Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

SEHEMU YA KUMI* SALMA MTAA WA SABA ❣️

9th Aug, 2025 Views 20



Baada ya mazungumzo marefu na changamoto kadhaa, Salma alikuwa ameanza kuruhusu moyo wake kuupokea upendo wa Fariss kwa uzito zaidi.
" Fariss naomba usiniache kwajili ya matendo yangu unajua kwenye maisha yangu sijawahi kukaa kwenye usiano kwa muda mrefu kama hivi. Nakupenda sana Fariss na kama nilivyokwambia juwa nitaacha mambo yote na kufuata kile unachotaka.

Fariss alilidhika kiganja cha Salma na kukipeleka karibu na mkono wake na kumbusu.
" Nakupenda sana Salma na kama itaamua kubadilika basi una nafasi kubwa kwenye maisha yangu .
Waliendelea kuongea mambo mengi kuhusu maisha yao na kupeana ahadi nyingi.

Siku za mwanzo Salma aliamua kujikaza na kukaa nyumbani kwao hakuwa akitembea ovyo yani kutoka nje bila sababu maalumu na hata kilipokuwa na sherehe mtaani alijitahidi kujizuia. Mashoga zake walimpitia lakini hakwenda japo walimwambia kuwa anaringa sababu Kapata mwanaume mwenye pesa.
" Salma siku hizi una ringa sana tangia umepata huyo mwanaume wako anayekuja na Kigari chake hapa basi atukohiwi .
" Hayo ni yenu jamani ongezeni niwezavyo lakini msimamo wangu ni kuwa siendi.
" Kumbuka na wewe ni mtoto wa hapa mtaa wa saba umekua hapa litakuja jambo lako sijui utasimama na nani.
Salma alipuuza lawama za wenzie alijifungua ndani.
Farris alikuwa akimtoa mara kwa mara walienda kutembea kwenye sehemu maarufu hususani mahoteli makubwa pia alimkutanisha na watu wake wa karibu na kumtambulisha kama mpenzi wake.
Hata Meyael alipomuona jinsi Salma alivyokuwa kabadilika anawaza vizuri aliamini kuwa Fariss ana haki ya kumganda kuanzia siku hiyo Meyael hakuingilia penzi lao wala kuongea neno kuhusu Salma.

Siku moja mama Salma alitoka kwenye mizunguko yake akiwa kashikilia nguo mkononi. Aliingia chumbani kwa Salma na kumrushia.
" Kijora hicho cha sale.
" Sale ya nani?
" Zuwena.
" Lakini unajua siku hizi huwa sipendi kwenye hizo sherehe.
" Wewe mtoto usiache mbacgao kwa msala upitapo huyo mwanaume wako asikutoe kwenye asili yako . Kwanza anakupangiaje maisha wakati hata hajakuwa na hao watu wasomi huwa hawana maana hata kidogo mwisho wa siku inaachwa hapo anachukua mwanamke wa kuendana nae. Kwani mwanangu hata television huwa huangalii wewe watu wanavyohitaji ? Mtoto wa uswahilini anadanganywa kumbe mwanaume ana mwanamke wake ulaya.

Maneno ya mama yake ni kama yalimkatisha tamaa Salma akaona kile alichokiongea mama yake ni kitu sahihi. Alichukua kijora na kukuangalia kama limepanuliwa mpasuko itakayomuwezesha kupiga mwamba wakati wa kucheza.
" Sherehe ni lini vile?
" Kesho jioni ndio mambo yanaanza.
" Sawa nitaenda.
" Hayo ndio maneno sasa.

Kesho yake jioni Salma alikuwa akijiandaa kutoka kwenda kwenye sherehe.
Alisimama mbele ya kioo, akipaka poda laini kwenye mashavu yake huku akijipamba kwa ustadi. Alivaa kijora chake cha sare kile cha mtoko chenye rangi ya zambarau chenye mauwa makubwa makubwa meupe. Akijiwekea vizuri tayari kwa kutoka .
Lakini kabla hajatoka, alisikia sauti ya mwanaume ikisikika kutoka sebuleni.
Akisikiliza kwa makini akagundua ni sauti ya Fariss Aliikumbuka sauti alikuwa akizungumza na mama yake .
Moyo wake ulishituka Kwa haraka alivua kijora alichovaa na kutupia kando na kujifunga kitenge, kisha akaruka juu ya kitanda kana kwamba alikuwa amepumzika muda . Alijilaza akijaribu kudhibiti pumzi zake zilizokuwa zikitoka kwa kasi.
Baada ya dakika kadhaa, mlango wa chumba chake ulifunguliwa polepole. Fariss aliingia.
Alisimama mlangoni na kumtazama kwa mshangao.
"Salma... unalala muda huu?
Salma alijifanya anaingilia maumivu.
"Salma upo sawa kweli? Aliuliza Fariss kama ana hofu.
"Ah... nimesikia kichwa kinauma ghafla. Nikalala tu."
" Unajihisi homa?
Fariss alitembea hadi pembeni ya kitanda. Akamuangalia huku akimpima joto kwa kiganja chake.
" Mwili wako hauna joto sana.
" Sina homa ni kichwa tu.
Fariss alimuangalia vizuri usoni kisha akauliza.
"Salma, hivi kweli kichwa kinauma au ulikuwa unaenda sehemu?
Salma alishituka akakaa na kumuangalia.
" Nitoke niende wapi bila kuaga na nimekwambia naumwa kwani huamini?
" Mtu mwenye maumivu ya mwili huwa hawi hivyo.
" Vipi?
" Umejiremba usoni kwako kama vile ulikuwa unataka kutoka .
Salma hakuwa na cha kujitetea alinyamaza kimnya.
Fariss akachukua mkono wake na kuushika .
"Angalia, Nakupenda kwa sababu naona juhudi zako. Ila kama kuna jambo unataka kusema, ni bora useme sasa kuliko kufanya kwa siri."
Salma alimuangalia Fariss kwa macho yaliyojaa woga na upendo.
"Sio rahisi kuacha kila kitu mara moja. lakini nipo kwenye njia hiyo. Siendi , najizuia lakini naona kama ni ngumu sana kwa kuacha haraka haraka . Farris naomba unipe muda kidogo.
Fariss alitabasamu.
"Najua, na hilo ndilo linalonifanya nikuone wa thamani. Nitakusaidia kushinda hicho kipindi. Lakini tafadhali, kuwa muwazi na mimi."
Unataka kwenda kwenye shuhuri?
Salma aliitikia kwa kichwa.
" Sawa vaa nguo twende.
" Na wewe unaenda? Salma aliuliza kwa mshangao.
" Kwaajili yako nitakwenda. Ila sio siku zote.
Salma alimtazama kwa macho yaliyokuwa na machozi kidogo.
"Umenifanya nijione kuwa bora, Fariss."
" Wewe ni bora kwangu.
Walikumbatiana kwa upole.
Baada ya hapo Salma alivaa kijora chake na kuweka nywele zake vizuri.
" Tayari.
" Umependeza sana.
"Asante . Salma aliangalia chini kwa aibu
Baada ya hapo walitoka pamoja wakaelekea kwenye shuhuri huku Salma akiwa haamini kama Fariss ameamua kumsindikiza nae aliniambia anatarajiwa kucheza kwa tahadhari maana mwenye mali yupo analinda mali yake.

Full 1000
Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SEHEMU YA KUMI* SALMA MTAA WA SABA ❣️  >>> https://gonga94.com/semajambo/sehemu-ya-kumi-salma-mtaa-wa-saba
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest