Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

SEHEMU YA TISA* SALMA MTAA WA SABA ❣️

7th Aug, 2025 Views 25



" Mama yangu anaongea sana mzowee mama wa uswahilini maneno mengi.
Fariss alitabasamu kisha akasema
" Usijali kawaida , hata hivyo muda umeenda nataka kuondoka sasa.
" Sawa twende nikusindikize.
Fariss alijua Salma anataka kumsindikiza haraka ili aende kwenye ngoma.
" Salma naondoka na najua unataka kwenda kwenye huo utamaduni wenu sasa nakuomba kuwa makini sitegemei kuona kitu cha ajabu kwenye mitandao ya kijamii pia naomba ujiheshimu wewe ni mwanamke wa mtu anaejielewa.
" Sawa leo nitajishikilia kidogo hata hivyo sitaenda kukaa sana.
Wakisindikizana mpaka barabarani Fariss akapanda kwenye gari yake akaondoka na Salma bila kupoteza muda alikimbilia kwenye shuhuri.

Fariss aliendesha gari lake kwa utulivu. Alikuwa na mawazo mengi kichwani, macho yake yakiangalia barabarani. Hali aliyokutana nayo pale mtaa wa saba nyumbani kwakina Salma ilimshuhurisha moyo na akili. Hakujua kama alipaswa kucheka au kulia, lakini kitu kimoja alikifahamu alimpenda Salma kwa moyo wake wote.
Ila familia yake yote ilikuwa changamoto.

Akiwa njiani kuelekea nyumbani, akapiga simu kwa Meyael,
" Niambie baba wa mtaa wa saba.
Meyael alimtania na Fariss alitabasamu na kusema
“Bro nakuja nyumbani kwako nataka tuongee.”
" Unakaribishwa.

Dakika thelathini baadaye Fariss alikuwa amefuka nyumbani kwa Meyael, uso wake ukiwa umejaa msisimko mchanganyiko wa mshangao na huzuni.
Meyael akamwangalia rafiki yake kisha akatabasamu, “Nimeambiwa ulikuwa mtaa wa saba... umeokoka au umepotea?”
Fariss alitikisa kichwa huku akishika paji la uso.
“Wewe acha tu Meyael... sijui nianzie wapi. Yaani nimekutana na familia ya Salma. mama yake nilikutana naye vichochoroni akanikokota kama mkwe, akaniburuza hadi nyumbani. Halafu loh! Nikapewa chakula kwa sahani ya plastiki... wali na maharage yaliyotiwa nazi , Mashaallah ulikuwa mtamu mama mkwe anajua kupika.
Meyael aliangua kicheko.
" Usiniambie kuwa umeshajulikana mpaka ukweni.
" Ndio nilianza na shemeji na sasa mama mkwe.
" Eheee baba mkwe haujamuita?
" Kwa maongezi nilivyosikia ni kwamba hayupo kwenye maisha yao.
" Amefariki au?
" Hata mimi sijui.
Ila inavyomuuma Salma ndio mama yake alivyo kwahiyo Salma hajaokota zile tabia.
" Wacha weee.
" Yani siku ya kwanza tu nimeongea hela ya marejesho...
Meyael alicheka kwa sauti mpaka machozi yakamtoka,
“Fariss! Yaani umeshindwa ujanja na mama mkwe hadi anakuvua noti?!
Sasa ulifikiri upendo wa mtaa wa saba ni wa hisia tu? Huo ni mzigo unaokuja na familia nzima. Karibu kwenye reality!”
Fariss naye alicheka kidogo, lakini alibaki na huzuni fulani moyoni.
“Lakini bro... Salma ni mzuri, ni tofauti. Ila kuna kitu kinaniuma. Nilipomuangalia usoni, niliona alivyokuwa akijisikia.
" Farris unajua upofu wa mapenzi utakupoteza huwezi kubeba familia ya aina hiyo kwanza ina tabia za ajabu kaka Kibaka, mama kama hivyo na Salma nae ni mcheza chura.
Kauli ya Meyael ilimchukiza Fariss. Alifurahishwa na maneno ya kuwakashifu.
" Unanikosea sana Meyael hupaswi kuwaongezea vibaya sababu hujui sababu ya wao kuwa hivyo.
" Sawa lakini ukweli huwa unauma.
" Sitaki kugombana na wewe . Alisema Fariss huku akinyanyuka na kuondoka.
" Masikini sijui yule mtoto wa uswahilini kampa nini mpaka anakuwa haelewi kinachoendelea.

Kesho yake, Fariss alipanga kukutana na Salma sehemu tulivu cafe ya kisasa pembezoni mwa jiji, mbali kabisa na kelele za mtaa wa saba. Salma alifika akiwa amevaa gauni lenye staha, rangi ya samawati, nywele zake zikiwa zimefungwa vizuri.
Salma alimkuta Fariss kashafika .
Fariss alipomuona akanwambia
“Leo umekuwa wa tofauti,”
" Asante ila haya yote sababu ni wewe mpenzi wangu maana hata huko mtaani nasifiwa sana na wengine wanasema sasa ndio napaswa kujiita rasmi jina la malkia wa mtaa.
Fariss alikuwa anacheka tu.
Walikaa wakapiga soga kidogo, kisha Fariss akasema kwa utulivu,
“Salma... naomba usichukulie vibaya nitakachokuambia.
Salma kama alishituka kidogo.
" Wewe unataka kuniambia nini? Unataka kuniacha? Maana sio kawaida kuwa mpole hivyo yani unaongea kwa hisia flani
" Umefika mbali sana Salma, Naomba leo usikilize tu.
Salma alivuta pumzi alitulia akawa anasikiliza.
"Najua unajitahidi sana, najua hujajitengenezea maisha yako jinsi ila nataka nikuelewe vizuri zaidi.”
"Unaanzia mbali sana na sijui unataka kunielewa kivipi? Farris kama mama yangu alikosea ile jana tunaweza kuongea tu tukayamaliza .
" Wala mama yako hakunikosea kuna mambo nataka kujua kuhusu wewe.
Salma alinyamaza, akimtazama kwa macho ya kuuliza.
Fariss akaendelea,
“Najua baba yako hayupo… nataka unieleze kidogo kuhusu familia yako yani maisha yako kiujumla.
Salma alishusha pumzi kisha akaanza kusema.
“Fariss… maisha yangu hayajawahi kuwa rahisi hata siku moja Baba alikuwa mlevi, nikisema mlevi ni mlevi haswa aliacha familia na kwenda kuishi kwa mwanamke mwingine. Alituacha na mama wakati tukiwa wadogo. Hakuna aliyetusimamia shule ipasavyo, hakuna aliyejua kama tunaenda shule, tunaandika, tuna daftari au kalamu. Mzazi alikuwa akiitwa shule hakuna alienda mama alikuwa anasema
" Nikienda shule Mtakula nini ? Anaondoka anaenda kwenye shuhuri zake za ukungwi
ndio maana hata elimu yangu haikukamilika. Mama alikuwa kungwi, anahangaika kwenye sherehe ,maharusi, kitchen party, hata tohara. Ndiyo kazi zake.
Dada zangu wengi ( sasa) alibeba mimba kabla ya muda, Abuu, kaka yangu amekuwa kibaka. Na mimi… nimejifunza kuishi tu. Kuna siku tunakula, kuna siku tunalala njaa. Ila bado napambana.”
Farris hatupati muongozo mzuri tangia hapo mwanzo tulizurula kama chokoraa au kama kuku wa kienyeji ikifika asubuhi kila mmoja anashika njia yake jioni wote tunarudi bandani.

Fariss alibaki kimya kwa muda. Alimkazia macho Salma, si kwa kumhukumu, bali kwa kumuonea huruma.
“Nashukuru umeniambia haya. Inaniuma sana. Lakini sasa naelewa... tatizo si wewe, ni malezi. Ni mfumo uliokulea. Salma, nakupenda. Lakini tunahitaji kujifunza maisha mengine. Niko tayari kukusaidia kuona dunia nje ya mtaa wa saba.”
Salma alimtazama kwa mshangao.
“Unamaanisha nini?”
Fariss alishika mkono na wake kwa upole.
“Namaanisha... nataka kukutoa kwenye hayo mazingira. Nitakupeleka sehemu tofauti. Tutaenda kwenye semina, tutahudhuria matukio ya watu waliostaarabika. Utaona dunia nyingine. Sitaki ubadilike kwa sababu yangu tu, bali kwa sababu yako pia. Una thamani kubwa sana, Salma.”
Salma alilia kimya kimya. Hakuzoea kumuona Fariss aliongea kwa makini kiasi kile na tabasamu lake lililokuwa limebeba huruma .
Siku hiyo alikuwa anaonekana kama mtu mzima, anayetaka kusimamia jambo kiende sawa.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SEHEMU YA TISA* SALMA MTAA WA SABA ❣️  >>> https://gonga94.com/semajambo/sehemu-ya-tisa-salma-mtaa-wa-saba
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest