Alex alimuelezea mama Kitu kuhusu yale ya kule kwa doctor , mama akasema sawa nitakwenda
Kule Tuliambiwa twende Siku ya J3, siku ilifika tukaenda mie, alex pamoja na mama
Doctor alitukalibisha vizuri,
Akaanza kuongea na mama , mi na Alex tulikuwa kimyaa kujua anataka nini kutoka kwa mama
Doctor alijitambulisha kwa mama akamwambia nimekuita hapa kuna vitu nahitaji kujua wakati salma alipo kuwa mdogo yaaan kuanzia siku ya kwanza ulipo mzee kuna changamoto yeyote labda alipitia ??
Mfano homa kali, au alizaliwa kwa njia isiyo ya kawaida , ama alipata tatizo huko hospital, tukachana na Hospital makuzi yake nyumbani yalikuwaje mpaka pale alipo anza shule ama alipo anza kujutambuaa ?? "
Mama alinitazamaa kweli , alikuwa kama kuna kitu anafikiria unajua mpaka mimi niliogopa tena nikasema hee au niliwahi kufa nikiwa mchanga mbona mama ananitazama kwa huruma sanaaa??
Doctor akawambia kuwa huru mama mimi nahitaj kumsaidia salma bado hatujachelewa tunaweza kuamsha ubongo wake na ukachangamka tena , ila tujue tu tatizo ni nini ??
Mama akasema
"Nilipo shika ujauzito wa salma, nilipitia mambo mengi sana ya heka heka zisizo na kawaida kabisa, nilipambana kama mama ili kuvuka hicho kipindi , mpaka inafika miezi kumi na moja kasoro nilikuwa bado sijajifungua , hospital waliniandikia tarehe niende kwenye Operation, ilikuwa bado siku tatu ifike tarehe ya Op ndio nikapata uchungu
Nilijifungua kawaida mwanangu lakini hakulia kabisaa, alikuwa kachoka sanaaa ,alipewa huduma za haraka haraka baada ya kugundua bado kipo haii ,alikaa Chini ya uangalizi maalumu zilipita siku mbili ndio mwanangu alilia ..
Tulika sana hospital mana afya yake ilikuwa mbaya bado na mie nilikuwa mwenyewe hakukuwa na msaada na baba yake ndie alienisababishia shida mie wala hakutokea ....."
"Embu mama unaweza kunambia ni shida gani labda alikusababishia baba yake ambae alikuwa mumeo!!?"
"Baba salma , tangu nilipo shika mimba ya salma alibadilika sana , alikuwa ananinyanyasa mnoo, alinipiga karibu kila siku na sehemu zake za kupiga ni tumbini na usoni hakujali hata kama nina mimba , Nilijua hata mimba inaweza kuhalibika Lakini haikuwahi hata kutikisika sikuwa na pakwenda na nilikuwa na mtoto mdogo ambae ni dada yake salma ....
Kushinda njaa na kulala njaa ilikuwa kawaida na huku nina ujauzito naweza naliza wiki nzima nakinywa tu uji basii hakuna kitu kizito nakula .. "
Mungu wangu yaan kwa mara ya kwanza ndio najua kuwa mama yangu kumbe kuna maisha aliwahi kupitia magumu kiasi hichii yaan daah nilijikuta najiskia vibaya sana laiti ningewahi kujua walai nisingekuwa namjibu vibaya enzi zile akinituma nakataa anainuka mwenyew , nilitamani kulia jamani mama aliongea mengi manyanyaso aliyopitia kwa baba yanguu
"Uliwahi hata siku moja kumshtak??" Doctor alimuuliza ye mwenyewe alikua anasikitika mama akasema hakuwahi kushtaki selikarini lakini kwenye familia alipeleka kesi kila siku na hakuna mabadiliko yeyote
"Pole sanaa!"
"Nimepoa"
"Kwahiyo maisha yalikuwaje baada ya kurudi nyumbani na mtoto"
"Nilikaa Hospital wiki tatu , hali ya mwanangu ilikuwa hivyo hivyo, hakuwa analia kabisa , nilirudi nyumbani sikumkuta mume wangu na mtoto wangu nilimkuta kwa majirani ambae ni dada yake Salma, tangu hapo nilianza kumlea mwanangu kwa shida sanaaa
Hakuwahi kucheka mwanangu, muda ulienda zaidi ya kukaa tu hakuwahi kutembea wala kutambaa
Mpaka inafika miaka mitatu mwanangu alikuwa anakaa tu chini ,shingo yake haikuwa imekaza ilikuwa imelegea ,
Nilijuwa mwanangu atakuwa hivyo lakini kuna mtu aliniambia kuwa kuna mazoezi ya mtoto wa aina yangu na atakuwa sawa
Ndio nilianza kufatilia niliambiwa gharama zake
Niliongeza nguvu ya kufanya biashara, ili nipate pesa , nilimuanzishia mazoezi
Mungu mkubwa sana baada ya miaka miwili mwanangu alibadilika sana alianza kujifunza kutembea na hata alikuwa anacheka kitu nilichomshukuru sana mungu
Ulifika muda ,alianza kuongea yaan ile kwa kujifunza , ndipo hapo nilimuanzisha na shule ili achangamane na wenzie
Mpaka leo sikuwahi kumwambia yey nini kilimfika kwenye kuzaliwa kwake ..
Doctor alinitazama sana , kisha aliendelea kumuuliza mama maswali maswali mengine ,kipindi nilipo anza shule makuzi yangu yalikuwaje mama aliongea yoote .
Doctor akatuambia sawa muda umeisha,,Juma tano uje Salma , mama nimemaliza kazi na wewe..
Tuliondoka mpaka nyumbani kwa mama , nilimwambia Alex naomba nibaki na mama , akanambia haina shida nitakufata kesho nikasema sawa ..
Nilihisi mama anatakiwa kupata faraja kwangu zaidi kuliko wengine wotee ,
Baada ya alex kuondoka ,nilimwambia mama pole sana
Mama alicheka akanambia wewe ndio polee , uliteseka sana kuanzia ukiwa tumboni
Nilihis kulia aisee ,niliacha tu machozi yanitoke , nikikumbuka mie niliibeba mimba yangu ya kwanza,nikiwa nipo kwenye kupoooza ,nikalia nikasema mungu nateseka
Kumbe mama yangu aliteseka zaidi na hakuwa na mtu hata wa kumfariji
ITAENDELEA..
KWETU morogoro.
   
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.