Meyael alimuangalia Fariss jinsi alivyokuwa anachsnganyikiwa kwaajili ya Salma.
" Kwahiyo na wewe umeamua lipi kati ya kuachana nae au kumbeba pamoja na mizigo yake?
" Bado nina nafasi ya kumbadilisha.
Fariss alinyanyuka kwenye kiti na kuvaa kiti lake kisha akatoka ofisini.
Majira ya jioni Fariss alikuwa mtaani wa saba walikuwa wamesimama kwenye kichochoro huku akiwa wameegemea ukutani pale kichochoroni waliongea kwa bashasha, walionekana kuwa na furaha isiyoelezeka. Fariss alikuwa akimshika nywele za Salma polepole huku macho yao yakitazamana kwa hisia kali.
"Unajua Salma, sijawahi kufurahia company ya msichana kama yako... we ni tofauti kabisa na wanawake niliowahi kukutana nao , unanikosha sana .Fariss alisema huku akitabasamu.
Salma alicheka kwa sauti ya chini, "Utanielewa tu kwa muda... we mwenyewe utashindwa kuacha huu mtaa."
" Dhamira yako ni kuniteka kazima mpaka Mohamed kwetu na kuja kukaa kwenu.
" Ikiwezekana.
" Basi usijali muda sio mrefu nitahakikisha kambi.
" Utaweza maisha ya uswahilini?
" Kwaajili yako nitaweza.
Alafu Salma tuache utani unajua nataka nikuchukie lazima kama vipi nikuweke ndani kabisa ili mali zangu ziwe salama ...
" Yani hapo roho inakiuka unaona kama huku sipo salama kabisa.
" Hilo ni jibu salma unajua mambo unayofanya utakuja kuniita na presha.
" Yani wewe ulitakiwa tu kunizoea nina mambo mengi lakini kwenye swala la mapenzi huwa najiheshimu sana huwa sichanganyi wanaume wawili au zaidi kwa wakati mmoja. Nakupenda Fariss ndio maana mpaka sasa nipo na wewe na huko mitaa ya jirani kuna shuhuri najua leo wataulizana kwanini sijatokea huko.
Farris alimuangalia usoni huku akiniambia
" Yani hujui tu ninavyohusika unavyoongelea hivyo vigoma vyenu vya ajabu natamani hata serikali iingilie kati vipigwe marufuku.
" Vipi unafikiria nini?
" Hakuna kitu, vipi kama tukaenda sehemu kutulia?
" Fariss mpenzi umetoka kazini unatakiwa kwenda nyumbani kupumzika .
" Ahaaaa unataka niondoke ili wewe uende ukadandiwe na wanaume huko kwenye ngoma zenu za ajabu.
" Ohoooo yani sijui kuna shetani gani anapenda kutuchonganisha kila tukikutana tunaanza kwa raha na furaha ila kumaliza tunamalizia kwa Shari.
" Yote unataka wewe Salma huna huruma kabisa na moyo wangu.
Ghafla sauti ya mwanamke mkubwa ilikatiza ikisema
"Salma! Unafanya nini hapa?"
Salma alishtuka, alipoangalia nyuma alimkuta mama yake akiwa kasimama mikono kiunoni na mitandio kaweka shingoni.
"Naongea," Salma alijibu kwa hofu huku akimwachia mkono Fariss.
"Mmmh... Unaongea sawa, lakini swali langu ni unaongea na nani? Huyu ni nani hapa mtaa wa saba sijawahi kumuona?"
Salma alimeza mate kwanza kisha akajibu "Mama huyu ni... ni... Fariss."
Mama alimtazama Fariss juu chini kama anampima urefu Kisha akasema kwa sauti ya juu,
"Aah! Mkwe si ndiyo?"
Fariss alijawa na mshituko, hakutegemea mama atasema hilo. Fariss alipojiandaa kusema neno, salma akakatiza,
"Bado hatujafika huko ndio....
" Sawa lakini najua ndio mkwe maana taarifa ninazo kuwa umepata mwanaume pedeshee. Ila kusimama vichochoroni ndio tabia gani? Kwani nyumbani hupaoni? Kama mgeni anaelekea na mwenye heshima zake mlete nyumbani jamani!"
" Farasi karibu nyumbani.
" Mama acha kuharibu majina ya watu ni fariss sio farasi.
" Majina mengine magumu jamani haya baba nifuateni nyuma twendeni nyumbani.
Mama Salma alitangulia
Salma aligeuka na kumwambia Fariss, "Usiogope, mama yuko hivi kila siku."
Mama akaanza kutembea mbele huku akiwaambia, "Twendeni jamani, msinipotezee muda. Naenda mbele mnifuate."
" Salma kuna usalama kweli isije ikawa shida ?
Fariss alihisi kama ameanguka kwenye mtego, lakini akavumilia. Walifika kwakina Salma, nyumba ya rangi ya blue iliyochakaa . Kabla hata hawajakaa vizuri, mama Salma alianza kuongea.
"Aaah jamani! Karibu sana kijana. We ni mgeni hapa. Hii nyumba si ya kifahari lakini tuna roho safi. Hatuna kitu ila tinavutu."
Kama imezoea AC basi hapa hakuna ac wala deni kuna vipepeo.
Salma akacheka, "Mamaaa acha kejeli bana."
" Lazima nimwambie ukweli si inapenda binti wa uswahilini bwana .
Mama alitoka jikoni na kuja na sahani za wali na maharage,
“Kula chakula kijana. Kama hujawahi kuonja maharage ya mtaa wa saba leo ndio siku yako.”
Chakula cha ukweni hicho nimepika mama mkwe wako yaani hilo harage limewekwa nazi ya kutosha wewe onja mwenyewe utaniambia.
" Asante mama.
" Kula Fariss asimuogope huyu mama wa maneno mengi.
Fariss akaanza huku akitabasamu ilikuwa ngumu abaki kwake kukutana na familia ya aina ile.
Baada ya kumaliza kula mama Salma alirudi sebleni akakaa chini ya mkeka na kunyoosha miguu.
" Asante mama, tamu sana mama.
" Nilikwambia kupika nimefundishwa na bibi yangu mwanakombo alikuwa anakaa Mkanyageni huko Tanga kwa mapishi alikuwa balaa sasa urithi wake wote kaniachia mimi .
Badae ya kuongea akavuta leso yake na kujifuta jasho.
"Sasa baba nina ombi moja tu...
" Ombi gani mama? Alisema Fariss huku akisikiliza kwa makini ombi kutoka kwa mama mkwe wake
" Nipatie hela ya marejesho. Kuna mtu nilichukua kwake elfu ishirini, alafu nikachelewa kulipa nikamuomba anivumilie siku mbili sasa leo ndio siku ya mwisho. Na kama sikutoa, kesho patakuwa hapatoshi hapa uwanjani.
Khaaaaa mama mbona unanitia aibu hili ni swala la kumwambia mgeni na ndio kwanza umeonana nae leo?
" Wewe mtoto sijui mchawi umechukua roho ya shangazi yako mwajuma hutaki mti apate. Unakumbuka baba yenu ni mlevi tu na aliwakimbia kaenda kuishi kwa Hawara ajawatelejeza nikehangaika kama hayawani ......
" Mama naomba achana na hizo habari unaongea nini mbele ya mgeni wangu una....
Ilibidi Fariss aingilie kati
" Usija Salma.
Fariss alimtuliza Salma kisha akatoa Wallet
na kumpatia shilingi elfu hamsini.
Mama alizopokea zile hela na kuzibusu alafu akasema,
“ asante sana mwanangu, Mungu mkubwa, huyu kijana ni wa kubarikiwa sana Salma usimwache, ukimwacha utakula huu na hasara juu.
Wenzako wanaotafuta hizo nafasi wanaenda mbio kwa waganga ili wapate wanaume kama hawa.
Mama Salma linyanyuka akatoka nje na kuwaacha Salma na Fariss wakiwa kimnya.
.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.