Haikupita hata mwezi juddy alifariki na taarifa tulipewa na Zakia mwenyew, nilimuombea apumzike kwa amani tu , sijui ndio mambo ya mganga au ni mungu tu ameamua sijui yeye
Hakuna hata aliewaza kwenda msibani
Nilishukuru sana mungu mambo yote kuisha na nina amani tena , Alex aliipangisha ile nyumba , tukatafuta nyumba ingine kwa ajili ya kuishi
Baada ya miezi minne ya ndoa ndio ,nilijikuta nina ujauzito afu nilikuwa nishaweka kijiti daah
Ilibidi tu nikatoe zangu kile kijiti nilee mimba yangu huku nasimamia biashara zangu mwenyewe
Mtoto wa juddy alikuwa yupo kwao na Felix na kilikuwa kimekuwa kikubwa tu , Sikutaka pia awe karibu yangu mana Felix alikuja tena kuomba msamaha kwa Alex na kuomba ile Famili Friends iendelee
Mi nilimwambia alex sihitaji ukaribu na huyu mtu mana mtoto wake anakuwa huyu afu ni mtoto wa juddy na akikuwa mkubwa akaja kupata story ya mama yake anaweza nichukia mie na kudhani ndie nilimuuwa mama yake
Hapana sitaki awe karibu yangu, Alex alinielewa kweli akamwambia Felix hatuwezi kuwa karibu tena kama zamani
Felix alielewa tu akasema sawa haina shida .
Nilijigungua salama kabisa tena nilipata mapacha wote wa kike , Alex akasema hao ndio wa mwisho hakuna kuzaa tena nikasema sawa mungu atukuzie watoto wetu hilo ndio muhimu
Nilinaki na watoto wawili yaan wale wa kike afu wale wa kiume anao mama yaan mama mkwe alikataa kabisa kunipa akasema atawatunza yeye tu ..
Ukweli nilikuwa na maisha ya furaha sana sana ..
Siku moja Alex alirudi kutoka safari wakati huo alikua ameanza kufanya tena kazi kwenye Shirika binafs la ndege
Akanambia mke wangu kuna kitu nahitaji tufanye
Nikamuulize kipi tenaa ??
Hapo watoto wangu wana kama miezi 7 hivi
Akanambia
"Mke wangu ,nataka ukutane na mtu hapa anaweza kukusaidie lile tatizo"
Mmh nikajiuliza tatizo gani tenaaa??
"Lipiii"
"Nataka urudi tena shule, nataka ujue kusoma "
Heee jamani kumbe hii kusoma ipo tu jamani nilikuwa nishasahau kabisa kama sijui kusoma
"Mume wangu!!!!" Sikuona kama naweza mana hata mara ya kwanza nilifeli ndo nilikuwa sina hata majukumu kabisa sembuse leo??
Akanambia we tulia mke wangu mi nitafanya lolote na utaweza kuna mtu nahitaji kesho twende ukaonane nae
Nilikubali tu sa nitafanya ninii??
Kesho yake akanambia twende huku ,nilijiandaa vizuri tukatoka , safari iliishia kwenye Jengo moja hivi mikocheni ilikuwa ni Ghorofa ndefuu
Tunaingia kwenye Lift mpaka Ghorofa ya 5 hapo alex aliniongoza kwenye Chumba flani mlangoni paliandika Doctor
Sikujua Doctor wa nini hata, nilifata tu nyuma
Nilimkuta mwanamama mmoja hivi , alitukaribisha kwenye kochi zilikuwa pale Ni kama ofisi flani hivi
"Huyu ndie mke wangu anaitwa salma,, salma huyu ni mtaalamu wa Saikolojia anaitwa Doctor Lian naomba uwe Comfortable tafadhali " alex alinitambulisha kwa yule mama
"Salma karibu sana" alinikaribisha huku ananyoosha mkono na tabasam kama lote
Nilikuwa na kiwasi wasi cha mbali, nikasema asante Doctor
Mi nilijua napelekwa shule au kwa mwalimu mwisho naletwa kwa Doctor wa Saikoloj et
"Tunaweza kuanza ,njoo hapa"
Aliniambia nimfate nikasimama kwa Mbele kulikuwa na kutanda hivi kidogo dogo akanambia lala hapo , nililala akawasha mwanga karibu kabisa na Uso wangu
"Unaitwa nani???" Aliniuliza baada ya muda kidogo ule mwanga kunimulika usoni
"Salma Omar"
"Una watoto wangapi??"
"Wa nne"
Yaan nikawaza hivi mie naonekana kama sina akili vizuri auu??
Mbona ananiuliza maswali ya kipuuzi hivyo et??
"Mumeo anaitwa nani??"
"Alex"
"Unafanya kazi gani??"
"Biashara!!"
"Sawa tumemaliza, unaweza kuinuka"
Nilishangaa kwahiyo hapa ndo kala hapa hela mmh
Akamwambia Alex ,Kesho mlete alex akasema sawa, alijaza jaza baadhi ya karatasi na pale alikuwa ananiuliza nikijibu anaandika hata sijui alikuwa anaandika niniii ..
Kesho yake tena alex alinichukua Tukaenda yaani hapo bado sielewi kwanini naenda kwa huyo doctor
Tulifika akatukaribisha vizuri tu akanambia tena njoo hapa kitandani , nilipanda pale nikalala kama jana
"Salmaa!!' Aliniita yule mama
'Abee"
"Umeanza kusoma shule ukiwa na miaka mingapi"
"Miaka 6"
"Ulikua ukiichukia shule ??"
"Hapana"
"Embu nambie kipi ulikuwa hukipendi shule yaan kilicho kuwa kina kuboa sanaa ukiwa shule"
"Nilikuwa sipendi sana ugomvi, lakini haikufanya niichukie shule"
"Ooh naa......"
Aliniuliza maswali mengi kuhusu shuleni nilikuwa napenda nini?? Mwalimu wangu mkuu ni nani mara ufauru wangu
Nilijibu yote kabisa, Doctor akasema saw inuka ,niliinuka nikaenda kukaa pembeni ya Alex kwenye kochi
Doctor aliandika andika akanambia Umelelewa na nani??
Nikamwambia mama yangu akanambia sawa Alimgeukia alex akasema sioni kama kuna shida yeyote ni ubongo tu ndio ulikuwa mzito na hapo kuna tatizo tunaita... alitaja hilo tatizo Mi hata sikumbuki mana gumuu
Akamwambia Alex kuwa hii inaweza kuwa alipata shida akiwa mdogo sana , naona nianzie hapo
Naomba niongee na mlezi wake ..
Basi tuliondoka alex akasema sawa anakwenda kuongea na mama.
Tulipo toka pale tulienda moja kwa moja kwa mama nyumbani alex alimwambia mama kuwa kesho tunaomba twende wote...
ITAENDELEA.....
KWETU morogoro.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.