Bryan alikubaliana na maoni ya marafiki zake alitulia akiwa anasubiri mipango yao wanayopanga. Siku moja Bryan alikuwa yupo kwenye safari zake na dereva wake walipita sehemu akamuona Maria akiwa kabeba beseni kichwani.
" Hebu simamisha gari. Dereva alisimamisha gari Bryan alishuka na kuanza kumfuatilia Maria .
" Maria, Maria.... Bryan aliita Maria aligeuka alipomuona Bryan moyo wake ulishituka alitamani kukimbia lakini akasimama . Alipomkaribia karibu Maria akamwambua
" Kwani bado Mimi na wewe tunadaiana?
" Hapana....
" Sasa mbona tunafuatana Kama tulishamalizana?
" Kwahiyo Ni vibaya hata kusalimiana? Maria aliona ajabu hakutegemea Kama Bryan amebadilika kiasi kile.
" Unajua siamini Kama umenifuata na kuja kunisalimia tu.
" Mbona kitu Cha kawaida Sana , nimefanya hivi ili uamini Mimi na wewe sio maadui. Maria aliachia tabasamu . Lile tabasamu la Maria lilizidi kuvuruga akili ya Bryan akawa anamuangalia moja kwa moja . Mara wakasikia mtu anamuita Maria
" Maria unajua nakusubiri wewe alafu umejisimamisha hapo. Maria aliondoka haraka bila hata kuagana na Bryan. Bryan aliondoka huku akiwa anageuka nyuma anamuangalia Maria.
Baada ya siku mbili kupita Derick anawapigia simu Jordan na Bryan na kuwaomba baada ya muda wa kazi wakutane BM bar.
Ilipofika jioni wote watatu walikutana BM bar walikunywa na kupiga story . Baada ya hapo Derick akaanza kuongea kile alichowaitia.
" Nilikuwa na wazo la husu kuwakutanisha Bryan na Maria. Bryan alikuwa makini kusikiliza.
" Mnaonaje weekend hii tukaenda sehemu tukaweke kambi Kama siku mbili tatu, Ila hatutaenda wenyewe tutaenda na wapenzi, Maria nae atakuwepo....
" Atakuwepo kivip, umeongea nae?
" Hapana Ila hatuwezi kushindwa kumshawishi.
" Unafikiri itakuwa kazi rahisi kumshawishi?
" Upo na master plan kwahiyo tulia , Kuna dada mmoja huwa ananitafutia wafanya kazi hasa ninapokuwa na shughuri na ndio aliemtafuta Maria kipindi kile naweza kuongea nae akamtafuta Maria. Nitafanya Kama Nampa kazi baada ya hapo tutakutana sehemu husika Sasa hapo hutatakiwa kuzubaa bro tukiwa huko itatakiwa kumaliza kila kitu. Derick alimaliza kuongea Jordan alimpa mkono wa kumpongeza
" Hapo umeweza Kaka huu mpango umekaa vizuri Sana na sehemu ya kwenda ni forest maana kule Kuna vivutio vizuri.
Bryan alikuwa kimnya maana hakuwa na uhakika Kama Jambo wanakipanga kitaenda kutimia
" Vipi Kaka mbona kimnya hivyo?
" Hamna shida Mimi nawasikiliza nyie.
" Usijal nitatimiza mipango yangu na wewe jiandae na maneno mazuri kwaajili ya kumvuta Maria awe wako.
"Nitajitahidi japokuwa Nina muda mrefu sijajihusisha na maswala ya mapenzi.
" mapenzi Ni hisia ukimuona maneno matamu ya kumueleza yatakuja tu kikubwa unatakiwa kuwa romantic.
" Na Kama alishindwa sisi typo tutampa darasa. Wote waliishua kucheka na kuendelea kutaniana
Baada ya maongezi kila mmoja aliondoka. Kesho yake Derick alifanya mpango wa kumtafuta Maria mpaka akafanikiwa kuwasiliana nae na badae walikutana
" Maria nimeambiwa wewe Ni mpishi mzuri Sana ndio maana nimekutafutia kwaajili ya kwenda kutupikia Mimi na marafiki zangu .
" Sawa boss kwanza nashukuru Sana kwakunipatia hiyo kazi.
" Usijali nitakulipa vizuri, unatakiwa siku ya ijumaa mida ya saa tatu asubuhi uje nyumbani kwangu hapo ndipo tutaanzia safari yetu.
" Sawa boss nimekuelewa Sana tu.
Hatimae siku ya ijumaa ilifika Maria alijiandaa na safari alipomaliza akaenda nyumbani kwa Derick huko alikutana na Derick akiwa na mpenzi wake Monica. Derick aliwasiliana na wakina Bryan ili waanze safari pamoja. Bryan alitoka na gari lake na Jordan aliondoka na gari yake akiwa mpenzi wake Vivian. Pia kulikuwa na gari lilikuwa limebeba mizigo pamoja na mahema hili liliendeshwa na dereva.
Walipofika walushuka kwenye gari wakakuta wenzo wameshafika wamekaa kwenye vimvuli vya miti huku wakinywa red blue. Maria alishituka kumuona Bryan na muda huo Bryan alikuwa akimuangalia huku akitoa tabasamu kwa mbali. Maria aliangalia pembeni kwa muda alipogeuka akakuta bado Bryan anamuangalia.
Derick na mpenzi wake walienda kuungana nao Maria alikuwa bado kasimama Bryan akamuita
" Maria mbona umejitenga njoo ukae hapa. Maria alimuangalia boss wake Derick alafu akamfuata
" Samahani naweza kuanza kazi?
" Pumzika Maria Sasa hivi kila kitu kipo kaa ufurahie pamoja na sisi. Maria alienda kujitenga mwenyewe maana watu walikuwa wawili wawili kasoro yeye na Bryan. Bryan alichukua boksi la biscuits za chocolate na red blue moja akaenda kukaa karibu na Maria. Alifungua kopo la red blue akampatia, akachukua kipande Cha biscuit akampa huku alimkaribisha.
" Karibu pia kuwa na amani.
KWETU morogoro.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.