Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

SEHEMU YA KUMI NA NANE* A STRANGER WHO STOLE HIS HEART❣️

9th Aug, 2025 Views 18



"Loveness Yuko wapi ?" Mr zamba aliuliza kwa kufoka

" Yupo chumbani lakini hutakiwi kumfokea uncle "
" Wewe ni nani wa kutupangia, yeye ni binti yetu akikosea ni lazima kuadhibiwa "
alisema bi Adeline

" Loveness...loveness " aliita Mr zamba kwa kupayuka loveness alitoka akiwa anatetemeka sana

" Uliondoka hapa Tanzania kwenda kufanya upuuzi huko ,tunataka utuambie hiyo mimba ni ya nani ?" Alifoka Mr zamba

" Daddy ,mom naombeni mnisamehe haki ya mungu tena sikupanga iwe hivi "

" Huwezi kutuletea aibu kwenye familia yetu na hiyo mimba utaenda kutoa ,mke wangu mchukue"
Mr zamba alitoa amri Bi Adeline alitaka kumshika loveness Elian alienda kumzuia

Na muda huo Winnie alikuwa amefika mlangoni alitaka kufungua mlango ila maneno aliyoyasikia kutoka kwa Elian yalimkata maini alikosa nguvu hata za kusimama vizuri..

" Loveness hatoenda kokote kwasababu mimi ndo baba wa mtoto " Elian alisema hivyo kumtetea loveness na mtoto wake aliyeko tumboni lakini hakujua kama Winnie amesikia kila kitu

" Ndomana sihitajiki hapa tena "
Winnie aliondoka huku machozi yakimtoka hakutaka kwenda nyumbani kwao alienda moja kwa moja kuonana na Sonia pamoja na Tracy aliwaelezea kila kitu

" Yule Elian kumbe na yeye ndo wale wale hatuwezi kukubali twendeni ni lazima alipie "
alisema Sonia

" Ndiyo haiwezekani akufanyie hivi bila aibu yoyote kwa Richard ulituzuia tusifanye fujo lakini huyu hatumuachi " Tracy alisimama

" Hapana sitaki tena kujihusisha nae nataka tu kuwa na watu wa kunipa furaha ,upendo ili niweze kumsahau kwenda kumfanyia fujo hakutosaidia chochote "alisema Winnie

" Ni kweli rafiki yangu " Sonia alimkumbatia Winnie na Tracy nae akawakumbatia kwa juu

Ilipita week nzima bila Elian kumtafuta Winnie

" Elian kwani kulikuwa Kuna ulazima gani wa kusema kuwa wewe ni baba wa mtoto ona Sasa kinachotokea wazazi wanaanza kulazimisha ndoa tena " alilalamika loveness

" At least tumemuokoa mtoto kwanza na nimeagiza watu wakamtafute Collins usiwe na wasiwasi na kuhusu ndoa nimeshawaambia hatuwezi kufunga ndoa mpaka utakapojufungua na wakati huo Nina uhakika tutakuwa tumempata Collins "

" Asante sana Elian , na vipi kuhusu mpenzi wako Winnie unampango gani ?" Aliuliza loveness

" Oh mungu wangu nilikuwa naenda kusahau ngoja niende nikaongee nae "
Elian alienda Moja Kwa moja winners primary school akiwa kwenye gari alimuona Winnie aliongea na kucheka na Dominic walionekana kuwa karibu sana

"Kwanini wapo karibu hivi na alisema sio wapenzi "
Elian alikasirika sana alishuka kwenye gari alienda kuushika mkono wa Winnie akamvuta mpaka kwenye gari Dominic alibaki kushangaa tu

" Una nini wewe unaniumiza bhana " Winnie alilalamika

" Ulisema ni rafiki yako tu kwanini mpo karibu sana namna hio?"
aliuliza Elian kwa ukali

" Sidhani kama una haki ya kuniuliza Hilo swali Mr Elian "
Winnie alitaka kushuka kwenye gari Elian akamzuia

" Unamaanisha nini mbona sikuelewi ?"

" Usicho kielewa ni kipi hapo ,namaanisha mimi na Dominic ni wapenzi " Winnie aliongea vile ili kumuumiza tu Elian ila hakuna kweli kuhusu Hilo Elian aliuachia mkono wa Winnie alihisi kuumia sana ila alijikaza akatabasamu

" Hongera hatimae umempata mwanaume unayempenda na uliyeendana nae well done "
Winnie hakutaka kuendelea kukaa pale alishuka kwenye gari akaondoka Winnie aliamua kurudi nyumbani ,akiwa nyumbani alikuwa na mawazo sana yaliyopelekea mpaka kuzimia aliwahiswa hospital

" Doctor binti yetu anasumbuliwa na nini ?" Aliuliza bi Regina

" Mmmh binti yenu ni mzima Hana ugonjwa wowote ila anatakiwa kupunguza stress haziwezi kuwa nzuri kwa mtoto wake aliyekuwepo tumboni "
alisema dactari mzee Patrick ,bi Regina na bi flora walibaki kushangaa Winnie aliruhusiwa kurudi nyumbani

" Winnie binti yangu unaweza kutuambia baba wa mtoto wako ni nani ?"
Aliuliza bi Regina kwa upole

" Winnie aliweka mkono wake mmoja juu ya tumbo lake akaanza kulia

" Winnie acha kulia ,kulia hakusaidii kitu "
alisema bi flora

" Naombeni mnisamehe ila siwezi kumtaja baba wa mtoto huyu ni mtoto wangu peke yangu "
aliongea Winnie huku anafuta machozi

" Utakapokuwa tayari kutuambia tupo hapa kukusikiliza "
bi Regina alikuwa mpole sana siku hiyo Winnie hakutaka kuficha aliwaambia Sonia na Tracy kuwa yeye ni mjamzito

" Sasa utafanya nini Winnie ?"

" Nitamleta huyu mtoto mwenyewe sishindwi kufanya hivyo "
alijibu Winnie huku anatabasamu na mkono wake aliiweka juu ya tumbo lake

Ulipita mwezi mzima bila Winnie na Elian kukutana ila kila mmoja alimkumbuka mwenzie mimba ya Winnie ilifikisha miezi mitatu na kwa upande wa loveness mimba yake ilifikisha miezi minne

" Tumbo likianza kuonekana sijui itakuwaje ?"
Winnie alijiuliza mwenyewe akiwa anatembea pembezini mwa barabara bila kutarajia Kuna gari nyeusi ilipaki pembeni yake na dakika moja tu ilitosha kwa watekaji kumpandisha kwenye gari na kuondoka nae

" Mnanipeleka wapi ?" Winnie alipiga kelele watekaji waliamua kumzimisha Winnie alikuja kuamka akiwa ndani ya jengo moja lililochoka sana na alikuwa amefungwa kamba aliangaza huku na huku aliwaona wanaume wawili waliovalia vinyago vyao usoni wakikagua pochi yake

" Si nilikwambia zero lazima ni yeye hatukukosea hata kidogo na kikubwa zaidi umeona hii kadi ni mjamzito "
aliongea vuvuzela huku anachekelea

" Ndomana nakuaminia vuvu Yani huwa hukosei hata kidogo na Mr Elian ni lazima atatoa kiasi chochote tutakachomtajia " alisema jambazi mmoja aliyeitwa zero

" Nyie ni kina nani?" Aliuliza Winnie , vuvuzela na zero waligeuka kumuangalia

" Umeshaamka mrembo wa Mr Elian CEO tajiri katika umri mdogo " aliongea zero huku anacheka kicheko Cha kumfanya mtu atetemeke kwa uoga ila Winnie alijikaza

" Mtakuwa mmekosea na kumteka mtu tofauti mimi Sina uhusiano wowote na huyo mtu wala simfahamu " Winnie alimua kumkana Elian

" Hahaha usitufanye sisi ni watoto wadogo fungua simu yako na tutahakikisha sisi wenyewe "
vuvuzela alimkabidhi Winnie simu baada ya kumfungua kama za mikononi

" Siwezi kufungua simu yangu na kwanini nifanye vile mnavyotaka nyie ?acheni kupoteza muda kwangu hamtopata chochote "
Winnie aligoma kufungua simu yake

" Kweli wewe ni mrembo na jasiri sana ndomana Mr Elian alikupenda kirahisi ,tunaweza kukuumiza wewe pamoja na mtoto wako kama hautatoa ushirikiano "
alisema zero Winnie alianza kuogopa alishika tumbo lake

" Tafadhali nawaomba msije mkajaribu kumuumiza mtoto wangu "
Winnie aliongea huku analia

" Kama hutaki iwe hivyo basi Fanya kila kitu tunachokwambia ,fungua simu yako na umpigie mr Elian "
alisema zero Winnie alifanya kama alivyoelekezwaA

Offer offer offer
Soma yote kwa sh 600

Whatsp 0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SEHEMU YA KUMI NA NANE* A STRANGER WHO STOLE HIS HEART❣️  >>> https://gonga94.com/semajambo/sehemu-ya-kumi-na-nane-a-stranger-who-stole-his-heart
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest