Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

NIPE YOTE DADY 56~57

7th Aug, 2025 Views 46



Alijibu "Unaweza kwenda itakufuata " jibu hilo lilinishtua nikasoma mara mbili mbili na kumtumia ujumbe " Selim naomba urudi nyumbani tuongee mume wangu".

Ujumbe ulipokelewa ila hakujibu zaidi ya kuni bleutic na kukaa kimya ,siku ile nililia jamani nililia mpaka nikaa kiwa natetekeka sasa sijui kwasababu ya kulia sana nilianza kupata kizunguzungu na kichwa kuuma sana , nilijitahidi kuinuka ili nipande kitandani ila nilidondoka na kupoteza fahamu.

Nilikuja kuamka nikiwa hospital nikakuta Jabir ndio yupo pembeni yangu, alivyoona nimeamka akaniuliza ninavyojisikia.

Nilijibu niko sawa na kumuuliza kwann niko hapo, kabla hajajibu akaingia doctor na kuniangalia akaniuliza najisikiaje nilijibu kuwa niko sawa japo nahisi kichwa kizito kiasi .

Doctor akaniambia kuwa natakiwa kutokuwa na msongo wa mawazo maana nitamuweka mtoto hatarini kitu ambacho hakitakuwa salama kwa afya yangu .

Nilishtuka na kuuliza "samahani mimi ni mjamzito?'"

"Ndio unaujauzito wa mwezi mmoja na nusu "

"Sorry sielewi doctor mbona mwezi uliopita niliingia kwenye siku zangu sasa inakuwaje nakuwa namimba ?"

"aam madam hilo linawezekana sana na kama huamini unaweza kupima tena ila huo ndio uhakika wewe ni mjamzito"nilibaki kimya Jabir alinipa hongera kisha akatoka na kunifuatia chakula nje maana nilikuwa nahisi njaa .

Jambo lakuwa na ujauzito sikulifurahia sana wala pia sikuchukia kiufupi nilikuwa sieleweki kitu pekee nilichokuwa nawaza ni ndoa yangu .

Niliona kabisa inaenda kufa na kibaya sijui shida au chanzo nini maana kila kitu kimetokea ghafla sana , basi Jabir alirudi nikala nilipomaliza nikapima vipimo vingine na kurudi nyumbani.

Tulifika nikakuta gari la Selim likiwa limepack nje kuonesha kwamba amerudi, nilishuka haraka na kuingia ndani nikakuta wanajagawia watoto zawadi .

Kwa mwendo wa unyonge nilisogea na kusalimia kama kawaida Selim hakuitika Nasra akanihug pale na kujichekesha eti alinimiss , sikutaka kuonesha tofauti yoyote hivyo nikajifanya kuchangamka kama kawaida.

walipomaliza kuwagawia zawadi watoto Selim aliingia chumbani nikamfuata na kumkumbatia kwa nyuma akanitoa na kusema " Talaka yako hiyo hapo mezani unaweza kuendelea na maisha yako kuhusu watoto watakaa hapa nyumbani na mama yangu"

Nilihisi kupigwa shot machozi yalinitoka bila kikomo nikapiga hatua mpaka mezani na kuchukua karatasi kweli ilikuwa nu talaka tena tatu.

Hivi naelewaka ninaposema talaka tatu ? nilihisi mwili wote umelowa jasho nikamuuliza "Selim mume wangu hiki ni nini baba "

"Umekuwa kipofu kwamba kusoma hujui ? "
"Hapana sio kwamba sijui ila sielewi kwann unipe talaka tena tatu ni kosa gani nililofanya mpaka kufikia hatua unachukua maamzi kama haya "

"Sikia mwanamke sina mda wakubishana au kuongea na wewe chakufanya saizi chukua kila kilicho chako ondoka kwenye maisha yangu milele"

"Selim kweli unaelewa unachokiongea mume wangu ? najua ndio hatuko sawa ila tunaweza kuongea na kuwekana sawa kama siku zote "

"Kuongea ? unaona rahisi sana nakuuliza unaona rahisi ?"

"Ndio mume wangu yanaongeleka hata kama itakuwa ni ngumu ila tunaweza kuongea yakaisha na kila kitu kikarudi kuwa sawa kwani hakuna tatizo lakudumu hata hivyo sijui kwann haya yote yametokea ,zaidi nahisi ni shetani tu anataka kututenganisha "

"Shetani ametokea wapi unafanya ujinga wako huko alafu unakuja kusema shetani ? "

"Selim mimi nimefanya nini mume wangu ee kuwa muwazi basi ili nijue nimekosea wapi maana naona kama unanituhumu kwakitu nisicho kijua "

"Nimekwambia sina mda wakuongea we chukua vyako ondoka , hizo habari za nimekosa nini hazina msaada wowote " nilijitahidi sana kuongea na kutaka kujua shida nini ila wapi mwisho akakasirika na kunitoa ndani kwa nguvu .

Nilipiga magoti huku nikilia na kumsihi anisamehe japo sikujua kosa langu nilipi ila hakunisikiliza , alinitoa mpaka nje na kuchukua nguo akanitupia huku akifoka .
Cha kushangaza mama yake hakuongea kitu akawa amekaa sebleni huku akinywa juice kwa mlija watoto walilia dada akawachukua na kwenda nao chumbani.

Nilibaki nalia nje nikiomba kufunguliwa mlango ila hakutoka , mara malango ulifunguliwa akatoka Nasra nikakimbia haraka na kusema "Nasra nisaidie kuongea na Selim asiniache tafadhali"

Nasra alitabasamu na kunishika akanisogeza pembeni kidogo kisha akasema "Unaumia sanaee? pole sana ila hayo ndio maumivu ya kuachwa na mimi niliumia hivyo hivyo unavyoumia wewe .

Kwahiyo bidada pole ila pia nikuambie tu kwamba mda wako wa kuwa na Selim umeisha sasa niwakati wangu."

Nilishtuka na kumuangalia akacheka kicheko cha dharau na kusema , "vip mbona umeshituka imekuwa surprise sana au hahahaa pole , najua ndio utakuwa huamiani hiki unachokisikia ila nikwambie tu kwamba nilikuja kwenye hii nyumba kuchukua kilicho changu na namshukuru Mungu nimepata .

Tena kwa kutumia njia rahisi sana , sasa Selim ni wangu na kizuri zaidi anafurahia penzi langu kiasi cha kuona alipoteza mda kuwa na wewe .

So dear sister unaweza kuondoka mbaaali utuache na maisha yetu na watoto wetu"

Nilihisi kuzimia nisielewe anachokisema nikweli au naota inamaana Selim ametoka na Nasra kweli dada yangu wa damu hapana.

Nilibisha na kumwambia "Nasra kama umekuja kunitisha sitishiki kwasababu namuamini mwanaume wangu najua hawezi kufanya ujinga kama huo ndio hatuko sawa ila haimaanishi kuwa ameniacha "

Alicheka sana na kusema " amakweli huna akili hivi nikuulize kwa ufahamu wako unadhani kwann nilikuja kupanga karibu na kwako au unafikili kuwa nikweli nilishindwa kulipa kodi ya nyumba au nilikosa kazi hadi nikubali kufanya kazi kwenye kampuni yenu jibu ni hapana .

Au unafikilia ni kwann amebadilika ndani ya mda mfupi? kwanza jibu unalo maana siku ile ulitumia sim yangu kumtafuta baada ya kuona hakujibu ila kwangu akajibu so huo ndio ukweli, Kwamba nilifanya yote kwasababu nilikuwa ninalengo langu na limetimia , na hii ndio asili yangu kilicho changu kitabaki kuwa changu daima .

Kwa hiyo kwasasa unatakiwa kuondoka kwenye maisha yangu na mume wangu mtarajiwa embu subiri kwanza "

Alitoa lock kwenye sm yake na kunionesha picha nikitoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango baada yakuona picha akiwa na selim kitandani .

Hakuishia hapo akaniambia " okay hii unaweza usiamiani acha nikwambie kwa maneno Selim maumbile yake yako ............ " nyie hakuna siku niliyochoka mwili mpaka roho yani alitaja maumbile yake ya siri jinsi yalivyo mpaka alama aliyokuwa nayo kwenye kalio akaitaja hadi saizi ya boxsa anayovaa hadi rangi anazopendelea zote akataja .

Niliishiwa nguvu na kukaa chini huku machozi yakinitoka .
KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NIPE YOTE DADY 56~57  >>> https://gonga94.com/semajambo/nipe-yote-dady-56-57
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest