Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

NDOA YA MIE : 10

7th Aug, 2025 Views 5


MTNZ: ZAMRATA MBWANA (ZM)
NO: 0698095257

Tulipoishia ni Pale Juma anaumia sana baada ya Majibu ya Ndoa ya Zenafa Kukubaliwa..

Masiku Kazaa yalipita na Zenafa hakuwa na Furaha hata kidogo Kuhusu iyo Ndoa anayotaka Kuolewa Alitafuta Mda ambao Baba Yake Alikuwa kakaa Peke ake na Kumfata

Zenafa : "Baba ni Kweli umekubali Kunitoa Sadaka Kisa tu Tamaa ya Pesa ?"

Zenafa Aliongea huku Machozi yakianza Kumlenga

Baba : "Zenafa Ayo Maneno Umeyatolea wapi ? "

Baba Zenafa Aliongea kwa Ukali Kidogo kisha Akanyamaza Kimya na Kumuangalia Binti yake kwa Upole

Baba : "Samahani Binti yangu. Haijalisha nilikuwa nakupiga Malangapi? Nimekufokea Mala ngapi Lakini Nakupenda Binti yangu na Sihitaji Uteseke "

Zenafa : "Acha ! Inatosha Baba Unanipenda mimi upendo gani unaouzungumzia hapa ? Kati ya Baba na Mtoto kwenda kuniozesha kwa Mwanaume Nisiyemjua ?"

Zenafa Alianza Kuongea huku machozi yakimwagika

Baba : "Ndiyo Sitaki Uendelee Kuteseka Hapa Zenafa Ni Kheri Uolewa uko Labda utakuwa Nafuraha "

Zenafa : "Oh! Furaha , Furaha gani unayo izungumzia hapo kwenda Mahala nisipopajua na kuolewa na Mwanaume Nisiye mjua Baba ?"

Baba Yake Zenafa Alijinamia chini kwa Mda na kuinua kichwa Chake

Baba : "Zenafa Binti Yangu Unaniona hii hali yangu sio wa Kupona leo au Kesho nitachelewa sana , na kama unavyo ona mna mke na hawo Dada zako je ni nani atakae Wahudumia Mwanangu ni Wewe Fanya kwaajili yangu Basi Mwanangu, Pia Binti yangu Mimi nishazeeka Mda Wowote naweza Nikafa Sasa Wewe utaishi Maisha gani hapa Kijijini Mwanangu na huna ndugu "

Baba Zenafa Aliongea huku Machozi yakimwagika kwa wingi

Zenafa Alikaa Kimya kwa Muda huku Akitafakari maneno ya Baba yake

Zenafa : "Sawa Baba nitaolewa "

Zenafa Alisema hivyo, Baba yake Zenafa hakuamini Masikio yake na Aliachia Tabasamu pana . Wakakumbatiana ...

Zenafa Amekubali kuolewa. Ndoa ilitangazwa Kijiji Kizima Na Mahali ilitolewa yote Kiasi cha Milioni 1 Na Mzee Kazumari Aligharamia . Galama zote za Shughuli na Juma ndo Alie enda Kuoa kama Mbadala wa Mahili yani Alimuolea Mahili .

Siku ya Ndoa Zenafa Alipendeza sana Alipodolewa Vizuri na Kuvyeshwa Nguo nzuri . Juma Alizidi Kuchanganyikiwa Alivyomuona Zenafa Ndani ya Shela Zuri yani Aliwaza kama Ndo Anakuwa wake Kweli . Alivyoambiwa Akamchukue mkewe Alimwangalia Usoni kwa Mda Mrefu

"Umependeza sana Zenafa Wewe ni mrembo kuliko nilivyokuwa Nafikiria eti "

"Asante Juma "

Juma Aliongea hayo Maneno na kuachia Tabasamu Lakini Alivyokumbuka mke Hakuwa wake Bali ni Wamahili Tabasamu lote lilipotea Gafla

Hatimae Ndoa ilipita na Zenafa Alikuwa Mke Halali wa Mahili Kazumari. Walimchukua Zenafa na Kumkodia Chumba Walipofikia Wao pia na Siku ya Pili Safari ya Kuelekea Dar es Salaam ilianza Majira ya Asubuhi kutoka Iringa hadi Jioni Waliingia Katika Jiji la Dar es Salaam .

Zenafa Kwa Mala ya Kwanza Alikanyaga Kati Jiji la Dar bila Kumjua Mume Mwenyewe Amekubali tu kwaajili ya Kumlizisha Baba yake Mzazi

"Habar "
"Salama Shikamoo "
"Malhaba "
"Khe ! Mzee Kazumari Naona umeamua kuongeza House girl mpya "

Mzee Kazumari : "Hapana Mkwe Wangu Fifi huyu ni Mke wa Mahili nimemuolea Mahili "

Fifi : "Eti nini ? Mamaaaaaa!!!"

Fifi Alipaza Sauti na Kumuita Mama Mkwe wake Kwa Sauti Hakuamini maneno Aliyosikia . Fifi Alikuwa Mke wa Mtoto wao mkubwa wa kwanza Kaka yake Mahili Alieitwa Faridi.

Mama yake Mahili . Bi Tausi Alikuja Hupesi kwa Kushuka Ngazi Kutoka juu ya Chumbani kwao Nyumba yao ilikuwa ni ya Golofa Vyumba vya Kulala Vilikuwa Juu

"Ushaanza Fifi kuna nini tena ? Oh!Mzee Kazumari Umeludi Mumewangu "

Aliongea Bi Tausi nakuachia Tabasamu Pana Walisalimiana

"Karibu Binti "
"Asante "
"Mzee Kazumari kuna Rafiki yako yeyote Aliekuagizia House girl maana kwa Hapa Nyumbani Sijui kama kuna Uhitaji wa House Maid kwa Sasa ?"
"Hapana Mkewangu hakuna Alieniagiza na Wala hatuhitaji House Girl huyu Binti unae Muona Hapo Mbele yako sio Binty binti tu. Anaitwa Zenafa ni Mkweo ni Mke wa Mahili nimemuolea "
"Eti nini we Mzee !!! Ivi hicho unachokiongeakinatoka Mdomoni kwako au Naota ? Ulimuuliza Mahili ili Suala au Umekulupuka ?"
"Naomba uniacha Bi Tausi nimechoka na Safari usinichoshe Zaidi. Mahili Sijamshilikisha ila Kwakuwa Ni Mwanangu na Mimi kama Ndo baba yake Mzazi atakaa na uyu mke "
"Acha Mambo yako Mzee Kazumari usifanye vitu kama umechanganyikiwa Sawa ? Mahili unajua Fika kama Anampenzi wake Sasa kwanini Umletee huyu Bushman ?"

Mama Mahili Aliongea kwa Hasila Kuonesha Ajapendezwa Kabisa na ilo Swala la Mwanae Mahili kuolewa Mke bila Kushilikishwa

Mzee Kazumari Alimuita Mfanyakazi Mmoja na Kumwambia Amkalibishe Zenafa kwenye Chumba cha Mahili

Mzee Kazumari Alimaliza Kuongeana Kupanda Juu ya ngazi na Kuelekea Chumbani kwake .

Bi Tausi Alijishika Kichwa na Kukaa kwenye Sofa Alivulugwa mno

"Mungu Wangu nitamwambia nini mimi Mahili lazima atanilaumu na atasema nilikuwa najua hili kabla "

Alikuja House girl na Kumpeleka Zenafa Katika Chumba cha Mahili Ambacho kilikuwa juu ya Golofa pia kilichokuwa Tulivu na Upepo Murua na Madirisha Makubwa ya Vioo

Zenafa Aliingia Katika Chumba cha Mahili kwa Mara ya Kwanza na Alikanyaga Sakafu lain na ya Baridi Kitanda Kilicho tandikwa Vizuri kwa Mashuka Myeupe na Mito iliyo Pambwa Vizuri

Alifika na Kuweka Shangazi kaja lakoMlangoni

"Waooo! Chumba kizuri sana "

Alisema Zenafa nakuanza Kuzunguka Chumba Kizima na Aliiyona Picha Kubwa iliyopo ukutani Ambayo Alikuwa Mkaka Handsome boy Aliepiga Kifua Wazi huku Akiwa Kavaa Suruali Ya Jinsi Picha Haikuwa Yakuonyesha mtu Mzima mzima ilionyesha Nusu lakini ilivutia sana

Picha Haikuwa ya Mtu Mwengine bali ilikuwa ni Picha ya Mahili

Zenafa Alivyoiyona ile Picha Aliganda kwa Mda na Kuiyangalia kwa Umakini

"Ni Picha Nzuri sana bila Shaka Atakuwa ni yeye huyu "

.........

Fifi : "Mama itakuwaje Sasa , Tutamwambia nini Mahili Mungu "

Aliongea Fifi huku Aking'ata ng'ata Vidole vyake

"Mama Nashauli Uyu Binti tukamuweke Vyumba vya House girl yani Mahili Asimkute Chumbani kwake "

Wakati Wanaongea hivyo Mala Mahili Aliingia. Kutoka Kazini Akiwa Kavalia Suti Alifika na Kusalimia. Na moja kwa moja Alielekea Chumbani kwake

Bi Tausi Aliinuka na Kumuangalia Mwanae anavyoelekea uko Chumbani

"Mahi.

Alijaribu Kumuita Lakini Alisita

Mahili Alipandisha Ngazi Taratibu na Kuanza Kulegeza tai na Kuingia Chumbani kwake Alishangaa Mlango wa Chumba chake Kuwa Wazi na Taratibu Alipiga hatua na Kuelekea Chumbani Gafla Alipokelewa na Mshangazi Kaja Mlangoni Ambolo lilitaka Kumdondosha "Mamaaaa"

Lakini Zenafa Alifika Upesi na Kumdaka Na Wote Walidondokea Chini Na Zenafa Akawa Chini Mahili akawa kwa Juu wakabaki Wanangaliana Usoni

ITAENDELEA 11.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NDOA YA MIE : 10   >>> https://gonga94.com/semajambo/ndoa-ya-mie-10
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest