamehe haki ya mungu tena sikupanga iwe hivi "
" Huwezi kutuletea aibu kwenye familia yetu na hiyo mimba utaenda kutoa ,mke wangu mchukue
" Mr zamba alitoa amri Bi Adeline alitaka kumshika loveness
Elian alienda kumzuia
Na muda huo Winnie alikuwa amefika mlangoni alitaka kufungua mlango ila maneno aliyoyasikia kutoka kwa Elian yalimkata maini alikosa nguvu hata za kusimama vizuriA
Offer offer offer
Soma yote kwa sh 800
Whatsp 0784468229.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.